Ugonjwa wa kiungulia

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,527
14,400
Kiungulia ni tatizo linalowapata watu wengi. Kiungulia ni hali ya kukukosesha raha ya kusikia kuwaka moto kwenye eneo la kifua na kuenea hadi shingoni na kwenye koo. Ukiwa na kiungulia unaweza kusikia ladha ya uchachu nyuma ya koo. Kiungulia kinaweza kudumu kwa muda mfupi au kikaenda kwa saa kadhaa. Kiungulia huwa kikali zaidi baada ya kula au ukilala mara baada ya kula.

Ukiwa na kiungulia cha mara kwa mara au kikali, unaweza kuwa na matatizo ya kiafya ya chronic acid reflux, au gastroesophageal reflux disease (GERD) au pengine ujauzito. Kiungulia kinaweza kutibika nyumbani kwa dawa za kununua.

Dalili Za Kiungulia
Unapokuwa na kiungulia unaweza kuziona dalili zifuatazo:
. Kuwaka moto sehemu za kifua hali inayodumu kwa dakika au saa kadhaa
. Maumivu ya kifua ukiinama au kulala
. Kuwaka moto kooni
. Ladha ya uchachu, ya chumvi, asidi nyuma ya koo
. Shida katika kumeza.

Kiungulia Husababishwa Na Nini?
Ili kujua kwa nini kiungulia kinatokea, ni muhimu kujua jinsi umio (esophagus) na tumbo vinavyofanya kazi. Unapokula, chakula huteremka kupitia kijibomba kirefu kinachounganisha mdomo na tumbo. Kijibomba hiki huitwa esophagus. Chini ya esophagus kuna vali (valve), inayoitwa esophageal sphincter. Vali hii hufunguka ili kuachia chakula kipite na . Chakula chenye mafuta mengi
. Bidhaa za nyaya
. Pombe
. Juisi zinazotokana na matunda ya jamii ya michungwa
. Vinywaji vyenye kafeini
. Vinywaji vyenye kaboni.
Hali nyingine zinawezoweza kusababisha kiungulia ni:
. Unene
. Uvutaji wa sigara
. Kuwa na msongo mkali wa mawazo
. Kuvaa nguo zinazobana na mikanda.


Tiba Kwa Ajili Ya Kiungulia
Mara nyingi kiungulia huweza kutibiwa nyumbani kwa kununua dawa au kwa kubadili staili ya kuishi. Kuwa na kiungulia mara chache ni kitu cha kawaida na mara nyingi hakuleti madhara makubwa. Lakini endapo unapata kuingulia mara kwa mara na kikali, unahitaji msaada wa tiba kwani inaweza kuwa ni dalili ya tatizo sugu kama la GERD. GERD huweza kusababisha matatizo makubwa zaidi kama esophagitis (hali inayoweza kuharibu tishu za umio), Barret’s esophagus au hata kansa. Wakati mwingine daktari anaweza kuhitaji kuchukua kipimo cha endoscopy kujua chanzo cha tatizo. Endoscopy ni uchunguzi wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kutumia kifaa kinachopindika kinachotoa mwanga.

Kuidhoofisha esophageal sphincter ya chini. Kuacha kuvuta sigara kunashauriwa kwa afya njema, na kuiimarisha vali hiyo.

Kulalia upande wa ushoto. Kulala kwa upande wa kushoto kunaweza kuuboresha mmeng’enyo wa chakula na uondoaji wa tindikali kwenye tumbo na umio haraka zaidi.

Kunyanyua sehemu ya juu ya kitanda chako. Kunyanyua sehemu ya juu ya kitanda kutafanya kichwa na kifua kuwa juu zaidi ya miguu. Weka matofali ya nchi sita au vitabu chini ya mihimili ya juu ya kitanda chako. Usitumie mito. Mito inaweza kuleta msukumo mkubwa zaidi juu ya tumbo na kukuongezea kiungulia.

Weka plani ya mazoezi yako ya mwili. Subiri angalau saa mbili baada ya kula ndipo ufanye mazoezi. Mazoezi ya kabla yanaweza kuamsha kiungulia. Yafaa kunywa maji mengi kabla na wakati ukiendelea na mazoezi. Maji husaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia ukosefu wa maji mwilini.
 
Dawa za kienyeji au kizungu?
Tumia nyanya mkuu.
Menya maganda ya nyanya(ile ngozi ya juu kabisa isiwe na nyama nyingi), weka kikaangio jikoni kipate moto then yapike kwa moto mdogo ukikoroga mpaka yabadilike rangi na kuwa meusi.
Subiri yapoe, yasage kwa kiganja yawe unga kisha ifadhi kwa ajili ya matumizi.

Kila uhisipo kiungulia unalamba kidogo inasaidia sana.
 
Kula tangawizi inasaidia kutibu kiungulia. Unaimemya unatafuna, haitochukua mda

Wengine naona wanalamba majivu, dakika chache tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom