Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,236
Kwa yeyote anayejua tiba mbadala ya typhoid please naomba msaada.Nikisema mbadala namaanisha matunda,mizizi,mimea ama vyakula.
Bwana Yesu asifiwe.
===============
Bwana Yesu asifiwe.
===============
Homa ya matumbo
Homa ya matumbo husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhi. Ugonjwa huu huambukizwa kwa mtu kula au kunywa chakula au maji yalio na kinyesi cha mu aliyambukizwa.[SUP][1][/SUP] Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu.
Dalili
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
- Homa kali
- Kutoka kwa majasho mengi
- Kuharisha (bila ya kutoa damu)
- Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.
Katika wiki ya kwanza:
Katika wiki ya pili:
- Joto la mwili huongezeka
- Kichwa huuma
- Kukohoa
- Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
- Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Wiki ya tatu:
- Homa huongezeka
- Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
- Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
- Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
- Kutapika kwa mgonjwa
- Ini la mgonjwa huvimba
- Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu ikimalizika, homa huanza`kutilia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.
- Matumbo hutoa damu.
- Matumbo hutoboka
Matibabu
Mara nyingi, homa ya matumbo haiuwi binadamu. Dawa kama ampicillin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, Amoxicillin and ciprofloxacin hutumika kutibu wagonjwa katika nchi zilizoendelea.
Hatua za kuzuia kupata homa hii
Historia
- Usafi wa mazingara na wa kibinafsi ni hatua bora ya kujikina kutokamana na ugonjwa huu.
- Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hivyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
- Homa hii hueza kuenea kwenye mazingara ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
- Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majinaTyphim Viiliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.
Mnamo mwaka 2004-05, janga la homa ya matumbo lilizuka katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoathiri watu 42,000 na kuuwa watu 214 (kulingana na ripoti ya shirika la World Health Organisation).
Waathiriwa maarufu
- Mary Mallon, aliyejulikana kama Typhoid Mary.
- Louisa May Alcott, mwandishi wa Little Women.
- Charles Darwin, mwanasayansi, aliathirika pindi alipoenda nchini Chile mnamo 1835.
- Eugenia Tadolini, alikufa mjini Paris mnamo 1872.
- William Wallace Lincoln, mtoto wa tatu wa Abraham Lincoln, ambaye ni rais wa 16 wa Marekani, pamoja na Mary Todd Lincoln, walifariki kutokana na maradhi haya mnamo February 20, 1862.
- Wilbur Wright, alikufa mnamo May 30, 1912 baada ya kuugua homa hii.