Uganda: Waziri wa Mambo ya Nje asema Waganda wanaokufa njaa ni wajinga

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Waziri wa masuala ya kigeni nchini Henry Oryem Okello amesema kwamba waganda wanaokufa njaa ni wajinga miezi kadhaa baada ya baadhi ya maeneo kukumbwa na njaa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, umasikini na ukosefu wa usalama miongoni mwa sababu nyengine.

Akizungumza na runinga ya NTV Uganda, alisema kwamba hali ya hewa ya taifa hilo ni nzuri kwa wakuilima kupanda chakula cha kutosha.

''Hao ni wajinga wajinga zaidi ambao wanaweza kufa njaa nchini Uganda. Hawa ni wajinga kwasababu kuna chakula cha kutosha Uganda. Ukifanya kazi kwa bidii kuna ardhi yenye rutba Uganda, hali ya hewa ni bora licha ya mabadiliko kiasi. Iwapo utaweka juhudi maradufu kwa kuamka mapema lima shamba lako na kupanda mbegu na kulinda mimea yako kwa kweli utakosaje kupata chakula'', aliuliza bwana Oryem.

Matamshi yake yanajiri siku chache baada ya rais Museveni kuuambia mkutano wa viongozi kutoka maeneo yasioegemea upande wowote kwamba picha za kusikitisha kwa raia wa Uganda wanaoonekana kukumbwa na njaa kaskazini mashariki mwa taifa katika jimbo la Karamoja sio uhalisia wa hali ya bara la Afrika.


 
Back
Top Bottom