Uganda: Mlinzi wa mgombea wa Urais Bobi Wine, amefariki dunia ikidaiwa ni kwa kugongwa na gari la Jeshi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Ripoti za vyombo vya habari Uganda vinakariri mashahidi wakisema kwamba Francis Kalibala, aligongwa na gari la jeshi la Uganda UPDF wakati msafara wa Bobi Wine ulikuwa unarudi Kampala kutoka Masaka katika kampeni.

Katika taarifa kupitia mitandao ya kijamii Bobi Wine amesema “nasikitika kutangaza kifo cha mmoja wa walinzi wangu Francis Kalibala aliyegongwa na gari la jeshi namba H4DF 2382 ambalo liliziba njia karibu na Busega na kutuzuia kupita.” Ameandika Bobi Wine na kuongeza kusema“Francis amefariki mda mfupi baada ya kufika katika hospitali ya Rubaga.”

Lakini msemaji wa jeshi la Uganda Brig. Flavia Byekwaso amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Francis alianguka kutoka kwa gari lililokuwa linaendeshwa kwa mwendo wa kasi.

“Francis hakugongwa na gari la jeshi la UPDF. Alianguka kutoka kwa gari namba UBF 850Z .” amesema Byekwaso katika ujumbe wa twitter.

Waandishi wa habari wajeruhiwa vibaya

Kabla ya tukio hilo, waandishi kadhaa wa habari walishambuliwa na polisi na kujeruhiwa vibaya.

Waandishi hao walikuwa wanafuatilia tukio ambalo polisi walimzuia Bobi Wine kufanya kampeni na kuzua makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa Bobi wine katika mji wa Masakaa.

Waandishi walipigwa na kujeruhiwa na mabomu ya kutoa machozi.

Wamelazwa hospitalini mjini Masaka.

Miongoni mwao ni mpiga picha wa televisheni ya Bobi Wine ya Ghetto TV, Ashraf Kasirye, mwandishi wa shirika la habari la Nation Media Group – NTV Ali Mivule.

“Gesi ya kutoa machozi ilitumika kutawanya wafuasi wa Bobi Wine na kwa bahati mbaya waandishi wa habari walijeruhiwa,” amesema msemaji wa polisi Fred Enanga.
 
It's far better to be called stupid because I exercise my unparalleled natural intelligence, than to be extolled as a smart hero -- all the while fully brainwashed.
In a way, you're also brainwashed, under the guise of exercising your so called natural intelligence.
 
Askari Police wa Uganda, hawana utofauti na Police Enzi ya Makaburu wa RSA.
 
Kwa viongozi wanaonyanyasa wananchi wake ni Mseveni ,Mungu angemchukua tu kwakweli ili aache kuendelea Kumwaga damu
 
Huu upumbavu wa kushabikia mauaji huwa mnapewa nini?
Sifurahii mauaji na wala pia siungi mkono umamluki wa Bobi Pombe. Huyo jamaa anapaswa awe ndani kitambo tu, anairudisha nyuma Uganda kimaendeleo. Hana vision, ni just a puppet kama mapuppet wengine. Fani ya Bobi Pombe ni rapping, ndiyo kazi inayomfaa. Go M7 Go!!! M7 30 tena!!!
 
Kwa viongozi wanaonyanyasa wananchi wake ni Mseveni ,Mungu angemchukua tu kwakweli ili aache kuendelea Kumwaga damu
Hujaelewa kitu. Bobi Pombe kazi aliyopewa na Bobi A ni kuhakikisha wanafanya machafuko ya kutosha ili ku-undermine credibility na mafanikio ya M7. Sasa wanavuna jeuri yao!!! M7 amewapatia nafasi ya kufanya kampeni, wao wanatumia kuisambaratisha nchi. Haiwezekani! Haiwezekani!! Haiwezekani!!! Huyo rapper akamatwe mara moja apelekwe studio akaimbe muziki hukoo Uingereza.
 
Tatizo hawa mamluki wamekuwa wanaharakati mpaka wamesahau uzalendo wa nchi yao. Bobi Wine is just like a pen in the hands of EU & Washington
Unahabari pia kuwa wakili Wa Bob wine in yule yule aliyekuwa akimtetea mgombea wa chandimu Lissu,sijui anaitwa Robert Amsterdam,? Hawa vijana wetu Wa sasa bure kabisa ,wamekubali kutumika na mabeberu ili kuvuruga amani ya nchi zao,
 
Unahabari pia kuwa wakili Wa Bob wine in yule yule aliyekuwa akimtetea mgombea wa chandimu Lissu,sijui anaitwa Robert Amsterdam,? Hawa vijana wetu Wa sasa bure kabisa ,wamekubali kutumika na mabeberu ili kuvuruga amani ya nchi zao,
Pathetic, intolerable shame to these poor guys!
 
In a way, you're also brainwashed, under the guise of exercising your so called natural intelligence.
You better revisit the definitions before you ever speak anything. I am seriously sorry and sorrowful for you.
 
Nausikitikia uzao wako, hakika watalaani sana wewe kuwa baba yao wakiyasoma haya matapishi unayoyaandika humu
Nashukuru kwamba hawatakuwa puppets kama hawa madalali wanaokubali kugawa na kusalimisha utu wao na nchi yao kwa Wazungu. Hii ni aibu isiyovumilika inayopaswa kuwekwa ukurasa wa mbele wa Guinness World Records
 
anairudisha nyuma Uganda
emoji1254.png
kimaendeleo. Hana vision
Hapa ndipo unapaswa kutoa ufafanuzi ili nielewe
 
Back
Top Bottom