Uganda imepiga marufuku Kuagiza furnitures (samani) Nje ya Nchi, Kenya imezuia Kuagiza vitanda Nje ya Nchi, Tanzania tunasubiria nini?

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Tanzania tunasubiria nini Kuzuia au kuweka Kodi kubwa kwenye bidhaa za Nje ya Nchi Ili kuwasaidia mafundi Wetu hususani kwenye furnitures?

Mbona Nchi zingine zinafanya na zinaweza sie Watunga sera, Wanasiasa na wachumi Wetu Wana shida gani?

=======

Rais wa Kenya, William Ruto amepiga marufuku kuagiza vitanda kutoka china na kuwataka Wakenya kutumia kitanda kilichotengenezwa nchini humo kwani hakihitaji mambo mengi.

“Kwani kutengeneza kitanda hapa si unahitaji mbao, nyundo, randa na msumari, kama hutaki kulala kwa hiyo kitanda lala chichi mpaka ukubali kulala kwa hiyo kitanda.” – Rais William Ruto

EA Radio
 
Importation costs na inflation ndio mama wa kushuka thamani kwa fedha yetu hapa nchini, wachumi sidhani kama wanalielewa hili
 
Tanzania tunasubiria nini Kuzuia au kuweka Kodi kubwa kwenye bidhaa za Nje ya Nchi Ili kuwasaidia mafundi Wetu hususani kwenye furnitures?

Mbona Nchi zingine zinafanya na zinaweza sie Watunga sera, Wanasiasa na wachumi Wetu Wana shida gani?

=======

Rais wa Kenya, William Ruto amepiga marufuku kuagiza vitanda kutoka china na kuwataka Wakenya kutumia kitanda kilichotengenezwa nchini humo kwani hakihitaji mambo mengi.

“Kwani kutengeneza kitanda hapa si unahitaji mbao, nyundo, randa na msumari, kama hutaki kulala kwa hiyo kitanda lala chichi mpaka ukubali kulala kwa hiyo kitanda.” – Rais William Ruto

EA Radio

Furniture ndugu? Vipi maziwa kutoka uarabuni?

IMG_20230822_142121.jpg

Pichani ni kopo la maziwa Pendwa ya unga "Al Mudhish" kutokea Uarabuni kwa wajomba zetu. Kusikokuwa hata na ng'ombe wa maziwa.
 
Quality tunazingatia?

Nimewahi kufanya kazi ofisi moja ya umma kwa wiki 6 kwenye viti vya keko... nilitoka naumwa mgongo vibaya mno... Viti sio ergonomic kabisa, matairi wameweka ya machela! Havishuki wala kupanda, havina tofauti na vimbweta.
 
Back
Top Bottom