Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajilikiwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

For more consultation,you may contact us through +255786989713
 
Kwa wale wafugaji ambao tayari wamekwisha kuanza ufugaji wa kuku,leteni changamoto zenu tutawasadia kusudi msonge mbele.Sisi ni mkusanyiko wa wataalam wa mifugo by professional lkn pia ni wazoefu wa muda mrefu kwenye hii kada.Pia tuna watu waliobobea kwenye maandiko ya uanzishwaji wa mradi(Project write up) na mpango wa biashara yaani Business plan
Kwa wafugaji waliojikusanya pamoja wanaweza kuwasiliana nasi tukawapa mafunzo ya namna ya ufugaji bora,si tu wa kuku ni kwa mifugo yote.Tutawaeleza kwa uwazi na ufasaha mkubwa wa namna ya kutengeza pesa kupitia ufugaji.Watanzania bila umasikini inawezekana.

Sisi tuko Morogoro,chuo kikuu cha kilimo Sua,but tuko movable kulingana na mahitaji ya anayetaka kuanzishiwA MRADI.
Kumbuka kuanzisha mradi bila kuwa na elimu yake ni sawa na kutembea huku ukiwa umefumba macho.
 
kichwa mbovu nipo Arusha na ninampango wa kuanza kufuga kuku ila target yangu ni kuku wa nyama chotara nina target ya kuanza na kuku 350. Nimepitia post zako naona ziko pouwa sana zitanisaidia ila hiyo PDF naomba unitumie kwenye hii mail


edmasongroup@yahoo.co.uk
 
Mkuu mambo vipi? mimi mwenyewe nina mpango wa kuanza hii kazi Mwezi Ujao mungu akipenda, Ila nina maswali machache.

1. Je kati ya Kuku wa Kienyeji pure na Hawa Chotara ni wapi wazuri wakufuga kibiashara?

2. Na kuhusu hawa kuku Parents, Je kuna kuku special kabisa ambao ni Parents? au ni kuku tu hawa wakawaida wa Mayai unaweza kuselect wachache wakawa Parents?

Mkuu naomba msaada kwa hapo make inanitatanisha sana kuku parents ni wapi na wa mayi ni wapi.

3. Mkuu mimi nataka kabisa niwe na totoresha na kuuza vifaranga ila ukiachilia mbali Kuku ni tainclude na Kanga, Bata Mzinga na Ndege wengine, na Mashine ya Kutotoresha nimepata kutoka Nchini Kenya kuna kampuni kule huwa inaagiza kutoka Uturuki na ni ya mayai 1000
 
Mkuu mambo vipi? mimi mwenyewe nina mpango wa kuanza hii kazi Mwezi Ujao mungu akipenda, Ila nina maswali machache.

1. Je kati ya Kuku wa Kienyeji pure na Hawa Chotara ni wapi wazuri wakufuga kibiashara?

2. Na kuhusu hawa kuku Parents, Je kuna kuku special kabisa ambao ni Parents? au ni kuku tu hawa wakawaida wa Mayai unaweza kuselect wachache wakawa Parents?

Mkuu naomba msaada kwa hapo make inanitatanisha sana kuku parents ni wapi na wa mayi ni wapi.

3. Mkuu mimi nataka kabisa niwe na totoresha na kuuza vifaranga ila ukiachilia mbali Kuku ni tainclude na Kanga, Bata Mzinga na Ndege wengine, na Mashine ya Kutotoresha nimepata kutoka Nchini Kenya kuna kampuni kule huwa inaagiza kutoka Uturuki na ni ya mayai 1000

Asante mkuu kwa swali lako,kifupi kuku pure wa kienyeji na chotara wanaolipa zaidi ni chatora. Kuku wa kienyeji pure wanakuwa na slow growth rate na miili yao huwa ni midogo, hivyo huchukua muda mrefu kuvunwa lakini pia wanapovunwa huwa na uzito mdogo ambao hupelekea wauzwe kwa bei ndogo.

Chotara wao huwa na tabia za kuku wa kienyeji na kisasa. Wanachukua tabia ya kuku wa kisasa kwenye uzito na ukuaji.Michotara huwa mikubwa na hata ukuaji wake uko fasta ukkilinganisha na kuku pure wa kienyeji.Pia kuku chotara wanachukua tabia ya kuku wa kienyeji kwenye ustahimilivu wa magonjwa, ladha ya nyama na mayai na uwezo wa kuatamia.Chotara humuhakikishia mfugaji faida kwa haraka.

Kuhusu kuku wazazi, hawa ni kuku maalum, sio hao wa mayai,ila ni wazazi wao,ambao wanaagizwa kutoka nje ya nchi.Wanakuwa mchanganyiko majike na madume kwa ajili ya kurutubisha mayai.Mayai yakishatagwa huokotwa na kutibiwa kuuwa wadudu ambao huyaharibu mayai hivyo kupelekea mayai kushindwa kutotolewa vizuri,na pia kuzuia baadhi ya vimelea visababishavyo magonjwa kutoka kwa kuku wazazi kwenda kwa vifaranga. Hawa kuku ni ghari kidogo hivyo unahitaji mtaji mkubwa ila hii biashara ya utotoreshaji wa vifaranga inalipa sana kuliko ufugaji wa kuku wa mayai au nyama.

Ila kama unataka kutotoresha chotara ni rahisi tu,tafuta kuku wako wa kienyeji majike na uwe na madume ya kisasa aina Rhode Ireland red au aina nyingine yeyote, then uta cross,mayai yake utaingiza kwenye machine. Kuku wa kienyeji ukibahatika kupata kuchi wale wa Singida na Dodoma itakulapa zaidi.Utotorehaji wa aina hii wafugaji wengi hufanya.
 
Asante mkuu kwa swali lako,kifupi kuku pure wa kienyeji na chotara wanaolipa zaidi ni chatora.Kuku wa kienyeji pure wanakuwa na slow growth rate na miili yao huwa ni midogo,hivyo huchukua muda mrefu kuvunwa lakini pia wanapovunwa huwa na uzito mdogo ambao hupelekea wauzwe kwa bei ndogo.

Chotara wao huwa na tabia za kuku wa kienyeji na kisasa.Wanachukua tabia ya kuku wa kisasa kwenye uzito na ukuaji.Michotara huwa mikubwa na hata ukuaji wake uko fasta ukkilinganisha na kuku pure wa kienyeji.Pia kuku chotara wanachukua tabia ya kuku wa kienyeji kwenye ustahimilivu wa magonjwa,ladha ya nyama na mayai na uwezo wa kuatamia.Chotara humuhakikishia mfugaji faida kwa haraka.

Kuhusu kuku wazazi,hawa ni kuku maalum,sio hao wa mayai,ila ni wazazi wao,ambao wanaagizwa kutoka nje ya nchi.Wanakuwa mchanganyiko majike na madume kwa ajili ya kurutubisha mayai.Mayai yakishatagwa huokotwa na kutibiwa kuuwa wadudu ambao huyaharibu mayai hivyo kupelekea mayai kushindwa kutotolewa vizuri,na pia kuzuia baadhi ya vimelea visababishavyo magonjwa kutoka kwa kuku wazazi kwenda kwa vifaranga.Hawa kuku ni ghari kidogo hivyo unahitaji mtaji mkubwa .Ila hii biashara ya utotoreshaji wa vifaranga inalipa sana kuliko ufugaji wa kuku wa mayai au nyama.

Ila kama unataka kutotoresha chotara ni rahisi tu,tafuta kuku wako wa kienyeji majike na uwe na madume ya kisasa aina Rhode Ireland red au aina nyingine yeyote, then uta cross,mayai yake utaingiza kwenye machine.Kuku wa kienyeji ukibahatika kupata kuchi wale wa singida na dodoma itakulapa zaidi.Utotorehaji wa aina hii wafugaji wengi hufanya.

Mkuu asante sana kwa maelezo mazuri mno, nashukuru sana mkuu wangu. Hau Parents wanapatikana vipi? means majogoo na Majike? make niko Arusha na vipi huwa hakuna Vifaranga wake? Hii ishu ni ngumu sana but sitakata tamaa bali nitapambana kikamilifu
 
Mkuu asante sana kwa maelezo mazuri mno, nashukuru sana mkuu wangu. Hau Parents wanapatikana vipi? means majogoo na Majike? make niko Arusha na vipi huwa hakuna Vifaranga wake? Hii ishu ni ngumu sana but sitakata tamaa bali nitapambana kikamilifu

Kama unahitaji parent stock,nipigie nitakupa mwongozo mzuri. Kwa kifupi, kuku wazazi huingizwa nchini toka wakiwa vifaranga, nawe utawakuza mpaka watakapoanza kutaga kisha mayai yataokotwa na kuwekwa tayari kwa kutototoreshwa kwenye machine. Mayai ya parent hayaruhusiwi kuingizwa nchini.
 
Kama unahitaji parent stock,nipigie nitakupa mwongozo mzuri. Kwa kifupi, kuku wazazi huingizwa nchini toka wakiwa vifaranga, nawe utawakuza mpaka watakapoanza kutaga kisha mayai yataokotwa na kuwekwa tayari kwa kutototoreshwa kwenye machine. Mayai ya parent hayaruhusiwi kuingizwa nchini.

Hapa ndo kuna kazi, kwa nini hawaruhusu kuingiza mayai? Na kuna mtu akaniambia hata hao vifaranga ni razima upate kibari kutoka wizara ya migugo ndo uruhusiwe kuingiza hao kuku, na hizo nchi za nje ni zipi? Na kuna jamaa kaniambia kenya wanapatikana hao parents.

Ok mkuu nitakupigia unipe infor zaidi
 
Hapa ndo kuna kazi, kwa nini hawaruhusu kuingiza mayai? na kuna mtu akaniambia hata hao vifaranga ni razima upate kibari kutoka wizara ya migugo ndo uruhusiwe kuingiza hao kuku, na hizo nchi za nje ni zipi? Na kuna jamaa kaniambia kenya wanapatikana hao parents,

Ok mkuu nitakupigia unipe infor zaidi

Ni kweli ili uagize kuku wazazi lazima uwe na kibali kutoka wizara ya mifugo.Nchi ambazo wanapatikana ni Uholanzi, Uingereza, Marekani, Brazil na south Afrika. Kenya wanapatikana kuku wazazi wa nyama. Makampuni mengi hapa nchini yanaagiza kutoka uholanzi kwa layers parent stock hata mwenyewe nimewa kuagiza kutoka huko na kwa broilers parent stock wanaagiza kutoka Kenya. Ni miradi inayolipa sana sema inahitaji mtaji mkubwa kidogo kwani kuna gharama ya kuwanunua kuku wenyewe,chakula na machine za kuangulia vifaranga.
 
Kazi kweli, Hao kuku wana nini special cha kuwafanya wasipatikane Tanzania? Na je, ina maana kuku wa kisasa wa mayai akiwekewa jogoo, hili yai halitatotorewa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom