Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

kwa kweli this thread is the best ever,hapa watu tushindwe tu wenyewe kuchakarika maana wenzetu wametusaidia kuchanganua kila kitu.mbarikiwe sana.
 
Kwa jinsi nnavyo ielewa biashara ya kuku, lazma uwe na uwezo wa kutengeneza chakula, uje vizuri yale madawa ya chanjo, uwe umejipanga kuhusu umeme/mkaa kwa ajili ya joto, aina ya vifaranga wakuanza nao coz kunavifaranga kuanzia 750/= mpaka 1250/= kwa jinsi bei inavyokwenda juu ndo ubora unaongeza!

Fanya utafiti wa soko, bei ya kuuzia against matumizi, kwa kuku 1000 watakuwa wanakula mifuko 2 mpaka mi5 kwa siku, na mfuko mmoja ni 27,000/= nadhani. Kama ni kuku wa nyama, hawa huwa wanakua kwa wiki 4 mpaka 5, ila hapa inategemea na jinsi unavyowapa msosi!

Ukiwanyima msosi wanadumaa, ukiwapa msosi vizuri wananenepa kinoma! Ila mchanganyiko wa kwenye vyakula uwe sahihi(dagaa, damu, chokaa, pumba kavu za mahindi, etc) Usimamizi nao unahitajika sana, coz hawa kuku wa nyama huwa wanakula usiku na mchana! Na kabla ya kuwaweka lazma upige dawa(fumigate) banda lote, na vyombo vyao vya maji unatakiwa kuvifanyia usafi kila siku.

Siku wakifika hao vifaranga unatakiwa uwapige glucose kama watakuwa wamechoka ili wapate nguvu, tofauti na hapo utaanza kuingia hasara ya mapema kabisa. Ila wanalipa sana kama utawafuga inavyotakiwa! Soko la kuku haliishi, kila siku demand inaongezeka!

Mshindwe wenyewe!
 
Kuku wa wapi ni wazuri nazungumzia wa mayai? Interchick, Kibo, Kibaha Education, wa kuagizia Malawi, please naomba ushauri
 
Vifaranga kutoka kampuni karibu zote ni wazuri, ila ukiwa unaenda kununua kwa mara ya kwanza, tafuta mtu ambae ameshafuga aina ya kuku unaotaka kuwafuga, atakushauri vizuri zaidi!
This business is very tricky kwenye kununua vifaranga, ukiwa mgeni utabambikwa mpaka ukome!
 
Dada Pearl ana uzoefu wa Biashara ya kuku wa kienyeji na kwa mujibu wa maelezo yake yeye anafanya mpaka packing; Tunaomba naye mchango wake kwa upana zaidi
 
Kwa wenye uzoefu wakati wa kununua ni vitu gani vya kuangalia?
 
Kuku wa wapi ni wazuri nazungumzia wa mayai? Interchick, Kibo, Kibaha Education, wa kuagizia Malawi, please naomba ushauri
Interchick ni wazuri ila wagumu kupata na expensive
Kibaha / Mkuza nao ni wazuri sana
Pia kuna hawa wanakuja toka Arusha/ Moshi kwa ndege siju ndio Kibo ni wazuri pia, hawa nimeishawafuga wote.
Vifaranga wanaosumbua ni wa Bagamoyo wanawaita "amadori" not sure of spelling.. kwakweli hawa wiki ya saba bado vidoogo pia mara wana minyooo ah hawa kwakweli wanasumbua sana ingawa ni cheap
 
Dada Pearl ana uzoefu wa Biashara ya kuku wa kienyeji na kwa mujibu wa maelezo yake yeye anafanya mpaka packing; Tunaomba naye mchango wake kwa upana zaidi

Ni kweli atupe mchanganuo wao kibiashara, mie sikuweza kuwafuga kwa wingi hawa wa kienyeji
 
Vifaranga kutoka kampuni karibu zote ni wazuri, ila ukiwa unaenda kununua kwa mara ya kwanza, tafuta mtu ambae ameshafuga aina ya kuku unaotaka kuwafuga, atakushauri vizuri zaidi!
This business is very tricky kwenye kununua vifaranga, ukiwa mgeni utabambikwa mpaka ukome!

Kweli kabisa has madalali wa Tazara, ila kwa ma agent kama ubungo tanesco, sinza, interchick sio rahisi kukuuzia fake maana utawarudia na kulalamika. Tazara wanaweza kukuuzia vijogoo wa kulea miezi 6 badala ya broiler wiki 6!
 
Interchick ni wazuri ila wagumu kupata na expensive
Kibaha / Mkuza nao ni wazuri sana
Pia kuna hawa wanakuja toka Arusha/ Moshi kwa ndege siju ndio Kibo ni wazuri pia, hawa nimeishawafuga wote.
Vifaranga wanaosumbua ni wa Bagamoyo wanawaita "amadori" not sure of spelling.. kwakweli hawa wiki ya saba bado vidoogo pia mara wana minyooo ah hawa kwakweli wanasumbua sana ingawa ni cheap

Asante Mama Joe
 
Niliingiza vifaranga 1,000 vya nyama - vikadumaa vyote - nusu vikafa- badala ya kupata hardly 3200*1000= 3.2m. nikajikuta napata laki Sita. kwa hiyo wageni wa ufugaji this business is so risk - usije kopa pesa ukaingia kwenye biashara hii utahama nyumba kukwepa deni la watu.

Anza na mtaji wako mwenyewe ili uwe kwenye safe side.
 
Nilianza biashara hii mwishoni mwa mwaka jana lakini inaelekea I was carried away na hizi statement kuwa soko ni kubwa sana. sasa napata sghida sana kuwauza ingawa nilifanya akikl ya kutoanza na kuku wengi. Nina batch ya kuku 200 ambao next week wanafikisha wiki 6 tayari kwa kuuza, anayejua soko tafadhali anifahamishe
 
ukweli unaweza pata uchizi kwa biashara hii,nilishataka kunywa sumu baada ya kuamka asubuhi na kukuta kuku 322 kati ya 500 wamekufa na takriban 40 wameparalise,na ndiyo kwanza wamefikisha wiki nne na nusu,yaani nilichanganyikiwa nikatamani afadhali hela yangu ningepigia lagha nikaongeza damu na kuweka heshima bar
 
jerome ndio maana tunajifunza kutoka kwenu and how we should be prepared when it comes to the worst
 
Nilianza biashara hii mwishoni mwa mwaka jana lakini inaelekea I was carried away na hizi statement kuwa soko ni kubwa sana. sasa napata sghida sana kuwauza ingawa nilifanya akikl ya kutoanza na kuku wengi. Nina batch ya kuku 200 ambao next week wanafikisha wiki 6 tayari kwa kuuza, anayejua soko tafadhali anifahamishe
Inategemea uko wapi, mie nipo manispaa ya Kinondoni, soko langu kubwa ni wenye baa, hoteli wachoma chips. Lakini soko zuri pia ni watu wenye baiskeli au wanaopeleke sokoni au wauza sokoni wenyewe. Be flexible wakifika wiki ya 3 tu anza kutafuta soko: Urafiki, Kinondoni, Kawe hat soko la Ilala pia. Baa na hotel za jirani au supermarket kama una mtu. Zunguka hukosi soko
 
wadau ,

wale wote mnaotaka kufahamu kuhusu kufanya mradi wa kuku vizuri mtafuteni aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania,bibi Hasna Mwilima.

lakini alikwisha pata wafadhili kwa ajili ya mradi huo mkubwa, kwa ajili ya akina mama,kabla hajapigwa chini.

mwenye simu yake awashirikishe wengine
 
Asante Kapuchi, umoja unasaidia sana, mfano mtaani kwetu tuko kama wanne hivi yaani mie sijawi kumwita Dr wa mifugo wala nini, mmoja akiend akufata chakula mbali kwenye unafuu basi unaweza kumpa na hela ya petrol anakuletea. Nikianza kuuza lazima nijue nani kauza karibuni au anauza wakati huo basi tunapeana namba za simu yaani hata tuwe wote na kuku wakuuzwa hatukosi soko, wateja wanajua wakija hapa leo kesho waende pale inasaidia sana.
Nadhani mwenye namba ya Mama Mwilima atupatie, na hii biashara sio kina mama tu hapa ni kina baba wengine wastaafu yaani inatunza familia zao kabisa na kuweza kujenga au kuwekeza kwingine.
 
Kwa wenye uzoefu wakati wa kununua ni vitu gani vya kuangalia?
Kuna broiler lakini anakuwa na shape ya vijogoo: umbo refu na miguu/ vipaja vyembamba. Broiler kwa kawaida anakuwa na shepu ya tetea au jike.
Sasa vifaranga vya amadori / Bagamoyo vina shape ya vijogoo ingawa navyo vinakua kwa wiki 6 ila unakuta vipaja vidogo, sasa mteja siku zote anaangalia miguu, vipaja vidogo hata awe kilo 1,5 hawataki. Walinisumbua na kunifukuzia wateja wangu kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom