singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,531
KINYUME cha taswira ya miaka mingi kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia viongozi wake wakuu, hasa Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa, ni chama kinachopinga ufisadi, mambo yameripotiwa kugeuka katika baadhi ya ngome za chama hicho nchini.
Kwa muda mrefu sasa, Dk. Slaa amekuwa akijipambanua kuwa kinara wa kupinga ufisadi na akiwa Mbunge wa Karatu hadi kufikia mwaka 2010, amekwishafanya kazi ya kufichua uozo mkubwa uliopata kufanywa na watendaji wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini sasa Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na chama hicho imekubwa na kashfa za ufisadi.
Hali hiyo ilibainishwa bungeni mjini Dodoma jana na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mary Chatanda, ambaye aliweka bayana kwamba si tu Halmashauri ya Karatu ambayo ni ngome ya kisiasa ya Dk. Slaa, imeoza kwa ufisadi bali hali pia hali ni hiyo hiyo kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akisema mbunge huyo ‘ametafuna' kifisadi fedha za maendeleo ya mfuko wa jimbo.
Akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) jana bungeni mjini Dodoma, Chatanda alidai hakuna mbunge fisadi kama Lissu katika kutafuna fedha za mfuko wa jimbo.
"Nawashangaa hawa wapinzani wanapiga kelele hapa kuhusu ufisadi wakati ndio wanaoongoza kwa ufisadi. Hakuna mbunge ambaye anatafuna fedha za mfuko wa jimbo kama Lissu, tunaomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akamfanyie ukaguzi maalumu,"alisema Chatanda
Alisema wapinzani wamekuwa wakipiga kelele kukemea mafisadi na kudai kwamba CCM ndio wanaofanya ufisadi wakati Halmashauri ya Karatu inayoongoza na Chadema ndiyo kinara katika kuendeshwa kwa ufisadi uliopindukia.
"Halmashauri ya Karatu ambayo ni ya Chadema ndiyo fisadi kuliko, kuna mbunge wa upinzani, Cecilia Pareso, nilimuuliza kuhusu yule fisadi ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Karatu, kwamba amechukuliwa hatua gani akanijibu…yule hatagombea tena au hatapita,"
"Kwa hiyo wao wanapiga kelele za nini hapa ndani (bungeni) wakati maeneo machache tu wanayoongoza wananuka ufisadi? Wakipewa nchi itakuwaje?," alihoji Chatanda ambaye amewahi kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha na kwa sasa ni Katibu wa CCM, mkoani Singida.
Akizungumzia kauli iliyotolewa na baadhi ya wabunge wa Chadema kwamba Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama hicho, Rose Kamili, alipigwa na kusababishiwa ulemavu na baadhi ya wanaCCM alisema huo ni uongo uliokithiri, akisistiza kwamba mbunge huyo alipata ajali kabla ya kwenda kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga.
"Wapinzani mkiwa hamna hoja ni vyema mkanyamaza kuliko kuongea uongo, Kamili ni rafiki yangu siku nyingi lile tatizo la mkono alilonalo hakusababishiwa na CCM bali alipata ajali na hata kipindi akiwa anataka kwenda kwenye kampeni nilimuuliza kuhusu mkono wake uliokuwa umepachikwa chuma, akajibu kwamba hawezi kuacha kwenda kwenye kampeni chama chake kitamuelewa vibaya,"
"Yaliyotokea Kalenga kipindi kile siyo yaliyomfanya Kamili kuumia mkono bali alikuwa tayari ana chuma kwenye bega hivyo alitoneshwa kidonda, acheni kuudanganya umma kwamba CCM imeumiza mtu. Hakuna kitu kama hicho," alisema Chatanda.
Hata hivyo kauli hiyo ilimfanya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, kuomba kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mussa Azzan Zungu, ambapo alisema wakati tukio hilo likitokea katika uchaguzi huo mdogo wa Kalenga alikuwapo na alishuhudia mbunge huyo akipigwa na kuumizwa na CCM.
Chanzo: Raia Tanzania