Ufisadi Tanzania: Tatizo ni Serikali au wananchi?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
1. Ukifanya kazi kwenye baadhi ya taasisi nyeti za umma kama TRA, Bandari, Polisi hasa TRAFFIC, n.k., usipoonekana unapata mafanikio ya harakaharaka, utaitwa mjinga usiyejua "kuchukua " hela zilizo nje nje

2. Kwa sasa ukienda kwenye baadhi ya maduka yanayotoa risiti ya EFD, ukitaka risiti, watakuambia watakuandikia lakini hawataandiki bei halisi uliyolipa. Kama ulilipa shilingi milioni mbili, wanaweza wakakunadikia laki mbili. Na badhi ya hayo maduka ni ya "viongozi"

3. Miaka ya nyuma , nilimsikia jirani yangu mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa ana roho mbaya!

Kisa? Alidai kuwa ndiye aliyemchongea mpaka akaachishwa kazi. Ni pale kulipotokea uwizi kwenye hiyo kampuni ambapo wafanyakazi wote waliokuwa wakihusika na hicho kitengo walihojiwa. Japo hakumsikia huyo jirani yake akimtaja, aliamini kuwa alimtaja kwa sababu ndiye mtu pekee aliyekuwa akiyajua mambo yake.

Je! Kusema ukweli ni kuwa na roho mbaya?

4. Kuna biashara nyingi ambazo zinaaminika si za wamiliki walioandikishwa bali za "wakubwa" fulani waliopo Serikalini. Wao ni vivuli tu.

Kama huo si unafiki ni nini?

Kama hizo ndizo "tabia" au mitazamo ya Watanzania wengi, kuna uhalali wa kuilaumu Serikali kwa ufisadi?

Nitakosea nikisema tabia za kifisadi Tanzania zimeanzia "majumbani" kwenye familia za Watanzania?
 
Back
Top Bottom