Ufisadi huduma ya chanjo ya 'yellow fever' hapa nchini

Yes na mi najua ni elf 5!
Japo sikuchoma


Amini usiamini Mnazi mmoja na JNIA, wanatoza 20'000 na kuendelea, nimekwenda na ndugu zangu 3 times wanatoza hivyo, japo hivi karibuni Mnazi mmoja walikuwa wamesitisha huduma tangu 6.12.2016
 
Ni chanjo ya ghali sana hebu fikiria watumishi tu wa Idara za afya nchini kuipata imekuwa shida KUTOKANA na serikali kutokuwa na uwezo au uzembe wake omba mungu kuwa unauwezo na pesa hiyo
 
Nahitaji kadi ya hii chanjo ila sitaki kuchomwa sindano(sipendi sindano). Nahitaji ndani ya hii wiki na ile inayokuja.

sio tupigane 55000 lkn kama mkuu hapo juu.
 
Shikamoni wandugu.

Kumekuwa na figisufigisu nyingi sana katika huduma ya chanjo ya homa ya manjano /chanzo ya kimataifa (Yellow Fever Vaccination),hasa gharama ya huduma hii.

Gharama hiyo hapa nchini hutofautiana sehemu na sehemu, kituo na kituo wakati ni huduma hiyohiyo inayoratibiwa na Wizara ya Afya Jinsia na Watoto hapa nchini Tanzania.

Mathalani, ukienda:-

1. Hospital ya Mnazi mmoja ya jijini Dsm, wanatoa hiyo huduma kwa TZS 55,000 (Elfu Hamsini na tano);

2. Holili Mkoani Kilimanjaro TZS 20,000 (Elfu Ishirini);

3. Azam Marines pale Posta - Dsm wanatoza TZS 20,000

4. JN & K International Airports wanatoza 40 USD


Sasa basi, gharama ya huduma hii kwann inadiffer wakati huduma zote zinaratibiwa na Wizara (moja) hiyohiyo?

Ni mradi wa mtu binafsi au nn hapo?

Kama jipu lipo, lipasuliwe.
Mm nimechanja kwa elf20 pale mnazi mmoja
 
Huu ni udhaifu wa wizara husika. Kwa nini wasiweke bei elekezi kwenye mtandao wao au kubandika gharama halisi kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma nchi nzima kuzuia ulanguzi huu wa mali za serikali? Mwambieni Kigwangalla haya ndiyo muhimu kuliko kuhangaika na mashoga.
 
View attachment 475472Nimekuwekea na picha mkulu ujionee hiz vitu ni bora ziwekewe utaratibu wa kuambiwa bei kabisa kua hapa ni kiasi flani ndio upate chanjo kuna watu wanapigwa mpaka laki ,je vipi kuhusu yale maswali ambayo yapo kwenye ile fomu ya kujaza kabala hawajaku vaccinate
Mkuu wanauliza na maswali gani mkuu?
Kwa mwanza ni sehemu gani wanatoa mkuu?
Niaandae kiasi gani mkuu ndo nitapata?
 
Malipo halali ni Tsh. 20,000 kwa waTanzania, wasio waTanzania ni dola 50. Huyo anayesema alipata huduma kwa 10,000 alikumbana na vishoka akapewa kitabu feki. Ndiyo maana serikali kupitia Wizara ya Afya iliamua kubadili vitabu na mihuri. Kwa ufafanuzi zaidi anaweza kuwasiliana nami au aingie www.moh.go.tz.
 
Kitabu hiki ni cha zamani, nenda kwenye kituo kinachotoa huduma hiyo ukabadilishe. Kuna form utajaza, kama ulipata cha kuuziwa itabidi uchome sindano kwa gharama halali ya Tsh. 20,000
Mkuu kwani hiyo vaccina si valid for ten years ?Kamani ndio kuna umuhimu upi wa kubadili ilhali sikununua kitabu nilipatiwa chanjo kabisa ndipo nikapatiwa hicho na mara ya mwisho nimetoka nacho 2015 .Naomba mwongozo plz
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Back
Top Bottom