Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,338
- 9,766
Ndugu zangu Watanzania,
Uongo ukizungumzwa sana bila kujibiwa au kukanushwa kwa hoja unaweza kuonekana kama ukweli hasa kwa watu wanaopata Taarifa kwa kusimuliwa tu na watu wengine. Mh Rais alizungumza na kuliambia Taifa kuwa changamoto za umeme zinakwenda kumalizika na kuisha ndani ya miezi sita Tuu. Lakini hakumaanisha kuwa ndani ya miezi sita kutakuwa na kiama au janga la umeme Nchini.
Mh Rais alimaanisha kuwa ndani ya miezi hiyo sita serikali yake inakwenda kumaliza ukarabati na matengenezo ya mitambo yote ambayo ilikuwa haijafanyiwa marekebisho na matengenezo kwa muda mrefu,lakini pia ndani ya muda huo serikali yake inakwenda kuongeza megawati za umeme kwa kutumia vyanzo vingine vya umeme kama vile umeme wa gas na jua, ndani ya muda huo serikali ya Rais samia inakwenda kukamilisha mradi mkubwa wa bwawa la mwalimu Nyerere litakalotupatia zaidi ya megawati 2115 zaidi au nyingi zaidi tunazozalisha kwa sasa mega watti 1900 kwa kutumia vyanzo vyote vya umeme.
Mh Rais alimaanisha kuwa kwa sasa Kama Taifa hatupaswi kutegemea chanzo kimoja pekee cha umeme kwa kuwa inakuwa changamoto hasa ikitokea ukame. Lakini pia shughuli zinazotegemea umeme zinaongezeka kila siku kutokana na kasi ya ukuaji wetu wa uchumi, unaotokana na kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara,hivyo kuhitaji kuwa na umeme wa kutosha kutoka vyanzo mchanganyiko.
Nimeona niliweke wazi hili maana wengine kupitia mitandao ya kijamii wanapotosha na kusema uchumi wetu unakwenda kufa na kusinyaa kutokana na kupungua kwa uzalishaji viwandani unaotokana na kutokuwepo kwa umeme kwa miezi sita. Niseme tu kuwa huo ni uongo na upotoshaji ambao wananchi tunapaswa kuupuuza ,kwa kuwa kwa sasa serikali inaendelea kupambana na kuongeza megawati 100 kila mwezi ili kuelekea katika kilele cha kumaliza changamoto hii ambapo kwa sasa tunakabiliwa na upungufu wa megawati 400.
Lakini pia bwawa la Nyerere limefikia 92% ya ukamilikaji wake na hivyo mapema mwakani linakwenda kuanza kazi kwa kishindo ,kasi na haraka sana na hivyo kumaliza kabisa tatizo hili ,ambapo tutaweza kuuza umeme mwingine nje ya nchi kutokana na kuwa na ziada ya kutosha.
Wengine wanauliza mbona Tatizo hili halikuwepo miaka michache iliyopita? Jibu ni kuwa Hali hii inatokea kwa sasa kwa kuwa kasi ya uchumi wetu kukua ni kubwa sana ambayo imepelekea shughuli nyingi zinazotegemea umeme kuongezeka kwa kasi nchini,uwekezaji mkubwa unaofanywa nchini kutokana na sera nzuri za serikali yetu kumepelekea mahitaji ya umeme kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana na hivyo vyanzo tulivyokuwa navyo kuzidiwa katika kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji yetu kwa sasa.
Lakini pia kwa sasa mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri sana uzalishaji wa umeme hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba tulikuwa tunategemea umeme wa maji ,hivyo ukame umekuwa ukiathiri kwa kuwa kina cha maji katika mabwawa yetu kimekuwa kikipugua wakati wa kiangazi kutokana na ukame mkubwa. Hii ndio sababu serikali yetu kuamua sasa kuanza kutumia vyanzo mchanganyiko ambavyo ndani ya miezi sita kazi itakuwa imekamilika. Na siyo kweli kwamba kuna mtu au watu au kikundi cha watu wanafanya hujuma katika mabwawa yetu kwa kufungulia maji.kwakuwa kila mtu anajionea hali ya ukame iliyopo maeneo mbalimbali.
Kwa hiyo Tuendelee kuwa watulivu na wavumilivu wakati serikali yetu ikiendelea kufanya kazi usiku na mchana katika kumaliza changamoto hii ambayo itabaki katika historia vitabuni. Serikali yetu kwa sasa inachukua hatua au suluhisho la muda mrefu na siyo kufanya zima moto halafu tukawa watu wakulia lia mgao wa umeme kila mwaka inapofika kiangazi. Mwisho natoa Rai kwetu watanzania tuendelee kutunza vyanzo vyetu vya maji,misitu yetu tusiikate Kate hovyo kwa kuwa ndio vyanzo vya mvua, hivyo tutunze mazingira yetu ili yatutunze na pia tupande miti yakutosha katika maeneo yetu kwa wenye nafasi ya kutosha.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.