Uelewa wa maswala ya kisheria ni mdogo sana Tanzania

Jukwaa lirudishwe upya

  • Ndio

    Votes: 2 100.0%
  • Hapana

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    2
  • Poll closed .
Jan 28, 2024
47
48
Binafsi nadhani kuna haja ya jambo kufanyika ili kuongeza uelewa wa maswala ya kisheria baina ya watanzania. Najua sheria ni noble professional lakini hii aimaanishi ni wale waliosoma sheria tu ndo wanapaswa kuijua sheria, NO kila raia anatakiwa awe japo na uelewa wa kawaida kuhusu sheria (legal besic understanding).

Tukizingatia sheria ipo katika maisha yetu ya kila siku, Mfano; Makazini (kunasheria za kazi), Mwaswala ya ndoa (kuna sheria za ndoa), migogoro mbalimbali kama vile ya aridhi (kuna sheria za aridhi), mirathi (kuna sheria za mirathi) na maswala ya mikataba (kuna sheria za mikataba) n.k, hivi vyote ni maisha yetu ya kila siku kwaio ni muhimu japo kuelewa sheria ya maswala muhimu katika maisha yetu.

Kuongeza uelewa wa sheria kutasaidia watanzania kujua wajibu na haki zao, lakini pia itasaidia kuwafanya watanzania kuelewa pale haki zao zitakapovunjwa na nini wafanye na wapi waende na ndani ya muda gani ili kuweza kupata haki zao.

Ni aibu kuona watanzania wanashindwa japo kujua mpangilio wa mahakma (court hierarchy system) za Tanzania kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufaa, wanashindwa hata kujua mamlaka tofautitofauti (Jurisdictions) za mahakama izo, isitoshe wengi hudhani Kisutu ndio mahaka kuu ya Tanzania (what a shame). Pia asilimia kubwa ya watanzania hudhani kuwa sheria ni katiba, watu hudhani katiba ndiyo iliyosema kuua ni kosa, hudhani katiba ndiyo iliyosema wizi ni kosa n.k. Na, wengine hushindwa hata kutofautisha kati ya kesi za madai na jinai (unakuta mtu anadai ila anapeleka kesi polisi badala ya mahakamani) ,pia hushindwa kutofautisha kati ya mwanasheria na wakili ama jaji na hakimu na haya yote yanaashiria jamii yenye uelewa mdogo wa maswala ya sheria.

Nadhani kuna haja kubwa ya hili jukwaa kurudi upya na kutoa wigo wa watu kudiscuss juu ya maswala mbalimbali ya kisheria kwani dunia ya sasa imehamia kwenye technology so sidhani kama kuna haja yakufanya mikutano ya kisheria ili kutoa elimu ya kisheria, nadhani majukwaa kama haya ndio yanatakiwa kutumika zaidi ili kufikisha meseji kwa watu wengi zaidi na kwa haraka.

Ni wazo tu lakini wadau​
 
Hili ni wazo zuri sana tena sana,ila ninachoweza kusema ni kwamba si kwamba watu hawana au hawakuwa na uelewa wa sheria hapana ila wengi tumegundua,hapa nchini ukitaka kupata stress tafuta kuwa na uelewa wa sheria.
au haki zako za msingi kikatiba na kisheria.

Nikupe mfano wangu binafsi.ninayo mingi,ila naweka mmoja tu
Nilikamatwa na polisi wa barabarani kwa kunibambikia kosa,
nikalikataa,akasema kama hukubali nikupeleke mahakamani
ili sheria ichukue mkondo wake nikakubali,akapanda kwenye gari yangu
tukaendesha kutoka shauri moyo Ilala DSM hadi kituo cha polisi msimbazi.

Akanipeleka kwa boss wake,nadhani alishaongea naye,yule boss nakumbuka
alikuwa na nyota tatu,ile kuniona tuu akaniambia nyie ndo wale wabishi
hata hajanisikiliza,akaniambia tunakuweka ndani wakati kesi yako inaandaliwa
ili kesho upelekwe mahakamani,akaniambia mdhamana upo wazi ita ndugu zako
waje wamekamilika kivitambulisho ili wakudhamini. Nikaangalia muda wote niliokwishatumia
niingize na ndugu zangu kisa buku 30,ikabidi nilipe niondoke.

Kama pia uliwahi kwenda mahakamani kwa kesi yoyote au kwenda kusikiliza
tu,utagundua ukitaka kupata stress jihusishe na sheria inayokutetea,badala yake
unaamua kuwa raia mwema na kumwomba Mungu akuepushe na majaribu
na ikitokea ukaenda mahakamani basi Mungu akutetee.
 
Pia kuna ndugu yangu mkulima aliibiwa nyanya zake shambani,
akafanikiwa kumkamata mwizi wake akampeleka polisi.
Yule mwizi akakubali wayamalize baada ya polisi kujiridhisha kwamba kweli
zile nyanya ni yule mkulima. Yule mtuhumiwa akakubali kuzilipa zile nyanya
kwamba pale hana pesa ila kwa kuandikishana kule atalipa baada ya muda fulani
Baada ya ule muda kupita yule ndugu hakulipa.akasema nipelekeni mahakamani.

Kwenda mahakamani,hakimu akasema lete uthibitisho wa ule wizi
wakati huo nyanya zimeishaoza(ah,ah,ah,ah)
Ndugu yangu akawaambia polisi walikiona hicho kithibitisho waitwe,
hakimu akamwambia polisi ni mashahidi wa jamuhuri siyo wa kwako.
ndugu yangu akawa hana la kuongeza hapo hiyo kesi inasikilizwa imepita miezi sita.
Ndugu yangu akapoteza nyanya,muda na pesa za nauli.

ukitaka kupata stress hapa nchini, ijue sheria bila cheo serikalini.utaona rangi zote.
 
Hili ni wazo zuri sana tena sana,ila ninachoweza kusema ni kwamba si kwamba watu hawana au hawakuwa na uelewa wa sheria hapana ila wengi tumegundua,hapa nchini ukitaka kupata stress tafuta kuwa na uelewa wa sheria.
au haki zako za msingi kikatiba na kisheria.

Nikupe mfano wangu binafsi.ninayo mingi,ila naweka mmoja tu
Nilikamatwa na polisi wa barabarani kwa kunibambikia kosa,
nikalikataa,akasema kama hukubali nikupeleke mahakamani
ili sheria ichukue mkondo wake nikakubali,akapanda kwenye gari yangu
tukaendesha kutoka shauri moyo Ilala DSM hadi kituo cha polisi msimbazi.

Akanipeleka kwa boss wake,nadhani alishaongea naye,yule boss nakumbuka
alikuwa na nyota tatu,ile kuniona tuu akaniambia nyie ndo wale wabishi
hata hajanisikiliza,akaniambia tunakuweka ndani wakati kesi yako inaandaliwa
ili kesho upelekwe mahakamani,akaniambia mdhamana upo wazi ita ndugu zako
waje wamekamilika kivitambulisho ili wakudhamini. Nikaangalia muda wote niliokwishatumia
niingize na ndugu zangu kisa buku 30,ikabidi nilipe niondoke.

Kama pia uliwahi kwenda mahakamani kwa kesi yoyote au kwenda kusikiliza
tu,utagundua ukitaka kupata stress jihusishe na sheria inayokutetea,badala yake
unaamua kuwa raia mwema na kumwomba Mungu akuepushe na majaribu
na ikitokea ukaenda mahakamani basi Mungu akutetee.
Pole sana kwa changamoto hiyo ndugu yangu, nikiri wazi tu kwamba hayo mambo yapo hususani katika vyombo vya usalama (especially polisi) na ndomaana kila kukicha wannchi huwa wanalalamikia swala la polisi kuvunja haki zao (wanannchi) na nadhani ni RUSHWA ndiyo inayowasumbua. Lakini swali lakujiuliza ni dogo tu. Je, kujua sheria kunakusaidia chochote? Kama ni ndio, basi nadhani ni muhimu kizijua sheria.

Kuhusu hiyo kesi ya mkulima wa nyanya, nadhani ata apo juu kwenye uzi nimelizungumzia, swala la watu kushindwa kutofautisha kati ya jinai na madai. Ni wazi kua wizi ni jinai lakini na hauwezi kidai ulipwe katika jinai. Na uzuri walipokua polisi walishakubaliana kulipana na hivyo ndugu yako (mkulima) alitakiwa kwenda kushitaki juu ya madai yake tu si kurudisha kesi ya wizi tena.

Tukumbuke jinai unatakiwa kuthibitisha pasi na kuacha shaka (prove beyond reasonable doubts) ambayo ni ngumu kidogo kuliko madai ambayo yenyewe inategemea uwezekano (balance of probability). Kwaio nadhani ili kulipwa malalamiko (madai) yake, ndugu yako alitakiwa kufungua kesi ya madai angeachana na hilo la wizi na angetumia yale maelezo yaliopo polisi (kua mdai wake alikubali kulipa) kama ushaidi.

Kwaio binafsi naona bado ipo haja ya elimu ya sheria kutolewa kwa wingi na uwazi (kwa kila mmoja)​
 
Ni
Kwaio binafsi naona bado ipo haja ya elimu ya sheria kutolewa kwa wingi na uwazi (kwa kila mmoja)
Nani mtoaji wa elimu ya sheria? labda tuanzie hapo.
Kwa maoni yangu,ni kwamba watoaji wa elimu ya sheria
hawawezi kuitoa kwa sababu wananufaika na watu kutojua sheria,
Na kwa bahati mbaya wanaoijua hata kwa kusikia au kusoma makala
kidogo,wakijaribu kuitumia wanaambulia matatatizo
kuliko wangejifanya wajinga wa sheria.

Nitoe kisa kingine,cha kukamatwa na polisi wa barabarani,na hapa kimsingi alikuwa
sahahihi katika kunikamata kwake, Nilipita barabara ya "one way" kutokea upande usioruhusiwa
kwa sababu lile bango la kuzuia lilikuwa halionekani. Yule ndugu hakuwa kwenye uniform ya police
alivaa nguo za kawaida ila alikuwa na redio mkononi.

Nikamtaka anipe uthibitisho kwamba ni police,hilo tu lilimfanya ahamaki
Nakumbuka mke wangu akasema atakuwa police si unaona radio call
Nikamwambia,mimi kazini natumia radio call na siyo police.
Akanionyesha kitabulisho.

Basi bwana yule na mwenzake wakaniambia nigeuze gari twende kituoni
nikatii nikageuza gari twende,kama ninavyosema Mungu mara nyingi huwa ananinusuru.
Kuna jambo lilitokea wenyewe wakaniachia,lakini walishakasirika kana kwamba nimefanya
kosa kubwa kuomba uthibitisho.
 
Naunga mkono kwamba kuijua sheria ni vizuri ili kuepuka kuivunja,
Ila kuitumia kwenye maisha ya kila siku gharama yake ni kubwa kuliko kujifanya huijui.
Ningeshauri watendaji wote wa vyombo vya umma,wakipewa hiyo elimu
na wakaitumia kuhudumia umma kwa mujibu wa sheria,sisi raia wa kawaida tutaijua tuu,
Maana tutajikuta kila kitu kipo kwenye mpangilio unaotakiwa.

Kuna haja gani ya police mwenye kamera ya kudhibiti mwendo wa magari
kujificha porini? sheria inamtaka ajifiche porini? ok,umemaliza kujificha porini ili uwabambe
wanaoenda mwendokasi,mara mtu anapata ajari mbele yako na kufariki kabla hujamtoza faini
inakuwa imesaidia nini?
 
watoaji wa elimu ya sheria hawawezi kuitoa kwa sababu wananufaika na watu kutojua sheria
Upo sahihi, lakini hii kwangu naitafsiri kama ubinafsi (gatekeepers) hata jana ili swala lilijitokeza humuhumu JF 👉ushaidi. Na sioni faidi yeyote ya ubinafsi huu. Kwangu mimi Kuelimisha wananchi kuhusu haki zao za kisheria naona hakuondoi fursa kwa wanasheria, bali kunaweza kuongeza mahitaji ya huduma zao. Wananchi walio na uelewa wa sheria wanaweza kutambua haki zao na kujua wakati gani wanahitaji msaada wa kitaalamu kutoka kwa wanasheria.

Kwa mfano, mtu anayejua haki yake ya kusikilizwa lanaweza kutambua kwamba anahitaji mwanasheria ili kumwakilisha vyema. Hii inaweza kupelekea ongezeko la wateja kwa wanasheria kwa sababu wananchi watakuwa na uwezo wa kutambua na kuchukua hatua pale wanapoona haki zao zinakiukwa.​

Kwa hivyo, elimu ya sheria si tu inaimarisha jamii kwa kuwapa wananchi uwezo wa kujitetea, bali pia inaweza kuwa chanzo cha fursa mpya kwa wanasheria. Inaleta mazingira ambayo wananchi na wanasheria wanaweza kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya pande zote mbili na kwa ajili ya haki na usawa katika jamii.
Na kwa bahati mbaya wanaoijua hata kwa kusikia au kusoma makala
kidogo,wakijaribu kuitumia wanaambulia matatatizo
kuliko wangejifanya wajinga wa sheria.
Huu mimi nautafsiri kama uonevu wa mamlaka na sizani kama uonevu unanafasi katika Tanzania ya sasa(lakini bado upo), lakini naamini kutojua sheria kunafanya uonevu huu kuwa mkubwa Zaidi ukilinganisha na jamii inayofahamu sheria.

Kutojua sheria kunaweza kuchangia katika kuongezeka kwa uonevu kwa sababu watu wanaweza kutotambua wakati haki zao zinakiukwa au hawajui jinsi ya kuchukua hatua za kisheria kujilinda.

Elimu ya sheria ni muhimu sana katika kupambana na uonevu kwa kuwapa wananchi uwezo wa kujitetea na kudai haki zao. Jamii iliyoelimika kuhusu sheria inaweza kusimama imara dhidi ya uonevu na kuhakikisha kwamba kila mtu anatendewa kwa haki na usawa mbele ya sheria.

Kwa kuongeza uelewa wa sheria, tunaweza kujenga Tanzania ambayo wananchi wake wanaweza kushiriki kikamilifu katika masuala ya kisheria na kisiasa, na hivyo kuchangia katika ujenzi wa demokrasia thabiti na utawala bora. Hii itasaidia kupunguza uonevu na kujenga jamii yenye haki na usawa kwa wote.​
Nikamtaka anipe uthibitisho kwamba ni police,hilo tu lilimfanya ahamaki
Nakumbuka mke wangu akasema atakuwa police si unaona radio call
Nikamwambia,mimi kazini natumia radio call na siyo police.
Akanionyesha kitabulisho.
Nadhani kuhamaki kwake tu kunatupa jibu tosha kuwa kunafaida ya kujua sheria ndio maana hata alihamaki, kwangu mimi nadhani usingeonyesha kuwa unauelewa wa maswala ya sheria mambo yangekua hovyo zaidi. Hivyo binafsi bado naona nafasi na nguvu ya sheria katika jamii yeyote ile duniani especially kwa nnchi iliyo chini ya utawala wa sheria kama hii yetu.​
Nakumbuka mke wangu akasema atakuwa police si unaona radio call
Nadhani hii inaonyesha wazi kua kama mkeo angekua na ujuzi juu ya haki yake ya kudai kitambulisho kwa polisi hata asingesema hivi. Na inaweza kuwa ushaidi kuwa bado jamii inahitaji kuelimishwa zaidi kuhusu maswala ya sheria.​
 
Naunga mkono kwamba kuijua sheria ni vizuri ili kuepuka kuivunja,
Ila kuitumia kwenye maisha ya kila siku gharama yake ni kubwa kuliko kujifanya huijui.
kubaliana na wewe kwamba kujua sheria ni muhimu ili kuepuka kuvunja sheria. Hata hivyo, ninatambua wasiwasi wako kuhusu gharama za kuitumia sheria katika maisha ya kila siku. Ni kweli kwamba wakati mwingine, kujihusisha na masuala ya kisheria kunaweza kuwa na gharama kubwa, iwe ni kwa muda, fedha, au hata kwa hisia.

Lakini, kujifanya hujui sheria si suluhisho la kudumu. Kutojua sheria kunaweza kusababisha madhara makubwa zaidi, kama vile kupoteza haki zako au kushindwa kujitetea unapodhulumiwa. Kujua sheria kunakupa nguvu ya kuchukua hatua stahiki na kujilinda wewe na wengine dhidi ya ukiukwaji wa haki.

Ni muhimu kutafuta usawa kati ya gharama za kujihusisha na sheria na faida za kujua haki zako. Jamii inapaswa kujitahidi kufanya elimu ya sheria kuwa nafuu na inayopatikana kwa urahisi ili kila mtu aweze kuitumia bila mzigo mkubwa.​
Ningeshauri watendaji wote wa vyombo vya umma,wakipewa hiyo elimu
na wakaitumia kuhudumia umma kwa mujibu wa sheria,sisi raia wa kawaida tutaijua tuu,
Maana tutajikuta kila kitu kipo kwenye mpangilio unaotakiwa
Wazo lina afya sana hili, naunga mkono 🤝.
Kuna haja gani ya police mwenye kamera ya kudhibiti mwendo wa magari
kujificha porini? sheria inamtaka ajifiche porini? ok,umemaliza kujificha porini ili uwabambe
Hii inakera sanaa na mimi ni moja ya wahanga wa hili swala tena kwa kuonewa. Polisi alijificha kabisa kichakani ili kuvizia Abv 50, na alinipiga picha kabla hata sijafika katika kibao cha 50 lakini nikaambiwa nime over speed.​
 
Back
Top Bottom