UDOM: Utumiaji wa Smartphone kwenye mitihani unaharibu elimu

UDOM SR

Member
Jan 25, 2014
47
26
Ufanyaji wa mitihani kwa kutumia smartphone sasa ndio imekuwa fasheni ambapo hata wale wanafunzi wachache ambao walikuwa hawaamini katika cheating za mitihani sasa wamekata tamaa katika kutumia akili zao. Maana wenzao wanaotumia smartphone wanapata course work kubwa na GPA kubwa hivyo inawakatisha tamaa.

Tatizo la smartphone hapa UDOM ni kubwa kiasi kwamba limekuwa likisumbua hata utawala wa chuo na walimu hasa wakati wa kutoa matokeo. Imefikia mahali matokea ya UE hapa Udom hayawezi kutoka mpaka yafanyiwe Standardization. Sababu kubwa ni mbili. Ama wanafunzi wamefaulu kupita kiasi yaani wote wamepata A au wamefeli kupita kiasi.
Kufaulu kupita kiasi.

Kunatokea pale ambapo mwalimu anayefundisha somo hasimamii vizuri wakati wa test hivyo kuwafanya wanafunzi wote kufaulu kupita kiasi na kuwa na course work kubwa.

Hii ikienda hadi kwenye mitihani ya mwisho UE usimamiaji ukawa mbovu basi tegemea mwisho wa siku matokea yawe standardized kwa vigezo wanavyo tumia wao, either watakata marks kadhaa kwa kila mwanafunzi au worse ni mwalimu mwenyewe wa somo kupeleka marks za UE alizostandardize kwa kutumia vigezo vyake ambavyo mara nyingi vinaleta manung'uniko kwa wanafunzi ambao havijawa-favor.

Kufeli kupita kiasi.

Kunatokea pale ambapo kwenye mitihani ya UE, kunakuwa na usimamizi mkali kiasi kwamba hata mwanafunzi akiomba kwenda chooni anasindikizwa. Hili likitokea tegemea wanafunzi kufeli sana hata kama walikuwa na course work kubwa.

Scientific Proof: Njoo UDOM si ajabu, ni kawaida sana kumkuta mwanafunzi aliepata Course work ya kati ya 30 hadi 35 ya 40, akirudi September kufanya supplementary ya somo.

Haiingii akilini katika rational thinking ya kawaida kwamba mwanafunzi kafanya test 2 na assignment 2 kwa uwezo wake kafikisha marks 35, halafu eti aje kufanya UE ambayo most of the time ni dublicate ya maswali yaleyale ya test, ashindwe kupata marks hata 10 kati ya 100. Hii inaonyesha kuwa kuna uwezekano wakati wa UE mwalimu aliesimamia alibana sana ikashindikana kutumia smartphone.

Kinachonishangaza zaidi ni kuwa huko kwenye cabinet ya kupitisha matokea ambako uongozi wa chuo uliojaa ma-proffesor, hakuna anayeona hili ‘GAP'. Ndio maana nasema matatizo ya Elimu UDOM ni makubwa zaidi ya yanavyoonekana.

Ukweli ni kwamba matatizo mengi ya kielimu yanayoonekana kwa wanafunzi UDOM yana-reflect nature na aina ya walimu wengi tulionao ingawa sio wote(ila ni wengi).

System ya kuajili walimu UDOM ina tuhuma nyingi sana, kuna tuhuma kuwa ili uajiriwe UDOM lazima kuwepo na memo unless iwe ni field ambayo haijawa ‘saturated'. Yaani screening ya waombaji wa nafasi za ualimu UDOM imebase kwenye nepotism sana badala ya professionalism, sana sana kwenye baadhi ya college. Hili linasemwa sana.

Evaluation system za walimu hazifanyiwi kazi. Matatizo mengi ya walimu tumeyaandika kwenye zile fomu za evaluation ambazo zinajazwa kila mwaka lakini hakuna hata anaye-bother kuangalia nini wanafunzi wameandika na kufanyia hata uchunguzi wa ukweli wa kile kinachoandikwa. Kuna walimu wako extremely incompetent kwenye baadhi ya masomo kiasi kwamba kila anachoulizwa na wanafunzi darasani anatengeneza defence kwa kuwaambia kuwa " hilo swali nawaachia kama assignment, mtakuja ku-present wiki ijayo".

Haiwezekani kila swali wanafunzi wanalokuuliza useme ni assignment. On top of that kuna topiki kibao kawaachia mjisomee wenyewe kwa kichaka cha "SELF STUDY". Yaani akiingia kwenye kipindi mpaka anatoka assignment ziko si chini ya 4. Halafu huyo mwalimu anatoa maswali hay ohayo kwenye test, assignment, tutorial hadi UE unalikuta. Sasa hapo mwanafunzi unam-examine nini? Uelewa? Uwezo wa kumeza?au!!!! Pathetic!

Ni hatari sana kwa maendeleo ya elimu kusipokuwa na effective mechanism in place ya kucheki nini kinaendelea huko madarasani. Kuna walimu ili ufeli mwanafunzi inabidi uondoke chuo usifanye mitihani, kwa kuwa kwenye test anaruhusu smartphone wanafunzi wanatumia mbele yake anawaona. Nafikiri hawa ni wale walimu waliofika hapo walipo kwa staili hiyohiyo.

Kama Uongozi wa chuo ungekuwa serious kufuatilia issue wanafunzi wanazo-raise kwenye zile fomu za evaluation, ungeweza kupata sehemu ya kuanzia kwa baadhi ya issue. Kuna wanafunzi wanarisk kupata favor za kielimu kutoka kwa walimu kwa kuamua kuwa honest na kuandika matatizo ya walimu wao, pamoja na kuwepo kwa risk ya kuweza kuwa disclosed kwa sababu wanaokusanya hizo fomu ni walimu haohao.

Hii tabia ya walimu kufundisha with 100% impunity lazima ifike mwisho ili walimu wanao-underperform na ku-misbehave wawe accountable.
 
Achambwembwe.
We unataka lecturer akupe nini ndo ulizike?
Eti mnafeli sana kwa standardization ya marks.!!!!!!!.
Maraa Ooooh atufundishwi, assignment zimekuwa nyingi.!!!!!!!
Je mwanafunzi wa Open aseme nini?!!!!!!
Familia inamsubiri.
Kazini kila siku.
Saa kumi jioni lecture room.
Akirudi nyumbani hoi.
 
Duuuh. ...nipo department of PSPA unayoyasema na niki refer na department yangu wewe ni muongo mtupi
 
Kuna ukweli flani uliyoandika mleta mada nimewahi kusikia kwa waliotoka pale. Hayo mapungufu wayafanyie kazi hasa favouratism pale ndo sehemu yake na udini.
 
Watunge mtihani maswali MCQ tu. Then limit time, mfano kila swali dakika mbili. Hata huo mda wa kufungua smartphone ataupatawapi. Tatizo lecturer anatunga maswali matano ya Maelezo ambayo nikigoogle neno moja napata content nzima ya swali.
Hapo nadhani tatizo ni walimu, wanapaswa kutambua huu ni wakati wa technologies/ digitali,. Bado wanatunga mitihani kama ya miaka ya 1980. Teachers must change n cope with the changing technology
 
Achambwembwe.
We unataka lecturer akupe nini ndo ulizike?
Eti mnafeli sana kwa standardization ya marks.!!!!!!!.
Maraa Ooooh atufundishwi, assignment zimekuwa nyingi.!!!!!!!
Je mwanafunzi wa Open aseme nini?!!!!!!
Familia inamsubiri.
Kazini kila siku.
Saa kumi jioni lecture room.
Akirudi nyumbani hoi.

Lol...wee ni mdau wa udom nini?
 
Sidhani Kama ni udomu tuu..Hata vyuo vingine vina ishu km hizo...Fanya research utagundua
 
Alafu mi nashaangaa kuhusu zile form za evaluation unakuta lecturer anakuja darasani kulalamika mmemjazia ovyo,kwanini wanawaonesha.Pia umesahau swala la walimu wengi kuuza vitabu usiponunua wanakutisha,pia wengine watunga open book test ili ununue vitabu vyao.Kuna most of lectures wa Udom wanapenda hela hawajui wanafunzi wengi hawana mikopo na ni watoto wa wakulima..dah hii mada imenigusa sana sijui niwaanike hadharani walimu wababaishaji? Ila sio solution ngoja nipite wakuu.
 
Mambo hizo si kwa UDOM tu, vyuo vingi sana vina challenges hizo hasa hiyo ya smartphones
 
Watunge mtihani maswali MCQ tu. Then limit time, mfano kila swali dakika mbili. Hata huo mda wa kufungua smartphone ataupatawapi. Tatizo lecturer anatunga maswali matano ya Maelezo ambayo nikigoogle neno moja napata content nzima ya swali.
Hapo nadhani tatizo ni walimu, wanapaswa kutambua huu ni wakati wa technologies/ digitali,. Bado wanatunga mitihani kama ya miaka ya 1980. Teachers must change n cope with the changing technology

hyo kwel.. MCQ ndo mambo yote... kama hujui hujui kwel.. hamna mambo ya kujaza porojo page mbili
 
Kuna mengi hutokea hadi mtu anafaulu. Wengine husoma, wengine husomewa, wengine ndio waibiaji kabisa.
 
Back
Top Bottom