UDINI: Uchafu Chini ya Kapeti tunajidanganya wasafi - Zitto

Status
Not open for further replies.
ZITTO mnafiki. Analeta hizi habari sasa hivi.
Angekuwa na nia dhati angeleta hizi taarifa zamani.

Vilevile anasahau ya kuwa zile meseji zilizotumwa Tanzania nzima za kusema WAISLAMU MSIMCHAGUE PADRI SLAA SABABU ANATUMIKIA KANISA NA ATAWANYIMA HAKI WAISLAMU KAMA ATACHAGULIWA

Meseji hizo zilitumwa kwa wapiga kura hadi vijijini.
Hizi meseji ziliwapa hofu wananchi na kuchochea kampeni za misisikitini na makanisani.

Hakuna mtu aliyekemea hizi meseji hadi leo hii!
 
tunahitaji watu kama kina zitto wanoweza kuweka wazi mambo badala ya kuficha. lawama zote ziwaendee sisiemi kwa kupabdikiza chuki kwamba cuf ni chama cha kidini 2000 na 2005 na chedema 2010 ili iweze kuwatawala baada ya kuwagawa. na bado shonza na mwampamba anaendelea kuzunguka na nape kupandikiza udini. hatutaki udini hapa kwani madhara yake hakuna wa kuzuia. mbona huku uraiani tunashirikiana waislamu na wakristo kwa kila jambo? kikwete chukua hatu za haraka kuitisha mjadala wa kitaifa.kama shida ni mahakama ya kadhi wapewe wanaoitaka nchi ibaki na amani
 
Ni kweli, mkuu nadhani serikali inajukumu kubwa la kukabiliana na chokochoko zote za kidini nakuchukua hatua kali na haraka kwa wahalifu wote wanaotenda uhalifu unaovuta hisia za kidini. Wachochezi wote pamoja na rekodi zao ktk cd,dvd nk.

Pia viongozi wetu waache kulalamika waanze kutende,lakini zaidi nikuwa mabadiliko yawe ktk mtazamo na matendo nasio kukemea udini ktk maneno,lakini upande wa pili wanakaa na viongozi wa dini zao na kupanga mikakati michafu. Wakumbuke mwisho wa uovu ni aibu kwao kwani ukweli utafahamika. Mungu ibariki Tanzania.
 
"Sisi Freemasons; mnatukashifu sana, Mnatukebehi sana, Mnatutukana sana...Lakini muda wote tumekuwa tukionyesha upendo kwa Wakristo na Waislam bila ya ubaguzi! Igeni uvumilivu wetu kwa mustakbali wa nchi yetu" by B.W.M
 
Imani yangu kwa Zitto ni kidogo sana lkn kwa hili aliloongea ameonuesha ana uelewa wa hali ya juu ila uwa anaamua kufanya makusudi.Swala la imani huungozwa kiimani akili huwa hamna na kila mmoja yupo sahihi kwa imani yake.Kama upande mmoja utakosa imani na serikali na kuona inaonewa Mh Zitto tutegemee mchafuko.Kama makanisa yanachomwa moto na hakuna kinachoendelea unafikiri patakuwa salama?Hoja yako mh inafaa iwafikie rais na watendaji wake ni suluhiyo tosha
 
Mh. Zitto ninakupongeza kwa kuthubutu kuandika hili. Hakika upo sawa kuleta mjadala huu. Ninachojua mimi vita hii si kama tunavyoiona ni kubwa mno na wanaojua kuwa kuna Mungu wanapaswa kuingia magotini kumwuliza Mungu. Tutapigana kweli na kuumizana wakati kiukweli vita hii ni ya rohoni. Tukumbuke siku zote maneno yanaumba. Wakati wa kutaka kuingia Ikulu suala la udini lilisemwa sana kama njia ya kutumia watu wasio na uwezo mkubwa wa kufikiri kutoa kura zao. Hata kama wakati ule ilikuwa ni njia ya kupata kura leo yanatimia na imekuwa ni chanzo cha yote haya.

Watanzania tunahitaji toba kwa Mungu atusamehe kwanza kwa uumbaji wa hoja hizi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi. Ni ukweli usiopingika kuwa chama kilichoko madarakani ndiyo mwanzilishi wa yote haya. Mahubiri yasiyokuwa na msingi ya udini ndiyo yamezaa haya. Naomba nieleweke kuwa madhehebu ya kidini nayo yalihusika katika hili isipokuwa kwa Kiongozi mkuu kutaja udini hadharani kwa ajili ya kujipatia kura ni mlango wa kumfungulia adui kwa watu wengi kwa maana ya nafasi yake na imani waliyonayo wananchi wengi kwake. Ikumbukwe pia kwamba watanzania wengi hawana uwezo mkubwa wa kufikiri na kama Mh. Zitto alivyosema AKILI ZINAWEKWA PEMBENI NA IMANI INAONGOZA ni wazi kwamba mtu kama Rais anapoliongelea jambo fulani impact yake ni kubwa sana katika jamii. Kwanza hatutegemei atasema kitu ambacho hakipo na bila kupima tunajikuta tunapigana.

Niseme tu kwamba tunamhitaji Mungu atusaidie katika hili ili amani yetu iendelee kuwepo. Nchi yetu kwa sasa si nzuri sana kama tunavyofikiri. Hongera Zitto but put more effort kuhakikisha muafaka unafikiwa. Tumia nafasi yako uliyonayo hata kama wanasema huna moral authority but kutambua tu jambo hili na kuliweka kwenye mjadala ni hatua kubwa. Kila mtu anakosea lakini ni heri anayefanya kitu kuokoa mazingira. BIG UP
 
Mimi ni mmoja kati ya watu ambao wanamtilia mashaka sana ZITO!... Ndani ya chama chake yeye ndiye kiongozi wa makundi hatarishi. Yanayohubiri ukanda, ukabila na udini!... Na wafuasi wake hata baada ya kuhamia CCM wanahubiri UDINI, UKABILA NA UKANDA. ...Shonza na Mtela wamefanya kazi hii kwa muda mrefu na mwanasiasa huru - Habib Mchange kueneza sumu hii!.

Swali langu kwa Zito amesaidiaje kumnyamazisha ustaadhi - Hassan ambaye alitoa CD agosti mwaka jana kuagiza wakristo wauawe!.. Au atasema hajaziona?!.. CD hizi zimepelekea wapadri wawili Zanzibar wapigwe risasi!...

IGP huyu na serikali hii haitaaminiwa na wakristo waliowengi kama USTAADHI ILUNGA hatafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
30214

Amakweli ukiwa na chuki huchagui silaha ya kutumia. Ilunga amezungumza February, 2012. Zitto si Polisi wala Mahakama..ulitaka afanye nini kumyamazisha. Ampige risasi kama inavyofanyika kule Kenya? Al muhimmu..Nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya Sheria, ikiwa Mtikila aliyesema kama Kikwete..tena wakati huo akiwa bado ni Raisi kuwa ni Gaidi na ana ajenda ya kuusambaratisha Ukristo hivyo wakristo wasimchague..hakuonekana na hatia na mpaka sasa anadunda mtaani.

Ila Ponda aliye na kesi ya Uvamizi wa Kiwanja tuhuma sawa na Mchungaji Mwingira wa Efatha yeye anaozea Mahabusu na Mchungaji anapeta tu!

Kikwebo
 
30214

Amakweli ukiwa na chuki huchagui silaha ya kutumia. Ilunga amezungumza February, 2012. Zitto si Polisi wala Mahakama..ulitaka afanye nini kumyamazisha. Ampige risasi kama inavyofanyika kule Kenya? Al muhimmu..Nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya Sheria, ikiwa Mtikila aliyesema kama Kikwete..tena wakati huo akiwa bado ni Raisi kuwa ni Gaidi na ana ajenda ya kuusambaratisha Ukristo hivyo wakristo wasimchague..hakuonekana na hatia na mpaka sasa anadunda mtaani.

Ila Ponda aliye na kesi ya Uvamizi wa Kiwanja tuhuma sawa na Mchungaji Mwingira wa Efatha yeye anaozea Mahabusu na Mchungaji anapeta tu!

Kikwebo

Usidanganye Ustaadhi ILUNGA amerekodi mikanda ya kuagiza waislamu waue wakristo muda mfupi baada ya sensa. Mikanda hii imeanza kuzagaa mtaani septemba mwaka jana. Imeanza kuuzwa kama njugu oktoba hadi leo. Kama kweli Zitto kabwe ni Mwislamu mwenye mapenzi mema na watu wa imani zote anayetegemea kuwa rais - amefanya jitihada gani kuwashauri watu hao?!
 
Tukio la mauaji ya Padre limetokea juzi tu, na hakujakaliwa kikao chochote cha Bunge tangu mauaji, sasa hiyo 'Mheshimiwa Spika' ni ya lini?

Ukisoma vizuri utagundua kwamba hiyo ni makala ya Zitto Kabwe kwenye gazeti la Raia Mwema na amenukuu hotuba yake aliyoitoa bungeni mwaka 2008.
 
Kwa kuijenga Amani ya Nchi yangu niipendayo Tanzania na kuhuisha uhusiano na kuaminiana Kati yetu Watanzania , Mheshimiwa Zitto nitahubiri maandiko yako na kuyasambaza popote nitakapojaaliwa. Mungu ibariki Amani ya Tanzania. Tunakuhimidi na Kukutukuza ewe Mola wa mitume yote iliyopita, Mola wa Ibrahim, Ismael, Isaac, Jacob, Nouh, Jesus na Muhammad na Mola wa Watanzania wote.

Peace
 
ZITTO mnafiki. Analeta hizi habari sasa hivi.
Angekuwa na nia dhati angeleta hizi taarifa zamani.

Vilevile anasahau ya kuwa zile meseji zilizotumwa Tanzania nzima za kusema WAISLAMU MSIMCHAGUE PADRI SLAA SABABU ANATUMIKIA KANISA NA ATAWANYIMA HAKI WAISLAMU KAMA ATACHAGULIWA

Meseji hizo zilitumwa kwa wapiga kura hadi vijijini.
Hizi meseji ziliwapa hofu wananchi na kuchochea kampeni za misisikitini na makanisani.

Hakuna mtu aliyekemea hizi meseji hadi leo hii!

Watu wengine bwana, hamuwezi hata kuficha upumbavu wenu? sasa hapa ni kwamba hujasoma au hujaelewa??? maana habari inaanza kwa kunukuhu aliyoyasema bungeni mwaka 2008, anaenda mbele na kueleza aliyoyatenda kwa vitendo kukemea udini jimboni mwake mwaka 2010 wakati wa campaign.
Mwenzetu umefanya lipi?
 
waasisi wa udini ni wakristo rais mkristo ni bora rais muisilam hafai ujinga hu umepitwa na wakat waisilam hutuburuzwi tena mkapa aliua waisilam pengo almpongeza leo analeta unafiki amani haipatikani kwa unafiki wamaasik ofu
 
"Ngome yangu ya kampeni ilikuwa Kagunga. Ndipo nilipoweka nguvu zangu maana ninapendwa na nilifanya mambo makubwa. Siku chache kabla ya kampeni, ilikuwa siku ya jumanne nikaitwa kwenda Kagunga kwamba mambo yameharibika sana. Nikataharuki na kupanda boti la kukodi na kwenda Kagunga nikafika saa nne usiku. Wenyeji wangu wakaniambia kuwa wametangaziwa kanisani kwamba Zitto asipewe kura kwa sababu akienda Bungeni ataleta mahakama ya kadhi. Nikaomba kuongea na viongozi wa dini kesho yake asubuhi, wakaja wachungaji 11 (Kagunga kuna makanisa mengi sana). Nikawauliza ni kweli kwamba mimi nisipewe kura kwa sababu ya uislamu wangu? Wakasema hayo ndio maagizo na wameshawaambia waumini."

hayo maneno ni mazito na kwa kweli yanauma na kuumiza......

1. wachungaji wanakiri kupokea maagizo na maelekezo toka juu, hiyo juu maana yake ni makao makuu ya kanisa.

2. wachungaji wanakiri kutekeleza maagizo kwa kutoa maelekezo kwa waumini wao kuwa wasimpe kura zitto

3. matokeo ya uchaguzi ni kwamba zitto alipata kura chache sana katika eneo hilo tofauti na mwanzo.....tunajifunza nini kutokana na mistari hii mitatu hapo juu>?????????????????????

1. maagizo kama hayo alitolewa sehemu mabalimbali hapa nchini, kwa zitto likiwemo
2. maagizo hayo yalitekelezwa kwa asilimia mia moja na athari yake ni kwamba watu walipiga kura kwa mazingatio ya udini
3. taifa limegawanyika na wanaoligawa ni viongozi wa dini.

4. viongozi wa dini wameacha kuhubiri dini sasa wanahubiri siasa,

maoni.

1.viongozi wa dini wanaopenda siasa waondoke kwenye nyumba za ibada ambapo wanawapotosha waumini wao, waingie kwenye siasa rasmi na wagombee uongozi wa kisiasa.
2.watanzania tuwaogope viongozi wa dini wanaohubiri siasa na ubaguzi badala ya kuhubiri umoja upendo na amani. tena tuwaogope kama ukoma.
 
Usidanganye Ustaadhi ILUNGA amerekodi mikanda ya kuagiza waislamu waue wakristo muda mfupi baada ya sensa. Mikanda hii imeanza kuzagaa mtaani septemba mwaka jana. Imeanza kuuzwa kama njugu oktoba hadi leo. Kama kweli Zitto kabwe ni Mwislamu mwenye mapenzi mema na watu wa imani zote anayetegemea kuwa rais - amefanya jitihada gani kuwashauri watu hao?!

Mkuu hebu tuliza hasira na chuki binafsi dhidi ya mtu na badala yake kaa utafakari anachosema,hata kama una hangover. Zitto alithubutu ku-address mambo haya ya udini tangu mwaka 2008,wewe bado umeng'ang'ana amefanya nini. By the way,Zitto sio polisi,sio mahakama na wala sie anayeongoza dola. Na tena sio msemaji wa waTanzania wote,kila mtu ana haki ya kutoa maoni kama wewe ulivyoandika hapa. Kama huna hoja nyamaza uelimike.
 
Mh. Zitto kaanika maneno yenye "busara" kuhusu suala hili lakini nachelea kusema hayatuelekezi kwenye kiini cha kuibuka kwa kasi kwa tatizo la udini katika awamu hii ya serikali. Hoja aliyoitoa ni rahisi kwa mtu yeyote mwenye upeo mzuri kuielewa lakini ni ya kawaida na ya ujumla sana. Tishio la udini liko kila mahali duniani. Hata wakati wa Nyerere lilikuwepo na alilizungumzia mara kwa mara. Lakini aliweka mikakati ya muda mfupi na mrefu kulidhibiti "lisivuke mstari". Serikali zote makini duniani zinafanya hivyo. Huwezi tu kuwatafadhalisha wananchi wajichunguze na kuondoa tatizo. Blanket resolutions do not help. The average man is self-centered and irrational when it comes to personal interests. Ndio maana kuna sheria, taratibu na vyombo vya udhibiti.

Raisi na serikali yake wawe wakweli kuhusu tatizo hili kufikia hatua hii ya militancy. Kwa mfano, ni nani aliyeanzisha na kueneza hoja ya nchi kuendeshwa na "mfumo kristo"? Kwamba hata wakijaa waislamu kwenye uongozi wa juu bado hawana uwezo wa kuudhibiti mfumo huo unaowadhulumu waislamu haki zao; kwamba Kardinali Pengo akiongea serikali nzima inagwaya na kubadili msimamo wake! Kama serikali haihusiki na sumu hiyo, basi ijitokeze wazi na kukanusha kwamba kuna mfumo huo wa kidini uliopora madaraka yake ndio maana inashindwa kusimamia "haki za waislamu" hata kukubali Zanzibar iwe "huru"!

Akina Zitto wataongea "maneno mazuri" lakini bila kuwatwisha wajibu wanaohusika wachukue hatua kwa mujibu wa madaraka tuliyowapa na kutarajia sie wananchi "tujirekebishe", basi tukae kusubiri miujiza. Watu waanzishe na kupalilia janga halafu yakiharibika tunaanza kuleta hadithi za Oprah: eti tujichunguze na kujirekebisha! Mwambie mwizi atumie busara (awe muungwana) asiibe - eti sio kitu kizuri! Ibelieve they love that kind of naïvette.The real world doesn't work that way! We just need able leadership in this case.

Well said! Hakika tukiendelea kutowakemea na kutowathibiti kwa nguvu zote wanaoendekeza na kuupalilia udini kwa maslahi na sababu zao; taifa letu litasambaratika na kuwasababisha maafa makubwa kwa kila mmmoja wetu. Wenye dhamana na mamlaka ya kuhakikisha nchi yetu inajengeka kama mahali bora pa kuishi bila kujali dini, kabila, jinsia au rangi, wanatakiwa wasimame kwe nafasi zao na wasimamie vyema na kiadilifu majukumu yao. kw hapa tulipofika, sharti waweke wazi mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu ya kupambana na tunavyofanya sasa,
 
Mauaji na vurugu za kidini zinazotokea sasa hivi ni matokeo ya mfumo mbovu na kandamizi ulioasisiwa na Rais wa kwanza wa nchi hii. Watu wameendelea kukumbatia mfumo huu,na hata pale jamii ya watu waliokandamizwa walipopaza sauti walinyamazishwa na hata kuuliwa.Walioko upande ambao uko favoured na system hawako tayari ku-admitt tatizo hili. Watu wenye nia njema waliothubutu kusema nchi hii ina udini waliitwa majina mabaya,wadini,magaidi,msimamo mkali,wahuni..watu walikuwa wanakamatwa na kupigwa na hata kupoteza maisha.

Ni ujuha wa hali ya juu kusema udini nchi hii umeanza mwaka huu au mwaka jana,..kumekuwa na udini tangu Rais wa kwanza anashika madaraka. Leo tunalaani mauaji ya Padri mmoja Zanzibar, na watu wasiojulikana,na kusema serikali ni dhaifu kwa sababu padri mmoja ameuwawa,kwa maana nyingine Pengo ameihusisha serikali na mauaji. Vipeperushi alivyogawa Pengo kama evidence kuwa ya kuwahusisha moja kwa moja Waislam ni ishara kuwa vita ya udini kati ya Waislam na Wakristo imeshika kasi. Sioni tatizo kwa Muislam kuchoma msikiti au kumuua Sheik kisha akaandika ''sisi wakristo tutaendelea kuchoma misikiti na kuua Masheikh'',ni mfano tu.Lakini mwaka 1997/98 Masheikh na waumini wa Kiislam waliuwawa wakiwa kwenye ibada na watu wanaojulikana,polisi. Waislam wakalalamika lakini hakuna tume iliyoundwa wala timu ya wataalam kutoka nje na ndani ya nchi kuja kuchunguza. Hii ina maana kuwa Christians are better tha Muslims.!

Media iko biased,watu au vikundi vya watu wachache wamefanya lobbying ya hali ya juu kwenye tasnia ya habari. 98% ya vyombo vya habari vinamilikiwa na Wakristo au taasisi za kikristo. Na hata habari wanazoandika ni zile zenye mvuto kwenye jamii ya wakristo. Mwaka jana Waislam walifanya kongamano kubwa pale ukumbi wa Diamond Jubilee,kuhusu tafsiri ya mfumo kristo. Vyombo vya habari pamoja na kualikwa hawakwenda kuripoti kuhusu mjadala ule. Badala yake waliandika wanayojisikia kuandika. Mabandiko lukuki yaliletwa hapa kuwakashifu Masheikh. Leo tunacharuka kwa mauaji ya Padri mmoja!

Bila watanzania kuwa na dhamira ya dhati kukomesha kansa hii ya udini,hakuna njia ya kuepuka vita ya kidini nchi hii. Tanzania hakutatokea vita ya kikabila,ila ya kidini,kwa mwenendo huu,na mfumo huu,na media hizi,vita yaja. Mwenyezimungu atunusuru.
 
Ni kweli, mkuu nadhani serikali inajukumu kubwa la kukabiliana na chokochoko zote za kidini nakuchukua hatua kali na haraka kwa wahalifu wote wanaotenda uhalifu unaovuta hisia za kidini. Wachochezi wote pamoja na rekodi zao ktk cd,dvd nk.

Pia viongozi wetu waache kulalamika waanze kutende,lakini zaidi nikuwa mabadiliko yawe ktk mtazamo na matendo nasio kukemea udini ktk maneno,lakini upande wa pili wanakaa na viongozi wa dini zao na kupanga mikakati michafu. Wakumbuke mwisho wa uovu ni aibu kwao kwani ukweli utafahamika. Mungu ibariki Tanzania.

Hebu kama watanzania tuelewe maana halisi ya UDINI; tafsiri yangu ni kuwa; ni ubaguzi na utayari kwa kutenda lisilo jema kwa binadamu mwenzako kwa sababu tu si wa imani yako. Tujiulize, je hivi ndivyo imani zetu zinataka? Na kama sivyo hatuoni kuwa tunapotoka kwa kuwasilikiza na kukubali kuaminishwa kuwa mtanzania au binadamu mwenzako ni adui kwa sababu tu ni imani tofauti nawe. Tuzinduke tuwakemee na kuwaumbua wale wote wanaoendekeza na kupalilia udini awe ni mwanasiasa, kiongozi wa dini au mwananchi wa kawaida. Pia tuwe macho sana na wageni na taasisi za kigeni zinazojifanya kuhubiri dini au kutoa ufadhili wakati malengo yao ni kuchochea chuki na chokochoko za kidini. Serikali inatakiwa kwa kutumia vyombo vyake kubaini na kuchukua hatua kali kwa wote wanaohusika. Tukumbuke, Tanzania ni nyumba yetu sote tuliyopewa na Muumba tusiendelee kuichafua!!! Imani ni suala binafsi la mtu na Mungu wake.
 
Nadhani hotuba ni ya 2008, sasa anzia Uchaguzi wa 2005, maana huko nakumbuka tulikuwa na chaguo la Mungu na la Shetani, unakumbuka?

OK, basi mi nitakurudisha 1995, ambapo Mkapa alichaguliwa, kipindi hicho bado nilikuwa mdogo ila nilishiriki katika kampeni zote zilizofanyika wakati ule, nilkuwa moshi. Alikuja mkapa uwanja wa mashujaa, na baadaye akaja lipumba na Nyerere, kwa wale waliokuwepo pale watakubaliana na mimi kuwa Nyerere alizomewa na waliokuwa wafuasi wa NCCR-Mageuzi huku wakionyesha alama ya vidole viwili, kama inayotumiwa na CHADEMA leo. Wagombea wa Moshi walikuwa Ndesamburo (CHADEMA), MTUI (NCCR) ABUU (CCM) na wengine namkumbuka mchekeshaji mmoja wa UPDP. Alishinda mgombea wa NCCR. wakati ule kilichokuwa kinahubiriwa zaidi ni UKABILA ( maana mrema ni Mchaga na watu wengi waliokuwa wanamuunga mkono walitokea kanda ya kaskazini) Udini haukuwa na Faida yoyote maana mpinzani mkuu wa CCM mrema alikuwa mkristo kama alivyokuwa mgombea wa CCM.

Mwaka 2000, mgombea wa upinzani aliyekuwa na nguvu ni Prof Lipumba CUF, sasa hapo ndo matatizo yalipoanzia, CUF kikawa chama cha kidini (waislam) CCM cha watanzania, kama kawaida waungaji wa Utaifa tuliendelea kuwa wanaCCM, na kuendelea na kampeni. Maaskofu nao walikuwa upande wa watanzania pia viongozi wa bakwata, na kina sheikh mtopea n.k. Wote hawa walikemea udini wa CUF, nakumbuka Sh. Yahya wakati huo akiwa msemaji mkuu wa BAKWATA alisema waziwazi kuwa hatuendi kumchagua Imam bali ni RAis wa Nchi. Hatimaye CCM walishinda, ila yaliyofuatia hapo, ilikuwa ni maandamano na fujo za hapa na pale za wote CUF na Waislamu, wakidai haki zao.


Mwaka 2005, ni ukweli usiopingika kuwa Kikwete alikuwa ni mwenye mvuto sana ndani na nje ya Chama chake, mpinzani mkuu wa kikwete alikuwa CUF, hivyo kupelekea kuwa Issue ya Udini isiwe na Mashiko, hivyo mambo yalibalance, kwa wakati wengi waliunga mkono CCM. Kama ilivyo ada viongozi wa Dini nao waliendelea kuhubiri amani na Upendo huku wakitoa kila aina ya sifa kwa mgombea huyu wa CCM. Katika ilani ya CCM 2005 mahakama ya kadhi ilikuwepo, very unfortunately hakuna hata kiongozi mmoja iwe wa kidini au wa kisiasa aliyelisemea hili, hivyo ilitakiwa wakati sasa wa utekelezaji ulipofika lianze kujadiliwa vizuri na kwa mapana yake. Very unfortunately hapa kukaanza migawanyiko ya wazi ya kidini, wakristo wanapinga waislamu wanaunga, matokeo yake serikali ikakaa upande wa wanaopinga, (Tayari dhana ya mfumo KRISTO ikaingia) wakati hayo yanaendelea, kukaanza tena malumbano kati ya serikali na madhehebu ya dini especially ya kikristu, suala la Tax exemption, nalo likatikisa. Hivyo hadi kufikia 2010, serikali na madhehebu ya kidini walikuwa wakipigana vijembe kianina.


Mwaka 2010: Kanisa katoliki wakatoa Ilani (Manifesto) na Waraka wa kichungaji, bahati mbaya leo siko na copy zake ningewawekea, ila natumai, wengi wetu walizisoma. Ilani ilikuwa nzuri tu. matatizo yaliyokuwepo ni kuwa kusingekuwepo na uwezekano wowote wa waislamu kuikubali hiyo kwasababu ilielezea wazi kabisa kuwa inapinga mahakama ya kadhi, wakati ambapo waislamu wengi walitaka mahakama ya kadhi iwepo. jambo jingine ni waraka ambao ulikuwa ukiwaelekeza viongozi mbalimbali juu ya kuwafundisha waamini wao juu ya Elimu ya uraia pamoja na ilani hiyo, tena ratiba ilionyesha kuwa ufundishaji huo utakwenda hadi chini kabisa kwa level ya jumuiya ndogondogo za kanisa hilo. hivyo kwa tafsiri ya haraka haraka ni kuwa ilani hiyo haikuandaliwa kwa ajili ya watz wote. jambo lingine nani atakeyeitekeleza ilani hiyo kwasababu tunavyoelewa ni kuwa kwa utaratibu wa nchi yetu ni vyama vya siasa tena vinavyoshiriki uchaguzi mkuu ndivyo vinaandaa ILANI ya UCHAGUZI (Dhana nyingine hiyo ikaingia). Suala hili lilipofika bungeni, wabunge waislamu walipinga uwepo wa Ilani hii, huku wabunge wakristo isipokuwa mzee Kingunge waliunga mkono, kwa bahati mbaya sana na mgombea wa CDM Dr. Wilbrod Slaa ni mmoja wa watu waliounga mkono ILANI hiyo, huku akisema wabunge wa CCM including mzee Kingunge walikuwa ni mafisadi ndo maana hawaitaki ILANI hiyo. Swali likabaki nani atakayeitekeleza ILANI hiyo. Kwa bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wa kiislamu nao ama kwa kutojua athari au la wakaamua nao kutunga na kuweka ILANI yao, ambayo kimsingi ilikuwa ni ya kujibu mapigo. Hapa kwa wenzetu wa kule kusini wanasema Ngoma Inogile.

Wakati wa uchaguzi tuliona Sarakasi nyingi sana za hawa viongozi wa kidini, wakitoa matamko kila kukicha ambayo mwisho wa siku yameendelea kuleta shida na yataendelea kuleta shida iwapo hatutaangalia tulipojikwaa ni wapi, maana kwasasa bado tunaangalia tulipoangukia.

Nawasilisha. i stand to be correccted
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom