Udikteta wa Mbowe: Msuguano Slaa na Mbowe waitikisa CHADEMA, Mafisadi wamteka Mbowe

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
LOWASA-2.jpg

Viongozi wakuu wa Chadema hawapo ila Mbowe peke anaonekana kubanana na Lowasa

Wimbi la kuanzishwa chama cha ACT kulikuwa na mengi yaliuyoongelewa kuhusu udikteta ndani ya Chadema unaofanywa na Mbowe, pia kwamba kuna msuguano kati ya Mbowe na Slaa, ingawa ilikanushwa lakini ufa huo unaonekana kujitokeza sasa.

images

Kilichoendelea ni CHADEMA kuonekana kumwandaa Slaa kuwa mgombea wa Urais. Pia Slaa kuonekana kukubalika kimataifa hata kualikwa na mataifa makubwa au jumuia za kimataifa duniani kama Marekani, Ujerumani na Umoja wa nchi za Ulaya.

images

UKAWA ilionekana NCCR wako radhi Dr Slaa awe mgombea, ila upade wa CUF Lipumba hakuridhika na alitaka yeye agombee. Mbowe alipoonekana kumilikiwa na kisha kummiliki Lowassa kuwa mgombea, Lipumba akapoa kwa vile wote yeye na Slaa wamekosa, huko alikokuwa mafichoni akajifichua na kuanza kuonekana katika vikao vya UKAWA.

images
images

Mgawanyiko Kamati Kuu CHADEMA kutokana na Lowassa
Katibu Mkuu Slaa, makamu wake bara John Mnyika na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu hawakushiriki mapokezi ya Lowassa wakati walionekana wako na moyo kwa mapokezi ya Lembeli na wengineo. Dalili kwamba Lowassa ni chaguo la Mbowe na kushinikiza kamati kuu waridhie matakwa yake.

images

Mbowe amkumbatia Lowasa anayewawakilisha Rostam na Chenge
CHADEMA ilijipambanua na kueleweka kwa umma kwamba wako kinyume kabisa na ufisadi na katu hawatakaa sahani moja na mafisadi, lakini leo Freeman Mbowe anakula sahani moja na fisadi Lowasa anayewakilisha mafisadi wenzake akina Rostam Aziz na Chenge.

mapacha-watatu-560x248.jpg

LOWASA AKWEPA MASWALI YA WAANDISHI KUHUSU KUWAKUMBATIA MAFISADI WENZAKE
Katika tukio la kukabidhiwa kadi za Chadema, Lowasa alipoulizwa na waandishi kuhusu yasemwayo na watu kwamba akiwa Rais atawakaribisha mafisadi wenzake Chenge na Rostam, hakujibu akakwepa na kusema tu anachukia ufukara na anataka watanzania wengi wawe matajiri. Hapo kuna jambo ambalo dhahiri analikwepa kuliweka wazi kuhusu uhusika wake kugombea urais nyuma yake wakiwamo mafisadi Chenge na Rostam. Akishakalia kiti cha magogoni ni mfalme nani wa kumnyoshea kidole?

images
images

Lowasa kukaribishwa CHADEMA na UKAWA badala ya uongozi CHADEMA
Lowasa akaribishwa na kukabidhiwa kadi ya Chadema na UKAWA badala ya safu ya uongozi wa Chadema. Jambo la kufikirisha na kuonyesha dhahiri kuna msuguano fulani na kwa vyo vyote jibu litapasuka maana uvundo huu hauwezi kuendelea muda mrefu.

Zengwe la kuteua mgombea urais CHADMA
Imedhihirika Mbowe ana kauli ya mwisho nani achukue fomu ya kugombea urais na bila yeye kuidhinisha haitafanyika na ndivyo ilivyotokea, wakati huo huo yeye Mbowe alishakuwa na mgombea wake fisadi Lowasa.

Wakati watanzania wakiwa na kiu ya kutangaziwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema mazingira tatanishi yameendelea kwa kuchelewesha kwa makusudi hadi Lowasa alipokatwa CCM Mbowe akamkumbatia.

CHADEMA IMEPASUA UFA MKUBWA MUHIMU KUZIBA HARAKA
Siyo siri na wengi wamebaki kunyamaza kuangalia movie inayoendelea huku Mbowe akijipongeza kumpata fisadi Lowasa huku wengi wa wanakamati kuonekana kutomwunga mkono na mgomo baridi ni pale waliposusia tukio la kumsafisha Lowasa Buguruni ofisi za CUF kisha kufuatiwa na tukio la Lowasa kukabidhiwa kadi za Chadema Bahari Beach Hotel. Huko kote aliyekuwa kifua mbele toka Chadema alikuwa Mbowe wakati watendaji wakuu wengine wa chama wakisusia.

Mbowe na Lowassa watafanya nini mkutano mkuu wa CHADEMA ukimkata Lowassa?
Mkutano Mkuu wa Chadema una nafasi ya kumchagua mgombea kiti cha Urais kwa kura na si kwa shinikizo la mwenyekiti. Iwapo Dr Slaa ataamua kuchukua form za Kugombea Urais kadiri ya msukumo wa wanachama wengi wa Chadema na watanzania, kisha mkutano mkuu ikatokea kumkata Lowasa chaguo la Mbowe nini hatima ya Lowasa na Mbowe atajisikiaje ndani ya Chama?

MBOWE KAIDHALILISHA CHADEMA/TANZANIA NA KUKIPASUA VIPANDE VIWILI

Mbowe amekidhalilisha chama chake kwa kumkumbatia Lowasa kinyume cha maadili ya chama chake na bila ridhaa ya chama chake chenye haiba ya kupinga kwa nguvu zote ufisadi nchini. Asipokatwa Lowasa mpasuko huu umeshajidhihirisha kutoka ndani ya Kamati kuu, hakuna hasara ya kumtosa Lowasa kwa vile Chama kilikuwa na mshikamano kabla ya Lowasa. Kimsingi ujio wa Lowasa umesababisha mpasuko mkubwa wa wanachadema na watanzania wapenda mageuzi nchini.

CCM IMEWEZA KUWADHIBITI MAFISADI HAWA CHADEMA IMETEKWA NA MAFISADI

CCM waliweza kulithibiti hili kundi la mafisadi wanaotaka kumpitisha mmoja wao kuwa Rais wa nchi, lakini Mbowe kaingia kichawakichwa na hatimaye umakini usipokuwepo kumkata Lowasa utawala wake utakuwa wa maumivu kuliko tunachoshuhudia sasa hivi utawala wa Kikwete.
Lowasa ni mfalme si mtu wa kukaa kujadili na watu nini kifanyike ila anaonekana ni wa mfumo wa kifalme kutoa amri.

Akiwa rais atawaingiza na kuwapatia nafasi nyeti mafisadi wenzake, nani wa kumnyoshea kidole wakati katiba inamlinda?
user-online.png
Dr.W.Slaa

Today 06:20
#1
JF Senior Expert Member
verified.png
Array

Join Date : 1st July 2008
Posts : 681
Rep Power : 0
Likes Received1359
Likes Given282

[h=2]
icon1.png
Re: Dr. Slaa kuwasilisha leo mpango mkakati wa ushindi mbele ya Sekretarieti[/h]
Yericko,

Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.

sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.

Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.

Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.​

naona umethitishiwa kua mbunge wa ludewa si wewe ulikuja na thread hapa ukisema lipumba atoswe ukawa waungane na lowassa umalaya wa kisiasa kwa kijana mwandishi kama wewe aibu acha kufitinisha waru unaamini kweli Mbowe anaweza fanya kitu bila baraka ya dr Slaa unajua wale wanavyofanya kazi au unasimuliwa na kuwageuka baada ya kuwa na uhakika wa kupitishwa ubunge na pindi chana kuanguka we are watching you dumila kuwili acha uchonganishi wa kimtandao
 
Kwanza kitu walichokifanya leo viongozi wa Chadema kumpokea Lowassa viongozi wote wakubwa na kumpa fomu huku tundu lissu akisema kabisa ukiunda serikali yako(yaani anamwambia lowassa) inamaanisha kuwa uongozi wa Chadema umeshampa nafasi lowassa ya kuwa mgombea wa uraisi kwa iyo zoezi la kuchukua fomu limetangazwa kama geresha tu.
CCM wagombea wote walienda kuchukua fomu na wakifika ofisini wanamkuta mohamed seif khatibu tu anawapa fomu wao ndo wanaenda kujielezea huko. Hamna hata mgombea aliyesindikizwa na mwenyekiti au aliyeanza kama kutangazwa kuwa ndo mshindi.

Hizi ndo mistakes ambazo Chadema mnazifanya na kwa watu wenye akili wanajua kumbe nyie mmeshanunuliwa tayari na vitu vyote mnafanya kama maigizo tu.

Kusema kweli hata mie sijaamini maneno ya tundu lissu na mbowe wakati lowassa anachukua fomu, at least you werte supposed to show that kuna fair ground/play kwenye michakato yenu.

CHADEMA/UKAWA MMETIA AIBU NA SITASHANGAA DR. SLAA AKIAMA KWA SABABU MMEONYESHA NI WANAFIKI WA HALI YA JUU NA KIBAYA ZAIDI HAMUWAFANYII UNAFIKI WATANZANIA TU, HADI NYIE WENYEWE MNAFANYIANA UNAFIKI.

KWELI FEDHA MWANAHARAMU.
 
Tafuta mbinu za kuokoa chama chako kuliko kupiga porojo hizi ambazo hazikisaidii chama.
 
naona mnaihurumia kweli chadema wana ccm!!! hahahahahaha mme paniki eeeeee!!! mtaanda makala nyingi sana suprise yenu jumapili uwanja wa taifa pale temeke pale!!!!
 
Kazi mnayo mwaka huu. mmezoea vya kunyonga, sasa ukawa mwaka huu haiwaponyeshi. lazima mnyongwe
 
naona umethitishiwa kua mbunge wa ludewa si wewe ulikuja na thread hapa ukisema lipumba atoswe ukawa waungane na lowassa umalaya wa kisiasa kwa kijana mwandishi kama wewe aibu acha kufitinisha waru unaamini kweli Mbowe anaweza fanya kitu bila baraka ya dr Slaa unajua wale wanavyofanya kazi au unasimuliwa na kuwageuka baada ya kuwa na uhakika wa kupitishwa ubunge na pindi chana kuanguka we are watching you dumila kuwili acha uchonganishi wa kimtandao

Mapokezi ya Lembeli wa Kahama yalikuwa na hisia ya aina yake na kuonyesha mshikamano wa viongozi wa Chadema, lakini kinachoendelea kwa Lowasa licha ya kwenda kumsafisha pale Buguruni, lakini Bahari beach ambako ilikuwa ni tukio la kichama na kichadema zaidi kumpokea mwanachama mpya, mwenyekiti Mbowe aliyeonekana wakati katibu mkuu, naibu wake Mnyika na mwanasheria mkuu Lissu kukosekana kwa kuwataja wachache. Je wauona ufa huo? Jipu litapasuka tu tusubiri.

Viongizo wa UKAWA halikuwa jukumu lao kumkaribisha Lowasa ndani ya chadema, wao wangekuwa wageni waalikwa tu na viongozi wakuu wa Chadema ndio waliotakiwa kulipamba tukio lile.
 
Uchambuzi kama huu ndio unazidi kututoa machozi wengine!!!......reputation ya cdm iliyojengwa kwa miaka si chini ya 10 inaungushwa kwa siku mbili tu....inauma sana.....hakyanani hakuna kauli ya dr slaa no my vote to cdm

machoz ya nini?? hujui hiido kete yao ya mwisho!!! mfamaji haishi kutapa tapa!!! ulizani wa takaa kimya wasije na uchafu kama huu!!! CDM daimaaaaaa!!!! mta hahaha sana ila suprise ipo!!!! kimya kingi kina mshindoooo!!! peopleeeeeeeeeeeeeee!!!!!

lazima wahahe maaana hali mbaya!!! na ndio mbinu pekeee waliobakiza mkiamini uchafu kama huuu mtu anaandika kwa malipo ya milion 5 anajivua taaluma yake ujue huyo ni masikini wa kutupazzzz
 
Mtaji wa chama chochote cha SIASA ni watu.....LOWASA kaongeza idadi ya watu CDM, LOWASA kapunguza idadi ya watu CCM hilo mtake msitake na tunajua linawauma sana, cha kufanya ni CCM kujipanga kujua wataokoka vp na haya mafuriko, mambo ya kuja na kujadili ishu za CDM hapa ni kumkatisha tamaa Makomeo wa watu, maana tangu juzi ni kama mumemsahau hv......khs kutoelewana kati ya viongozi wa CDM huko ni kuingilia mambo ya nyumba za watu, hembu tuambieni nyie kule lumumba kweli kuna maelewano,au wengine wanafurahia lichama linavyoyumba huku wakitamani litote wagawane mbao?
 
Ndio hivyo Slaa anaondoka, na washirika wenu wa UKAWA wanasepa maana wameshasoma upepo unavyovuma nje, sasa mtabaki na lowassa wenu anawaozea, hahahhaha kweli ukijenga msingi wa nyumba kwa tope basi Hata dhoruba dogo tu haubaki salama
 
Mapokezi ya Lembeli wa Kahama yalikuwa na hisia ya aina yake na kuonyesha mshikamano wa viongozi wa Chadema, lakini kinachoendelea kwa Lowasa licha ya kwenda kumsafisha pale Buguruni, lakini Bahari beach ambako ilikuwa ni tukio la kichama na kichadema zaidi kumpokea mwanachama mpya, mwenyekiti Mbowe aliyeonekana wakati katibu mkuu, naibu wake Mnyika na mwanasheria mkuu Lissu kukosekana kwa kuwataja wachache. Je wauona ufa huo? Jipu litapasuka tu tusubiri.

Viongizo wa UKAWA halikuwa jukumu lao kumkaribisha Lowasa ndani ya chadema, wao wangekuwa wageni waalikwa tu na viongozi wakuu wa Chadema ndio waliotakiwa kulipamba tukio lile.

wewe nani uwapangie majukumu viongozi wa UKAWA ????? ccm huko hamna kazi zakufanya????? hahahahahahahaha mmeshikwa pabayaaaaa????? mtakaaaaaaa
 
Ndio hivyo Slaa anaondoka, na washirika wenu wa UKAWA wanasepa maana wameshasoma upepo unavyovuma nje, sasa mtabaki na lowassa wenu anawaozea, hahahhaha kweli ukijenga msingi wa nyumba kwa tope basi Hata dhoruba dogo tu haubaki salama

leo mna kazi!!!! hahahahahahah!!! eti slaaa anaondoka!!! ndo kete yenu yamwisho hiyo!!!! mpo majininazama mnarusha mikono na miguu!! hakuna boya!!! uzuri tunaelewa mmepewa kafungu muwachanganye watanzania!!! uzuri hawa changanyikiwi!!! upepo na goli la mlono kwishney!!!!

peopleeeeeeeeess wamepaniki hawa jamaaaaa
 
wewe nani uwapangie majukumu viongozi wa UKAWA ????? ccm huko hamna kazi zakufanya????? hahahahahahahaha mmeshikwa pabayaaaaa????? mtakaaaaaaa

Pole yako, mimi si mwanachama wa chama cho chote cha siasa, na siko tayari kuwa mtumwa wa chama ila mtu huru nisiyefungamana na upande wo wote, ni mvutiwa na itikadi za kuwaletea watanzania maendeleo na kuondokana na stress zinazoweza kuzuilika na utawala bora. Lengo ni kuipa likizo kwanza CCM ijitafakari na watakaporudi watakuwa makini wasijisahau kama wanavyofanya kwa mazoea sasa.

Laiti ungenijua, pole ndugu.
 
Mtaji wa chama chochote cha SIASA ni watu.....LOWASA kaongeza idadi ya watu CDM, LOWASA kapunguza idadi ya watu CCM hilo mtake msitake na tunajua linawauma sana, cha kufanya ni CCM kujipanga kujua wataokoka vp na haya mafuriko, mambo ya kuja na kujadili ishu za CDM hapa ni kumkatisha tamaa Makomeo wa watu, maana tangu juzi ni kama mumemsahau hv......khs kutoelewana kati ya viongozi wa CDM huko ni kuingilia mambo ya nyumba za watu, hembu tuambieni nyie kule lumumba kweli kuna maelewano,au wengine wanafurahia lichama linavyoyumba huku wakitamani litote wagawane mbao?

Sharti la Lowasa kuhamia Chadema ni uanachama au kuutaka urais?
 
hahahaha!!! tume wajua mmepewa fungu na uenezi wa chama chenu muendeleee kuichafua chadema sasa mmechokoza nyuki!!!! chadema haichafuki kwa hoja dhaifu kama hizo!!!

jf na nyie hiii kitu muitazame!!!! hawa watu watu wamepanik!!! hahahahahahah
 
leo mna kazi!!!! hahahahahahah!!! eti slaaa anaondoka!!! ndo kete yenu yamwisho hiyo!!!! mpo majininazama mnarusha mikono na miguu!! hakuna boya!!! uzuri tunaelewa mmepewa kafungu muwachanganye watanzania!!! uzuri hawa changanyikiwi!!! upepo na goli la mlono kwishney!!!!

peopleeeeeeeeess wamepaniki hawa jamaaaaa

Endelea kujiliwaza
 
Pole yako, mimi si mwanachama wa chama cho chote cha siasa, na siko tayari kuwa mtumwa wa chama ila mtu huru nisiyefungamana na upande wo wote, ni mvutiwa na itikadi za kuwaletea watanzania maendeleo na kuondokana na stress zinazoweza kuzuilika na utawala bora. Lengo ni kuipa likizo kwanza CCM ijitafakari na watakaporudi watakuwa makini wasijisahau kama wanavyofanya kwa mazoea sasa.

Laiti ungenijua, pole ndugu.

hahahahahaah!!! nakujua unataka nikutaje????
 
Back
Top Bottom