Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.

Ni vyema, lakini Je tcra nguvu waliyonayo wanaitumia ipasavyo au ....???
Mkuu Kibanga, TCRA yeye ni regulator tuu wa vyombo vya utangazaji, nguvu zake na mamlaka yake yanaishia kwenye vyombo vya utangazaji tena katika utekelezaji wa kanuni na taratibu na sio prosecutor wa jinai. Makosa ya mtandao ni makosa ya jinai, prosecutor ni DPP.

Nimenote WhatsApp na Facebook wamewafikia, thanks God, jf hatujafikiwa, let's be responsible social media contributors kwa kusema ukweli daima.
Paskali
 
pasco kuna wanaokuheshimu na kuna wanao kudharau. kulingana na attachment uliyoiweka yeye yuko sawa zaidi yako. kwanza jiulize kwa nini hayo yote yametokea? kwa nini aitwe... kama hakuna visababishi vinavyolandana? kwa nini uitwe malaika au mtakatifu kama hujalandana na tabia zao? ukweli ni kwamba ukweli huchoma zaidi ya uongo
 
Kaka Pasco, hoja yako hasa ni ipi? Unaandika mambo mengi lakini hulengi kwenye hoja. Unathibitishaje kuwa unaouita uzushi ni uzushi au uongo kweli? Kwani hakuna uzushi na uongo unaotetewa? Uongo ni uongo;ukweli ni ukweli
Mkuu Mwanasheria nguli mbobezi Petiro, kuona hoja ni ipi pia kunahitaji kiwango fulani cha level ya uelewa kuweza kuona hoja ya uzi huu ni ipi, ukiwa uko below level ya uelewa huo, hutaona hoja ni ipi!.

Tuhuma zimetolewa kuhusu uongo na uzushi mitandaoni na japo haikusemwa ila mlengwa pia ni jf.

Hoja ni kila zikitolewa shutuma za uongo au uzushi, dawa ni kwa shutuma hizo zijibiwe kwa ukweli na facts.

Nikatolea mfano uzushi wa udikiteta na uvunjaji wa katiba, ulipoibuliwa na Chadema na katika UKUTA, nikasema kama katiba imetoa hakiya kuandamana na kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa popote then rais akapiga marufuku mikutano hiyo mpaka 2020, ili kuufuta uzushi wa udikiteta, msemaji wa serikali alipaswa kusema tuu ukweli kuwa rais sio dikiteta bali amepiga marufuku mikutano ya kisiasa hadi 2020 kwa mamlaka gani chini ya kifungu gani au sheria gani inayompa mamlaka rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa amri inayopingana na katiba, then hoja ya udikiteta na uvunjifu wa katiba inakufa natural death.

Uzushi na uongo unakanushwaje? , unakanushwa kwa kusema ukweli, na sio kuacha tuu kwa vile ni uongo na uzushi, hivyo unaamua kuupuuza tuu huo uongo huku uongo huo ukiendelea kusemwa na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hivyo hugeuka kuwa ni ukweli na sasa uongo huo umeingizwa hadi UN!.

Ufafanuzi huu ni wa level ya sekondari ila
kama bado hujaelewa naweza kukufafanulia kwa low level zaidi ya watoto wa primary.
Paskali
 
Uongo ni taarifa,kauli au habari isiyo na ukweli inayotolewa na mtu mwenye nia ya kuaminisha kuwa huo ni ukweli. Ukweli unabebwa na taarifa,kauli au habari yenye ukweli.
Mkuu Peter uongo ukisemwa unakanushwaje bila kuusema ukweli? .
Mfano nikikuzushia kuwa Petro Mselewa ni Mwanasheria mbobezi mwenye shahada ya uzamivu kwenye fani ya sheria, lakini hiyo shahada yake ni shahada fake kutoka vyuo vya uchochoroni ndio maana anajenga hoja kama mwanafunzi wa shule ya msingi! . Usipokanusha na uongo huo ukiendelea kurudiwa rudiwa unageuka ukweli , hata ukijenga hoja za ki masters lakini zitaonekana ni za shule ya msingi.
Paskali
 
Mkuu Mwanasheria nguli mbobezi Petiro, kuona hoja ni ipi pia kunahitaji kiwango fulani cha level ya uelewa kuweza kuona hoja ya uzi huu ni ipi, ukiwa uko below level ya uelewa huo, hutaona hoja ni ipi!.

Tuhuma zimetolewa kuhusu uongo na uzushi mitandaoni na japo haikusemwa ila mlengwa pia ni jf.

Hoja ni kila zikitolewa shutuma za uongo au uzushi, dawa ni kwa shutuma hizo zijibiwe kwa ukweli na facts.

Nikatolea mfano uzushi wa udikiteta na uvunjaji wa katiba, ulipoibuliwa na Chadema na katika UKUTA, nikasema kama katiba imetoa hakiya kuandamana na kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa popote then rais akapiga marufuku mikutano hiyo mpaka 2020, ili kuufuta uzushi wa udikiteta, msemaji wa serikali alipaswa kusema tuu ukweli kuwa rais sio dikiteta bali amepiga marufuku mikutano ya kisiasa hadi 2020 kwa mamlaka gani chini ya kifungu gani au sheria gani inayompa mamlaka rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa amri inayopingana na katiba, then hoja ya udikiteta na uvunjifu wa katiba inakufa natural death.

Uzushi na uongo unakanushwaje? , unakanushwa kwa kusema ukweli, na sio kuacha tuu kwa vile ni uongo na uzushi, hivyo unaamua kuupuuza tuu huo uongo huku uongo huo ukiendelea kusemwa na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hivyo hugeuka kuwa ni ukweli na sasa uongo huo umeingizwa hadi UN!.

Ufafanuzi huu ni wa level ya sekondari ila
kama bado hujaelewa naweza kukufafanulia kwa low level zaidi ya watoto wa primary.
Pasco.
Kwa hiyo kukanusha tu basi inatosha? Na katiba zetu si ndio hizi wakati mwingine zinatafsiriwa na mahakama na wakati mwingine jeshi na polisi ndio watoa tafsiri
 
Kaka Pasco, hoja yako hasa ni ipi? Unaandika mambo mengi lakini hulengi kwenye hoja. Unathibitishaje kuwa unaouita uzushi ni uzushi au uongo kweli? Kwani hakuna uzushi na uongo unaotetewa? Uongo ni uongo;ukweli ni ukweli

Pasco, anatumia mbinu ya 'kejeli (satire)' kufikisha ujumbe wake, linganisha bandiko lake la leo na lile la jana kuhusu Profesa Shivji - kwa lugha ya hisabati, anasema kama X = Y na Y = Z je msomaji huoni hiyo inamaanisha X = Z?
 
Kanusho la kutufunga mdomo ni kumruhusu Lowasa afanye mikutano ya kisiasa,maandamano nk,nasema Lowasa kwa kuwa makatazo yote mlengwa hasa ni yeye
 
Hoja na ushauri wako uko vizuri Pasco... Labda nao wanatunga uongo ilihali wako busy kufanya kazi kimya kimya... Maana washajua wapinzani wetu ni watu wa kelele badala ya kutoa mawazo mbadala na kwa heshima.
 
Kwa hiyo kukanusha tu basi inatosha? Na katiba zetu si ndio hizi wakati mwingine zinatafsiriwa na mahakama na wakati mwingine jeshi na polisi ndio watoa tafsiri
Mkuu Kajiru, nimeeleza kazi ya kwanza ni kukanusha na kazi ya pili ni kuusema ukweli.
Pasco
 
Mkuu Peter uongo ukisemwa unakanushwaje bila kuusema ukweli? .
Mfano nikikuzushia kuwa Petro Mselewa ni Mwanasheria mbobezi mwenye shahada ya uzamivu kwenye fani ya sheria, lakini hiyo shahada yake ni shahada fake kutoka vyuo vya uchochoroni ndio maana anajenga hoja kama mwanafunzi wa shule ya msingi! . Usipokanusha na uongo huo ukiendelea kurudiwa rudiwa unageuka ukweli , hata ukijenga hoja za ki masters lakini zitaonekana ni za shule ya msingi.
Pasco
Mkuu Pasco kwanza naitwa Petro na si Petiro. Halafu,unapojibu usiwe unadharau au kukejeli watu kaka. Tazama ulivyonikejeli na kunidharau
 
Mwenye macho haambiwi tazama na lisemwalo lipo na Kama halipo linakuja,hata Kama ungekanusha vipi lakini huwezi ukafanikiwa kuwadanganya watu wazima wanaoweza kuona kwa macho Yao na wenye akili za kutambua jambo la kweli ni lipi na la uwongo ni lipi.
 
Back
Top Bottom