Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
Wanabodi,
Baada ya rais Magufuli kuombea malaika watoke mbinguni kuja kuifunga mitandao ya kijamii yenye uongo na Uzushi kama humu jf, wana mitandao wote resiponsible hatuna budi kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kuitumia mitandao ya kijamii more responsibility kwa nia njema (in good faith) ya kujenga, kuwa wakweli na hata tukikosoa tukikosoa constructively kwa kukosoa ili kujenga na sio kukosoa ili kubeza.

Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho wake unageuka kuwa ndio ukweli, hivyo dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukiletwa humu, kama kuna mwenye ukweli autoe tuu hapo hapo ili kutoupa fursa uongo huo kuendelea kusema.

Nakiri kupandisha uzi huu baada ya kuwa inspired na bandiko la mwana jf huyu.
Mh rais kwanza Napenda kukupongeza kwa Kazi nZuri Na jitihada zako ambazo zinaanza kuzaa matunda, songa mbele maana tunakuombea pamoja Na changamoto hizo tutafika. Lengo la kuandika andiko hili Ni kukushauri Na kukuunga mkono juu ya sikitiko lako juu ya upotoshaji mitandaoni.

Ushauri wangu Ni mfupi kuwa dawa ya Moto Ni Moto Na kwamba ili kukabiliana Na upotoshaji huu , dawa sio kuizuia Bali kuwawezesha wafanyakazi wa serikali kukabiliana Na upotoshaji huu kwa kuwa tayari kueneza ukweli kupitia mitandao hiyo hiyo . Kwa kuanzia kila msemaji Au afisa Habari wa wizara Na vitengo vya serikali afundishwe namna bora ya kutumia mitandao hiyo . Pili iwepo sera ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii kwa kila kitengo cha serikali Na Tatu TCRA waongezewe uwezo wa kushughulikia wahalifu wa mitandaoni kwa kupewa mafunzo zaidi...

Wadau tuongezee....

Moderators: please Naomba msiunganishe uzi huu Na mwwingine .
Mkuu Sema, naunga mkono hoja.
Dawa ya uongo uzushi na upotoshaji ni ukweli, utoaji majibu kwa uharaka na usahihi.

Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho unageuka ukweli na mfano mdogo ni hii dhana ya udikiteta, ni uwongo tuu na uzushi kumzushia rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa ni dikiteta kwa kitendo tuu cha kupiga marufuku mikutano ya hadhara.

Uzushi huu ulianzia humu jf na mwanzilishi namjua!, haukukanushwa, uzushi huu ukadakwa na Chadema mara wanaibuka na ukuta, haukukanushwa sasa hadi sasa neno dikiteta limeanza kuwa rasmi.

Iwapo Ikulu yetu ingekuwa na mtu wao humu jf na wakaukanusha mara moja uzushi ule kwa kuusema ukweli jina la udikiteta isingekuwepo.

Katiba imetoa uhuru wa kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhara, rais alipopiga marufuku mikutano hiyo ilikuwa ni kazi ndogo tuu watu wake kuingia humu na kueleza Mhe rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu fulani fulani, basi kusingekuwepo hoja ya udikiteta wala ukuta, lakini kitendo cha mpaka leo hii ninapoandika hapa hakuna kanusho lolote lenye kuonyesha mamlaka ya rais kutenda kinyume cha maelekezo ya katiba, kunapelekea uwongo huo wa udikiteta kuonekana kama ndio ukweli wenyewe.

Kila uongo ukiachwa unageuka ukweli na ukikanushwa unafutika.
Paskali
 
Mkuu Pasco ni kazi sana kukanusha kila jambo na hilo la kuweka vifungu ndiyo ugumu wenyewe wa kukanusha habari maana hakuna basis za kusimamia.Katiba na sheria inavunjwa sana,mfano mikutano ya hadhara kupigwa stop, kuteuliwa makada wa CCM ambao hawajawahi kuwa watumishi wa umma wakati sheria zinataka angalau umekaa kuwa mkuu wa idara miaka saba ndiyo majina yanapendekezwa kwenda Tamisemi.Sijui watumishi wa umma wanajisikiaje maana leo hata Wema Sepetu anaweza kuteuliwa kuwa mkurugenzi.Ni vizuri rais wetu akasoma kwanza sheria kuhusu chochote kabla hajafanya lolote.
 
Wanabodi,
Baada ya rais Magufuli kuombea malaika watoke mbinguni kuja kuifunga mitandao ya kijamii yenye uongo na Uzushi kama humu jf, wana mitandao wote resiponsible hatuna budi kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kuitumia mitandao ya kijamii more responsibility kwa nia njema (in good faith) ya kujenga, kuwa wakweli na hata tukikosoa tukikosoa constructively kwa kukosoa ili kujenga na sio kukosoa ili kuweza.

Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho wake unageuka kuwa ndio ukweli, hivyo dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukiletwa humu, kama kuna mwenye ukweli autoe tuu hapo hapo ili kutoupa fursa uongo huo kuendelea kusema.

Nakiri kupandisha uzi huu baada ya kuwa inspired na bandiko la mwana jf huyu.
Mkuu Sema, naunga mkono hoja.
Dawa ya uongo uzushi na upotoshaji ni ukweli, utoaji majibu kwa uharaka na usahihi.

Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho unageuka ukweli na mfano mdogo ni hii dhana ya udikiteta, ni uwongo tuu na uzushi kumzushia rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa ni dikiteta kwa kitendo tuu cha kupiga marufuku mikutano ya hadhara.

Uzushi huu ulianzia humu jf na mwanzilishi namjua!, haukukanushwa, uzushi huu ukadakwa na Chadema mara wanaibuka na ukuta, haukukanushwa sasa hadi sasa neno dikiteta limeanza kuwa rasmi.

Iwapo Ikulu yetu ingekuwa na mtu wao humu jf na wakaukanusha mara moja uzushi ule kwa kuusema ukweli jina la udikiteta isingekuwepo.

Katiba imetoa uhuru wa kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhara, rais alipopiga marufuku mikutano hiyo ilikuwa ni kazi ndogo tuu watu wake kuingia humu na kueleza Mhe rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu fulani fulani, basi kusingekuwepo hoja ya udikiteta wala ukuta, lakini kitendo cha mpaka leo hii ninapoandika hapa hakuna kanusho lolote lenye kuonyesha mamlaka ya rais kutenda kinyume cha maelekezo ya katiba, kunapelekea uwongo huo wa udikiteta kuonekana kama ndio ukweli wenyewe.

Kila uongo ukiachwa unageuka ukweli na ukikanushwa unafutika.
Pasco
Umeandika point kubwa. Uzee huu sitaki shida. Ila nina swali: Pasco, hivi Marais/Mawziri wakuu (kwa nchi zinazosimamiwa mna mawaziri wakuu) wana mamlaka inayomruhusu kutumia fedha anavyotaka? Mfano kunua ndege aliamua na nani au sheria/katiba inamruhusu! Mzee wa kanisa alimuahidi njia je anaruhusiwa kisheria/kikatiba kuamua hivyo anapojisikia. Nadhani maamuzi kama hayo ndiyo yanayoleteleza dhana hiyo. Kutumbua bila kuwasikiliza wahusika mfano marehemu wa Dar etc!
rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, Pasco ndio maana huwa nakwambia kuwa waandishi mnajikomba! Sasa sentensi hiyo ni ya nini? Just sema Rais, Kuonyesha loyalty!
Lakini umeandika vizuri!
 
Hii inadhihirisha Rais hana udikteta wowote, ni mtu wa haki na mfuata sheria na taratibu. la sivyo angeamuru tu kuzimwa!Lakini hafurahishwi na kejeli naye kama mtu mstaarabu angependa constructive arguments.
 
Naomba mnieleweshe kwani kwa hili mimi ni mjinga kabisa. Dikteta ana sura gani? Je Dikteta ana tabia zipi? Nawezaje kutambua kuwa mtu huyu ni dikteta? Je wanaosema kuwa mpendwa wetu JPM ni dikteta wameona nini kwake?
 
Mkuu Pasco ni kazi sana kukanusha kila jambo na hilo la kuweka vifungu ndiyo ugumu wenyewe wa kukanusha habari maana hakuna basis za kusimamia.Katiba na sheria inavunjwa sana,mfano mikutano ya hadhara kupigwa stop, kuteuliwa makada wa CCM ambao hawajawahi kuwa watumishi wa umma wakati sheria zinataka angalau umekaa kuwa mkuu wa idara miaka saba ndiyo majina yanapendekezwa kwenda Tamisemi.Sijui watumishi wa umma wanajisikiaje maana leo hata Wema Sepetu anaweza kuteuliwa kuwa mkurugenzi.Ni vizuri rais wetu akasoma kwanza sheria kuhusu chochote kabla hajafanya lolote.
Sio kazi kubwa kukanusha uongo.
Kilichopo ni kuwa kila mtu ni mwoga na anapima upepo kuwa mkuu anaegemea wapi ndio azungumze.
Inawezekana Raisi ana nia njema (ingawa kwa yeye kutokea CCM siioni hiyo nia njema).
Tuingie kwenye hoja.
Baada ya uchaguzi panakuwa na makandokando mengi hasa uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kama wa mwaka jana na hata mimi nisingeruhusu soon after uchaguzi mikutano na maandamano.Kilichotokea ni kuwa hapakuwa na mtu wa kutoa taarifa kwa kina na kwa usahihi.Vitisho mwanzo mwisho.
Kuhusu ndani ya serikali,hoja ya jwanza kubwa ilikuwa kuhamishwa bil 400 kwenda Ujenzi ( wizara iliyokuwa chini ya Raisi),maelezo ya kina hayakupatikana.
Bunge tunaliona jinsi linavyokwenda,kwa kweli tuombe Mungu tufike salama lakini nina wasiwasi mbele ya safari kwani tumeona Naibu spika alivyoingia,kuondoa live coverage (kwa sababu zinazogongana-pesa hakuna,watu wafanye kazi mchana).
Mheshimiwa Raisi chukua maneno ya Jenerali na uwe Magufuli the lawgiver,waache watu wakukosoe (wasikutukane),implement mipango yako kwa kufuata katiba,tumia na boresha taasisi zilizopo na utapata amani.One man show itakutia stress na stress isije kusababishia ukakosa kufaidi pensheni ya U raisi.
 
Naomba mnieleweshe kwani kwa hili mimi ni mjinga kabisa. Dikteta ana sura gani? Je Dikteta ana tabia zipi? Nawezaje kutambua kuwa mtu huyu ni dikteta? Je wanaosema kuwa mpendwa wetu JPM ni dikteta wameona nini kwake?
Dikteta anajulikana!Kama ukimtukana au kumsema vibaya ukiwa mlimani, hufiki mataa ya ubungo tayari utakuwa marehemu!Huwezi kumtukana Dikteta hadharani halafu bado ukaendelea kula kuku mtaani!Hakuna udikteta Tanzania, wala hakunan chembe ya dalili!Tuna uhuru wa kuzungumza chochote, hata kama unatukana huna hatia mpaka mahakama iseme!Ndio maana watu wanautumia uhuru huu vibaya sana
 
Pascali nimekusoma kaka,labda kwakuwa umesema labda huyo afisa hbr atakuja kutuwekea hicho kifungu cha katiba kinachokataza mikutano ya hadhara.
 
Naona ndg yangu Pasco, kama vile una kitu fulan ulitaka kukifungua kwenye fundo la moyo ila ukaogopa 7m kukutoka fasta. Huo uongo na uzushi ni upi unao uona kuwa JPM anatupiwa au anapakaziwa?? Uwe muwazi tu ili pia weye usaidie kuukanusha.
Kuna mtu kakuuliza hapa kuwa, nchi yenye baraza la mawaziri, lenye makamu wa rais, na waziri mkuu, labda na bunge. Yawezekana kiongozi mmoja tu aamue kununua ndege 2 cash bila kikao?? Yawezekana aamue tu kupeleka ruzuku mashuleni bila hata ushauri?? Hajaziweka mfukoni mwake akawapeleka wanaye shopping Marekani; kitu ambacho kama kweli angelikuwa dikteta angeliweza fanza lakini kanunua kitu cha kuletea maendeleo nchi yetu. Swali ni ; Je, alijadiliana na nani?? Kuamua tu na kupiga marufuku mikutano ya siasa till 2020, alijadiliana na nani? Uamuzi wa mtu mmoja weye waona sawa?
Ila umesema vizuri sana Pasco haswa hapo Ikulu imekosa hata msemaji mmoja tu wa kuelewesha wananchi kuhusu utata wa maswali ka haya. Ikulu ingelifaa iwe na wepesi wa kuelezea haya. Nadhani Katiba ndiyo kiongozi chetu hivyo tendo lolote kinyume na katiba hata liwe zuri ni kutumia nguvu kinyume na katiba.
HAKIKA; mkulu sio dikteta ila ayafanyayo japo ni nia njema angetakiwa aulize kaushauri tu hata kama ni kwa kushinikiza wenzie. Naomba usomaye unielewe usijenielewa vibaya. Miye si mchochezi tena nampenda saana tu rais wangu kwani ni amri ya Mungu kwangu kuwa lazima nimpende na kumuombea
 
Kaka Pasco, hoja yako hasa ni ipi? Unaandika mambo mengi lakini hulengi kwenye hoja. Unathibitishaje kuwa unaouita uzushi ni uzushi au uongo kweli? Kwani hakuna uzushi na uongo unaotetewa? Uongo ni uongo;ukweli ni ukweli
Nakubaliana na wewe mkuu, uongo hauwezi kuwa ukweli na ukweli hauwezi kuwa uongo. Uongo ni wa muda tu, haudumu. Lakini ukweli unadumu, hata ukijaribu kuupindisha mwisho wa siku utajidhihirisha!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wanabodi,
Baada ya rais Magufuli kuombea malaika watoke mbinguni kuja kuifunga mitandao ya kijamii yenye uongo na Uzushi kama humu jf, wana mitandao wote resiponsible hatuna budi kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kuitumia mitandao ya kijamii more responsibility kwa nia njema (in good faith) ya kujenga, kuwa wakweli na hata tukikosoa tukikosoa constructively kwa kukosoa ili kujenga na sio kukosoa ili kubeza.

Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho wake unageuka kuwa ndio ukweli, hivyo dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukiletwa humu, kama kuna mwenye ukweli autoe tuu hapo hapo ili kutoupa fursa uongo huo kuendelea kusema.

Nakiri kupandisha uzi huu baada ya kuwa inspired na bandiko la mwana jf huyu.
Mkuu Sema, naunga mkono hoja.
Dawa ya uongo uzushi na upotoshaji ni ukweli, utoaji majibu kwa uharaka na usahihi.

Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho unageuka ukweli na mfano mdogo ni hii dhana ya udikiteta, ni uwongo tuu na uzushi kumzushia rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa ni dikiteta kwa kitendo tuu cha kupiga marufuku mikutano ya hadhara.

Uzushi huu ulianzia humu jf na mwanzilishi namjua!, haukukanushwa, uzushi huu ukadakwa na Chadema mara wanaibuka na ukuta, haukukanushwa sasa hadi sasa neno dikiteta limeanza kuwa rasmi.

Iwapo Ikulu yetu ingekuwa na mtu wao humu jf na wakaukanusha mara moja uzushi ule kwa kuusema ukweli jina la udikiteta isingekuwepo.

Katiba imetoa uhuru wa kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhara, rais alipopiga marufuku mikutano hiyo ilikuwa ni kazi ndogo tuu watu wake kuingia humu na kueleza Mhe rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu fulani fulani, basi kusingekuwepo hoja ya udikiteta wala ukuta, lakini kitendo cha mpaka leo hii ninapoandika hapa hakuna kanusho lolote lenye kuonyesha mamlaka ya rais kutenda kinyume cha maelekezo ya katiba, kunapelekea uwongo huo wa udikiteta kuonekana kama ndio ukweli wenyewe.

Kila uongo ukiachwa unageuka ukweli na ukikanushwa unafutika.
Pasco
Kutetea uongo na kupinga hali halisi iliyopo ni kujitoa ufahamu.

Kwa Pasco linaeleweka lazima atetewe JPM hata kama kajidhihirisha alivyo mbele ya kila mwananchi anaejali.

Si bure juhudi zake zinalipa
 
Dawa ya uongo ni kutenda na si kila wakati kukalia kujibu maneno ya wachonga mdomo wasiokua na maana na wazushi na wambeawambea.Some people are fools and if you indulge in argument with them you may be seem to be even more fool.Do not argue with a fool,they may not notice the difference.
 
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho unageuka ukweli na mfano mdogo ni hii dhana ya udikiteta, ni uwongo tuu na uzushi kumzushia rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa ni dikiteta kwa kitendo tuu cha kupiga marufuku mikutano ya hadhara.
Uzushi huu ulianzia humu jf na mwanzilishi namjua!, haukukanushwa, uzushi huu ukadakwa na Chadema mara wanaibuka na ukuta, haukukanushwa sasa hadi sasa neno dikiteta limeanza kuwa rasmi.
Naona Pasco umeanza 'kumkana Yesu mara 3'.. Kulikoni? Au ndiyo kuisoma namba?:):)
 
chaguzi zake ni jibu tosha yeye ni wa aina gani ktk moja ya sifa ya dikteta ni kusifiwa hapo uliemsifia utapewa cheo tu au kuandaliwa mazingir salama kwa wale wakosoaji siku zote huwa taabuni ,,,,,SIWEZI KUMPA MTOTO WA JIRANI CHAKULA WAKAT WA KWANGU ANA NJAA!!! TUMEAGIZWA UPENDO KWA NINI WASILE PAMOJA HICHO KIDOGO?
 
Sijaona mantiki ya hoja ya hii thread. Kimsingi, mfumo wa vyama vingi ni uwanja wa mapambano ya kifikra unaohusisha makundi yenye maslahi tofauti na kila kundi likijaribu kulikosoa, na kujijenga kutokana udhaifu wa, kundi lingine. Kukosoa na kukosolewa ndio mchezo wenyewe! Jambo lingine ni kwamba, as long as politics always lacks objectivity, in democratic politics there must always be a space for dissenting views. Kukosoa ni haki ya kikatiba kwa sababu binadamu hawezi kuwa sawa na nyumbu. Na Magufuli atakosolewa sana kwa sababu ana udhaifu mkubwa unaofanya iwe rahisi kwake kukosolewa. Hana itikadi (political and social beliefs) inayomuongoza; wala hana mrengo wa kiuchumi (economic school of thought) anayoegemea; na kwa hivyo hana maono wala dira; na mwishowe hana mikakati wala vipaumbele. Utendaji wake ni 'ad hoc'; kila siku na agenda mpya!
 
Back
Top Bottom