Udhaifu wa Spika Ndugai na vituko vyake ni matokeo ya ujenzi wa #MfumoMagufuli aka #MfumoJiwe

Sam Naipenda

Member
Mar 1, 2018
97
720
wakuu, kwa masikitiko makubwa nimeona taarifa ya spika wa bunge mh ndugai akimwamrisha CAG kufika mbele ya kamati ya maadili ya bunge kwa kile kilichotajwa kama kulivunjia heshima bunge. hadi sasa nataka kuamini kwamba habari hizi ni za uzushi na vichekesho vya mitandaoni kuonesha uhatari wa #MfumoMagufuli au #MfumoJiwe unaojengwa na rais magufuli..

kama ni kweli spika kafanya hivyo basi kitendo hiki kinathibitisha kile nilichoweka hapa wiki iliyopita hapa juu ya madhara ya #MfumoJiwe (Ujenzi wa "Mfumo Magufuli", hatari na janga kwa taifa kuliko Rais Magufuli mwenyewe). niliwambia kwamba #MfumoJiwe ni hatari na una madhara makubwa kuliko anayeujenga. #MfumoJiwe unatengeneza nchi ya watu na viongozi wa ajabuajabu wasiotaka kutumia akili, hekima, wala busara katika kazi zao na yale wanayoyasema. ni mfumo unaodharau taratibu za kisheria na kikatiba pale unapotaka kutimiza matakwa ya anayeujenga yaani magufuli. ndugai ni moja ya matunda mabovu kabisa ya ujenzi wa #MfumoJiwe. ni spika ambaye anaendeshwa kwa rimotikontroo kutokea ikulu na aisiyejiamini hata kidogo

kama alikua hakumbuki vizuri akumbushwe tu kwamba yeye ndio spika wa kwanza katika historia ya nchi kupiga mtu hadharani kwenye mkutano wa uchaguzi. ndio spika wa ovyo na asiye na maadili ya kutosha kuongoza shombo tukufu cha kutunga sharia na #MfumoJiwe umemweka pale ukijua kwamba yeye ni dhaifu na udhaifu wake unarahisha sana ujezi wa #MfumoJiwe. ndugai ndio spika pekee katika historia ya Tanzania ambaye kaacha mamlaka makubwa ya kikatiba aliyokabidhiwa na nchi na kujigeuza kuwa msaidizi binafsi wa magufuli. hii ndio mana haoni aibu kutamaka hadharani kwamba hata uundaji wa kamati za bunge anampigia simu magufuli kumuuliza amweke nani (rejea kauli yake siku akipokea taarifa ya kamati ya kuchunguza madini ya tanzanite).

spika ndugai ndio spika pekee katika historia ya Tanzania ambaye kila siku yuko pembeni na magufuli kwenye muvi zake za kuzindua miradi na matukio mengine ya ajabuajabu hapa ikulu yasiyokwisha. spika anayeacha majukumu yake ya kuongoza chombo cha kuwawakilisha wananchi, kuihoji na kuisimamia serikali na kudhibiti nguvu ya rais na badalayake kuwa mwimbaji mashairi ya kumsifia rais na ujenzi wa #MfumoJiwe. huyu ndio spika dhaifu kuwahi kutokea ambaye hana aibu wala kujisikia kichefuchefu kusimama mbele ya makumi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini kuonesha ni kibaraka cha magufuli kwa kutangaza kwamba eti kapokea barua ya mbunge wa chadema kuhamia chichiemu. hii ndio ilikua kauli ya maana na hekima kabisa toka kwa spika mbele ya wanadiplomasia wa kimataifa. huyu ndiye spika dhaifu kabisa anamsikia rais akilidhalilisha bunge kwa kuhoji hata kiti cha spika kinavyofanya kazi na bado anasimama kumsifia akitabasumu bila kumwajibisha huku akiwa na mamlaka kisheria kupitia bunge analoliongoza.

kitendo cha ndugai kumtisha CAG anayetimiza majukumu yake kisheria na kikatiba na mwenye uhuru wa kutoa maoni yake kama rais juu ya utendaji wa bunge kama chombo cha uwakili, kinaonesha ni kwa jinsi gani anafanya kazi kwa akili na fikra za kushikiwa. ndugua kadhaulisha bunge letu na kulifanya kuwa tawi la chichiemu. spika kalifanya bunge kuwa chombo cha kuwaonea wapinzani. spika anayetoa kauli za ajabu na za kitoto na asiyona aibu kuonesha jazba zake hadhari mbele ya bunge takatifu akitoa kauli za vitisho na dharai kama anagombana na mke wake nyumbani.

hii ndio hatari kubwa ya #MfumoJiwe. mfumo unaodhoofisha mifumo ya kitaifa na kikatiba kutumiza matakwa ya magufuli. mfumo unaoweza kumfanya kila mtu mchumia tumbo na asiye na fikra huru kupiga makofi na kuimba ngonjera za kumsifu magufuli hata anapotukanwa au kuchapwa viboko. mfumo unaowalazimisha watumishi wa umma kuandamana kumsifia anayefanya maisha yao kuwa magumu. mfumo ambao bunge limebadilishwa kuwa tawi la chichiemu likiongozwa na wasaidizi binafsi wa rais magufuli.

#UdhaifuWaSpikaNdugai ni matokeo ya ujenzi wa #MfumoJiwe. ni wazi kwamba anataka kumdhalilisha CAG kwa matakwa ya bosi wake magufuli ambaye alishaanza siku nyingi kufanya hivyo. magufuli alimdhalilisha CAG mbele ya umma kwa kumlazimisha kumsafisha kuwa serikali yake haijapoteza trilioni 1.5 na ameamua kumyima nguvu ya kusimamia matumizi ya serikali yake kwa kuinyima ofisi ya CAG fedha inazohitaji kutumiza wajibu wake kisheria. ni wajibu wa kila mtanzania kuona athari ya #MfumoJiwe na kuwa na ujarisi wa kuupinga na kumpinga anayeujenga maana ni janga kwa taifa na utatuumiza kwa miaka mingi.

tumkumbushe ndugai kwamba yeye ni spika dhaifu kuliko wote na ndio sababu ya kuwa na bunge dhaifu kwa matakwa ya ras magufuli katika ujenzi wake wa #MfumoJiwe

watumishi tukutane Dodoma karibuni
 
Constutution of Tanzania 1977 (As Ammended from time to time)
143(6) In the discharge of his functions in accordance with the provisions of subarticles (2), (3) and (4) of this Article, the Controller and Auditor-General shall not be obliged to comply with the order or direction of any other person or Government Department, but the provisions of this subarticle shall not preclude a court from exercising jurisdiction to enquire into whether the Controller and
Auditor-General has discharged his functions in accordance with the provisions of this Constitution or not.
The Public Audit Act, 2008
13. Independence and status

The independence and status of the Office of the Controller and Auditor-General shall be as provided for under Article 143 of the
Constitution.
14. Immunity from legal proceedings
No action or other proceedings shall lie against the Controller and Auditor-General or any public officer, audit firm or expert authorized
by him for or in respect of the findings of any audit examination or inspection carried out by him in good faith in the exercise or purported exercise of powers under this Act.
 
Constutution of Tanzania 1977 (As Ammended from time to time)
143(6) In the discharge of his functions in accordance with the provisions of subarticles (2), (3) and (4) of this Article, the Controller and Auditor-General shall not be obliged to comply with the order or direction of any other person or Government Department, but the provisions of this subarticle shall not preclude a court from exercising jurisdiction to enquire into whether the Controller and
Auditor-General has discharged his functions in accordance with the provisions of this Constitution or not.
The Public Audit Act, 2008
13. Independence and status

The independence and status of the Office of the Controller and Auditor-General shall be as provided for under Article 143 of the
Constitution.
14. Immunity from legal proceedings
No action or other proceedings shall lie against the Controller and Auditor-General or any public officer, audit firm or expert authorized
by him for or in respect of the findings of any audit examination or inspection carried out by him in good faith in the exercise or purported exercise of powers under this Act.

#MfumoJiwe hauruhusu kusoma na kutafakari katiba na sheria kabla ya matamko na maamuzi. hayo sio misingi ya ujenzi wake. ni mfumo wa kibabe na jeuri na kuonesha nguvu
 
Kwani hua hawasomi mipaka ya madara yao??,mbona sheria apo ipo waz ata rais hawez kumuwajibisha?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndugai kwa kuwa ni supporter mkuuu wa ikulu, ni vema angemshawish jamaa kutengua uteuzi wake, lkn kumuita kibabe anaweza asifanikiwe na akaishia kuabika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom