UDART (Mwendokasi) umulikwe

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Habari iwe nanyi,

Ndugu zangu hawa watu wa UDART wana madharau makubwa sana kwa wananchi wa nchi hii.

1. Madereva wa mwendokasi wananyanyasa sana abiria, yaani wanaweza kuamua kwa makusudi kuegesha magari kwa madai ya kuwa mbele ya muda. Hili limekuwa likitokea hasa kwenye terminals kama Feri, Kimara na Morocco.

2. Unapopanda kwenye terminal ya kuanzia kama Morocco, Kimara au Feri hawasemi gari ni express, wanakuja kutangaza njiani. Mfano jana tumepanda mweno kasi dereva akakataa kuao gari feri kwa madai kwamba hana mafuta, wananchi tukaingia, jamaa akatufungia ndani akatoka kwa dk 15 watu tumekaa tunamsubiri tu, aliporudi akawasha gari bila hata ya kuongeza mafuta. Hakusema gari ni express lakini tulipofika DIT akatangaza gari ni fire na kwamba kituo cha kwanza ni Korogwe. Ikabidi wale wa manzese na wengine wa Ubungo maji tufike hadi Korogwe ndipo turudi nyuma.

3. Siku ya mvua kubwa ile hawa watu walikuwa wanakata tiketi huku wakijua magari hamna.

Jamani hawa watu wamulikwe kwakweli maana wanasababisha kero, usumbufu na unyanyasaji kwa rais.

Kindikwili kwasasa DSM.
 
watanzania wengine bado vichwa maji...unapandaje gari inayoenda kimara unashuka manzese au mapipa wakati kuna gari za morocco na ubungo na hizo gari haswa za ubungo kwenye terminal zote kivukoni gerezani huwa zinaondoka zikiwa tupu unamkuta mtu anagombania gari la kinara anashuka manzese..mnakera ukiwemo wewe mleta mada...na ni bora gari za kimara zote ziwe express mziogope .
 
na expressvinayoanzia kusimama kimara korogwe express zinaanzia kibo.
 
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana, tuna tabia ya kuponda na kudharau kila kitu chetu hatuwezi kuendelea kwa namna hii, hata wale tunaotamani kuwa kama wao, walianza hivi hvi kwa shida.
wako watu wanatamani aje mzungu au tu kampuni yoyote ya nje itoe huduma watalizika, lakini sasa hivi kwa kuwa kuna mswahili mwenzao wanaona kila kitu kibaya, hapana tubadilike maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe kuanza kupenda kujali na kuthamini vya kwetu.
mradi unazo changamoto, ndiyo, lakini hiyo ni hatua ya ukuzi kwa kitu chochote kama ambavyo kila mtu ana changamoto zake za maisha, wakati mwingine tunalalamika kwa ajili ya kulalamika tu, unasema umependa Express mimi ni msafiri mzuri wa usafiri huu, morocco hakuna express, wewe ulipanda ya wapi.
Mwendokasi pamoja na changamoto zake umetusaidia sisi wengine tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali, tuwakosoe kwa haki ili pia waweze kufanyia kazi haya tunayosema, lakini tukiwakosoa kwa matatizo yasiyokuwepo hata kama una nia njema unaonekana mbambasiahaji
Mfano changamoto kubwa kwenye mradi huu ni wingi wa abiria Vs idadi ya mabasi, Hili kila siku tunamabiwa mradi huu uko kwenye mpito, anatafutwa mtu wa kutoa huduma kamili na serikali, sasa kama huduma ziko kwenye mpito mwekezaji wa sasa anawezaje kuwekeza ili aongeze mabasi bila uhakika anakuwa na kazi hiyo kwa muda gani? hili hata waandishi wa habari hawalifanyi wanauliza abiria tu, kila stori ni kulalamika kukaa kituoni muda mrefu, wawafuate serikali waseme wanaongeza mabasi lini?
 
1. Madereva wa mwendokasi wananyanyasa sana abiria, yaani wanaweza kuamua kwa makusudi kuegesha magari kwa madai ya kuwa mbele ya muda. Hili limekuwa likitokea hasa kwenye terminals kama Feri, Kimara na Morocco- DART kwenye mifumo ya Kompyta zenu wekeni Majina ya Dereva wa zamu na Namba ya gari kwenye Display.

2. Unapopanda kwenye terminal ya kuanzia kama Morocco, Kimara au Feri hawasemi gari ni express, wanakuja kutangaza njiani. Mfano jana tumepanda mweno kasi dereva akakataa kuao gari feri kwa madai kwamba hana mafuta, wananchi tukaingia, jamaa akatufungia ndani akatoka kwa dk 15 watu tumekaa tunamsubiri tu, aliporudi akawasha gari bila hata ya kuongeza mafuta. Hakusema gari ni express lakini tulipofika DIT akatangaza gari ni fire na kwamba kituo cha kwanza ni Korogwe. Ikabidi wale wa manzese na wengine wa Ubungo maji tufike hadi Korogwe ndipo turudi nyuma- Haya magari hayana makondakta- Unachotakiwa kuangalia Display na kusikiliza mfumo wa Kompyuta uliopo ndani ya gari.

3. Siku ya mvua kubwa ile hawa watu walikuwa wanakata tiketi huku wakijua magari hamna- Hapa wasimamizi wanafaa kushughulikiwa. Na pia Namba za Wasimamizi wa shifti husika iwe kwenye Display ilikuwa saidia wateja.
 
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana, tuna tabia ya kuponda na kudharau kila kitu chetu hatuwezi kuendelea kwa namna hii, hata wale tunaotamani kuwa kama wao, walianza hivi hvi kwa shida.
wako watu wanatamani aje mzungu au tu kampuni yoyote ya nje itoe huduma watalizika, lakini sasa hivi kwa kuwa kuna mswahili mwenzao wanaona kila kitu kibaya, hapana tubadilike maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe kuanza kupenda kujali na kuthamini vya kwetu.
mradi unazo changamoto, ndiyo, lakini hiyo ni hatua ya ukuzi kwa kitu chochote kama ambavyo kila mtu ana changamoto zake za maisha, wakati mwingine tunalalamika kwa ajili ya kulalamika tu, unasema umependa Express mimi ni msafiri mzuri wa usafiri huu, morocco hakuna express, wewe ulipanda ya wapi.
Mwendokasi pamoja na changamoto zake umetusaidia sisi wengine tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali, tuwakosoe kwa haki ili pia waweze kufanyia kazi haya tunayosema, lakini tukiwakosoa kwa matatizo yasiyokuwepo hata kama una nia njema unaonekana mbambasiahaji
Mfano changamoto kubwa kwenye mradi huu ni wingi wa abiria Vs idadi ya mabasi, Hili kila siku tunamabiwa mradi huu uko kwenye mpito, anatafutwa mtu wa kutoa huduma kamili na serikali, sasa kama huduma ziko kwenye mpito mwekezaji wa sasa anawezaje kuwekeza ili aongeze mabasi bila uhakika anakuwa na kazi hiyo kwa muda gani? hili hata waandishi wa habari hawalifanyi wanauliza abiria tu, kila stori ni kulalamika kukaa kituoni muda mrefu, wawafuate serikali waseme wanaongeza mabasi lini?

Aisee kwahiyo dereva kuegesha gari kwa madai ya kuwa mbele ya muda huku abiria wakiendelea kupoteza muda kituoni kwako siyo shida, dereva kudanganya hana mafuta anaegesha gari halafu anaondoka akiwa amewafungia watu ndani baadaye anarudi ndani ya dk15 na kuondoa gari bila kuweka hayo mafuta kwako ni jambo la kupongeza tu. KAMA WEWE NI MZALENDO WA KUPONGEZA HADI UJINGA WA MADEREVA KAMA HAWA BASI WEWE HUJUI MAANA YA UZALENDO. Management ya UDART ni mbofu kama wanashindwa kuwasimamia hata madereva wao, sijasema waje wazungu kwenye andiko langu nimesema hayo ni makosa na dharau kwa abiria
 
Kwani Paul Makonda Mungu wenu wa hapo dsm hajui hizi kero?

Shida kama hizi hata muandikeje kwenye mitandao wanajifanya hawaoni.

Ila ukitaka waone ndani ya nusu saa hadi magufuli ataona wewe watukane.
Kesho yake ymtu hadi magufuli kashasoma hilo tusi

Mwendo kasi watu wamelalamika sanaa sio jana .
Ila hawa miungu watu wapo kimya .. Wanawaza jinsi ya kumpiga lisu risasi.
 
watanzania wengine bado vichwa maji...unapandaje gari inayoenda kimara unashuka manzese au mapipa wakati kuna gari za morocco na ubungo na hizo gari haswa za ubungo kwenye terminal zote kivukoni gerezani huwa zinaondoka zikiwa tupu unamkuta mtu anagombania gari la kinara anashuka manzese..mnakera ukiwemo wewe mleta mada...na ni bora gari za kimara zote ziwe express mziogope .

Wewe hata DSM huijui unataka mtu wa manzese apande gari la morocco !!!!! acha watu wa dsm wajadili hoja. Hata hivyo hakuna sheria inayokataza kufanya hivyo. Kama gari ni express dereva aseme mapema kuliko kutangaza njiani.
 
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana, tuna tabia ya kuponda na kudharau kila kitu chetu hatuwezi kuendelea kwa namna hii, hata wale tunaotamani kuwa kama wao, walianza hivi hvi kwa shida.
wako watu wanatamani aje mzungu au tu kampuni yoyote ya nje itoe huduma watalizika, lakini sasa hivi kwa kuwa kuna mswahili mwenzao wanaona kila kitu kibaya, hapana tubadilike maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe kuanza kupenda kujali na kuthamini vya kwetu.
mradi unazo changamoto, ndiyo, lakini hiyo ni hatua ya ukuzi kwa kitu chochote kama ambavyo kila mtu ana changamoto zake za maisha, wakati mwingine tunalalamika kwa ajili ya kulalamika tu, unasema umependa Express mimi ni msafiri mzuri wa usafiri huu, morocco hakuna express, wewe ulipanda ya wapi.
Mwendokasi pamoja na changamoto zake umetusaidia sisi wengine tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali, tuwakosoe kwa haki ili pia waweze kufanyia kazi haya tunayosema, lakini tukiwakosoa kwa matatizo yasiyokuwepo hata kama una nia njema unaonekana mbambasiahaji
Mfano changamoto kubwa kwenye mradi huu ni wingi wa abiria Vs idadi ya mabasi, Hili kila siku tunamabiwa mradi huu uko kwenye mpito, anatafutwa mtu wa kutoa huduma kamili na serikali, sasa kama huduma ziko kwenye mpito mwekezaji wa sasa anawezaje kuwekeza ili aongeze mabasi bila uhakika anakuwa na kazi hiyo kwa muda gani? hili hata waandishi wa habari hawalifanyi wanauliza abiria tu, kila stori ni kulalamika kukaa kituoni muda mrefu, wawafuate serikali waseme wanaongeza mabasi lini?
Acha ujinga wa kudhani watanzani hawana uelewa.

Hizi gari kwa kweli ni unyanyasaji mkubwa umetawala.
Maafisa wa usafirishaji hawatimizi wajibu wao kukidhi matarajio yetu.

Iko siku jiji litakosa usafiri wa umma kitambo kidogo.
 
Huyu jamaa anadhani uzalendo ni kupongeza kila kitu hata kama kinafanywa kimakosa. Mradi huu ulikuwa mzuri sana ila wasimamizi na hawa UDART ndiyo wanaiharibu. Badala ya kuondolea wa dsm adha na kero wenyewe wamekuwa kero sasa.
 
Wewe hata DSM huijui unataka mtu wa manzese apande gari la morocco !!!!! acha watu wa dsm wajadili hoja. Hata hivyo hakuna sheria inayokataza kufanya hivyo. Kama gari ni express dereva aseme mapema kuliko kutangaza njiani.
Hebu ficha ukilaza wako nawewe, hujaona kasema mapipa au manzese, Morocco na Ubungo, Unakurupuka kuja kukosoa badala ya kusoma vizuri.

Au ulienda shule kusomea ujingaa?????
 
Aisee umekula leo? mbona una hasira za mwenye njaaa!
 
Yaitwa mwendokasi,
Huduma ya kughasi,
Hayana msaada nasi,
Kutubania tu nafasi,
Bora kupanda farasi,
 
Wewe hata DSM huijui unataka mtu wa manzese apande gari la morocco !!!!! acha watu wa dsm wajadili hoja. Hata hivyo hakuna sheria inayokataza kufanya hivyo. Kama gari ni express dereva aseme mapema kuliko kutangaza njiani.
mkuu unakurupuka soma vizuri nimetolea mfano mtu wa mpipa na manzese nikasema wamampipa anaweza panda la lorocco na manzese anaweza panda la ubungo ...then unapokuwa mtu mzima ni kujitambua sio kuongozwa kama mtoto embu tumia ata akili zako magari ya unungo mengi haswa apo kivukoni yanaondoka sit hazina abiria ila cha ajabu watu kama ww wansubiri la kimara ili ashuke manzese ...alafu express zote zimeandikwa kwenye display au ujui kusoma mkuu.
 
Tatizo si watanzania tumejaliwa sana kulalamika ukiangalia mambo mengine sisi ndo tunasababisha tukijifanya tunajua sana kumbe upepo tu..sikatai kuna mambo amabayo hayako swa upande wa DART mfano :mabasi kuchelewa kuwasili vituoni mtu anasubiri usafiri mda mwingi..kujaza kupitiliza ...mfumo wa malipo kutokuwa wazi haswa watumiaji wacard na kwatiketi pia usumbufu pia barcode scanner zinafail na kuletea foleni milango ya kuingilia stand. Ila usiniambie wa manzese kupanda gari la kimara tena express na ya ubungo yapo then unakuja kulalamika jukwaani.
 
Back
Top Bottom