Udanganyifu unaofanywa na vituo vya mafuta kuhusiana na risiti za efd

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Leo nimefika kwenye kituo cha mafuta ili kuweka mafuta kwenye gari langu. Walipomaliza kuweka mafuta wakanipa risiti ya EFD na baadaye kama kawaida yangu nikaipitia ili nisome kilichoandikwa.

Nilipoisoma nikakuta imeandikwa jumla ya fedha nilizonunulia mafuta na kuacha kuandika idadi ya lita nilizonunua.

Nilipochachamaa ndipo wakanipa risiti iliyoandikwa idadi ya lita nilizonunua na idadi ya hela nilizotoa. Mimi nadhani kuna tatizo.

Mteja anatakiwa apewe risiti inayoonyesha idadi ya lita ulizonunua na jumla ya fedha alizonunulia mafuta.

TRA mnatakiwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza juu ya kasoro hizi.
 
Back
Top Bottom