Ricky Blair
JF-Expert Member
- Mar 13, 2023
- 391
- 873
Ifike muda udikteta tu uje na kuwaondoa hawa madalali kwa nguvu hata km damu ikimwagika coz imezidi. Mtu hata raha huna ni harassment daily tu hata uwe na tiketi yako au la kwenda mikoani. Na pia ifike muda sio kila basi lipewe leseni ya kusafiri km halikidhi hadhi. Unakuta kampuni km 100 98 zote utumbo; na kila kampuni marufuku hao madalali; mtu ofisi naiona bado mimtu inakuja kunisumbua? Maana yake nn labda??na yote yanatoa ahadi ambazo mabasi hayana? Kwanini hawa watu serikali wanawaacha watusumbue sisi tu? Kwanini msiwapeleke Airport tuone wawasumbue na nyie; ethiopian airlines uku Qatar airlines uku tuone km kuna mgeni wa maana atashuka Dar airport. Na kila basi even luxury yamegeuka makosta jaman hata ham ya kusafiri mkoani sina. Bora niweke budget nipae tu yaani ukiachana na Abood na Shabiby na Tahmeed yote yaliyobaki ni utumbo tu. Hawa watu waondolewe jaman na wakatazwe kuwepo kw stend km hamna cha maana wanafanya stend kubwa zilizowekewa mageti km Mbezi Luis na zingine.