Uchunguzi: Chanzo cha matatizo katika sekta ya Umeme Tanzania na ujio wa IPTL

Jason Bourne

JF-Expert Member
May 11, 2011
200
438
Baada ya kuwa kwenye mgogoro wa umeme nchini Tanzani yapata miaka karibu 15 sasa, nimeamua kufuatilia hasa tatizo lilianzia wapi na nani waliohusika.

Nilianzia ndani ya Wizara ya nishati na madini kwa kufuatilia mikataba iliyoyaingiza nchini makapuni ya uzalishaji umeme,

Taarifa halisi na nyaraka zinabainisha kuwa tatizo hili lilianza baada ya mfanyabiashara maarufu bwana Rugemalia kuiingiza nchini kampuni ya IPTL kutoka Vietnam!

Mchakato unatajwa kuwa ndugu Rugemalila alikuwa akifanya biashara ya Mchele kutoka Vietnam mwaka 1995, katika harakati zake za kibiashara huko Vietnam aliweza kuunda urafiki na wanaotajwa kuwa wamiliki wa IPTL hii ya sasa.

Mwaka 1997 kulianza kutokea uhaba wa umeme tanzania ambapo ndani ya Wizara ya nishati na Madini kulipendekezwa itafutwe kampuni itakayozalisha umeme wa dharula wa haraka zaidi ili kunusuru taifa:

Kamishna wake alikuwa ni Ndugu Patrick Rutabanzibwa ambae katika uchunguzi umebaini ni ndugu na Rugemalila ambae ni mfanyabiashara na mmiliki wa Mabibo Heineken ya Ubongo,

Baada ya Rutabanzibwa kuona kuwa pale wizarani kuna mwanya wa kupiga hela aliweza kuongea na mdogo wake ambae katika nyaraka nyingi anatajwa zaidi kwajina moja tu la Rugemalila kuwa atafute kampuni ya kufanya kazi hiyo haraka sana!

Rugemalila bila kusita akawashtua washikaji zake ambao taarifa kutoka Vietnam zinasema waliokuja si wale waliokuwa na urafiki na Rugemalila bali ni marafiki wa marafiki wa Rugemalila kutoka Malaysia.

Na hawakuwa na sifa ya kiushawishi ya kufanya mradi wa kimataifa ingawa waliweza kushirikiana pamoja bila tatizo kwakuwa yalikuwa ndio malengo yao ya pamoja!

Makubaliano ya mkataba ilikuwa ni mashine zitakazoletwa na IPTL, zitakuwa na mfumo wa kutumia gesi na mafuta, hilo liliingizwa katika makubaliano ya mkabata kwakuwa tayari kulikikuwa na mradi wa songas uliokuwa ukiendelea kujengwa .

Katika uchunguzi ulioenda sambamba na mahojiano ya kijasusi, bwana Rutabanzibwa anasema miezi miwili baada ya kusaini mkataba ule alishangazwa kubaini kuwa IPTL inaleta mitambo inayotumia mafuta tu na alipouliza wasaidizi wake wakamuambia mkataba unasemaje? Akaamua kwenda kuangalia upya mikataba aliyohusika na yeye kuisaini lakini anasema "nilishangaa kuona kipengele kilichokuwa kikisema kuwa genereta hizo zitakuwa na uwezo wa kutumia gesi kimetolewa" nakuwa generata za mafuta mazito tu.

Baada ya kupandishwa nakuwa Katibu mkuu, anasema "nilizuia kuletwa kwa mitambo hiyo kwakuwa nilizungukwa na kubadilishiwa mkataba feki"

Uchunguzi umebaini Bwana Rutabanzibwa hakuzuia ama lengu la kuzuia halikutimilika na alihongwa!

Ukweli unabainika katika dokezo la 12/6/2001 toka kwa JK (rais sasa) likiwa limeandikwa kwa mkono na kalamu ya wino mwekundu "Kama nilivyokuahidi jana katika kikao chetu, waambie wailete hiyo mitambo kama ilivyo na mimi nitafanya kama tulivyokubaliana" chini ikasainiwa J Kikwete

Licha ya hivyo bado uchunguzi unazi kubaini ushirika wa karibu wa Jakaya Kikwete na mtu anaetajwa kuwa ni Rugemalila anaeonekana alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa Rutatabanzibwa na wavietnam wa IPTL.

Kwakuwa baada ya kufuatilia kwa kina imegundulika kuwa katika account ya bank (CRDB) ya biashara ya mchele ya Rugemalila, kila mwezi kiasi cha pesa Shilingi milioni 130 kilikuwa kikihamishwa kwenda kwenye account mbili tofauti lakini za mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Asha Salum Mohamed mkazi wa Arusha mjini,

Jambo la kuvutia zaidi nikuwa pesa hizo zikifika kwenye hizo account zilikuwa zikitolewa ndani ya masaa 48, na kuingizwa kwenye akaunti ya ya Abas Zuberi Musa (NMB) na hapo hutolewa siku hiyohiyo (Cash) na kupelekwa mojakwa moja katika akaunti ya siri ya Rais Jakaya kikwete iliyopo Standard Chartered Bank,

Abas Z. Musa kwa sasa ni mmoja wa usalama wa taifa watiifu kwa rais Jk na anaaminiwa sana kwa mambo binafsi ya rais!

Huo ndio ushikiano wa JK na Rugemalila katika biashara ya mchele,

Bado naendelea kufuatilia kwa undani kujua mambo makuu mawili kwanza:

(1) Kwanini aliamua kufanya biashara hiyo ya mchele kwa siri na kuchukua faida kwa siri kubwa hivyo?

(2) Iwapo Jakaya Kikwete alihusika moja kwa moja au kwa aina yoyote ya biashara ya IPTL

Nitafanya uchunguzu huu kwa undani na kujua nini hasa kipo kwenye tatizo la umeme Tanzania, ninaanza na IPTL kisha wengine watafuata!

Kwasababu za kiuchunguzi nyaraka sitaziweka hapa mpaka uchunguzi ukamilike wote!
 
Ukweli unabainika katika dokezo la 12/6/2001 toka kwa rais likiwa limeandikwa kwa mkono na kalamu ya wino mwekundu "Kama nilivyokuahidi jana katika kikao chetu, waambie wailete hiyo mitambo kama ilivyo na mimi nitafanya kama tulivyokubaliana" chini ikasainiwa J Kikwete

Chifu Jason bourne, hapo juu sijakuelewa vizuri. Unamaanisha Kikwete ndiye aliyesaini kama rais tarehe hizo? Kikwete si amekuwa rais toka mwaka 2005?!

Ebu fafanua hili chifu kabla haujaendelea na uchunguzi wako.
 
Last edited by a moderator:
Chifu Jason bourne, hapo juu sijakuelewa vizuri. Unamaanisha Kikwete ndiye aliyesaini kama rais tarehe hizo? Kikwete si amekuwa rais toka mwaka 2005?!

Ebu fafanua hili chifu kabla haujaendelea na uchunguzi wako.

Alikuwa Waziri nimeweka mabano kuonyesha sasa ni rais!
 
Last edited by a moderator:
Chifu Jason bourne, hapo juu sijakuelewa vizuri. Unamaanisha Kikwete ndiye aliyesaini kama rais tarehe hizo? Kikwete si amekuwa rais toka mwaka 2005?!

Ebu fafanua hili chifu kabla haujaendelea na uchunguzi wako.
alikuwa mambo ya nje na kuna kipindi alikuwa waziri wa nishati na madini.
DHAIFU
 
Pongezi kwako mkuu, inahitaji utulivu na ufuatiliaji wa hali ya juu kupata hizi habari. Ama kwa hakika Kikwete kaanza mbali na hii nchi na sembuse katika kila kitu either cha faida au hasara nchini kina mkono wake. Kila la kheri mkuu
 
Jason, kwani IPTL siyo ya Malaysia?

Kuna mkanganyiko mkubwa hapo mkuu, kwenye nyaraka za majadiliano wanatajwa kuwa ni wa Vietnam, watu halisi waliopo sasa ni wa Malaysia, sasa sijui nani wahusika walio kwenye nyaraka au waliopo sasa?
 
Karibu tena JB. We missed u. Hasa kwenye thread za kiintellegencia. Songa mbele ninakuaminia sana. Muda si mrefu Tanzania itarudi mahala pake mara baada kila lililo chini ya kapet litakuwa linawekwa juu kweupe
 
Aminia sana JB, ukimaliza hili tupe majina ya walioweka hela zetu huko duniani kwa siri. Hii habari ya muuza mchele na IPTL si ngeni akilini mwangu nilishaisikia. Thanks again JB. Jamani tuichangie JF iendelee kuwepo coz itatupa majina ya wezi wetu wote ili wakati wa kuichukua iwe rahisi na kunyonga mmoja baada ya mwingine. Big JB
 
JK mwizi, fisadi. Kumbe udhaifu wake unatokana na madudu haya hawezi kukemea wakati na yeye ni mwizi
 
Karibu tena JB. We missed u. Hasa kwenye thread za kiintellegencia. Songa mbele ninakuaminia sana. Muda si mrefu Tanzania itarudi mahala pake mara baada kila lililo chini ya kapet litakuwa linawekwa juu kweupe
Nashukuru tupo wote ndugu usiku na mchana tuna ipigania nchi yetu!
 
Bila jf haya ningeyapata wapi? Hakika mungu umeileta jf ije kulikomboa taifa letu!
 
Back
Top Bottom