AlP0L0
JF-Expert Member
- Apr 23, 2011
- 6,114
- 4,371
Sasa kama ni ukweli unataka wakanushe nini?Mojawapo ya chanzo cha matatizo katika nchi changa no ubaguzi ambao huasisiwa na wachache ,husasan Tabaka Tawala / Wassomi kwa malengo ya Kimkakati.
Nchi yetu Ina bahati kidogo ,kuwa iliwekwa msingi ya kpunguza visabqbishi ikiwemo ,ubaguzi wa kiimani,kmakabila au wa kijiografia!
Kwa kuwa tabia hizi ni za kibinadamu hazijaisha kabisa!
Kuna Mwandishi mmoja wa Historia anaitwa Mohamed Said .Mwandishi huyu no maarufu Sana kwa kuandika Historia ya Tanganyika na Zanzibar.Na kwa mujibu wake ,yeye huandika Historia ambayo anasema ..ilifichwa,makusudi .
Hapa nitatoa mifano ambayo Mwandishi huyu anaandika ambayo inaweza kuleta chuki na mtafaruku katika jamii!
Awali,amebainisha Histori ya TANU,haiwataji baadhi ya Waislam,ili kuficha jitihada za Waislam kudai Uhuru wa Tanganyika! Sijawahi kusikia au kuona hili likikanushwa!
Pili,anaandika na kusisitiza kuwa Wizara ya Elimu,imekuwa ikitumia Uwiano wa 20:80 ktk kuchagua Wanafunzi Kidato chakwanza...hapo 20 ni Waislam!
Mwisho,hivi karibuni amehoji uhalali wa Gaudensia Kabaka kuwa Mwenyekiti wa UWT CCM!,ilhali yeye, alizuia ujenzi wa msikiti na kuwanyanyasa Waislam Chuo Kikuu Cha Dodoma!Kuwa inakuwaje huyu anaioghoza Taasisi iliyoasisiwa na Waislam kina Bibi Titi!?
Bahati mbaya kwangu,sijui uhalali wa shutuma hizi.Ila ni shutuma kubwa ambazo zinalenga kupandikiza chuki!Hapa zijazungumzia mtazamo wake kuwa Nyerere alipokelewa na kutunzwa na Waislam akitokea Bara na akaja kuwa tenga!
Swali langu ni je,inakuwaje wauhusika wanafumbia macho uandishi huu! Kukaa kimya ni kumpa kibali na wasomaji wake tumuamini!
Madhara yake ni makubwa!
Tafadhalini wahusika Serikali,CCM msiache kulizungumzia makala hizi ambazo Mimi huzisoma hapa Jamii Forum!