UCHIZI katika Nchi: Kauli ya Mch. Gwajima...

Maneno yakishatamkwa hayarudi tena kinywani.Hakika ujumbe umefika kwa wahusika na umepokelewa.
 
Mi tatizo la wingi wa watu halinisumbui sana. Lakini kinachonisumbua ni huo mfumo wa nusu kwa nusu walioanzisha. Mtu anaweza kujiuliza, hivi baada ya kukubali hasa sisi watanganyika kutungwa kwa sheria mbovu hii ya mchakato wa katiba, tutakuja kukataa tena, kama Wazanzibar wakitaka kwenye katiba Mpya kila kitu cha Muungano kiwe nusu kwa nusu? Mchakato huu wa Katiba umejengwa kwenye falsafa mbaya sana. Hatuwezi kuja kukubali siku wakisema, wabunge iwe nusu kwa nusa, wizara pia iwe pasu kwa pasu, idara zote iwe pasu kwa pasu. Hii ni mbaya kuliko zote. Wabunge wetu ni hatari sana kwa nchi yetu.
 
Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo ili mradi havunji katiba wala kuhatarisha amani. Muungano unajadilika toka zamani umeshasikia mambo ya G55? sio dhambi hata kidogo. Kuchoma makanisa na kufanya fujo sio kutoa maoni ni kuhatarisha amani tunahitaji nguvu kubwa sana kukuonyesha tofauti? Hizi dini zipo tu tena nyingi sio za asili ya Afrika nashindwa kuelewa kwa nini mpaka leo tunazishabikia na kusahau utu na ustaarabu wa Mwafrika. Bado tuko utumwani.
 
"Kipande cha nchi Chenye idadi ya wakaazi Milioni Moja Tu Kinaungana na Kipande kikubwa cha nchi chenye zaidi ya watu zaidi ya Milioni arobaini na Tatu, halafu vipande hivi viwili vinakuwa na Nguvu sawa kwenye Kuunda Hatma ya Nchi (Katiba), Huu ni Uchizi.. "Mch Gwajima, Sunday speech Leo.

.
Viongozi wa dini mlimpigia debe JK kuwa ni chaguo la Mungu. Kweli ni chaguo la Mungu kwa kusudi hilo. CHLOROQINE ANAZOWAPA ZIMEZENI HUKU MKIWA MMEINUA MIKONO JUU NA KUMSHUKURU MUNGU KWA MAJI HAYO YA UCHUNGU.
.
 
afanye maombi( kama ilivyo kawaida yake) ili amfufue mwalimu JK NYERERE halafu amuite chizi kwa KUTENGENEZA MUUNGANO HUU TULIONAO SASA....... other wise uchizi anaouongelea anamtukana baba wa taifa letu.
craaaaaap
Hivi maana ya baba wa Taifa ni nini. Mbona mimi sio Mzanaki. Mimi nina baba yangu. Sitaki kumdhalilisha mama yangu. Ukome kunihusisha mimi.
 
UAMSHO wakisema hawataki muungano wanafunguliwa kesi za kuhatarisha usalama wa nchi! Mchungaji akisema, serikali inapiga makofi. Kweli mfumo kristo unafanya kazi yake mchana kweupe ndani ya serikali.

Hapa ndio mnapobadirihs maneno, kwani Uamsho wamefunguliwa kesi kwa kukataa Muungano? hivi sheikh Faridi si alijifucha then akadai katekwa na tukio hilo likasababisha mauaji? msipende kubadisha maneno, sometimes huwa mnaidhalilisha hata dini ya Mnyazi mungu kwa kutetea vitu kwa uongo, walifanya mikutano yao mingi tu ya kuukataa mungano hakuna aliyewachulia hatua, walipoaanza kuratibu mauaji na kujificha then unasababisha taharuki, serikali yeyote iliyo makini lazima ichue hatua, kama Na huyu Mchungaji nae ikitokea kaamrisha waumini wake wafanye fujo na pengine hata kuua raia wasio na hatia au hata kuamrisha kuchoma misikiti then serikali hiyo hiyo ikakaa kimya dhidi yake hata mimi nitakua wa kwanza kusema, serikali inapendelea! Maneno ya Mchungaji Gwajima yana ukweli sana tu.
 
Maneno ya Mchungaji Gwajima ni ukweli mtupu, lakini arudishe kadi ya machizi.
 
Huyu si ndiye aliyeuumbua KOVA na utesaji wa Ulimboka na sasa tena kaja na jambo kama hili ..Huyu ni another Fr. Mapunda. Refer: "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko" misingi ya TANU ndiyo inamuongoza Gwajima nini? ahahaaaaaaa.
 
Huyu si ndiye aliyeuumbua KOVA na utesaji wa Ulimboka na sasa tena kaja na jambo kama hili ..Huyu ni another Fr. Mapunda. Refer: "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko" misingi ya TANU ndiyo inamuongoza Gwajima nini? ahahaaaaaaa.
Hivi KWANINI watawala hawataki ku-face the reality wanayoiona?
 
Back
Top Bottom