Ucheshi wa mzee Mwinyi: Sukari imeingia sumu

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,335
24,229
images.jpeg
Tutamkumbuka mzee wetu Ally Hassan Mwinyi kwa kulielezea tatizo kubwa lililoathiri wengi, AIDS au UKIMWI.

Katika kuliekezea tatizo hilo, Mzee Mwinyi alitumia lugha rahisi iliyoeleweka kwa kila mtu: SUKARI IMEINGIA SUMU🤣🤣🤣🤣

"Sukari imeingia sumu, hasa pale tunapo ppp...papenda" alisema mzee Mwinyi

Enzi hizo ndo sukari iliingia sumu.

Watanzania nia wezangu sukari imeingia sumu. Kauli ya Mzee wetu Ally Hassan Mwinyi
 
1) Wa Morogoro kazaneni kwenye mihogo, Wahaya kazaneni kwny migomba, Wa Pemba …kwenye mikarafuu

bila ya kukazana hili baa la njaa halitotuacha salama

2) Vijana wanasema Nzi kufia dondani ( kwenye kidonda) ndio ada ( desturi ) yake

Mh. Rais Samia leo kasema walipokuwa kwny matembezi ya pale Leaders baada ya matembezi alihojiwa Mzee Mwinyi siri ya ukakamavu, akajibu jibu mara sijui mazoezi, sijui vyakula lakini akaomba aende chemba pembeni kidogo awaeleze vijana wa kiume …mie nimehisi kwa uungwana na ustaarabu wake kuna maneno alitaka kushauri vijana wa kiume akashindwa kuyaongea mbele ya kina Mama

kama kuna Mwandishi alienda chemba na Mzee itabidi atupe siri hiyo
 
Alishangaa sana kuona watu wa huku bara wanavyopora pesa nyingi za umma.

Akasema "kule kwetu Zanzibar ukisikia mtu keba (kaiba), ....keba ndala msikitini, keba mtandio harusini. Lkn huku bara ukisikia mtu keba, .....keba mabiliooooni ya fedha". (Lafudhi ya kizanzibari).
 
Back
Top Bottom