Uchaguzi 2020 Uchambuzi wangu katika ufunguzi wa kampeni wa vyama vikuu vitatu, CCM, CHADEMA na ACT Wazalendo

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
UCHAMBUZI WANGU KATIKA UFUNGUZI WA KAMPENI WA VYAMA VIKUU VITATU,CCM,CHADEMA NA ACT WAZALENDO.

Leo 12:50hrs 30/08/2020

Miaka yote ya uchaguzi Mkuu,Wapinzani walitambaa na kashfa za ufisadi kama ajenda yao kuu ya kuwaambia Watanzania,utakumbuka kashfa ya Ufisadi wa Kagoda,Meremeta, Epa,2005 kashfa ya Ufisadi wa Richmond 2010,kashfa ya Escrow 2015,hizi ndio zilikuwa ajenda zilizobebwa na Chadema ya Daktari Wilbroad Slaa,CUF ya Profesa Ibrahim Lipumba,na Nccr Mageuzi iliyokuwa ya Augustino Lyatonga Mrema.

Safari hii mambo yamekuwa magumu kwa Chadema,Act Wazalendo na wapinzani wote kwa kuwa ajenda yao kuu ya Ufisadi,imefanyiwa kazi na Rais John Pombe Magufuli,na sasa hakuna Ufisadi kabisa,hivyo kuwawia vigumu wapinzani kuendesha kampeni zao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2020,Rais John Pombe Magufuli alichukua ajenda zao zote na kuzifanyia kazi,hivi sasa nchi inasonga mbele,

Uchaguzi wa Mwaka huu 2020 Ndugu Tundu Lissu Mgombea wa Upinzani kupitia Chadema,hana hoja tena ya Ufisadi,Ndugu Tundu Lissu anahutubia Mambo yake binafsi kwenye kampeni,anasema "Nina damu ya Kenya na Ubeligiji,Mimi ndie mgombea wa uraisi ninaeongoza kua na kesi nyingi mahakamani na hivyo nimeweka rekodi,Tutaandamana Nchi nzima,Mwaka huu sitamuachia Mungu,corona ipo kwa sababu Wakenya wanakaa ndani ya nyumba zao,

Naomba Ndugu wananchi na wanachama wa kweli wa chadema tukichangie chama chetu kwa ajili ya kampeni za uchaguzi huu,Mwili wangu una vyuma,mwili wangu bado una risasi,Magufuli ni dikteta,Mimi ndio nilijaza form ya uchaguzi vizuri kuliko wagombea wote,Walikataa kunichangia hela ya ndege ya kunipeleka Nairobi, Ahsanteni hapa ndo tumefika mwisho wa mkutano wa kampeni zetu kwa Leo".

Kiukweli ni wazi Chadema haijajipanga vizuri kuanzia namna ya kuelezea sera na ilani ya chama mpaka mapokezi wanayopata katika uzinduzi wao,muda mwingi Mgombea wa Chadema analalamika,anatumia muda mwingi kuelezea vitu ambavyo havina maana,mfano wahuni anaowahutubia wakipiga kelele anakatisha hotuba anaanza kuwaeleza jinsi dunia inavyojua yeye kuitukana Tanzania,

Anaanza kueleza Tanzania itafungiwa misaada na na wazungu,Ndugu Tundu Lissu bado anawaza kutegemea wazungu tu,mpaka sasa haijulikani sera na ilani ni zipi baada ya Ndugu Tundu Lissu kutumia muda mwingi katika uzinduzi kumwaga lawama kwa Serikali, kulialia jukwaani kwa fouls walizofanyiwa wabunge, kufukuza media, kutafuta sympathy kwa kuonesha makovu yake akivua suruali na kuonyesha mguu,Ndugu Tundu Lissu ameshindwa kabisa kutuliza hisia zake binafsi,amekuwa kama mgeni katika taifa lake akielezea kufanya vitu ambavyo tayari Rais John Pombe Magufuli ameshavifanya,mfano kuondoa kodi za mizigo ya Wakulima barabarani,

Ukiangalia upande wa CCM na Mgombea wake Ndugu John Pombe Magufuli ni wazi wamejipanga vyema sana,Ndugu John Pombe Magufuli amepanda jukwaani na kwenda moja kwa moja kwenye kueleza mengi yaliyofanywa na Serikali yake,ujenzi wa vituo takribani 450 vya Afya, miundo mbinu ya barabara akiboresha na kujenga nyingine za njia nane,akielezea alivyojenga reli ya Umeme itayopunguza masaa ya safari Dar-Morogoro saa moja,Dar -Dodoma masaa mawili,Dar-Tabora masaa matatu,Dar -Mwanza masaa sita,

Katika anga akielezea ununuzi wa rada kubwa tano,kumbuka Miaka ya nyuma tulinunua rada moja tu ikatuletea mzozo wa Ufisadi mkubwa hadi waingereza kuamua kurudisha pesa,Ununuzi wa ndege kubwa kumi,Boeing,Airbus na Bomberdier,nidhamu makazini, namna nzuri ya kudhibiti public panic katika janga la corona tofauti na Chadema waliokuwa wanataka tujifungie ndani tufe na njaa,

Ndugu John Pombe Magufuli ameeleza alivyoweka mifumo mizuri ya ukusanyaji kodi na kuwa msimamizi mzuri wa kodi za wananchi, kupungua kwa gharama za nishati ya umeme, kudhibiti ufisadi na matumizi mabovu ya kodi zetu na mengine mengi,na pia akimaliza hayo huanza kuelezea nini atakifanya kwa miaka mingine mitano,kwa ufupi CCM wana mtiririko mzuri unaoleta ladha katika presentations zao za majukwaani.

Matukio mawili ya ufunguzi wa kampeni za Chadema pale Mbagala na Kawe jijini Dar es Salaam zinaonesha Chadema hawajajiandaa, hawakujipanga, hawakufanya maandalizi na wala hawana matarajio na matumaini ya ushindi, wameanza wakiwa wamekata tamaa na wametangaza kushindwa kabla ya kuanza kushindana pengine walimtarajia Ndugu Benard Membe apeperushe bendera yao, Ukiwapima na ukipima mikutano yao katika maeneo yafuatayo utakubaliana nami kuwa Chadema haijajiandaa,

1.Mkutano ulikosa maandalizi, kuanzia watu wa hamasa mpaka wazungumzaji,kila aliyesimama kuzungumza alionyesha wazi kabisa kuwa hakuwa amejipanga kuzungumza katika mkutano mkubwa kama huo wa ufunguzi ambao kimsingi ndio unatambulisha agenda ya Chama kwa wanachama na wananchi kwa ujumla wao.

Kawaida ya siasa za Chadema hutanguliwa na hamasa kubwa katika mitandao ya kijamii, mtaani na katika eneo husika la mkutano. Maeneo yote hayo hakukuwa na hamasa ya aina yeyote tofauti kabisa na ilivyokuwa Mwaka 2015 pale Edward Lowassa alipopeperusha bendera ya Chadema na kuitikisa CCM balabala huku kampeni zake zikipambwa na helkopta angani na mafuriko ya watu ardhini,

2.Idadi ndogo ya wanachama waliojitokeza kuhudhuria.
Labda kutokana na kukosekana kwa hamasa watu wachache sana walijitokeza katika viwanja hivyo ambapo imeonyesha kuwa kama vile watu wameupuuzia mkutano huo,Siku ya Mkutano wao wa ufunguzi Mbagala, eneo la Mkutano
Mbagala ni eneo la wakazi waislamu na kwa siku ya ijumaa kwa waislam inajulikana kuwa ni siku ya ibada,wameitenga siku hiyo kwasababu ni siku yao ya ibada na kwamba wanajipa mapumziko yasiyo rasmi katika kazi na shughuli zao,Sasa timing ya Chadema ilikosea kupanga mkutano huo kwa siku hii ya leo na eneo hilo.

3.Chadema wameifukuza TBC1 hivyo kufanya nafasi ya vyombo vya habari kuhudhuria mikutano yao kuwa finyu sana hasa baada ya maamuzi yao ya kuifukuza tbc katika mkutano wake,Chadema wamekataa kabisa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kulifanyia branding tukio lao na kulipa vibe ambayo ilitegemewa, matokeo yake Mwenyekiti ndio kaharibu zaidi baada ya kuituhumu TBC kuwa imekata matangazo.

4.Hotuba ya Mgombea
Katika siku kubwa kama ya uzinduzi hautakiwi kuzungumza vitu vyako binafsi, ni siku ya kuja kuwaeleza Watanzania nini Chadema imepanga kufanya sio siku ya kuja kusimulia matukio ambayo kwa miaka mitatu watu wamekuwa wakiyasikiliza,Wahuni ambao walikuwa wamekaa mbele wanapiga mayowe na kumfanya Mgombea akate hotuba na kuanza kujiambukiza kwao ili watulie na kuanza kuzungumza nao,hili nalo limepoteza muda wao wa kuongelea sera zao,

5.Nafasi ya wasanii na watu wa kutoa hamasa,
hakukuwa na msanii yeyote wa maana ambapo kwa mbagala wangeweza kutafuta waimba singeli hata watatu tu wangetosha kuongeza idadi ya watu na kuupa mkutano vibe linalostahili wao wamepiga taarabu,na mwisho kabisa,kuutumia Mkutano wa Ufunguzi kama sehemu ya tukio la fundraising,ni ujinga uliopindukia kuutumia mkutano ule kufanya fundrising badala ya kunadi sera, wakati huo kwa miaka mitano Mwenyekiti Mbowe amekuwa akikusanya milioni ya wabunge kwa kile alichokiita Mfuko wa Uchaguzi.

Nimalizie kwa kusifu mpangilio wa CCM katika kampeni zake zinazokonga nyoyo za watanzania,nipongeze chaguo la CCM,Rais John Pombe Magufuli ndiye mwenye kuongelea hatma ya kizazi cha Watanzania leo,kesho na kesho kutwa,kwa hakika Ndugu John Pombe Magufuli is the right presidential candidate who doesn't talk about personalities, but talks about the future generations of our beloved country Tanzania and for sure I can tell, has all the qualities of a good leader that we,Tanzanians supposed to have,

Lakini pia niungane na wana Chadema na Act Wazalendo kuwaomba wagombea wao wajikite kwenye kueleza sera na kutangaza ilani yao ya Uchaguzi,Mgombea wa Chadema Ndugu Tundu Antipas Lissu atumie muda wa kutosha angalau kati ya masaa mawili au moja na nusu kuchambua, kueleza na kunadi kinaga ubaga sera zinazobeba ilani ya chama.

Mgombea wa Act Wazalendo,Ndugu Benard Membe atumie muda mwingi kunadi sera za chama chake cha Act Wazalendo kujenga ushawishi na wananchi kuelewa kwa kina juu ya nini Ndugu Benard Membe amekusudia kuwafanyia endapo atapata ridhaa ya kuwaongoza 2020 -2025,nategemea pia kuona helkopta angani zikipambwa na bendera ya Act Wazalendo na picha za Ndugu Benard Membe,unogeshaji huu ukiwa sehemu ya kazi na bata.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Mbona Lissu ameshaihidi mengi
1.Kuboresha vipato vya watumishi wa umma
2.Kufuta kodi zinazofanya mazingira ya uwekezaji kuwa magumu
3.Kufuta idara ya maelezo
4.Suala la bima ya afya
5.Suala la kubadilisha mitaala ya elimu iwawezeshe watu kujieleza na kuhoji
 
EBU NIWAULIZE BAVICHA MNAHISI TUNDU LISSU ATAWAFANYIA NINI WATANZANI AKIBAHATIKA KUCAHGULIWA KUWA RAIS WA TFF MAANA URAIS WA TANZANIA NI WA MAGUFURI
 
Hakuna mpinzani Tanzania Bali Kuna wajasiriasiasa na wengine Ni mawakala wa wazungu (chadema/ACT)
 
.
FB_IMG_1596790033084.jpg
FB_IMG_15917747988552743.jpg
 
Rule against bias
Halafu una masters degree ndiyo Yale aliyoyasema lissu Jana kwenye kampeni kawe kwamba ubora wa elimu yetu uko chini.
 
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Yaa wengi wameenda shule ila walioelimika wachache sana. Huu ni uchambuzi wa mtu aliyeenda shule ila si msomi.
 
Hakuna mpinzani Tanzania Bali Kuna wajasiriasiasa na wengine Ni mawakala wa wazungu (chadema/ACT)
Wewe endelea kuharisha,ila lililo wazi kabisa ni hili
1.Kamati ya ccm na halmashauri yake,
2.Balaza la mawaziri na mwenyekiti wake,
3.Raisi Magufuli akiwa mwenyewe
4.Mahakama
5.Polisi na Majeshi mengine yote wanajua upinzani nchini upo tena mkubwa ingekuwa sio hivyo basi ccm isingefanya sarakasi zotee kupinga rasimu za katiba mpya,wala msingewabana wapinzani na vyombo vya habari na kuwanyima uhuru
Sasa mmekuja na mbinu mpya mliyoitumia wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa Engua Engua wapinzani nchi nzima hadi aibu hiyo ndio habari ya
mjini ninyi ni waogaa lakini wewe kwa vile ni Kalumekenge huwezi yaona haya wambie waache Figisu na kuiba kura kiukweli mna mambo mengi sana ya hofu kila ukiwepo uchaguzi hamjiamini.
 
Mbona Lissu ameshaihidi mengi
1.Kuboresha vipato vya watumishi wa umma
2.Kufuta kodi zinazofanya mazingira ya uwekezaji kuwa magumu
3.Kufuta idara ya maelezo
4.Suala la bima ya afya
5.Suala la kubadilisha mitaala ya elimu iwawezeshe watu kujieleza na kuhoji
Hawezi ona yote hayo ndio maana ameweka bango reeeefu halafu hamna kitu!!
 
Back
Top Bottom