MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 705
Waungwana,
Leo ninakuja kwenu (iwapo nitakuwa nimekosea mnikosoe), kwa mara ya kwanza kabisa, nikichambua undani wa Wabunge wa CCM kuikataa bajeti ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwaka wa Fedha 2009-2010, kama ifuatavyo.
Sasa kama yatatokea haya kesho, msiulize nimeyajuaje. Hakuna aliyeniambia. Ni tafakuri jadidi yangu ndio imenifikisha kufikia "uchambuzi" huu. Kama kuna mwenye maoni tofauti, naye anaombwa kuchangia.
Naomba Kuwasilisha!
Ahsanteni!
./Mwana wa Haki
Leo ninakuja kwenu (iwapo nitakuwa nimekosea mnikosoe), kwa mara ya kwanza kabisa, nikichambua undani wa Wabunge wa CCM kuikataa bajeti ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwaka wa Fedha 2009-2010, kama ifuatavyo.
- Nyote mnaelewa jinsi CCM ilivyogubikwa na kashfa nyingi, kuanzia Richmond, Meremeta Gold, Tangold, Kagoda, na EPA. Washauri/wabunifu/spin doctors wa CCM wakafanya tathmini na kubaini madhara ya muda mrefu na muda mfupi wa kashfa hizi zote, wakaona, bora waonekane kwamba "wanawajibika" kuliko kukaa kimya kabisa na kuyaacha mambo yaende kama yalivyo kwa sasa.
- Kuwajibika huku kulianza kwa Wabunge "machachari" kuanza kutoa taarifa mapema kwenye vyombo vya habari, siku chache kabla ya Mkutano wa Bunge kuanza, wakidai kwamba Bajeti hii imejaa "upendeleo". Hata kama madai hayo yalikuwa kweli, je, haupo uwezekano kwamba bajeti "ilipangwa vibaya" kwa makusudi, ili umma uone kwamba Wabunge wa CCM wanapigania maslahi ya umma, na si maslahi yao na ya chama chao?
- Kwa hiyo basi, kinachoendelea sasa ni kwamba, kwanza, leo mchana, majira ya saa saba, kulikuwa na Kikao Maalum cha Wabunge wa CCM, kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa, Jijini Dodoma. Tetesi za Dodoma zinasema kwamba "Wabunge wa CCM wamewekwa sawa" kwamba waikatae bajeti, ili Bunge livunjwe, wao wakiwa wamepata "ushujaa" wa "kuwatetea" wananchi, kwa "kuwajibika".
- Kesho jioni, Bunge likivunjwa, Uchaguzi Mkuu utaitishwa mapema zaidi kuliko ilivyo kawaida, CCM ikiwa inaonekana kupata ushindi wa kishindo, kwa kutumia "gia" ya "uwajibikaji kwa wananchi", hivyo kupata nafasi ya kukubalika, huku nyuma, kashfa zote za ufisadi zikiwa zimewekwa kando.
- Je, Wananchi wa Tanzania ni wasahaulifu kiasi hicho kwamba wataweza kuzisahau kashfa za Richmond, Meremeta Gold, Tangold, Dowans, EPA na nyinginezo (hata DECI....), kiasi cha kuwakubali Wabunge wa CCM ambao wanaonekana dhahiri kwamba "watacheza kiinimacho" ifikapo Alhamis, Juni 18, 2009?
- Je, kwa kuvunja Bunge kwa sababu ya "kuikataa bajeti", Wabunge watakuwa "wamewajibika" kweli kwa Wananchi, ama ndio "si hasa" yenyewe? Ni lini Wabunge "waliwajibika" kiasi hiki, mpaka kufikia "kuikataa bajeti"?
Sasa kama yatatokea haya kesho, msiulize nimeyajuaje. Hakuna aliyeniambia. Ni tafakuri jadidi yangu ndio imenifikisha kufikia "uchambuzi" huu. Kama kuna mwenye maoni tofauti, naye anaombwa kuchangia.
Naomba Kuwasilisha!
Ahsanteni!
./Mwana wa Haki