Uchaguzi Wabunge Afrika Mashariki (CCM), Rais Magufuli kweli ni Baba wa Demokrasia

Deo Shy

Member
Oct 18, 2016
98
300
Jana wajumbe wa sekretariate walivujisha majina 18 ya walioteuliwa na CCM kugombea ubunge wa Afrika Mashariki hata kabla ya usahili kufanyika. Kilikuwa kitendo cha kihuni, cha kufedhehesha na cha kutumia jina la Rais vibaya, eti hao 18 ndio Rais anawataka..

Leo asubui baada ya malalamiko hayo kusambaa Rais wetu mpendwa kaamuru wagombea wote 450 wakapigiwe kura na wabunge wa CCM, na washindi 6 kwa maana watakaoongoza kwa kura ndio watakuwa wawakilishi wa CCM hapo tarehe 4.4.2017 na kuchaguliwa na bunge zima.

Hongera Rais Magufuli... Hongera CCM
 
Kipi hasa cha kupongeza hapo?
Kamati kuu(Ambayo kwa sasa Rais ndio kila kitu) kuvujisha hayo majina 18 ya wagombea Au Rais kuamua kwa hasira majina yote 450 kwenda kupigiwa kura?

Nadhani tafsiri ya Demokrasia bado mleta mada hujaelewa. Demokrasia ni uhuru wa kusikilizana, Kupatana, Kuamua na Kuchagua.
 
Jana wajumbe wa sekretariate walivujisha majina 18 ya walioteuliwa na CCM kugombea ubunge wa Afrika Mashariki hata kabla ya usahili kufanyika. Kilikuwa kitendo cha kihuni, cha kufedhehesha na cha kutumia jina la Rais vibaya, eti hao 18 ndio Rais anawataka..

Leo asubui baada ya malalamiko hayo kusambaa Rais wetu mpendwa kaamuru wagombea wote 450 wakapigiwe kura na wabunge wa CCM, na washindi 6 kwa maana watakaoongoza kwa kura ndio watakuwa wawakilishi wa CCM hapo tarehe 4.4.2017 na kuchaguliwa na bunge zima.

Hongera Rais Magufuli... Hongera CCM
Huo wazimu...ina maana hao 450 kila mmoja akipewa dakika 5 kujieleza bungeni na dakika 5 masuali basi hatuchagui hao wabunge mpaka mwakani
 
Angefanya hivyo kabla ya yale majina 18 kuvuja!! Inaelekea kafanya kwa hasira ........... majina 450 kuyapeleka Bungeni siyo mchezo!!

Next time wakitokea 5000 nao atawapeleka!!?
 
Huo wazimu...ina maana hao 450 kila mmoja akipewa dakika 5 kujieleza bungeni na dakika 5 masuali basi hatuchagui hao wabunge mpaka mwakani
Kwenye vikao vyao wabunge wa ccm wanachagua 6 kati ya 450, hao 6 ndio ndio wataungana na waupinzani ndio mchakato utaanza Bungeni.
 
Jana wajumbe wa sekretariate walivujisha majina 18 ya walioteuliwa na CCM kugombea ubunge wa Afrika Mashariki hata kabla ya usahili kufanyika. Kilikuwa kitendo cha kihuni, cha kufedhehesha na cha kutumia jina la Rais vibaya, eti hao 18 ndio Rais anawataka..

Leo asubui baada ya malalamiko hayo kusambaa Rais wetu mpendwa kaamuru wagombea wote 450 wakapigiwe kura na wabunge wa CCM, na washindi 6 kwa maana watakaoongoza kwa kura ndio watakuwa wawakilishi wa CCM hapo tarehe 4.4.2017 na kuchaguliwa na bunge zima.

Hongera Rais Magufuli... Hongera CCM
Mkuu demokrasi ni pamoja na kufuata sheria,kanuni na taratibu ambazo wahusika wamejiwekea. Ikiwa mwongozo ulitaka kwanza kuwe na mchujo wa vikao vya chini na hayo yalifanyika kisha yakatupwa na kiongozi mkuu demokrasi iko wapi hapo? huoni kama maamuzi ya vikao yamepata changamoto? Kuna haja gani siku nyingine kuwa na vikao vya mchujo?
 
Hongera Rais Magufuli... Hongera CCM
Hivi nini maana ya neno hongera. Inaonekana bado sijaelewa matumizi yake hasa yanavyotumiwa na hasa mwanmzilishi wa " thread" hii pamoja na kuwa Kiswahili ni lugha yangu ya kwanza. Nifahamisheni na vipi lina nafasi katika hili.
 
Jana wajumbe wa sekretariate walivujisha majina 18 ya walioteuliwa na CCM kugombea ubunge wa Afrika Mashariki hata kabla ya usahili kufanyika. Kilikuwa kitendo cha kihuni, cha kufedhehesha na cha kutumia jina la Rais vibaya, eti hao 18 ndio Rais anawataka..

Leo asubui baada ya malalamiko hayo kusambaa Rais wetu mpendwa kaamuru wagombea wote 450 wakapigiwe kura na wabunge wa CCM, na washindi 6 kwa maana watakaoongoza kwa kura ndio watakuwa wawakilishi wa CCM hapo tarehe 4.4.2017 na kuchaguliwa na bunge zima.

Hongera Rais Magufuli... Hongera CCM
Unamshadidia JPM, kwa maamuzi ambayo hayana tija, kama kuna leakage unakubali weakness unarekebisha, vinginevyo ukijifanya mbabe wa kutoa maamuuzi ya papo kwa papo yatakugharimu sana, kukiri kosa na kufanya marekebisho siyo mbaya
 
Kwenye vikao vyao wabunge wa ccm wanachagua 6 kati ya 450, hao 6 ndio ndio wataungana na waupinzani ndio mchakato utaanza Bungeni.
Na wakipatikana sita,wanaotakiwa kuwa wabunge wa A.Mashariki ni wangapi?
 
Jana wajumbe wa sekretariate walivujisha majina 18 ya walioteuliwa na CCM kugombea ubunge wa Afrika Mashariki hata kabla ya usahili kufanyika. Kilikuwa kitendo cha kihuni, cha kufedhehesha na cha kutumia jina la Rais vibaya, eti hao 18 ndio Rais anawataka..

Leo asubui baada ya malalamiko hayo kusambaa Rais wetu mpendwa kaamuru wagombea wote 450 wakapigiwe kura na wabunge wa CCM, na washindi 6 kwa maana watakaoongoza kwa kura ndio watakuwa wawakilishi wa CCM hapo tarehe 4.4.2017 na kuchaguliwa na bunge zima.

Hongera Rais Magufuli... Hongera CCM
Kijana unashangilia ujinga,, hapo demokrasia iko wapi hapo? Hivi huoni kabisa kwamba hao waliokuwa wametuhumiwa ndo wataenda kurudi tena hao hao? Mimi ningemsifu kama hayo majina 18 angekuwa ameyafuta kwenye uchaguzi!!
 
Back
Top Bottom