Uchaguzi wa Wanafunzi Kidato cha Tano na vyuo ni kilio kwa Wazazi masikini

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
619
Na Mwl Matete

Siku tatu zilizopita serikali ilitoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo mbalimbali, kilichowastua wengi ni namna uchaguzi huo ulivyofanywa. Wazazi wengi wanalia hasa wale masikini ambao hawana uwezo wa kuwapeleka watoto wao shule binafsi (Private) kidato cha Tano:

1. Miaka yote tangu Uhuru na hata kabla Uhuru uchaguzi wa wanafunzi serikali hutumia selform ambao hujazwa na wanafunzi wenyewe kabla au baada ya kumaliza kidato cha NNE kwa kuangalia muenendo wa mtihani alivofanya. Mara nyingi wanafunzi hujaza hizi form kwa ushauri wa wazazi na walimu.

- Kwenye selform mwanafunzi huchagua tahasusi na vyuo anavyopenda yeye na wanaochagua hutumia machaguo ya mwanafunzi husika. Mwaka huu mambo hayakuwa hivo. Mtoto amefaulu PCB au PCM vizuri tu lkn anachaguliwa HKL kweli? (Mtasema shule za sayansi ni chache)

Lakini haiji akilini mtu amefaulu kwa Chemistry - A, Geography- B na Biology - B lakini anapelekwa kusoma HKL aliopata C-C-C. au amefaulu vizuri HGL lakini anapelekwa kusoma Computer, Physics na Mathematics. Aliomba hio?

2. Kituko kilikuwa kwa wale waliofaulu kwa Division one lakini unapangiwa kusoma Record Management na haukuiomba. Yupo kijana ana Division one points 14 lakini anapangiwa kusoma Hotel Management Singida. Hivi mimi mzazi tulikubaliana na wewe ulioko ofisini hapo Dodoma nataka mwanangu asome uhudumu wa Hoteli?

Mmoja ana Division I.16 amepangiwa kusoma certificate ya Community Development - Tengeru. Mliongea na mzazi wa huyu mwanafunzi akasema anataka mwanae asome maendeleo ya jamii?

Sio kwamba nabeza fani zingine LA hasha Bali kila MTU asomee anachokitaka, mi mwanangu ana kipaji cha kuchora anataka awe msanii wa uchoraji kama Masuod Kipanya na nimejaza selform, wewe unamlazimisha akasome mifugo au Record management kwa nini? Kisa uko ofisini unaamua wewe

- Nimesikitika kuona mwanafunzi mmoja amevaa mabango mengi mwili akilia amepata Div.I-14 amepangiwa kusoma Hotel Management - Bagamoyo

KINACHOONEKANA KWENYE HALI HII

1. Serikali imeona wanafunzi hawaendi kwenye vyuo vyao ambavyo hawatoi ajira na vyuo vingi vinakufa kwa kukosa wanafunzi sasa kilichopo ni kulazimisha wanafunzi waende kwa nguvu

2. Ile tabia ya TCU kula na vyuo vikuu hasa private kuwapangia wanafunzi inahamia vyuo vya kati imeanza baada ya chuma kuondoka. Mwendazake alikataa hii tabia (RUSHWAAAA), aliruhusu kila mwanafunzi asome chuo anachotaka na fani anayopenda! Sasa hivi tunalazimisha wanafunzi wakasomee Hotel Management!!!!

3. Inaonekana vyuo vya kati vimeomba vipewe wanafunzi moja kwa moja kutoka wizarani bila kujali vipaji vya wanafunzi, lengo lao ni kuwa na wanafunzi wengi ili wapate capitation. Wakufunzi wanajali pesa kwa kuuwa vipaji vya watoto wetu. Wizara nao kujali pesa ya asante wanawateketeza watoto wetu

4. Hii ni mbinu chafu ya kuwatengenezea shule binafsi pesa. Tunalazimishwa kwa nguvu kuwapeleka watoto wetu shule binafsi kusoma kidato cha tano. Kwasababu haiwezekani mtoto amesota sana kusoma na kupata Div.I-12 unamwambia akasome Ualimu wa Chekechea - Kasulu TC kisa Mkuu wa chuo kasoma na waziri wa ......

Wazazi wasio na uwezo watawapeleka watoto wao hizo Private zenu mnazozitengenezea soko?

Mzazi wa kutoka Machochwe, Buzilayombo au Kibanchabancha atasomesha mwanae kwenye shule zenu mlizojenga kama Feza, Mosabe, St. Francis nk?

My take:

1. Tunataka Uhuru wa Elimu, kila mwanafunzi asome anachokitaka, akuze talanta yake aliopewa na mungu sio kulazimishwa kisa kujaza vyuo.

2. Mhe. Waziri Mkuu we ni Mwalimu mwenzetu hili lisikushinde tusaidie wazazi masikini tunaotaka watoto wasome wanachokitaka na kukipenda sio anachokitaka Mkuu wa chuo cha utalii - Singida

3. Mhe Prof Ndalichako hizi self form wanazojaza wanafunzi ni za nini? Kazi zake ni nini.... Au mliiga kutoka kwa wakoloni bila kujua kuzitumia?

Tutumie selform.

SAMBAZA HII MPAKA AISOME MAMA. SISI NI WATOTO WA MAMA

NAMUAMINI ATATUSAIDIA

+255 752761116
 
Na Mwl. Matete

Siku tatu zilizopita serikali ilitoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo mbalimbali, kilichowastua wengi ni namna uchaguzi huo ulivyofanywa. Wazazi wengi wanalia hasa wale masikini ambao hawana uwezo wa kuwapeleka watoto wao shule binafsi (Private) kidato cha Tano:

1: Miaka yote tangu Uhuru na hata kabla Uhuru uchaguzi wa wanafunzi serikali hutumia selform ambao hujazwa na wanafunzi wenyewe kabla au baada ya kumaliza kidato cha NNE kwa kuangalia muenendo wa mtihani alivofanya. Mara nyingi wanafunzi hujaza hizi form kwa ushauri wa wazazi na walimu.

- Kwenye selform mwanafunzi huchagua tahasusi na vyuo anavyopenda yeye na wanaochagua hutumia machaguo ya mwanafunzi husika. Mwaka huu mambo hayakuwa hivo. Mtoto amefaulu PCB au PCM vizuri tu lkn anachaguliwa HKL kweli? (Mtasema shule za sayansi ni chache)

Lakini haiji akilini mtu amefaulu kwa Chemistry - A, Geography- B na Biology - B lakini anapelekwa kusoma HKL aliopata C-C-C. au amefaulu vizuri HGL lakini anapelekwa kusoma Computer, Physics na Mathematics. Aliomba hio?

2. Kituko kilikuwa kwa wale waliofaulu kwa Division one lakini unapangiwa kusoma Record Management na haukuiomba. Yupo kijana ana Division one points 14 lakini anapangiwa kusoma Hotel Management Singida. Hivi mimi mzazi tulikubaliana na wewe ulioko ofisini hapo Dodoma nataka mwanangu asome uhudumu wa Hoteli?

Mmoja ana Division I.16 amepangiwa kusoma certificate ya Community Development - Tengeru. Mliongea na mzazi wa huyu mwanafunzi akasema anataka mwanae asome maendeleo ya jamii?

Sio kwamba nabeza fani zingine LA hasha Bali kila MTU asomee anachokitaka, mi mwanangu ana kipaji cha kuchora anataka awe msanii wa uchoraji kama Masuod Kipanya na nimejaza selform, wewe unamlazimisha akasome mifugo au Record management kwa nini? Kisa uko ofisini unaamua wewe

- Nimesikitika kuona mwanafunzi mmoja amevaa mabango mengi mwili akilia amepata Div.I-14 amepangiwa kusoma Hotel Management - Bagamoyo 😭😭

KINACHOONEKANA KWENYE HALI HII

1. Serikali imeona wanafunzi hawaendi kwenye vyuo vyao ambavyo hawatoi ajira na vyuo vingi vinakufa kwa kukosa wanafunzi sasa kilichopo ni kulazimisha wanafunzi waende kwa nguvu

2. Ile tabia ya TCU kula na vyuo vikuu hasa private kuwapangia wanafunzi inahamia vyuo vya kati imeanza baada ya chuma kuondoka. Mwendazake alikataa hii tabia (RUSHWAAAA), aliruhusu kila mwanafunzi asome chuo anachotaka na fani anayopenda! Sasa hivi tunalazimisha wanafunzi wakasomee Hotel Management!!!!

3. Inaonekana vyuo vya kati vimeomba vipewe wanafunzi moja kwa moja kutoka wizarani bila kujali vipaji vya wanafunzi, lengo lao ni kuwa na wanafunzi wengi ili wapate capitation. Wakufunzi wanajali pesa kwa kuuwa vipaji vya watoto wetu. Wizara nao kujali pesa ya asante wanawateketeza watoto wetu

4. Hii ni mbinu chafu ya kuwatengenezea shule binafsi pesa. Tunalazimishwa kwa nguvu kuwapeleka watoto wetu shule binafsi kusoma kidato cha tano. Kwasababu haiwezekani mtoto amesota sana kusoma na kupata Div.I-12 unamwambia akasome Ualimu wa Chekechea - Kasulu TC kisa Mkuu wa chuo kasoma na waziri wa ......

Wazazi wasio na uwezo watawapeleka watoto wao hizo Private zenu mnazozitengenezea soko?

Mzazi wa kutoka Machochwe, Buzilayombo au Kibanchabancha atasomesha mwanae kwenye shule zenu mlizojenga kama Feza, Mosabe, St. Francis nk?

My take

1. Tunataka Uhuru wa Elimu, kila mwanafunzi asome anachokitaka, akuze talanta yake aliopewa na mungu sio kulazimishwa kisa kujaza vyuo.

2. Mhe. Waziri Mkuu we ni Mwalimu mwenzetu hili lisikushinde tusaidie wazazi masikini tunaotaka watoto wasome wanachokitaka na kukipenda sio anachokitaka Mkuu wa chuo cha utalii - Singida

3. Mhe Prof Ndalichako hizi self form wanazojaza wanafunzi ni za nini? Kazi zake ni nini.... Au mliiga kutoka kwa wakoloni bila kujua kuzitumia?
Tutumie selform.

SAMBAZA HII MPAKA AISOME MAMA.....SISI NI WATOTO WA MAMA

NAMUAMINI ATATUSAIDIA
 
Haya mambo ya combination yalishapitwa na wakati. Mwanafunzi apewe uhuru wa kuchagua kusoma combination anayoitaka.

Nchi kama Finland mtoto anaruhusiwa kusoma chochote anachokitaka.

Tuanze kubadilika, haya mambo ya combination hayana maana tena kwenye ulimwengu huu unaoenda kwa kasi. Kama mtoto anataka kusoma hkl aruhusiwe, anataka kusoma egm aruhusiwe. Hii ya kulazimishana kwa kigezo cha kufaulu hakina maana. Mtu anaweza kufaulu masomo ambayo hayapendi na anayoyapemda akafeli mtihani lakini haina maana kua hayawezi.

Mimi nilifaulu vizuri sana masomo ambayo sikua nayapenda kabisa, history, English, Biology, Kiswahili na Mathematics, hapo somo nilikua napenda ni Mathematics tu mengine hayo hata sijui nilifaulu vipi, nikachaguliwa heg, nikafika advance nikabadili na nikafaulu vizuri
 
Ndio maana inahitajika katiba mpya. Serikali hii imebweteka sana, haya maamuzi ni ya kifamilia kabisa haya, lakini bila kujali serikali inaingilia tu na kufanya maamuzi bila kujali japo hisia za watu.

I hate this
 
Hao waliochaguliwa vyuo vya kati wamshukuru Mungu.

Watasoma diploma kwa miaka 3 watakuwa na sifa ya kuajiriwa kuliko wale watakaomaliza miaka 2 na division one form six huku hawawezi kuajiriwa au kujiajiri.

Binafsi najuta kwenda five na six nilipomaliza form four.
Nilifanya ulofa sana kwa kutaka sifa.
 
Haya mambo ya combination yalishapitwa na wakati. Mwanafunzi apewe uhuru wa kuchagua kusoma combination anayoitaka.

Nchi kama Finland mtoto anaruhusiwa kusoma chochote anachokitaka.

Tuanze kubadilika, haya mambo ya combination hayana maana tena kwenye ulimwengu huu unaoenda kwa kasi. Kama mtoto anataka kusoma hkl aruhusiwe, anataka kusoma egm aruhusiwe. Hii ya kulazimishana kwa kigezo cha kufaulu hakina maana. Mtu anaweza kufaulu masomo ambayo hayapendi na anayoyapemda akafeli mtihani lakini haina maana kua hayawezi.

Mimi nilifaulu vizuri sana masomo ambayo sikua nayapenda kabisa, history, English, Biology, Kiswahili na Mathematics, hapo somo nilikua napenda ni Mathematics tu mengine hayo hata sijui nilifaulu vipi, nikachaguliwa heg, nikafika advance nikabadili na nikafaulu vizuri
Tatizo ni resources. Ukiruhusu mtu asome chochote utapangaje madarasa, vyumba vitatosha walimu watatosha, time table itakuaje,mitihani watafanyaje...n.k.

Combi bado zipo sana tu
 
Mwaka jana alisoma bure kwa kuwa ni maskini, mwaka huu anapaswa kulipa zaidi ya 1 m kulipia chuo. Kuna watoto wameshindwa kuendelea na chuo walikopangiwa kutokana na ufukara. Kuna haja ya kufikiri upya.
 
Hii ni hujuma kwa taifa kwa watu waliofanya selections, kuna vijana wawili walisoma Sayansi,mmoja kapelekwa community development,mwingine uhasibu hata Commerce wala Book keeping haja wahi soma.
Nini hiki kama siyo kuhujumu nguvu kazi ya kesho?
 
Halafu wakiulizwa wanakanusha ! Huyu Ndalichako ni shida sana , Kwa mara ya kwanza nailaumu sana JF kwa kumteua Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu , tulikosea sana , ikumbukwe kwamba Ndalichako aliteuliwa kwanza hapa jf halafu ndio Dr Magufuli akafuatia
 
Kuna baadhi ya mambo Magufuli alikiwa makini. Ujinga huu asingeukubali.
Usilitajetaje hili dikteta hata kwenye Mambo ambayo halikufanya cha maana. Hili dubwana liliharibu na kuizika kabisa sekta ya elimu.

Kama huna hoja kaa kimya, usituletee stori za dikteta uchwara kwenye mijadala muhimu.
 
Back
Top Bottom