Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na vijiji unafanyika vipi na una sura gani?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,350
Sijawahi kuona uchaguzi katika ngazi ya mtaa au kijiji popote, sijwahi kuona mabango ya wagombea katika ngazi hii, sijawahi kuona kampeni zake, sijui ni watu wangapi huwa wanachaguliwa na raia katika ngazi.

Pamoja na umuhimu mkubwa wa viongozi katika ngazi hii kila mara ninapohitaji huduma yao sijawahi kuelewa, kuona au kushiriki upatikanaji wao katika hizo nafasi.

Kwa wenye ujuzi na waliowahi kushiriki, utaratibu unakuaje kuanzia ngazi ya kupata wagombea wa vyama, nafasi ngapi na zipi za kugombea, kupitishwa kugombea na wanaosimamia uchaguzi, nani anasimamia huo uchaguzi, kampeni, upigaji kura na kuapishwa kwa viongozi vinafanyikaje.
 
Back
Top Bottom