Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Inawezekana kuwa Ridhwani yuko Tanzania anafanya research ya dissertation yake, na zaidi ya hayo inawezekana kuwa ameamua kuchukua mwelekeo tofauti kwenye masomo yak. Kilichonishangaza ni kuwa nilitegemea angekuwa kama anafanya MBA yuko hapo WARWICK instead of huko Hull na kama ni LAW basi HARVARD LAW SCHOOL pangemfaa zaidi kutokana na mfuko wa mzee wake na kama ni work expereince basi angefanyia hapo CLIFFORD CHANCE badala ya kwenda kuhangaikia mambo ya NEC katika kipindi hiki ambacho ilitakiwa akeep low profile zaidi na kuconcentrate na career yake
 
Dr Who kuna hoja nyingine unaandika, unamfanya mtu ajiulize uwezo wako wa kuanalyse mambo. Nani alikwambia kwamba mzee wako akiwa na mfuko mrefu, ni lazima/ni muhimu kwenda Harvard? si kama hivyo watoto wa wakubwa wote wangekuwa huko Harvard au oxford? Nani alisema kwamba ukitaka kupractice Law..uende C. Chance?..Nadhani ni vema ukawa unafikiria kabla ya kuandika!

Ni hayo tuu.
 
Masanja,

Yaani una post 3 na ya nne ni hii iliyomzungumzia Ridhwani...how interesting!Sasa kuna analysis gani unayotaka wewe maana naona umejibu lakini sioni analysis yoote uliyofanya zaidi ya couple of lines za majibu lakini you are entitled to have your opinion.


Ni kweli si kila mtu anataka kwenda Harvard au Yale au hata Stanford kama si St Andrews lakini ukweli ni aghalabu kwa kijana mwenye age range ya Ridhwani kutotaka kwenda kusoma kwenye Ivy league University na kama ndio anafanya hiyo law nikasema kuwa badala ya kuhangaikia mambo ya NEC basi angefanya mipango apate walau work experience au achukue nafasi za pro bono na one of the top Law firms kam CliffordChance , Allan % Overy au Linklaters mindhali yuko UK. Hivyo leo wewe unapata nafasi ya kufanya mazoezi na timu ya Ujenzi Rukwa halafu nafasi nyingine inapatikana ya Barcelona wewe utaacha kweli nafasi ya kufanya mazoezi na Barcelona?


Hii yote inawezekana kwa sababu ya refence au connections (japo watu wengine wanakasirika) lakini huwezi kufanikiwa katika dunia ya leo bila ya kuwa na connections au network nzuri sasa hebu niambie wewe ungekuwa na nafasi aliyonayo huyo Ridhwani ungetema chances kama hizo? Personally nadhani kuwa we should all sprire for the best na hata kama ikishindikana then walau hiyo second best na kama nafasi ipo why not?

Narudia tena huyu alitakiwa akeep low profile aachane na mambo haya ya siasa kwa sasa amalize masomo kisha baadae kama angetaka kuingia kwenye siasa then angetengeza grass roots na network ambayo ingemwezesha akaweza kuwa his own man badala kuwapa watu faida ya kuonekana kuwa anatumia kivuli cha mzee wake japo deep down inawezekana ana nia nzuri tu
 
Mzee Dar,

Sijakuelewa vizuri, exactly rais wetu anapigwa fix na nani? Na toka aingie urais mwaka 2005, ni fix ipi aliyowahi kupigwa unayoijua?

Ni lazima tuwe waangalifu na hoja nzito kama yako, kwa sababu rais wetu kama wengine wote duniani wanapewa majukumu ya kila siku kwa kutumia sheria za nchi, na ni majukumu ambayo sisi wananchi tumeona kuwa a sitting president atayaweza kwa kusaidiwa na wasaidizi wake, sasa rais atapigwaje fix, na huku tumemchagua kutokana na kutuhakikishia wakati wa kampeni kuwa anao uwezo kuliko wagombea wengine wote, sasa fix itatoka wapi?

Jamani tuache kuwapa free pass viongozi wetu, ni lazima tuwawajibishe, maana kama alivyosema Bwana Reagan, "The buck stops here, at the president"
 
Komandoo,
Vipi uncle party bado ipo?...mimi nataka kuvamia, mchango wangu mlangoni.
 
Quote: COMRADE44
JK interview on VOA with Shaka Saali was a flop.So much stammering and stuttering one lost the context of the statement or answer.By the way does anyone know who he was refering to in his answer to the very last question? "What is the low point during your time in office todate?" His answer " terminating the service of someone based on false information."Who was he refering to?

This is just one of the "fixes" he hates!
 
Mzee Dar,

Sijakuelewa vizuri, exactly rais wetu anapigwa fix na nani? Na toka aingie urais mwaka 2005, ni fix ipi aliyowahi kupigwa unayoijua?

Ni lazima tuwe waangalifu na hoja nzito kama yako, kwa sababu rais wetu kama wengine wote duniani wanapewa majukumu ya kila siku kwa kutumia sheria za nchi, na ni majukumu ambayo sisi wananchi tumeona kuwa a sitting president atayaweza kwa kusaidiwa na wasaidizi wake, sasa rais atapigwaje fix, na huku tumemchagua kutokana na kutuhakikishia wakati wa kampeni kuwa anao uwezo kuliko wagombea wengine wote, sasa fix itatoka wapi?

Jamani tuache kuwapa free pass viongozi wetu, ni lazima tuwawajibishe, maana kama alivyosema Bwana Reagan, "The buck stops here, at the president"

Quote: COMRADE44
JK interview on VOA with Shaka Saali was a flop.So much stammering and stuttering one lost the context of the statement or answer.By the way does anyone know who he was refering to in his answer to the very last question? "What is the low point during your time in office todate?" His answer " terminating the service of someone based on false information."Who was he refering to?


Komandoo ES
This is just one of the "fixes" he hates!
At least these are his own words. OK?
 
Aaaah wasomi bwana?...
Mpango huu nilikuwa nikiuona kwa watani zangu kumbe imeshakuwa deal!.
Just curious!
Niulize kitu kimoja, hivi kuna shule fulani duniani ambazo zinatoa elimu fulani na haina mfano wake?..Je, waliosoma Sweden, Holland, Aussie, Canada, Japan, Uchina, Russia France, Germany, Italy na kwingineko kote hawana elimu ya kweli isipokuwa vyuo hivi visivyojaa mkononi?..
 
Sababu ni nyingi ikiwemo kile ninachoita MREMA factor lakini zaidi ndugu zetu wa vyama pinzani hawajaweza kuonyesha kuwa ni best alternative ya CCM.....Hii ndio challenge kubwa anayokumbana mpiga kura wa Tanzania.

Tanzanianjema



Komandoo,

Of course CCM ndiyo walaumiwa number one kwa kuwaacha 80 % ya wananchi vijijini bila elimu ya maana ili waendeleze utawala wao (Nafikiri unanielewa). Wananchi nasi kwa kushindwa kutumia busara zetu. Kama tunataka mabadiliko inabidi yaanzie mijini especially Dar lakini TZ mabadilioko yanaanzia Tarime.
!!!

Kaka Mkandara, kukosa kuonyesha best alternative kwa upande wa vyama shindani (pinzani) ni ukweli wenye machungu ambao kwa anayetaka mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ni sharti awe tayari kuilamba.

Suala hili lipo katika pande mbili: Pande moja ni mazingira ya kisiasa katika nchi yetu na kwa upande mwingine ni kushindwa kwa tunaowaita wapinzani kufanya zaidi na zaidi.

Kuhusu mazingira ya kisiasa ni kuwa watanzania kwa ujumla ni watu waliokosa uthubutu wa kupokea kitu kipya ambacho hakionyeshi kuwa na faida ya haraka. Historia ya nchi yetu ni moja ya sababu lakini vilevile MREMA factor imewaumiza mno watanzania ambao enzi zile walikuwa tayari kujaribu ingawa kwa kufuata mkumbo. Sasa baada ya kosakosa ile CCM walikuwa wajanja wakatumia mfarakano kufananisha upinzani na vurugu, mfarakano na zaidi viongozi wasio makini. Kwa watanzania tunaothamini "amani" kuliko hata maji ya kunywa hii ni dozi nzito.

Kwa upande wa vyama upinzani, moja ni yale makosa yaliyofanyika enzi hizo ambayo kidogo yanapungua kwa sasa. Hata hivyo kwa muda mrefu wapinzani wameshindwa kuonyesha ubunifu zaidi ya kureact katika kila kile CCM wanachokifanya. Ukitoa CHADEMA katika miaka ya karibuni vyama vingine vimekuwa vinashindana kuigiza utamaduni wa CCM. Vingine wanashindwa kuiga mengine kwa kuwa tu hawana fedha na nguvu za dola. Sasa unapokuwa katika hali kama hiyo ni kwanini yule unayemuita mjinga (mpiga kura) abadili aliyemzoea na anayedhani kuwa anamjua (CCM).

Lakini tatizo lingine ni sura za vyama. Personalities zinazotoa picha ya chama. Tukubali kimoja, hapo bado sana. Watanzania wamechoka ujanja ujanja na watu wasio onyesha hata chembe ya hulka ya ukweli. Sasa kama wanaendelea kuona sura zinazowakumbusha ya CCM kila siku kwa nini wajaribu wakati wanaye wenye uhakika naye kuwa ataharibu lakini kimoja watakipata, "AMANI"

Katika hali kama hii ndio linakuja suala la kuacha kuwalaumu wanaoitwa CCM (kama afanyavyo Mr Zero) na kujitoa kuonyesha mtanzania mnayedhani ni mjinga kuwa kuna vitu na zaidi watu tofauti katika upande mwengine zaidi ya CCM. Hii ni challenge rahisi mno kama wenzetu walioamua kuchukua jukumu la kuwa wapinzani endapo nao wataonyesha uthubutu wa kwanza kujichunguza, kukubali mapungufu, kuwa tayari kujikemea hata mbele ya hadhara na kujenga imani kwa watanzania. Na kwa wale walio pembeni kulaumu CCM na Upinzani, ni jukumu lao kuacha kubwekea nje na kujiunga kumuonyesha mpiga kura kuwa There is a best alternative out ther.....

Kumbuka mnyonge kushinda ni lazima aonyeshe uzuri mara mia ya yule aliye juu. Hii ni kama mwanamke na uongozi...nadhani mnanipata.


Tanzanianjema
 
Nchimbi si kama anaandamwa ana anaonewa. Sithubutu wala siwezi kutetea uovu lakini kumuingiza Zitto katika uhalifu inapoteza maana halisi ya kumsulubu Nchimbi.
*Nchimbi anawekwa katika historia kutokana na utata wa kiifo cha Ipyana Malecela
*Anawekwa katika historia kutokana na kuponea chupuchupu kwa JAne Mihanji.
*Anawekwa katika kumbukumbu tena kuhusu Amina (Mwenyezi Mungu aiweke roho yake peponi Amin).

Kabla ya kifo cha Amina haya yote yaliwekwa wazi na tahadhari kubwa ilitolewa kuhusu hatari ya kumpoteza Amina na Mwanakijiji alibuni hata T-Shirt za Free Amina. Hali haikua nzuri hata kidogo.

Kwa tukio hilo, hata Medy anaweza kuwa ameingia tu mkenge lakini Medy na Zitto wao walikua na kila sababu ya kuona Amina anaendelea kuwapo duniani pamoja na kuwapo tofauti zao. Hata magazeti baadhi yalitumika na baadhi yalikua bendera kufuata upepo kwa lengo la kuuza. LAKINI Zitto ni mmoja wa watu walioumia sana kwa kifo cha Amina na hata hapa Dodoma, kila mtu anampa pole yeye kuliko hata Medy. Medy alimuacha japo ana mtoto naye bado alikua na kinyongo kikubwa naye. Hata hivyo hana sababu ya kumpoteza Amina, japo inaweza kuwa angefurahi Amina asifanikiwe akiwa nje ya himaya yake (ndio sababu alimuandikia Spika barua na kutoa kwa magazeti).

Kabla ya kifo chake Amina amemtaja sana Nchimbi. Kabla ya kuzibwa mdomo, Amina alisema wazi kwamba hana hakika kama ataweza kufanya press conf.

MWISHO NAULIZA WAHUSIKA, HII THREAD ILIKUA NI YA RIDHWAN KIKWETE, INAKUAJE KUNA MAMBO MENGINE AMBAYO YANAINGIA WAKATI KUNA THREAD ZAKE?
 
Nami nafikiri kweli mambo sio shwari sana ndani ya Chama Tawala,Kuna Mdau amenidokeza kuwa Hata Bwana mwenye Mbwembwe nyingi Didas Masaburi pia nae kapigwa nje kwenye kinyang'anyiro cha Ujumbe wa NEC!Mzee Sumaye na Mangula wamepitishwa lakini kwa mbinde kweli kweli,natumaini chekeche hili litawajenga zaidi CCM na sio kuwabomoa na kuanza kupakana matope hadharani!
 
MWISHO NAULIZA WAHUSIKA, HII THREAD ILIKUA NI YA RIDHWAN KIKWETE, INAKUAJE KUNA MAMBO MENGINE AMBAYO YANAINGIA WAKATI KUNA THREAD ZAKE?

Ni katabia tu kameanza ka kupindisha mada, kama ni makusudi au inatokea tu bado haijawa wazi...

kama nimesoma vizuri hapa kuna habari inayosema Ridhiwani yupo katika mchujo na habari nyingine inasema hayupo; ipi ni sahihi?
 
kutokana na kauli hii, jee anamaana kuwa safari hii mwenye kutaka kuwania urais Tanzania kwa kupitia CCM anaweza kuchukua fomu na kugombea pamoja na mkuu huyu au???????


...Ndani ya CCM hakuna kuhodhi madaraka'



Na Reuben Kagaruki

MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amesema ndani ya chama hicho hakuna mwanachama wa kuhodhi madaraka na kuwakumbusha kuwa kila mmoja asishangae wala kuchukia pale anapoona wana CCM wenzake wanajitokeza kugombea nafasi aliyoishikilia sasa.

"Ni haki yao kikatiba, hivyo mtu anapoamua kuitumia asionekane wa ajabu au anafanya hiana, si vizuri kuanza kutafuta mchawi...kama mchawi basi ni Katiba iliyoweka utaratibu wa miaka mitano."

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana wakati akihutubia Taifa kupitia wakazi wa mkoa huo wakiwamo wabunge, majaji na viongozi wa CCM ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.

Alisema moja ya sifa ya CCM ni kuwapo kwa demokrasia ya ndani ya chama. "Tumeweka utaratibu kuwa kila kiongozi ana umri wa miaka mitano katika uongozi, huo ndio mkataba wake na chama na wanachama...hakuna mwenye hatimiliki ya uongozi wa kudumu kwa nafasi aliyonayo," alisisitiza Rais Kikwete.

Alisema hakuna sababu ya watu waliokuwa wakishikilia nyadhifa ndani ya chama hicho wanapowaona wengine wanataka kugombea na kuanza kuhoji ni kwanini kaja, nani kamtuma.

"Ni dhambi kujengeana chuki kwa sababu hiyo. Najua kila mmoja wetu aliyepo madarakani angependa asipate mpinzani. Lakini, matumaini hayo yasiwe sababu ya watu kuwachukia wale wanaojitokeza kugombea nafasi tunazozishikilia," alisema Rais Kikwete.

Alisema pindi wanapojitokeza ichukuliwe kuwa ni jambo la kawaida kutokea, kwani hayo ndiyo matakwa ya Katiba ya CCM.

"Kununiana na kufanyiana vitendo vya uadui ni kinyume na misingi ya demokrasia ndani ya chama chetu. Nayasema haya kwa sababu nasikia kuna baadhi ya wilaya na mikoa zipo dalili hizo. Nawasihi msifanye hivyo. Tuzingatie maadili ya chama chetu," alisema Rais Kikwete.

Kuhusu kampeni, Rais Kikwete aliwataka wagombea wote kuzingatia kanuni na maadili ndani ya chama. Alisema kati ya mambo muhimu ni kuepuka kampeni chafu za kupakana matope na kuchafuliana majina.

Aliwataka wagombea wajinadi kwa ubora wa sifa zao au kama ni wapambe wanadi ubora na sifa za wagombea wao.

"Katu msifanye vitendo vya kukashifu au kuwapaka matope wagombea wenzenu. Vitendo hivyo vinajenga chuki na mfarakano miongoni mwa wanachama, jambo ambalo halina maslahi kwa chama chetu," alisisitiza Rais Kikwete.

Kuhusu rushwa, alisema ni jambo la hatari kwa kiongozi kupata uongozi kwa njia ya rushwa au kwa kununua kura. Alisema kufanya hivyo ni kitu haramu na ni kudhalilisha heshima ya chama

"Nawasihi wana CCM tusitoe rushwa kupata uongozi na tusipokee rushwa ili kumpigia kura mgombea...uongozi usinunuliwe na kura isiuzwe, uongozi wa CCM upatikane kwa ridhaa ya wanachama kutokana na kutoshelezwa na sifa na ubora wa mwombaji," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Nawaomba wasimamizi wa uchaguzi na hasa vikao vinavyohusika na uchaguzi, kuhakikisha vitendo vya rushwa na watoa rushwa na wapokea rushwa wanadhibitiwa. Tunatengeneza taratibu nyingine zaidi za kusaidia mapambano hayo."

Pia alikemea tabia ya baadhi ya wagombea au wapambe wao kutaka kushinda kwa kupandia migongo ya wengine. Alisema kuna baadhi wanaotumia majina ya watu wengine kupatia ushindi.

"Wapo wanaodai ati wanagombea kwa kutumwa au kutakiwa na wakubwa fulani...tena wanasema wakubwa wa ngazi za juu. Wapo waliodiriki kunitaja mimi kuwa ndiye ninayehusika. Watu hao ni waongo! Sijamtuma mtu yeyote kugombea, na sina mgombea popote, kwa ngazi yoyote.

"Nawaomba mnaposikia yeyote anasema hivyo, mjue ni mwongo. Mwambieni awaambie sifa zake za kufaa kwa nafasi anayoomba kwani mnamchagua yeye na si huyo anayedai amemtuma," alisema Rais Kikwete.

Aliwakumbusha wagombea kuwa kuna kushinda na kushindwa. Aliwataka watakaoshindwa kuwa tayari kukubali matokeo.

"Tuyachukulie (matokeo) kuwa ndio uamuzi wa watu bila ya kuweka nongwa, kujengeana chuki na kutafuta mchawi. Ndiyo demokrasia ilivyo. Tulizoee jambo hili," alisema Rais Kikwete.

Aliwataka wanaCCM wasiigeuze siasa ni vita na chuki kama ambavyo wanafanya baadhi ya watani (wapinzani) wao.

Hata hivyo, aliwataka wale wanaodhulumiwa waseme bila kufanya vitendo vya kuleta mgawanyiko au misukosuko ndani ya CCM.

Alisema kiongozi anaweza kutoka kwenye chama chochote, lakini kiongozi bora hawezi kutoka nje ya CCM.

Kuhusu wagombea alisema amefarijika kuona watu wengi wamejitokeza kuomba uongozi. Alisema waombaji ni rika zote, makundi yote katika jamii na wa viwango vyote vya elimu.

source:
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=3385
 
Ukweli ni kwamba wamepita tu kwenye mchujo wa kwanza, uchaguzi rasmi utakuwa tarehe 3, November, lakini ni clear kuwa watashinda!

Ila habari nzito, ni za Nchimbi kutochukua fomu kabisaa na kwamba yuko njiani kujitoa kabisaa kwenye siasa kutokana na impact ya kifo cha Amina Chifupa!

Ni very interesting story ambayo tunaifuatilia kwa makini na undani na tutaiweka hapa hapa giladi!

Halafu Muungwana sasa hivi yuko kwenye VOA live, kwa hiyo chungulieni rais wetu wakuu msikie anayosema!

Komandoo ES,

Unajua wakati mwingine unaniacha hoi. Kwenye baadhi ya hoja, you are spot on in terms of facts and details, lakini wakati mwingine, hata kwenye jambo dogo kama hili, you are way off. I can't think why.

Kwenye hili:

Ridhiwan hakugombea Ujumbe wa NEC. Aligombea kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kupitia wilaya ya Bagamoyo. Na kwa nafasi hiyo aliyoomba, mchujo haufanywi na NEC, therefore there is no way utaona jina lake limepitishwa au kutopitishwa leo/kesho.

Likewise with Masha. Hakuomba ujumbe wa NEC. Kwahiyo, hauwezi kusema amepita kwenye mchujo.

These are basic facts kwa mtu yoyote mwenye remote interest na siasa za Tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom