Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Mzee Mugongox2, heshima mbele mkuu ila sina sbabu ya kuwapa watu faida kwa kulumbana na wewe, kwa hiyo ninakupa ushindi!

Mzee Said Yakub,

Nilifikiri kuwa baada ya kuja mzima mzima, utakuwa umebadilika tabia, lakini ninaona spirit ni ile ile kama ulipokuwa TTJ, una lako jambo, karibu mkuu, ila kwenye hii ishu nimeamua kumsikiliza Mzee Bob. Mkandara, kwa hiyo sitawajibu tena, unless ikibidi tu!, so far sioni sababu!

Isipokuwa get ready na uchaguzi wa uliopita wa London, maana nina data zako wewe mwenye na u-candidate wako fake! nakula pumzi kwanza! Ishu ya credibility ni wewe mwenyewe uliyelivalia njuga, sio mimi, karibu mkuu!

Heshima mbele wakuu!


Shekhe hebu tuwasiliane kule kwenye FARAGHA....usiwape watu faida ya bure ili hali sisi tunadesturi zetu za kumaliza haya mambo kama wau wenye hekima zao
 
Ni vita NEC CCM

Mwandishi Wetu

SALOME Joseph Mbatia hatunaye. Amefariki dunia kwa ajali ya gari Jumatano iliyopita akiwa Njombe, mkoani Iringa. Kifo cha mama huyo mchapakazi aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55, kimemkuta akiwa katika harakati za kisiasa, akiwa katika hatua za mwisho za kujinadi aweze kupenya katika tundu la Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mpinduzi (CCM).

Hadi mauti yanamfika, Salome alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa anawania kupitia Kundi la UWT (Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania).

Na saa mbili kabla ya kifo chake, alikuwa mjini Iringa alikoacha vipeperushi vyake ili wapiga debe waendelee kumnadi huku yeye akiendelea kusaka kura wilayani Njombe. Kwa bahati mbaya, amefariki kabla ya kutimiza ndoto yake.

Salome alikuwa mmoja kati ya kundi kubwa la wana-CCM waliopitishwa kuwania nafasi 85 za ujumbe wa NEC kutoka makundi mbalimbali.

Lakini mchuano mkubwa zaidi unaofananishwa na 'vita ya kisiasa' unaonekana kuwa katika 'Kapu' la 'vigogo' 59 linalopaswa kutoa watu 20 tu!

Pengine ni kutokana na ugumu huo, kwa takriban miezi miwili ziara za viongozi wengi wa chama na serikali mikoani zilikuwa hazikauki - lengo kubwa likiwa kujinadi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa (CCM).

Katika kapu, kuna wazito kama Waziri Mkuu, Edward Ngoyai Lowassa, Frederick Tluway Sumaye, waziri mkuu aliyemwachia 'ziwa' Lowassa, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Rajab Makamba, naibu wake, Jaka Mwambi, naibu katibu mkuu wa zamani, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwambulukutu, orodha ndefu ya mawaziri na manaibu waziri pamoja na wabunge mashuhuri.

Wagombea wengine waliopitishwa katika kundi hilo ni pamoja na mkongwe wa siasa tangu enzi za TANU, 'babu' Kingunge Ngombale-Mwiru anayekabana koo na wajukuu zake katika kapu la CCM.

Kwa sasa, Kingunge mwenye umri wa zaidi ya 70, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia siasa na uhusiano wa jamii.

Wengine ni Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Shy-Rose Bhanji, Enock Chambiri, John Chiligati, Siwajibu Clavery, Dk. David Mathayo, Said Masoud Fundikira, Christopher Mwita Gachuma, Arbogast Godogodo, David Holela, Jared Kadunga, Charles Kagonji, Dk. Deodorus Kamala, Constantine Kanyasu, Profesa Juma Kapuya na Alhaj Said Kilahama.

Wengine katika kundi hilo ni Haidah Kilua, Abdulrahman Kinana, Lukas Kisasa, John Komba, William Lukuvi, Pascal Mabiti, Dk. Milton Mahanga, Amos Makala, Novatus Makunga na Mohamed Yakub Mamoon.

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Wilson Masilingi, Maurus Mhimbira, Mohammed Mkumbwa, Dk. James Msekela, Dk. Ibrahim Msengi, Jackson Msome, Profesa Idrisa Mtulia, Profesa David Mwakyusa, Aggrey Mwanri, Abeid Mwinyimsa na Job Ndugai.

Orodha ni ndefu kwani inawahusisha pia William Ngeleja, Dk. Banda Salim, Salim Khamis Salim, Abdul Adamu Sapi, Isidore Shirima, George Simbachamwene, Amos Siyantemi, Dk. Hashim Twaakyondo, Frank Uhaula, Profesa Samuel Wangwe, Stephen Wassira 'Tyson' na Nicholaus Mateso Zacharia.

Katika kampeni hizo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba kuna baadhi ya vigogo (majina tunayo), walilazimika kufanya kila linalowezekana lengo si kushinda ujumbe wa NEC tu bali pia kushika usukani katika pointi.

Mathalan, kigogo mmoja wa CCM amekuwa akizunguka na kusisitiza apigiwe kura akidai kwamba itakuwa aibu kwake kupenya kwa kura chache katika kundi hilo la 'kifo'.

Inadaiwa amekuwa akisisitiza kwamba ana uhakika wa kushinda, lakini anataka ushindi wa 'kishindo' utakaoonyesha kukubalika kwake badala ya kushika nafasi kwa mfano ya kumi katika nafasi hizo 20.

"Anasema waziwazi kwamba ana uhakika wa kushinda, lakini anataka kuongoza…" kimeeleza chanzo chetu.

Mtazamo huo pia upo kwa kigogo mwingine wa juu serikalini anayedaiwa kukosa usingizi na kuhimiza 'wakubwa' mikoani na wilayani kuhamasisha apigiwe kura ili aibuke kinara zaidi ya wengine katika kundi hilo.

Hao ni 'wakubwa', lakini na wengine pia hawakulala, kila mmoja anapigana kikumbo kivyake kuhakikisha anaibuka na ushindi katika Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia Novemba 3 mjini Dodoma. Mkutano huo ni maalumu kwa uchaguzi.

Mbali ya wagombea watakaochuana kuwania nafasi 20 za 'Kapu' na wengine waliokwishapatikana kwa tiketi ya mikoa, wagombea wengine na makundi yao ni kama ifuatavyo;

KUNDI LA UWT:

Katika kundi hili ambalo hayati Salome Joseph Mbatia alikuwa mmoja wa wagombea, wanaowania kuingia NEC ni Halima Mohamed Mamuya, Mbunge na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UWT.

Wengine ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Semamba Makinda, Waziri Sofia Mnyambi Simba, Waziri Margareth Simwanza Sitta, Sifa Amani Swai, Asha Ramadhani Baraka, Khadija Omar Kopa, wanahabari Jacqueline Liana na Jane Claude Mihanji.

Pia wamo Waziri wa Fedha, Zakia Hamdani Meghji, Kate Magdalena Kamba, Fatuma Adam Sapi Mkwawa, Rita Louise Mlaki, Chonjo Reginald Regina, Shamsa Selengia Mwangunga, Pindi Hazara Chana, Hajjat Amina Mrisho Said, Janath Mussa Kayanda, Sakina Said Kabeza, Anna Kilango Malecela, Jacqueline Noni, Anna John Magowa, Dk. Rehema Jonathan Nchimbi, Chiku Abdallah Sumbu Gallawa, Halima Meza Kihemba, Fatuma Kimario, Elizabeth Sanga Mwaifwani, Gulzar A. Sabir, Margareth Agness Mkanga, Lydia Thecla Boma, Zuhura Bashekhe Mikidadi, Ellen Makungu Bogohe, Ester Kabadi Nyawazwa, Mwanaidi Maliki Kiongoli, Zainab Matiku Vulu, Esha Hassan Stima, Diana Mkumbo Chilolo, Tatu Mussa Ntimizi, Aisha Omari Kigoda, Mwantumu Bakari Mahiza na Beatrice Matumbo Shelukindo.

KUNDI LA VIJANA:

Katika kundi hili wamo Mwamini Lusingu, Abdallah Ramadhani Mayomba, Omari Yusufu Kiriati, Zainab Rashidi Kawawa, Sixtus Raphael Mapunda, Vanessa Mugeta, Nape Moses Nnauye, Jerry William Slaa, Ashura Abubakar Suleiman, Neema Heri Mwakabonga, Deogratius Ndejembi, Edwin Mgante Sanda, Melkiado January, Penias Peter Kaindoa, Rajab Thabit Katunda, Beno Malisa, Paul Herman Kirigini, Lutengano George Mwalwiba, Sarah Msafiri Ally, Adela Albert Ng'atigwa, Rose Kashinde Juma, Magembe Boniphase Cornel Magembe, Pili Mwajiri Jabiri, Jasinta Venant Mboneko, Violete Mzindakaya Mpogolo, Raymond Stephen Mwangwala, Lucy Mayenga, Francis Issack Mtinga, Suleiman Masoud Nchambi, Hussein Mohamed Bashe na Rojas Yakob Shemwelekwa.

KUNDI LA WAZAZI:

Wanaowania U-NEC kwa tiketi ya wazazi ni Thomas Ngawaiya, Fortunata Moses Kabeja, Enoc Kalumuna, Selina Adolf Mkonyi, Mohamed Nassoro Nondo, Salim Shomvi Tambalizeni, Richard Hiza Tambwe, Mustafa Yakubu, Mussa Azzan Zungu, Ruth Msafiri, Henry Daffa Shekifu, Richard Said Nyaulawa, Innocent Kalogeris, Danhi Beatus Makanga, Azizi Jawad Aziz, Dickens Kulwa Shindika, Dk. Zainab Amiri Gama, Adam Kighoma Ali Malima, Mhandisi Stella Martine Manyanya, Athuman Rashid Mfutakamba na Mgosi Semtumbi Bakari.

Je, baada ya mchakato mzito wa kusaka kura, ni nani atakayeibuka na ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri katika medani ya siasa nchini? Tusubiri.

Source: Tanzania Daima
 
Hakuna chombo chenye nguvu Tanzania kama Mkutano Mkuu wa CCM, siyo Bunge, wala siyo Kamati Kuu. Na kutokana na hilo (nilibahatika kuwepo kwenye mkutano mkuu wa 1984) Watanzania watarajia zaidi ya kicheko bali pia machozi. Kuna watu wataanguka kwa kuzimia hasa pale Mwenyekiti atakaposema "Maswali"... Wajanja watakuwa wamewapanga watu wao wa kuwauliza maswali ya "kuwajenga" na wabaya wao watauliza maswali ya "kuwabomoa".

Hofu yangu ni kuwa kabla ya msiba huu haujatulia tunaweza kujikuta tunapata mingine sababu ya kile kinachojulikana kule Dodoma kama "Mizengwe". Kuna watu watalia sana.

Namwomba Mnyezi Mungu awape afya, uzima, uthabiti na uimara wa kusimama kuomba kura za NEC.
 
Mkuu kazi nzito sana, maana sasa moto unawaka, Mtandao bado wanajaribu kuibuka lakini the other side nao wanajipanga,

Ila Mtandao bado ku-recover kipigo cha Tom, kule Mbeya, na kipigo walichopigwa na Spika, kwenye ishu ya Malima,

Naona sasa wengine hawaishi Bagamoyo, wallahi tutajionea mambo!
 
Siasa za Tanzania za ajabu sana, utafikiri tupo katika mfumo wa chama kimoja, yaani wanasiasa wote wanatafuta uongozi kupitia CCM! Ajabu sana! Halfu tunalalamika kwa nini akina Mrema, Lipumba, n.k. hawastaafu, wastaafu wamuachie nani hasa kama wote hamtaki kutoka CCM?
 
Siku 5 kabla ya Mkutano Mkuu wa CCM:Njia nyembamba kwa wanamtandao maslahi

* Yadaiwa wapaniwa kupigiwa kura za fitna
* Wanaounga mkono juhudi za JK watajwa
* Nafasi ya Makamu Bara yawa gumzo zito


Na Waandishi Wetu

WAKATI Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM unatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma, wanaCCM wa kundi la Mtandao Maslahi wanaogombea nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wanadaiwa kukabiliwa mtihani mgumu katika mchuano huo.

Uchunguzi wa gazeti hili kutoka mikoa mbalimbali umebaini kuwa baadhi ya makundi ndani ya chama hicho yameungana kwa lengo la kuliangusha kundi hilo linalodaiwa kupigana kufa na kupona kujipanga kuhakikisha washirika wake wanashinda nafasi hizo ili kujiimarisha kisiasa ndani ya chama hicho kikongwe.

Makundi yanayolipinga kundi hilo, yanadaiwa kuundwa zaidi na wanachama ambao wagombea wao walishindwa kwenye kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2005 na kwamba hawapo tayari kuona chama kinaangukia mikononi mwa wanamtandao maslahi.

Wanachama wanaopambana na mtandao maslahi wanaelezwa kuwa ndio wanaotekeleza na kufuata maelekezo ya mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, kukijenga upya chama kwa kuua makundi na kuimarisha mashikamano wakati mtandao maslahi unadaiwa kuendekeza makundi na fitna ndani ya chama.

Baadhi ya wanaCCM wamekilaumu kitendo cha kundi hilo kudaiwa kuingilia kampeni, kusaidia baadhi ya wagombea u-NEC na wenyeviti ngazi ya mikoa ili washinde huku wakirubuni kwamba wanachama hao, wana baraka za viongozi wa juu wa chama na Serikali jambo ambalo Rais Kikwete aliwahi kulikemea na kutamka hadharani kwamba binafsi hajamtuma mtu yeyote kugombea nafasi yoyote ndani ya chama hicho.

"Kushindwa kwa wagombea wengi wa kundi hilo katika chaguzi za ngazi za mikoa na kushindwa kwa njama za kuwaengua wanachama wanaotoka nje ya kundi hilo ni salamu kuwa wanamtandao maslahi wajitayarishe kuangukia pua Kizota. Tutakata mizizi ya fitina kwa kuwanyima kura," alidai mjumbe mmoja wa mkutano kutoka Mkoa wa Kagera ambaye aliomba kuhifadhiwa jina.

Aliendelea kusema wanaCCM wasipokuwa makini chama chao kipo hatarini kubinafsishwa na wanamtandao maslahi na kudai kwamba kundi hilo linatumia fedha nyingi kuonesha lina mapenzi makubwa kwa chama lakini ukweli linafanya hivyo kwa maslahi binafsi.

Habari kutoka Mwanza zinaeleza kuwa baadhi ya vigogo wa chama na Serikali kutoka kundi la wanamtandao maslahi, wamekuwa wakitembelea mkoa huo huku wengine wakiendesha vikao usiku kujipigia debe huku na kushawishi wanachama wenzao, wasichaguliwe.

Makada hao kwa nafasi zao wanadaiwa kutumia vitisho kwa wanachama, viongozi na watendaji wengine wa chama ili kuhakikisha wanakidhi haja yao kuungwa mkono na kupata ushindi kwenye kinyang'anyiro cha Dodoma.

Baadhi ya wanaCCM jijini Dar es Salaam, juzi waliliambia gazeti hili kuwa kundi hilo linachangia kuzorotesha juhudi za mwenyekiti wa chama hicho Rais Kikwete kujenga upya na kuimarisha mshikamano ndani ya chama.

Habari kutoka Mbeya zinasema baadhi ya wanaCCM mkoani humo wanadia athari za kundi hilo wakati wa uchaguzi wa chama ngazi ya mkoa, zimeibua hasira kwa baadhi ya wanachama na sasa wanajiandaa kupigia kura za chuki dhidi ya wote wanaodaiwa vinara wa mtandao maslahi kwenye mkutano wa Kizota.

"Tunakwenda Dodoma nia yetu ni kuchagua NEC makini, hatuwezi kuendelea kujaza viongozi mahoka waliochoka kufikiri. Tunakwenda kuizaa upya CCM ambayo haitakuwa na viongozi wanaopenda sifa za unyapara, tutampatia zawadi muasisi wa Taifa letu marehemu Mwalimu Nyerere na Mwenyekiti wetu Rais Kikwete kwa kuchagua timu imara.

Wakati huo huo habari zaidi zinasema homa ya nani ataibuka kinara katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara inazidi kupanda miongoni mwa wana CCM .

Nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na mkongwe wa siasa nchini , Bw. John Malecela inamvuto wa aina yake katika mkutano wa Kizota.

Tayari wanasiasa kadhaa wamekuwa wakitajwa kupitia vyombo vya habari kuwa huenda wakachukua nafasi hiyo ambayo kikatiba haigombewi bali inatokana na mapendekezo ya Mwenyekiti wa chama.

Baadhi ya wanaCCM ambao wamekuwa wakitajwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho,Bw. Yusuf Mkamba, Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Bw. Abdulrahman Kinana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

Mbali na wanachama hao majina zaidi yamezidi kutajwa na wanaCCM katika nafasi hiyo,mbali na jina la Makamu Mwenyekiti wa sasa Mzee Malecela , majina mengine yaliibuka hivi karibuni ni pamoja na lile la Spika wa Bunge mstaafu, Bw. Pius Msekwa na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Bw. Philip Mangula.

Rehema Mwakasese anaripoti kuwa wanachama wa CCM wametakiwa kuacha tabia ya majungu na makundi hasa inapofikia wakati wa uchaguzi.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akiwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kushika nafasi ya Mwenyekiti CCM Wilaya ya Ilala, Bw. Suleiman Kalanje, alisema katika kipindi cha uchaguzi wanaCCM wana tabia ya kujigawa makundi jambo ambalo huwapa mwanya wapinzani.

Alisema wanaCCM hawapaswi kuwa na kisasi wanapokosa nafasi za uongozi katika uchaguzi kwani panapokuwa na ushindani ni lazima awepo mshindi na anayeshindwa hivyo kushindwa ni kawaida.

Alisema jambo muhimu kwa wanaCCM wakati huu ni kuongeza wanachama ili kukipa chama hicho nguvu.

Alisema katika kipindi cha uongozi wake amepanga kutekeleza yote aliyoahidi katika kuleta maendeleo ndani ya chama na umma kwa ujumla.

Aliwataka viongozi wenzake wa CCM kutekeleza ahadi zao ili kujenga imani ya chama kwa wananchi.

Source: Majira
 
Siasa za Tanzania za ajabu sana, utafikiri tupo katika mfumo wa chama kimoja, yaani wanasiasa wote wanatafuta uongozi kupitia CCM! Ajabu sana! Halfu tunalalamika kwa nini akina Mrema, Lipumba, n.k. hawastaafu, wastaafu wamuachie nani hasa kama wote hamtaki kutoka CCM?

ukiona hivyo upinzani hauna dili, kule mlisema watu wavijijini hawana uelewa hapa unaona wasomi walivyojipanga kugombea nafasi ndani ya ccm.

huku ndiko kusoma nyakati


kitila njoo kwa watu wa kweli watojua kukuenzi
njoo kwetu uingie hali utoke kwenye majonzi
kwenye mapenzi ya ghali yasio na pingamizi

njoo CCM njoo upumue baada ya kelele za wapingani wa maendeleo
 
Siasa za Tanzania za ajabu sana, utafikiri tupo katika mfumo wa chama kimoja, yaani wanasiasa wote wanatafuta uongozi kupitia CCM! Ajabu sana! Halfu tunalalamika kwa nini akina Mrema, Lipumba, n.k. hawastaafu, wastaafu wamuachie nani hasa kama wote hamtaki kutoka CCM?

Kitila Mkumbo,

Sadakta kaka, you are now well positioned to show other politicians that opposition ni watu makini sio wasanii au wababaishaji!!! Binafsi hata kama ningependa kuwa mwanasiasa siwezi kaa na mtu kama Mrema meza moja, kwa sababu Mrema Demokrasia hana habari nayo hata siku moja!!! kwa hiyo miungano yenu na kila mtu ati kwa kuwa ni mpinzani tu, hata kama sio mwenye nia ile mnayoamini ninyi ni aina nyingine ya usanii...

No wonder watu makini wengi bado wako kwenye NEC ya CCM, sasa kwa
nini msifanye mbinu za kuwavuna au wakija watachukua nafasi zenu za juu?
 
Mkuu kazi nzito sana, maana sasa moto unawaka, Mtandao bado wanajaribu kuibuka lakini the other side nao wanajipanga,

Ila Mtandao bado ku-recover kipigo cha Tom, kule Mbeya, na kipigo walichopigwa na Spika, kwenye ishu ya Malima,

Naona sasa wengine hawaishi Bagamoyo, wallahi tutajionea mambo!

Faraja yangu ni uzoefu wa Chama hiki kuyavuka mawimbi pasipo chombo kuzama,naamini kabisa Chairman anafahamu kuwa ule mrindimo aliokuwa anausikia mikoani sasa umetua mikononi mwake,tuzingatie hoja ya muhuni Butiku aliyotaka Chairman nyae siku kama hizo za Novemba aombe kiti tena kwa wajumbe na wajumbe watumie haki yao ya kuhoji na hatimaye wapige kura,shughuli ila ni vema tukajiandaa kuwaona majeruhi wengine si wa ajali barabarani bali ndani venue ya Kizota maana Chimwaga is no longer there.
Alamsiki
 
Posted Date::10/29/2007
Waziri Simba: Nasubiri kura za huruma
Jackson Odoyo


WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema licha ya afya yake kuendelea kuimarika taratibu, hawezi kuendelea na kampeni zaidi anategemea kura za huruma.


Simba ambaye anawania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), alipata mshtuko baada ya kusikia taarifa za kifo cha Naibu Waziri wake, Salome Mbatia ambaye alikufa kwa ajali mjini Njombe, Iringa.


Akizungumza katika Hospitali ya Hindu Mandali anakopatiwa matibabu juzi usiku, Simba alisema, anasubuliwa na matatizo ya mfumo wa mawasiliano kichwani mwake.


Alisema kabla ya kwenda Afrika Kusini kweye Mkutano wa Pan African Women, alikuwa ameanza kampeni Mkoa wa Rukwa ambako alikwenda kuelezea bajeti ya serikali.


Waziri Simba alisema, hivi sasa ingawa afya yake inaendelea kuimarika taratibu, hawezi kufanya kampeni hata akiruhusiwa na madaktari.


Hata hivyo, Simba alisema ugonjwa huo ulianza alipokuwa Afrika Kusini na Oktoba 15, mwaka huu alizidiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rand Clinic, mjini Johannesbarg na kulazwa kwa siku tano.


?Baada ya kupimwa madaktari waligundua matatizo katika mfumo wa mawasiliano ya kichwa changu,? alisema Simba.


Mkutano Mkuu wa CCM unatarajiwa kufanyika mjini Dodoma kati Novemba 3 na 4, mwaka huu.
 
Back
Top Bottom