Uchaguzi mdogo majimbo ya Ukonga na Monduli: CCM yashinda majimbo yote!

Kilichotenganisha binadamu na wanyama wengine kama mbwa au nguruwe ni utashi na aibu , ili uonekane binadamu lazima vitu hivi uwe navyo , hivi waliopiga kura wakiwa 500 , mgombea anawezaje kupata kura elfu 60 ?
Hayo ndiyo matatizo yako! Kuna kupiga kampeni ambapo ni tofauti na kupiga kura ambayo ni tofauti na kumtangaza mshindi. Sijawaji kkuona jimbo lina wapigakura 500.
 
Natoa hongera za awali kabisa kwa CCM kwani naamini wanaenda kuchukua majimbo yote mawili kwa kutumia mbinu zilizowafanya kuwa chama kikongwe Afrika na Duniani.
Wasipokuelewa hichi ulichoandika hapa basi ni sikio la kufa na wataendelea kushiriki kwenye maigizo ya ccm.
 
Mkuu wa mkoa ccm,kamati ya ulinzi nzima ni ccm,mkuu wa wilaya ccm,mkurugenzi ni ccm,msimamizi wa uchaguzi ni ccm,mawakala ni ccm,sanduku za kura ni za ccm,Pesa za uchaguzi ni za ccm,polisi ni ccm,wanaojumlisha matokeo ni ccm,anaetangaza matokeo ni ccm,halafu mpinzani ashinde kweli. Cha msingi ungeni mkono tu Pesa za kurudia uchaguzi zipo tele ni wao tu wanajichelewesha,yafaa kila mwezi tuwe tukirudia uchaguzi wa kuifurahisha ccm hadi 2025 itapendeza zaidi, tutakuwa mbali kimaendeleo, maana maendeleo hayawezi pelekwa kwenye upinzani.
Pesa inayotumika kurudia chaguzi ni pesa nyingi kisha CCM wanachakachua inatia hasira sana, wakumbuke wananchi wamechoka kudhurumiwa haki zao wanajiandaa kuja na tiba muafaka.
 
Jamani upinzani nao wanataka kushibisha matumbo yao, walau wangepewa hata jimbo moja ili wale. Tunajua hawa wote wako katika kuhangaikia matumbo yao na sie wananchi tunajitafutia mkate wetu. Nawapa pole wapinzani labda wajaribu tena hapo baadae huenda nao wakala
Tambua CCM wanataka kurejesha mfumo wa chama kimoja kisha wabadili katiba iwe kama ya China na Rais awe wa milele.
 
Wasimaimizi wa uchaguzi wa majimbo na Kata wanajua kinachoendelea ukweli ni kua mnaiba kura sio siri na huo ndio ukweli naongea nilichokiona yaani mna dhambi nyie watu hapana kwa kweli
Wakati kura zinaibiwa wewe unakuwa wapi? Kazi ya wakala ni nini?
 
R
Kama hujui yaliyotendeka Kinondoni bora ukae kimya, aliyebadilisha majina ya mawakala dakika za mwisho ni nani? Halafu mkashinikiza lazima hao wapya nao waapishwe. Hata mimi ningekua Mkurugenzi nisingefanya huo upuuzi.Tatizo lenu huwa mnasikiliza taarifa za upande mmoja. Hata Monduli jana mgogoro ulikua huo huo, wenyewe kwa wenyewe mkaanza kutuhumiana na kutokuaminiana mkataka kubadilisha mawakala tena. Walivyoenda ofisi ya Mkurugenzi walipomkosa, wakasema kawakimbia.

Zamani lema Arusha Mjini, alikua anakuja na mawakala wake asubuhi siku ya Uchaguzi ili kukwepa kujulikana. Walikua wakifika vituoni wanaonyesha barua za chama kuwateua na vitambulisho vyao basi, wanaruhusiwa kuingia vituoni. Baada ya utaratibu kuanza kufuatwa, huo ujinga haupo tena mawakala wote lazima watambulike mapema ndo maana unaona malalamiko yote haya.
Now that every one says the vote was rigged I request Chadema leadership to come out and reveal these Mazingaombwes that are frustrating every reasonable being..
 
Kwa matokeo haya ya Ubunge ni bora CHADEMA wajitoe tu kwenye siasa na waanzishe SACCOS au VIKOBA itawasaida kuliko kuwa na chama cha kisiasa. Wachagga na siasa wapi na wapi, nyie akina Mbowe fanyeni biashara ndiyo kipaji chenu, muoneni mwenzenu R. Mengi amejikita kwenye biashara na anatusua mapene!!
Matokeo yapi? Matokeo ya kweli chadema wameshinda iweje waacha siasa kisa matokeo ya kuchakachua kwa kutumia Polisi na NEC, tambua kuwa wananchi wa ukonga waliwapigia kura chadema lakini CCM kwa kuwatumia Polisi wamepora ushindi wa chadema, watanzania wanajua upinzani una nguvu na kama si CCM kuwapora ushindi leo hii upinzani ungekuwa na wabunge wengi.
 
Wakati kura zinaibiwa wewe unakuwa wapi? Kazi ya wakala ni nini?
Wakala wanafanyiwa visa na mizengwe kibao huko wewe Polisi wa CCM, wakuu wa mikoa. Wilaya na wakurugenzi wa CCM wakizuia kukaa mita 200 kulinda kura.
 
kunawatu hawakuutaka huu mfumo wa vyama vingi,yanaitajika mabadiliko meengi kuweka ushindani wa kisiasa uwe sawa,(mzani hauja balance),out of that,ningumu ngumu kushindana nao hao jamaa na wanajipanga vilivyo.
Hawajajipanga vilivyo ni Polisi na NEC wanapora ushindi tu, wananchi wanatimiza wajibu wao kwa kuwapa kura nyingi chadema na upinzani kwa ujumla lakini CCM Polisi na NEC hupora ushindi kwa njia za kibabe na nguvu.
 
Kwa margin hii kubwa sana ya ushindi (76,000 vs 8,000 na 65,000 versus 3,000), ni dhahiri kwamba:

1: Ushindi huo haukutokana na wizi wa kura kama ambavyo chadema walivyotaka kuwaaminisha wanainchi. Kwa mbinu ye yote ile huwezi ukaiba kura zote hizo, yaani almost 100% ya kura zote uziibe. It is impossible.

2: Baadhi ya mawakala wa chadema kukamatwa wakiwa na bastola na mapanga, ni ushahidi tosha kuwa chadema ndiyo walikuwa wakiiba kura na kuteka watu. Yaani walikuwa wanaiba kura kwa mbinu zote ikiwemo hata ya mtutu wa bunduki! Ikumbukwe kuwa kwa mura, panga ni silaha nzito kuliko hata SMG au AK47. Ndiyo maana chadema wanapenda sana mura, sasa mura kawageuzia kibao na kunasa silaha hizo nzito. Wamekwisha!
 
Back
Top Bottom