Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Status
Not open for further replies.
Aksante mkuu ila hawa ITV siyo wakutegemea sana wanabadilika kulingana na ukali wa jua! Mbona kampeni za CDM walikuwa hawaonyeshi wanatoa kiduchu tu wana tafuta wapi Magamba hawa ni wapuuzi wakati mwingine wakiona uchakachuaji unahitajika mtaona wata-stop kabisa!
 
duuuh! reporter wa mlimani tv kutoka igunga anasema watu wazima na wakina mama ndio wamejitokeza kwa wingi kupiga kura, vijana sio wengi kama walivyokuwa wakijitokeza kwenye mikotano, katika hali kama hii magamba wanaweza ibuka kidedea.
 
Updates:
-Watu wamefurika vituoni
-CCM wanaonekana kushinda
-Wale vijana wa Magwanda wamezuiliwa kuingia
-Kafumu ashangikiwa sana
- Magwanda hoi, njaa kali

We mwita25 bogus kabisa, nani athubutu kushangilia wakati wa upigaji kura? Una maID mengi hadi unajichanganya mwenyewe mwisho wa posho umewadia hakutakuwa na cha kuripoti baada ya uchaguzi huu.
 
Asubuhi nimefika hapa mjini Igunga nikitokea mji mdogo wa ZIBA, huko hali shwari vijana wamefurika kwenye vituo vya kupigia kura karibu vyote hapa mjini ila kwenye miji midogo ya MWISI, NGONGORO, SAKAMALIWA, IGURUBI, CHOMACHANKORO, juzi na jana hali nilishuhudia ilikuwa safi.

Nimefika Igunga wiki hii na nimefanya utafiti katika sehemu tajwa hapo juu. Nimewahoji wananchi 53 kila mji. CHADEMA imeteka Igunga kama kweli uchaguzi utafanyika kwa amani na "usawa" leo. Ila walimu walioanza kazi mwaka jana wa Igunga wamezuiwa kupiga kura. Wenyewe wanalalamika kunyimwa fursa ya kumchagua mwalimu mwenzao. Nitaupdate wakati wa kukusanya idadi ya kura matokeo.

Nimeacha namba zangu za simu ktk miji yote ya igunga.
 
Wakubwa mliopo eneo la tukio endeleeni kutupa habari angalieni movement zote zinazofanyika. Makarani wawe makini, 2010 nilisimamia uchaguzi huku Morogoro kuna wengine walikuja na shahada za marehemu chunguzeni kila kitu kwa uangalifu mara nyingine vyombo vya usalama hujifanya wako likizo kana kwamba hawaoni upumbavu unaofanyika due to their personal interest cha msingi umma wa watanzania unaangalia nini kinafanyika igunga hatua kwa hatua hivyo jitahidini kuwa wakweli kila tukio linalo fanyika.

Aidha zaidi ya yote tuzidi kumwomba Mungu asimamie uchaguzi huu ili haki ikatendeke na amani itawale katika hatua zote jeshi la polisi wanalojukumu kubwa kuhakikisha usalama wa raia na kura zao ajira walio nayo ni kwa neema ya Mungu hivyo wasiposimamia majukumu yao vizuri mungu anawaona hata mti usiotoa matunda hukatwa hata sisi wanadamu ni kama mti mbele za Mungu tusipotenda yatupasayo kwa uaminifu kwa kufuata sheria za nchi na amri za mwenyezi Mungu tutakatwa.

Kumbukeni ni watu wangapi wamekufa lakini wewe ni mzima hata sasa hujabaki iliufanye uovu utakaowaghalimu wanaigunga na watanzania kwa ujumla narudia tena usalama wa taifa na jeshi kwa ujumla msigeuke mamluki mkamkosea mungu wenu na watanzania kwa ujumla
 
hauoni kuwa mnawakosesha haki yao ya kupiga kura?
Nawashauri mara nyingine msirudie hiyo dhambi, jaribuni kuwaelimisha then muwape nafasi ya kuchagua hatima ya masha yao. Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli!!!!
Wameshindwa kupokea Elimu ya kuzikataa Tshirt, Kanga na Vilemba vya rangi ya njano na kijani magamba wanavyotumia kama chambo kuwanasa. Hatuna ujanja zaidi ya kutumia mbinu walizotuachia babu zetu, hadi pale TAKUKURU watakapoanza kuzuia rushwa ya manguo ya njano na buku buku za magamba. When one door is closed others are open
 
naamini safari hii nguvu ya umma itaongea...Wana-Igunga amkeni kumekucha achaneni na mazoea
make it today or never!!!
 
Asubuhi nimefika hapa mjini Igunga nikitokea mji mdogo wa ZIBA, huko hali shwari vijana wamefurika kwenye vituo vya kupigia kura karibu vyote hapa mjini ila kwenye miji midogo ya MWISI, NGONGORO, SAKAMALIWA, IGURUBI, CHOMACHANKORO, juzi na jana hali nilishuhudia ilikuwa safi. Nimefika Igunga wiki hii na nimefanya utafiti katika sehemu tajwa hapo juu. Nimewahoji wananchi 53 kila mji. CHADEMA imeteka Igunga kama kweli uchaguzi utafanyika kwa amani na "usawa" leo. Ila walimu walioanza kazi mwaka jana wa Igunga wamezuiwa kupiga kura. Wenyewe wanalalamika kunyimwa fursa ya kumchagua mwalimu mwenzao. Nitaupdate wakati wa kukusanya idadi ya kura matokeo. nimeacha namba zangu za simu ktk miji yote ya igunga.

weka namba yako jamvini tukupigie mkuu.
 
Updates:
-Watu wamefurika vituoni
-CCM wanaonekana kushinda
-Wale vijana wa Magwanda wamezuiliwa kuingia
-Kafumu ashangikiwa sana
- Magwanda hoi, njaa kali

mwita25, vijana wamezuiliwa,kafumu anashangikiwa..hebu fafanua je kwanini wamezuiliwa na kwanini kafumu anashangikiwa kama sikosei unaimanisha ana shangiliwa inamaana kampeni zinaendelea..
 
Wabeja sana Namhala Wa Jikoni...

Wana Igunga naona wameishabugi step, kama wameachia akina mama waende kupiga kura ujue tayari wameishachagua magamba. Kule Tarime na Musoma mjini huwa tunawaibia hawa akina mama vitambulisho vyao hadi sa12 jioni ili wasiende kukipigia kura chama cha magamba

Domokrasia ipigiwayo debe na CDM hii.
Pambaf.
OTIS.
 
vijana wanaonekana wametanda vituoni wakitaka kupiga kura sijui kwanini idadi ya wamama na wazee imepungua kwenye kupiga kura labda tungoje pengine wamama na wazee bado hawajaamka au walikuwa na mtazamo wa kunaweza kuwa na vurugu
 
Ndugu zetu wananchi wa Igunga chonde chonde chonde sana tunawaomba msithubutu kuchagua CCM kwani ni maafa makubwa kuiweka sisiem madarakana hasa kwa wakati huu tulionao sasa ambapo maisha yamekuwa magumu kupindukia sababu ya sera mbovu za ccm, ufisadi umeshamiri hali inayorudisha nyuma maendelea ya nchi yetu.
Angalieni, mahakana imebariki Dowans kulipwa mabilion ya pesa wakati nchi iko gizani kwa muda mrefu sasa, hakuna umeme na kero nyingine nyingi sana ambazo zimetokana na serikali legelege ya ccm.
wakati wa ukombozi ni sasa.
 
Updates:
-Watu wamefurika vituoni
-CCM wanaonekana kushinda
-Wale vijana wa Magwanda wamezuiliwa kuingia
-Kafumu ashangikiwa sana
- Magwanda hoi, njaa kali
Njaa kali ni kwa kila mtanzania tangu JK ameingia madarakani, ndio maana wananchi wa Igunga wameamua kuikataa njaa kwa kutupilia shimoni CCM. Wewe si unajikomba unafikiri utakaombolewa kupata u senior lecturer huku ukiwa na hako kaelimu kadogo, hakuna hiyo kitu.
Wana wa Igunga mungu yu pamoja nanyi fanyeni maamuzi sahihi kuikataa njaa na uhaba wa maji
 
mwita25, vijana wamezuiliwa,kafumu anashangikiwa..hebu fafanua je kwanini wamezuiliwa na kwanini kafumu anashangikiwa kama sikosei unaimanisha ana shangiliwa inamaana kampeni zinaendelea..
Mbona simu kutoka igunga zinasema vijana wamejitokeza sana?
 
ITV: wakaazi wa Igunga hasa vijana wanaotaka mabadiliko wamejitokeza kwa wingi na kuna misururu mirefu kwenye vituo kupiga kura
 
Vipi mitaani hakuna magari ya kuwasha na polisi wenye silaha kwa ajili ya kutisha wapiga kura?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom