Uchaguzi Kenya: Nani atakuwa rais mpya

Pwaaaa

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
248
67
Imebaki siku moja tu ya kesho wananchi wa kenya wafanye uchaguzi wa kumpata rais wao mpya. Swali langu kwa wana jf ni hili, nani atashinda na kuwa rais mpya wa kenya kati ya wagombea wote waliopo?. Mwaga maoni yako sasa!.
 
opions polls zote zilizoendeshwa mpaka muda wa mwisho kabisa inaonesha hakutakuwa na mshindi kwenye first round of voting. Kwa maana ya kwamba Bwana Raila na Uhuru wanategemewa kupata kupata kura zaidi ya asilimia 40% lakini hazizidi asilimia 50%.

Ila ajabu ni kwamba Bwana Mudavadi consistently amekuwa akitabariwa atapata kura za asilimia kati ya 4% mpaka 5%.

ikumbukwe kuwa uchaguzi wa Kenya hakuna issu of Simple Majority lazima mshindi apate zaidi ya asilimia 50%.

Kwa maana hiyo wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema Bwana Mudavadi ana hodhi mtaji TOSHA kwenye siasa za Kenya. IKumbukwe kuwa muungano wa Jubilee walimtapeli Bwana Mudavadi kuwa angekuwa mgombe wao. Vile vile Bwana Mudavadi baada ya kuhisi kuwa asingepita kwenye chama cha ODM cha Raila kuwa mgombea Uraisi aliamua kuondoka mapema kabla ya michakato ya uchaguzi ndani ya chama haijaanza.

Sasa swali ni kuwa kwenye second round of voting Bwana Mudavadi ataenda PANDE IPI?

JUBILEE ya UHURU ambao walimpateli kuwa angekuwa MGOMBEA WAO WA URAIS au CORD ambako aliondoka mapema baada ya kuhisi kuwa asingekuwa na nafasi ya kupata TIKETI ya kugombea URAISI.

Ila Afrika ina miujuza mingi you never know lolote laweza kutokea kwenye FIRST ROUND OF VOTING !
 
Imebaki siku moja tu ya kesho wananchi wa kenya wafanye uchaguzi wa kumpata rais wao mpya. Swali langu kwa wana jf ni hili, nani atashinda na kuwa rais mpya wa kenya kati ya wagombea wote waliopo?. Mwaga maoni yako sasa!.

Winner is Raila.
 
Kenya is for Kenyans and the future of Kenya is in the hands of the Kenyan Voters. Kwa democrasia ya Kenya ilivyokua na ilivyowazi basi the winner takes all and the Contestant with majority voters will in no doubt be announced a President elect! Siyo kama ya kwetu,wizi mtupu!!!!
 
JF siku hizi ndo wapiga kura wa Kenya? au ndo shekhe Yahaya wa Kenya????
 
Kesho wananchi wa Kenya wenye kukidhi vigezo vya kupiga kura watapiga kura kuchagua Rais na wabunge kutoka vyama mbali mbali.Mashirika mbali mbali yameshatoa tabiri ingawa yote yanaonyesha hakuta kuwa na mshindi katika round ya kwanza,Mshindi atatakiwa kushinda kwa zaidi ya 50%.Bwana Raila Odinga na Uhuru Kenyatta wanachua vikali uenda uchaguzi ukarejelewa kutafuta mshndi kati ya Raila na Uhuru.

Lolote laweza kutokea iwapo uchaguzi utarudiwa,Bwana Mudavadi akimuunga mkono mmoja wapo wa wagombea kati ya Uhuru na Raila aweza kuwa Rais wa Kenya.
 
Back
Top Bottom