Uchaguzi 2020 Ubunge Rorya 2025: Wenje tafadhali sana kachukue Jimbo

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Wakuu habari za asubuhi!

Siku chache zilizopita nilisoma uzi mrefu wa mwanajukwaa moja aliyejitambulisha kama mwalimu wa chuo cha MIST huko Mbeya na mzaliwa wa Rorya Mkoa wa Mara. Alieleza kinaga ubaga jinsi wilaya hiyo inavyotafunwa na makundi ya kitarafa linapokuja suala la uchaguzi akisema tarafa ya Girango na Luo Imbo kuwa ziko kwenye kundi la wateule na zile za Suba na Nyancha zikiwa kwenye kundi la watengwa. Labda kwavile toka alipozaliwa huyo mleta mada Wabunge wengi wametokea kwenye tarafa hizo mbili ukiacha mwaka 1995 ambapo mheshimiwa Mabere Marando kutoka Nyancha alipokuwa mbunge, kabla ya hapo Mbunge wa Muda mrefu alikuwa Oyombe Aila aliyetoka kowaki (Luo Imbo) na baadaye Prof Sarungi 2000 hadi 2010 na Lemeck Okambo Airo 2010 hadi leo.

Tukija kwenye suala la maendeleo Rorya nzima ni wilaya masikini, wenye watu masikini na ujinga ukitamalaki miongoni mwa wakaazi wake. Hakuna penye unafuu si hizo tarafa alizoziita Wateule au Watengwa rorya nzima maisha ya watu ni mabaya na wanaogelea kwenye umasikini mkubwa. Sababu ya umasikini wa Rorya kubwa hasa ni kutokana historia ya nyuma ambapo kabla ya tarehe 1/7/2007 wilaya hii ilikuwa sehemu ya wilaya ya Tarime, viongozi wa wakati huo (wakurya wakiwa wengi) walielekeza nguvu zao kujenga na kupeleka maendeleo Tarime kuliko Rorya.

Wizi mkubwa wa mifugo uliokuwa unafanywa ukishirikisha wakazi wa Rorya , wakazi wa Tarime na watu kutoka Kenya. Wakati huo wakazi wengi sana wa Rorya waliibiwa ng'ombe na hata wengine kuuwawa kikatili sana wakipigania mifugo yao. Sababu nyingine ya umasikini wa wana Rorya ni ukosefu wa mazao ya biashara. Nimetembea Rorya kwa kiwango cha kutosha watu wanalima mazo ya chakula kwa wingi kuliko mazao ya biashara. Mfano ukienda tarafa ya Girango yote kilimo kikubwa ni mihogo na mahindi tena kwa kiwango cha chakula tu. Kule Nyancha wanategemea kilimo kidogo na uvuvi wa samaki ambao nao hufanywa kwa kiwango duni sana. Kwa ujumla Rorya ukiona kilimo cha kahawa, alzeti au zao lolote la biashara basi ni kwa uchache sana.

Umasikini pia umechangiwa na ukosefu wa elimu bora, watu wa Rorya bado hawajapata shule ya kutosha. Wenye elimu wamejichimbia mijini wasiwe na msaada nyumbani na kibaya zaidi mtu wa Rorya akiwa na hela au kazi nzuri anataka yeye ndiye awe juu wengine wampigie tu magoti hawezi kunyanyua wenzake. Sababu nyingine ya umasikini wa rorya ni utamaduni mbovu wa jamii kuanzia kuoa wanawake wengi (ndoa za mitara), kuzaa watoto wengi , uchepukaji usio wa kawaida na pombe.

Rorya mara zote imechagua viongozi wabovu kwa kiwango kikubwa kuwawakilisha hali iliyochangia kukwama kwa wilaya hiyo kiuchumi. Hata Prof Sarungi hakufanya vya kutosha wakati akiwa mbunge na waziri, cha maana alichokifanya labda ni kupigania Rorya iwe wilaya , kupigania kuanzishwa kwa kanda maalumu ya Rorya/ Tarime ambayo imeleta amani na utulivu kwa sehemu lakini bado ujinga uliendelea kutamalaki miongoni mwa jamii ya watu. Amecha ubunge wakati Rorya ikigeuka kama jangwa kutokana na ukataji holela wa miti. Wote wameshindwa pakubwa kupigania Ranch ya utegi kuendelea na kazi ili kuzalisha ajira kwa raia, wote wameshindwa kushawishi wananachi kuacha mila mbovu zinazowadidimiza hasa ndoa za mitaara, kurithi wanawake, kuzaa watoto wengi kisha huwaendelezi, kuhamasisha watoto kusoma kwa kutoa motisha , kubuni na kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo cha biashara, na mengine mengi. Nawapongeza kwa yale waliyoyafanya ila Rorya inapiga hatua kwa uchache sana.

KWANINI WENJE AKACHUKUE JIMBO LILE
Kazi kubwa ya mbunge ni kuwasemea wananchi, kuwakilisha mawazo ya wananchi bungeni ili serikali iweze kufanyia kazi mawazo hayo, kubuni shughuli za maendeleo na kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo . Mbunge anatakiwa kuwa karibu na watu wake ili kujua changamoto zao na washirikiane kuyatatua. Kuna changamoto ambazo lazima serikali ndiyo itatue maana zinahitaji hela nyingi mfano kuleta umeme, miradi ya maji , hospitali nk lakini pia kuna miradi mbunge anaweza kubuni kisha akatafuta wahisani au akahamasisha wananchi na zikafanyika mfano utunzaji wa mazingira, vyanzo vya maji, kuhamasisha vijana kusoma kwa bidii na kwa malengo, kuhubiri ubovu wa mila na desturi mbaya , kuhamasisha watu kufanya kazi kwa kujituma miongoni mwa mengine.

Nina imani kwa Geografia ya wilaya na historia ya miaka 30 zilizopita Wenje akigombea kwa tiketi ya CHADEMA atashinda ubunge mchana kweupe, maana najua CCM bado watamrudisha LAKAIRO ambaye si kwamba hana nguvu bali kushindwa na WENJE ni kazi ndogo kuliko kushindwa na mwingine yeyote atakayegombea mfano OWAWA. Sababu ni rahis sana huyu Owawa aligombea mwaka 2015 na alitoa ushindani mkubwa sana ila tatizo anatoka tarafa moja na LAKAIRO tena jamaa Kaoa huko kwao hivyo ni vigumu sana kumshinda kwenye tarafa hiyo lakini wenje anauwezo wa kushinda Lakairo au yeyote yule kule Nyancha kisha akaokota kura kwenye tarafa nyingine na kwa hakika atashinda mchana kweupe.

WENJE KAMA UTAGOMBEA NA KUSHINDA USIJE UKASAHAU NA HAYA
1. Usiende kuvutana na serikali bali kashirikiane na serikali yoyote itakayoshinda ili kuishawishi kwa pamoja mlete maendeleo Rorya. Kumbuka Mbunge hana hela na bila support ya serikali hakuna unachoweza kukifanya.

2. Ujitahidi sana ndugu yangu ile bara bara ya Mika -Utegi -Shirati hadi Mpakani Kirongwe iwe lami (hapa ni kuishawishi serikali umuhimu wa barababra hii inayounganisha Rorya na Kenya).

3. Ushawishi serikali kujenga Meli za zise ya kutosha kutoka shirati kwenda Uganda na Kisumu na nyingine Shirati kwenda MUSOMA. Hii itainua Rorya kibiashara pakubwa sana (Inaweza kuonekana ngumu sana ila inawezekana maana hata watu binafsi wakishauriwa na kushawishiwa vyema watawekeza tu sehemu moja wapo).

4. Barabara ya kutoka Tarime kwenda Shirati kupitia bungire (Rodi)- Panyakoo- Masonga ijengwe kwa moram nzuri ili ipitike wakati wote bila kusahau barabara ya Utegi-Mirare-Changuge-Rodi hadi Mpakani na Kenya. Barabara ya Bukama kwenda mialo yote ya upande wa Nyarombe, Busanga nk ziwe kwa kiwango kizuri cha changarawe bila kusahau Barabara ya Utegi -kowaki-kwenda kinesi.

5. Mkuu ukazanie sana suala la utunzaji wa mazingira ukataji miti hovyo unaoendelea Rorya ni hatari sana.

6. Ushawishi watu kubadili namna ya kufuga ukizingatia watu washakuwa wengi kuliko ardhi badala ya mtu kuwa na ng'ombe wengi wape semina juu ya ufugaji wenye tija hasa wa ng'ombe, mbuzi, kuku na bata na ikiwezekana watafutie hata masoko Mwanza, Shirati , Musoma na hata Kenya hasa Kisumu.

7. Hamasisha sana juu ya elimu bora kwa vijana wetu , unaweza kuanzisha programs za garama nafuu kama kushindanisha shule na inayofanya vizuri unawapa hata mbuzi 2 au ng'ombe. Kutafuta wadhamini kumsomesha mtoto anayefanya vizuri kwa kila shule na zawadi kidogo kwa waalimu na shule zinazofanya vizuri.

8. Kashirikiane na serikali kutokomeza ndoa za utotoni, wanafunzi kupewa mimba na kuolewa kabla ya muda hili ni janga Rorya.

9. Kuhamasisha kilimo cha mazao ya biashara ili watu waachane na kilimo cha kujikimu tu. Pili unaweza kushirikiana na halmashauri. Muwapelekee wananchi mbengu bora za mihogo kama inayolimwa KISARAWE kuliko mbegu za hovyo zinazolimwa huko nyumbani.

10. Ujitahidi kuwe na shule za serikali walau 4 ( za Advance) moja kwa kila tarafa na walau shule moja ya wasichana.

11. Ujitahidi kuwe na ambulance pale Shirati hospital , utegi hospital na moja iwepo kule Kinesi

12. Ujitahidi kusukumu juhudi za kufufua Ranchi ya Utegi na kiwanda chake bila kusahau Ranchi ya Komuge

13.Ujenzi wa masoko mazuri shirati, randa, Kinesi, Ochuna nk

14. Maji safi na Salama (hili ni tatizo Rorya nzima)

15. Mawasiliano mazuri ya simu

16. Kashirikiane na Halmashauri na Serikali kuweka soko kubwa la samaki na ikiwezekana ujenzi wa kiwanda cha kuchakata samaki Busanga au nyamagaro

Na mengine mengine, nakutakia kila la heri na nawatakia wagombea wote wenye nia njema na Rorya awe CCM au CDM kila la heri

Kwanini nasema wenje na si mwingine?
Wenje anabebwa na eneo analotoka hasa ukizingatia wabunge karibia kwa miaka 20 wametoka eneo la utegi na miaka ya nyuma kabla ya 1995-2000 mbunge alikuwa wa jirani na utegi kwahiyo kule ziwani (nyancha) wamemis kupata mbunge na kwavile CCM watampitisha Lakairo tena basi wenje ana nafasi au mtu yeyote mzuri atakayeteuliwa na CHADEMA anayetokea Nyancha ila asiwe mgeni sana huko.

Pili tunataka msemaji wetu, mtu atakayepiga kelele juu ya mambo ya hovyo yanayoendelea, mbunifu na mwenye maono,kiongozi na muhamasishaji LAKINI MWENYE KUSHIRIKIANA NA SERIKALI si kugombana kila wakati. Ikitokea Wenje ukashinda tafadhali ukaishi Rorya muda mwingi ili ukawe karibu na watu na wakati wa mapumziko ukajenge chama.

NB: Haya ni maoni yangu binafsi sina interest na mtu maana mwenyewe ni mtegi tena jirani na Lakairo, ni mpenda maendeleo na muumini wa mabadiliko, muumuni wa maendeleo jumuishi yanayochangiwa na jamii na si kuletwa na mtu. CCM ikishinda sawa japo wametuangusha pakubwa kwa kutuwekea mwenyekiti wa CCM mkoa darasa la saba, mwenyekiti wa CCM wilaya darasa la saba, mbunge darasa la saba , mwenyekiti wa halmashauri darasa la saba na madiwani karibia 80% ni darasa la saba hapo maendeleo yatatoka wapi?

Kidikwili-Masasi
 
Uliyoyanena kuhusu Rorya ni ukweli mtupu tena wewe ni mwenyeji wa huko.

Nami naunga mkono tatizo ni tume yetu haiaminiki. Inaelekezwa ni nani wa kumpitisha . Na fitna ya wafanyabiashara wanao hakikisha wanaitawala wilaya ya Rorya, akiwemo mbunge wa sasa . Ambaye ameweka rekodi ya kutoka bungeni miaka 10 bila kutoa mchango wowote wa mawazo yake .

Kwa kweli Rorya inahitaji mabadiliko. Rorya tunayo shule nzuri ya waschana ya
Kowack girls. Lakini wanaosomesha watoto pale si wana Rorya ajabu na kweli .
 
Rorya kwa mara nyingine tena..Lakairo anaiva na jiwe anaweza kupitishwa tena na ccm alafu wanaRorya wakapate mateso mengine ya miaka 5.
 
Muda wa kujipigia debe huu. Ha ha ha

Ndugu mimi si ndugu Wenje hata kidogo wala sijui akina wenje wanaishi sehemu gani ila ninachojua ni kwamba akipewa nafasi rorya atashinda mchana kweupe. Simpigii debe huu ndiyo ukweli
 
yaani bubu Lameck Airo naye ni Mbunge 😂😂😂 Rorya siasa za "MA JADALA" mtaishia kuambukizana tu Ukimwi wenzenu wanaingia Uchumi wa Kati.

Mkuu kwa taarifa nilizozipata ni kwamba Juzi wakizindua hospitali ya wilaya pale Ingri juu alisema wazi hatagombea tena, hili kalisema mbele ya kadamnasi ila wakati naandika uzi nilikuwa sijaipata rasmi najua atakuwa upande wa Mjomba wake Ndugu David Wembe ambaye alikuwa akilinyemelea jimbo kwa muda mrefu
 
Mkono wa la kairo ni mrefu sana rorya. usipotembeeza noti sidhani kama wananchi watakuelewa..Rorya imezungukwa na jamii maskini zaidi na wengi hawajasoma kwahiyo ni vyepesi kurubuniwa wenje ajipange kwa kweli....
 
Uliyoyanena kuhusu Rorya ni ukweli mtupu tena wewe ni mwenyeji wa huko.

Nami naunga mkono tatizo ni tume yetu haiaminiki. Inaelekezwa ni nani wa kumpitisha . Na fitna ya wafanyabiashara wanao hakikisha wanaitawala wilaya ya Rorya, akiwemo mbunge wa sasa . Ambaye ameweka rekodi ya kutoka bungeni miaka 10 bila kutoa mchango wowote wa mawazo yake .

Kwa kweli Rorya inahitaji mabadiliko. Rorya tunayo shule nzuri ya waschana ya
Kowack girls. Lakini wanaosomesha watoto pale si wana Rorya ajabu na kweli .
Odhiambo mbona unatumia jina kama la familia ya Lameck mna undugu?, matatizo ya Rorya nayajua na nimeyaishi vizuri sana. Yaani CHADEMA wamtoe mgombea kutoka Ukanda wa ziwa victoria halafu aje azidiwe na watu wa Girango kwasasa? Si rahisi kwa mtazamo wangu sababu ziko wazi kabisa labda wahonge kuanzia Randa hadi ziwani
 
Mkono wa la kairo ni mrefu sana rorya. usipotembeeza noti sidhani kama wananchi watakuelewa..Rorya imezungukwa na jamii maskini zaidi na wengi hawajasoma kwahiyo ni vyepesi kurubuniwa wenje ajipange kwa kweli....
Ni kweli ndugu Opondo ila watu wameanza kumchoka Lameck na kwa taarifa nilizozipata hivi punde ni kwamba alitangaza hagombei tena, sasa huu ndiyo muda mzuri wa CDM kuchukua lile jimbo. Watu ni masikini na habari za "gonywa"ziko nyingi wakati huu ila jimbo liko wazi sana kwasasa
 
Mkono wa la kairo ni mrefu sana rorya. usipotembeeza noti sidhani kama wananchi watakuelewa..Rorya imezungukwa na jamii maskini zaidi na wengi hawajasoma kwahiyo ni vyepesi kurubuniwa wenje ajipange kwa kweli....
eeh
 
H
Wakuu habari za asubuhi!

Siku chache zilizopita nilisoma uzi mrefu wa mwanajukwaa moja aliyejitambulisha kama mwalimu wa chuo cha MIST huko Mbeya na mzaliwa wa Rorya Mkoa wa Mara. Alieleza kinaga ubaga jinsi wilaya hiyo inavyotafunwa na makundi ya kitarafa linapokuja suala la uchaguzi akisema tarafa ya Girango na Luo Imbo kuwa ziko kwenye kundi la wateule na zile za Suba na Nyancha zikiwa kwenye kundi la watengwa. Labda kwavile toka alipozaliwa huyo mleta mada Wabunge wengi wametokea kwenye tarafa hizo mbili ukiacha mwaka 1995 ambapo mheshimiwa Mabere Marando kutoka Nyancha alipokuwa mbunge, kabla ya hapo Mbunge wa Muda mrefu alikuwa Oyombe Aila aliyetoka kowaki (Luo Imbo) na baadaye Prof Sarungi 2000 hadi 2010 na Lemeck Okambo Airo 2010 hadi leo.

Tukija kwenye suala la maendeleo Rorya nzima ni wilaya masikini, wenye watu masikini na ujinga ukitamalaki miongoni mwa wakaazi wake. Hakuna penye unafuu si hizo tarafa alizoziita Wateule au Watengwa rorya nzima maisha ya watu ni mabaya na wanaogelea kwenye umasikini mkubwa. Sababu ya umasikini wa Rorya kubwa hasa ni kutokana historia ya nyuma ambapo kabla ya tarehe 1/7/2007 wilaya hii ilikuwa sehemu ya wilaya ya Tarime, viongozi wa wakati huo (wakurya wakiwa wengi) walielekeza nguvu zao kujenga na kupeleka maendeleo Tarime kuliko Rorya.

Wizi mkubwa wa mifugo uliokuwa unafanywa ukishirikisha wakazi wa Rorya , wakazi wa Tarime na watu kutoka Kenya. Wakati huo wakazi wengi sana wa Rorya waliibiwa ng'ombe na hata wengine kuuwawa kikatili sana wakipigania mifugo yao. Sababu nyingine ya umasikini wa wana Rorya ni ukosefu wa mazao ya biashara. Nimetembea Rorya kwa kiwango cha kutosha watu wanalima mazo ya chakula kwa wingi kuliko mazao ya biashara. Mfano ukienda tarafa ya Girango yote kilimo kikubwa ni mihogo na mahindi tena kwa kiwango cha chakula tu. Kule Nyancha wanategemea kilimo kidogo na uvuvi wa samaki ambao nao hufanywa kwa kiwango duni sana. Kwa ujumla Rorya ukiona kilimo cha kahawa, alzeti au zao lolote la biashara basi ni kwa uchache sana.

Umasikini pia umechangiwa na ukosefu wa elimu bora, watu wa Rorya bado hawajapata shule ya kutosha. Wenye elimu wamejichimbia mijini wasiwe na msaada nyumbani na kibaya zaidi mtu wa Rorya akiwa na hela au kazi nzuri anataka yeye ndiye awe juu wengine wampigie tu magoti hawezi kunyanyua wenzake. Sababu nyingine ya umasikini wa rorya ni utamaduni mbovu wa jamii kuanzia kuoa wanawake wengi (ndoa za mitara), kuzaa watoto wengi , uchepukaji usio wa kawaida na pombe.

Rorya mara zote imechagua viongozi wabovu kwa kiwango kikubwa kuwawakilisha hali iliyochangia kukwama kwa wilaya hiyo kiuchumi. Hata Prof Sarungi hakufanya vya kutosha wakati akiwa mbunge na waziri, cha maana alichokifanya labda ni kupigania Rorya iwe wilaya , kupigania kuanzishwa kwa kanda maalumu ya Rorya/ Tarime ambayo imeleta amani na utulivu kwa sehemu lakini bado ujinga uliendelea kutamalaki miongoni mwa jamii ya watu. Amecha ubunge wakati Rorya ikigeuka kama jangwa kutokana na ukataji holela wa miti. Wote wameshindwa pakubwa kupigania Ranch ya utegi kuendelea na kazi ili kuzalisha ajira kwa raia, wote wameshindwa kushawishi wananachi kuacha mila mbovu zinazowadidimiza hasa ndoa za mitaara, kurithi wanawake, kuzaa watoto wengi kisha huwaendelezi, kuhamasisha watoto kusoma kwa kutoa motisha , kubuni na kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo cha biashara, na mengine mengi. Nawapongeza kwa yale waliyoyafanya ila Rorya inapiga hatua kwa uchache sana.

KWANINI WENJE AKACHUKUE JIMBO LILE
Kazi kubwa ya mbunge ni kuwasemea wananchi, kuwakilisha mawazo ya wananchi bungeni ili serikali iweze kufanyia kazi mawazo hayo, kubuni shughuli za maendeleo na kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo . Mbunge anatakiwa kuwa karibu na watu wake ili kujua changamoto zao na washirikiane kuyatatua. Kuna changamoto ambazo lazima serikali ndiyo itatue maana zinahitaji hela nyingi mfano kuleta umeme, miradi ya maji , hospitali nk lakini pia kuna miradi mbunge anaweza kubuni kisha akatafuta wahisani au akahamasisha wananchi na zikafanyika mfano utunzaji wa mazingira, vyanzo vya maji, kuhamasisha vijana kusoma kwa bidii na kwa malengo, kuhubiri ubovu wa mila na desturi mbaya , kuhamasisha watu kufanya kazi kwa kujituma miongoni mwa mengine.

Nina imani kwa Geografia ya wilaya na historia ya miaka 30 zilizopita Wenje akigombea kwa tiketi ya CHADEMA atashinda ubunge mchana kweupe, maana najua CCM bado watamrudisha LAKAIRO ambaye si kwamba hana nguvu bali kushindwa na WENJE ni kazi ndogo kuliko kushindwa na mwingine yeyote atakayegombea mfano OWAWA. Sababu ni rahis sana huyu Owawa aligombea mwaka 2015 na alitoa ushindani mkubwa sana ila tatizo anatoka tarafa moja na LAKAIRO tena jamaa Kaoa huko kwao hivyo ni vigumu sana kumshinda kwenye tarafa hiyo lakini wenje anauwezo wa kushinda Lakairo au yeyote yule kule Nyancha kisha akaokota kura kwenye tarafa nyingine na kwa hakika atashinda mchana kweupe.

WENJE KAMA UTAGOMBEA NA KUSHINDA USIJE UKASAHAU NA HAYA
1. Usiende kuvutana na serikali bali kashirikiane na serikali yoyote itakayoshinda ili kuishawishi kwa pamoja mlete maendeleo Rorya. Kumbuka Mbunge hana hela na bila support ya serikali hakuna unachoweza kukifanya.

2. Ujitahidi sana ndugu yangu ile bara bara ya Mika -Utegi -Shirati hadi Mpakani Kirongwe iwe lami (hapa ni kuishawishi serikali umuhimu wa barababra hii inayounganisha Rorya na Kenya).

3. Ushawishi serikali kujenga Meli za zise ya kutosha kutoka shirati kwenda Uganda na Kisumu na nyingine Shirati kwenda MUSOMA. Hii itainua Rorya kibiashara pakubwa sana (Inaweza kuonekana ngumu sana ila inawezekana maana hata watu binafsi wakishauriwa na kushawishiwa vyema watawekeza tu sehemu moja wapo).

4. Barabara ya kutoka Tarime kwenda Shirati kupitia bungire (Rodi)- Panyakoo- Masonga ijengwe kwa moram nzuri ili ipitike wakati wote bila kusahau barabara ya Utegi-Mirare-Changuge-Rodi hadi Mpakani na Kenya. Barabara ya Bukama kwenda mialo yote ya upande wa Nyarombe, Busanga nk ziwe kwa kiwango kizuri cha changarawe bila kusahau Barabara ya Utegi -kowaki-kwenda kinesi.

5. Mkuu ukazanie sana suala la utunzaji wa mazingira ukataji miti hovyo unaoendelea Rorya ni hatari sana.

6. Ushawishi watu kubadili namna ya kufuga ukizingatia watu washakuwa wengi kuliko ardhi badala ya mtu kuwa na ng'ombe wengi wape semina juu ya ufugaji wenye tija hasa wa ng'ombe, mbuzi, kuku na bata na ikiwezekana watafutie hata masoko Mwanza, Shirati , Musoma na hata Kenya hasa Kisumu.

7. Hamasisha sana juu ya elimu bora kwa vijana wetu , unaweza kuanzisha programs za garama nafuu kama kushindanisha shule na inayofanya vizuri unawapa hata mbuzi 2 au ng'ombe. Kutafuta wadhamini kumsomesha mtoto anayefanya vizuri kwa kila shule na zawadi kidogo kwa waalimu na shule zinazofanya vizuri.

8. Kashirikiane na serikali kutokomeza ndoa za utotoni, wanafunzi kupewa mimba na kuolewa kabla ya muda hili ni janga Rorya.

9. Kuhamasisha kilimo cha mazao ya biashara ili watu waachane na kilimo cha kujikimu tu. Pili unaweza kushirikiana na halmashauri. Muwapelekee wananchi mbengu bora za mihogo kama inayolimwa KISARAWE kuliko mbegu za hovyo zinazolimwa huko nyumbani.

10. Ujitahidi kuwe na shule za serikali walau 4 ( za Advance) moja kwa kila tarafa na walau shule moja ya wasichana.

11. Ujitahidi kuwe na ambulance pale Shirati hospital , utegi hospital na moja iwepo kule Kinesi

12. Ujitahidi kusukumu juhudi za kufufua Ranchi ya Utegi na kiwanda chake bila kusahau Ranchi ya Komuge

13.Ujenzi wa masoko mazuri shirati, randa, Kinesi, Ochuna nk

14. Maji safi na Salama (hili ni tatizo Rorya nzima)

15. Mawasiliano mazuri ya simu

16. Kashirikiane na Halmashauri na Serikali kuweka soko kubwa la samaki na ikiwezekana ujenzi wa kiwanda cha kuchakata samaki Busanga au nyamagaro

Na mengine mengine, nakutakia kila la heri na nawatakia wagombea wote wenye nia njema na Rorya awe CCM au CDM kila la heri

Kwanini nasema wenje na si mwingine?
Wenje anabebwa na eneo analotoka hasa ukizingatia wabunge karibia kwa miaka 20 wametoka eneo la utegi na miaka ya nyuma kabla ya 1995-2000 mbunge alikuwa wa jirani na utegi kwahiyo kule ziwani (nyancha) wamemis kupata mbunge na kwavile CCM watampitisha Lakairo tena basi wenje ana nafasi au mtu yeyote mzuri atakayeteuliwa na CHADEMA anayetokea Nyancha ila asiwe mgeni sana huko.

Pili tunataka msemaji wetu, mtu atakayepiga kelele juu ya mambo ya hovyo yanayoendelea, mbunifu na mwenye maono,kiongozi na muhamasishaji LAKINI MWENYE KUSHIRIKIANA NA SERIKALI si kugombana kila wakati. Ikitokea Wenje ukashinda tafadhali ukaishi Rorya muda mwingi ili ukawe karibu na watu na wakati wa mapumziko ukajenge chama.

NB: Haya ni maoni yangu binafsi sina interest na mtu maana mwenyewe ni mtegi tena jirani na Lakairo, ni mpenda maendeleo na muumini wa mabadiliko, muumuni wa maendeleo jumuishi yanayochangiwa na jamii na si kuletwa na mtu. CCM ikishinda sawa japo wametuangusha pakubwa kwa kutuwekea mwenyekiti wa CCM mkoa darasa la saba, mwenyekiti wa CCM wilaya darasa la saba, mbunge darasa la saba , mwenyekiti wa halmashauri darasa la saba na madiwani karibia 80% ni darasa la saba hapo maendeleo yatatoka wapi?

Kidikwili-Masasi
Haya basi Wenje katuletee jimbo la Rorya mapema asubuhi.
 
Back
Top Bottom