UBINAFSISHAJI: BORA SHOES yakodishwa kuwa godown kisiri siri.

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,534
8,619
ubinafsishaji ni sera iliyoilazimu tanzania kufuata kuanzia miaka ya 1990...ikiwa ni sehemu ya urekebishaji wa uchumi[economic adjustment programmes]

ndani ya sera hii viwanda kama kiltex dar,kiltex arusha,tanzania lithol,pyrethrium,general tyre,tabora tex,mwanza tex,musoma tex,morogoro tex ....sungura tex,urafiki tex,ubungo garments....etc...

pia tunakumbuka viwanda kama Tanganyika parkers,tanganyika plastics[TEGRI],...BORA SHOES...

KWA leo naona bora nitoe mfano wa utapeli unaofanywa na hawa bora shoe...ambao wao walpewa kiwanda ili watengeneze viatu.....baada ya muda walisema viatu soko hakuna..wakasema watatengeneza malapa na magurudumu ya baiskeli....,lakini katika hali ya kusikitisha sasa hakuna uzalishaji wanaofanya bali WAMENGOA MITAMBO NA NAFASI ILIYOPATIKANA WAMEIKODISHA KWA WAFANYA BIASHARA MBALI MBALI KAMA MAGODOWN............Sasa watanzania tukiulize hivi ,hawa wawekezaji tuliwapa viwanda kwa bei chee ili wajeuze magodown au waendeleze viwanda tupate ajira?....inasikitisha sana...,hasa tunapokumbuka waziri wa biashara alipata kupita pale katika ziara ya kukagua viwanda vilivyobinafsishwa ..hasa vilivobadili matumizi.....ya mwanzo...

hali ya bora haina tofauti na tanganyika parckes na viwanda vingine vingi ambavo leo ni magodown.....na mitambo wameuza kama scrap......na kama pale kawe hana hata aibu anataka kuigeuza kuwa shoppin mall au aprtments .....sheria inasemaje....

nadhani ni bora serikali ikarudisha viwanda vyetu maana sheria inawalinda kwani wawekezaji wamekiuka makubaliano.....watanzania TUTAVIMILIKI UPYA VIWANDA VYETU KUPITIA SACCOS...AU USHIRIKANO AU HATA WATANZANIA BINAFSI WENYE MAPENZI NA NCHI YETU.......

NAWASILISHA UKWELI.......
 
Tatizo hatujui wakati wa huo ubinafsishaji MIKATABA ilisema nini?. Ndio maana kilio sasa ni mikataba iwe wazi kwa Wananchi...
 
Hakika kiwanda hiki ambacho muasisi wetu alikaa chini na kubuni vimegeuka kuwa kama magenge ya kuuzia nyanya. Sasa hiki kilichokuwa kikiitwa Bora Shoes leo ni magodown yanayokodishwa kwa makampuni ambayo hayana nafasi za kutosha katika viwanda vyao kama vile Kiwanda cha Sigara, Serengeti Brewaries na vinginevyo vingi.
Kaa chini tafakari............."Haki Elimu!!!!!!"
 
babu you are very right..its really sad kiwanda kilichokuwa kinaajiri zaidi ya watu elfu moja kama bora leo kinageuzwa biashara ya kukodisha magodown....ile mitambo yote wameeondoa wameuza kama scrap kwa wauza vyuma.....ianasikitisha sana kama mama nagu na chami wanakalisha makalio yao chini kwenye viyoyozi hawaji na sera ya kuhakikisha kuwa viwanda vilivyouzwa vinaendelea kuwa viwanda na sio magodown ...
 
Watanzania kwa namna moja ama nyingine tulikwenda mkenge sana na sera za ubinafsishaji, hatukuwa na dira ya kitaifa wakati wote wa zoezi hilo kiasi kwamba kuna ubinafishaji uliofanywa kwa asilimia 100 kwa hao wanunuzi wa viwanda vyetu.

Wachina ambao kwa kiasi fulani wanahusika sana na ujenzi wa viwanda vingi hapa Tanzania wao wana kauli moja juu ya mali ya umma "China's profits are China". Hili kwetu halikuwepo kwa wale waliopewa dhamana ya kubinafisha mashirika yetu. Na matokeo tunayaona sasa ikiwa ni pamoja na suala zima la ufisadi.

Labda huu ni wakati muafaka wa kurudia sera ya ujamaa na kujitegemea ambapo, ujamaa huu uwe na lengo la kuwandaa wananchi kusimamia rasilimali zao huku kujitegemea kukitoa nafasi ya serikali kuwawezesha wananchi kumiliki na kuendesha rasilimali zao. Vyama vya siasa visiwe na madaraka ya kuandaa na kusimamia sera na iwe serikali yenye mamlaka hiyo.
 
Last edited:
Mkuu Kibs, watanzania hatukwenda wkenye sera hii, tulipelekwa - tena kichwakichwa
Ni kipindi kipi kati ya hivi ambavyo tulipelekeshwa kama sio kuburuzwa?

  • Liberalisation...Ruska

Au
  • Sell fast at any price......Uwazi
 
..ukishauza kiwanda huwezi kumlazimisha uliyemuuzia jinsi ya kukitumia kiwanda hicho.

..halafu kiwanda au shirika jukumu na wajibu wake ni kutoa faida kwa share holders siyo kutoa ajira kwa wananchi.

..kuna mambo tulikuwa tunafanya unaweza ukajiuliza kama our parastatals were for profit entities.

..ukweli utabaki kwamba tulishindwa kuviendesha viwanda vyetu. hiyo ndiyo sababu tukalazimika/tukalazimishwa kuvibinafsisha.

NB:

..anayelalamika kuhusu kiwanda kama Bora atueleze ni lini mara ya mwisho alivaa kiatu kilichotengenezwa na kampuni hiyo.
 
...Bora ilikuwa mzigo tuu kwa walipa kodi na hakuna ushahidi wowote kama tungekuwa nayo ingeweza kujiendesha kwa faida,kutoa ajira na kulipa kodi..good riddance!
 
Watanzania kwa namna moja ama nyingine tulikwenda mkenge sana na sera za ubinafsishaji, hatukuwa na dira ya kitaifa wakati wote wa zoezi hilo kiasi kwamba kuna ubinafishaji uliofanywa kwa asilimia 100 kwa hao wanunuzi wa viwanda vyetu.

Wachina ambao kwa kiasi fulani wanahusika sana na ujenzi wa viwanda vingi hapa Tanzania wao wana kauli moja juu ya mali ya umma "China's profits are China". Hili kwetu halikuwepo kwa wale waliopewa dhamana ya kubinafisha mashirika yetu. Na matokeo tunayaona sasa ikiwa ni pamoja na suala zima la ufisadi.

Labda huu ni wakati muafaka wa kurudia sera ya ujamaa na kujitegemea ambapo, ujamaa huu uwe na lengo la kuwandaa wananchi kusimamia rasilimali zao huku kujitegemea kukitoa nafasi ya serikali kuwawezesha wananchi kumiliki na kuendesha rasilimali zao. Vyama vya siasa visiwe na madaraka ya kuandaa na kusimamia sera na iwe serikali yenye mamlaka hiyo.

Lawama zote ziende kwa CCM ndiyo wafanyao haya yote
 
CCM kwa namna moja ama nyingine walitupeleka mkenge sana na ubinafsishaji.........
 
CCM kwa namna moja ama nyingine walitupeleka mkenge sana na ubinafsishaji.........

Tom, siyo kwa namna moja au nyingine! Ni kwa namna zote ccm walituingiza mkenge.
Sera ya ubinafsishaji siyo mbaya kama ingeandaliwa vizuri kwa kushirikisha wadau wote na kuweka mbele maslahi ya wananchi. lakini ccm waliona wananchi ni wao tu. wakasingizia wanabinafsisha mashirika/ makampuni yanayoleta hasara. Ajabu wakaingilia na benki zetu NBC / NMB. Wenye uchungu na nchi yetu (Mwakyembe, Kaduma) walipopiga kelele kwamba hizi benki zinapata faida wakanyooshewa vidole na kuondolewa kwenye bodi za wakurugenzi.

Ukitoa mawazo tofauti na wao wanasema huyo/hao siyo wenzetu sasa sijui wenzao ni akina nani. nafikiri wenzao ni mafisadi wa EPA, RICHMOND, IPTL, KIWIRA, NET GROUP SOLUTION, RADA,NDEGE YA RAIS, MAGODOWN YA EPZ PALE UBUNGO NA QUALITY PLAZA, MEREMETA, ... endelea kutaja mengine
 
..ukishauza kiwanda huwezi kumlazimisha uliyemuuzia jinsi ya kukitumia kiwanda hicho.

..halafu kiwanda au shirika jukumu na wajibu wake ni kutoa faida kwa share holders siyo kutoa ajira kwa wananchi.

..kuna mambo tulikuwa tunafanya unaweza ukajiuliza kama our parastatals were for profit entities.

..ukweli utabaki kwamba tulishindwa kuviendesha viwanda vyetu. hiyo ndiyo sababu tukalazimika/tukalazimishwa kuvibinafsisha.

NB:

..anayelalamika kuhusu kiwanda kama Bora atueleze ni lini mara ya mwisho alivaa kiatu kilichotengenezwa na kampuni hiyo.

suala hapa si kuvaa viatu vya bora....koba na joka ..tunaongelea viwanda kubadilishwa matumizi kiholela ...kwa theory yenu mtaunga mkono hata mtu akiamua kununua kiwanda na kuamua kufugia kuku humo au kuishi.....simply kama pale tanganyika parkers wanapotaka kujenga nyumba waishi...

mnatakiwa mjuwe kuwa viwanda viliuzwa kwa mikataba ...wanaoshindwa wanatakiwa kurudisha au kunyanganywa.......sema ufuatiliaji hakuna..na sisi tumekuwa kondoo......

kama mtu amenunua kiwanda cha viatu anaweza kubadili matumizi na lazima kibakie kiwanda na sio vingonevyo...
 
philemon mikael,

..sijui mkataba wa ubinafsishaji wa Bora unasemaje. je, unaelekeza lazima mwekezaji azalishe viatu?

..Bora was no Tanzania Breweries,Sigara,or Twiga Cement. bidhaa za bora zilishapotea mitaani muda mrefu kabla hakijabinafsishwa. sasa kama amepatikana mnunuzi wa kumtua mzigo huo basi ni nafuu kwa wananchi.

..kama mwekezaji wa TBL, au Saruji, angeanza kufanya shughuli nyingine hata mimi ningelalamika. nasema hivyo kwasababu at least hawa walikuwa wanazalisha ingawa siyo to their full capacity and potential.

NB:

..viwanda kama SPM Mgololo, na Morogoro Polyester kwa kweli inaniuma sana kwamba tumeshindwa kuvifufua.
 
Msinikumbushe wakati ambao tulikuwa tukisikia gari la BORA limeingia wilayani kwetu basi kesho yake ni kwenda kupanga foleni ili upate cha ngazi saba, ikishindikana basi angalau ngazi nne,
 
Back
Top Bottom