Acha hizo yaani wewe unataka tukufungilie pandoras box sio?
Mbona GT unaruka Kimasai maana si Kimanga tena .
Acha hizo yaani wewe unataka tukufungilie pandoras box sio?
Mbona GT unaruka Kimasai maana si Kimanga tena .
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Uingereza, Abubakar Faraji amelaumiwa kwa kutumia jumuiya hiyo kwa maslahi yake binafsi. Hayo yameelezwa na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya waliodai wamemvumilia vya kutosha lakini kwa sasa wanahisi kwa maslahi ya wengi ni vyema akajiuzulu kwa faida ya watanzania waishio nchini hapa.
''Kwa kweli huyu bwana tangu ameingia imekuwa ni kutumia jumuiya hii kujinufaisha binafsi, tunashindwa kumuelewa hasa ni lini ataweka mbele maslahi ya watanzania'' alisema kiongozi mwandamizi wa Jumuiya hiyo ambae hata hivyo aliomba jina lisitajwe kwa sasa.
Abu Faraji ambae aliingia madarakani mnamo mwezi wa tatu baada ya kushinda uchaguzi inadaiwa kutumia madaraka, anajishughulisha zaidi na biashara ya kutuma mizigo nchini Tanzania ingawa tangu kuingia madarakani amekuwa na biashara nyingine kadhaa ambazo zinahusiana moja kwa moja na jumuiya ya watanzania waishio Uingereza.
Imedaiwa kuwa Abu Faraji kwa kutumia mwamvuli wa wadhifa wake amekuwa wakala wa taasisi ya kutuma fedha, Western Union ambayo humlipa kiasi kikubwa cha fedha ili waweze kuwafikia watanzania. ''Sasa badala ya kuingiza fedha hizi katika mfuko wa watanzania zitumike kwa maendeleo, Bwana Faraji amekuwa akidai kuwaleta Western Union kufadhili shughuli za Jumuiya ni mkataba wake binafsi na hivyo fedha hizo ni za kwake!'' alilalamika kiongozi huyo.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Abu Faraji aliwaburuza wajumbe wenzie wakubali yeye na aliekuwa Mwenyekiti Mwanzilishi Bi Norah Sumari wawe ndio waidhinishaji wakuu wa matumizi ya fedha za Jumuiya kwa kuwa ndio wadhamini wa akaunti ya Jumuiya, ''Kipindi kile hatukujua lengo lao kumbe walikuwa na njama maalum kwa vile sasa wawili hao wamesajili kampuni ABN REALESTATES wakishirikiana na Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Johnson Lukaza ambae ni mmoja wa waliotajwa kuhusika na kashfa ya BOT iliyopelekea kufukuzwa kwa Bwana Daudi Balali kama gavana wa Benki Kuu'' alisema.
Aidha kiongozi huyo alidai kuwa kwa kuwa Abu Faraji na Bi Norah Sumari ndio wadhamini wakuu wa akaunti ya Jumuiya kitendo chao cha kufungua biashara pamoja kinakwenda kinyume na maadili mema ya biashara kwa vile kuna uwezekano mkubwa wa fedha za jumuiya kutumiwa kwa miradi yao kwa vile ni wao pekee wenye mamlaka ya kuziidhinisha.
''Hivi sasa tunaandaa mkutano mkubwa kwa ajili ya kuhimiza uwekezaji nyumbani Tanzania na tunatarajia Rais Kikwete kuwa ndio mgeni rasmi, Abu na Norah wamejipa uratibu mkuu wa shughuli hiyo na hakika inahitaji fedha nyingi kutoka kwa wafadhili, sisi wajumbe tuna wasi wasi na matumizi ya mapato toka kwa wafadhili kwa vile ni wao tu ndio wanaojua nini kinaendelea na sisi tumewekwa kando, muda kama huu ilitakiwa tushirikishwe kuandaa mkutano huu lakini ni Abu peke yake na Norah ndio wanaouandaa sisi hata tukiulizwa tunaambiwa subirini mkutano muone vitu vyetu!'' alizungumza kwa masikitiko kiongozi huyo.
Jitihada za mwandishi wa habari hizi ziligonga mwamba kumpata Bwana Faraji kujibu tuhuma hizo za kumfanya Bi Norah kuwa mwenza wake kibiashara ingawa imebainika kuwa Bi Norah licha ya kuwa mjumbe wa kawaida kwenye jumuiya hiyo ana nguvu kubwa kutokana na ''kukumbatiwa'' na Mwenyekiti Faraji ambae humuweka mbele katika kila jukumu lenye fursa au mikutano na viongozi wakubwa wa nchi wakipita London kiasi cha kusababisha mgawanyiko baina ya Bwana Faraji na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bwana John Lusingu.
''Norah ukumbuke mdogo wake ndio alikuwa mmoja wa wahusika wa lile sakata la upimaji wa magari MOT na ndio maana kulikuwa na jitihada za jumuiya kuiunga mkono kampuni ya WTM Utility Services mpaka watu wa nje walipoingilia ndio Mwenyekiti akashtuka.
Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza ilianzishwa kutokana na jitihada kubwa ya Balozi Mwanaidi Maajar lakini hadi hivi sasa bado haijaonekana kufanya lolote kubwa katika kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania licha ya viongozi wake kuingia madarakani na ahadi kede kede ikiwemo ya kukusanya paundi 80,000 ndani ya miezi mitatu iliyotolewa na Mwenyekiti Abu Faraji wakati wa kuomba kura. ''Hata asilimia moja ya fedha hizo haipo kwenye akaunti, ni vichekesho kwa kweli, alifanya watu wajinga'' alisema kiongozi huyo ambae amedai kuwa amelazimika kuzungumza na Mwandishi wa habari hizi baada ya jitihada zake za kumtaka Mwenyekiti kuitisha kikao kujadili hayo kushindikana.
Hivi sasa ofisi za Jumuiya hiyo ndio pia makao makuu ya biashara za Bwana Abu Faraji na Bi Norah Sumari ambao kampuni yao ya ABNREALESTATES inashirikiana na Mfanyabiashara Johnson Lukaza ambae ametajwa kama mmoja wa wamiliki wa kampuni zilizojinufaisha katika utaratibu wa EPA sakata iliyosababisha aliekuwa gavana wa benki hiyo kujiuzulu.
Mwenyekiti Abu Faraji ambae hadi hivi karibuni alikuwa na heshima kubwa miongoni mwa Watanzania ameelezwa kuwa karibu mno na Balozi Mwanaidi Maajar ambae inadaiwa ndio hasa aliemshawishi Bwana Faraji agombee kwa vile anafahamiana na familia ya Bwana Faraji.
Mama yake Bwana Abu Faraji ni afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini ambae ana ukaribu mkubwa na Balozi Maajar tangu wakiwa shuleni pamoja.
Tanzania Association in UK
soma hii thread:
Jumuiya Ya Watanzania Uingereza Yadaiwa Kuwa Kigenge Cha Maslahi Binafsi
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8907
halafu inakuwa tamu zaidi hapa:
Time For Abu Faraji To Go
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=3091
Kamundu,
hawezi kuja Marekani kirahisi kwanza fungueni tawi la CCM ndipo anakuja na bakhshishi kama za UK. Unajua tena wenzenu wamejitengeneza kisawasawa ndani ya mwavuli wa Chama..Haa haa haaa!
refuse to kneel before the sights you choose to see - Under my Umbrela, ela ela he hehe hey!
halafu msisahau kuwa London ni kama USWAHILINI vile sasa muungwana naye kwa kuwa ni mswahili he feels more at home na waswahili wenzie London kuliko huko USA watu kutwa nzima mnaongea kidhungu tuuuuKamundu,
hawezi kuja Marekani kirahisi kwanza fungueni tawi la CCM ndipo anakuja na bakhshishi kama za UK. Unajua tena wenzenu wamejitengeneza kisawasawa ndani ya mwavuli wa Chama..Haa haa haaa!
refuse to kneel before the sights you choose to see - Under my Umbrela, ela ela he hehe hey!
RANT la nini sasa. Kwenye vitabu vitakatifu wanasema ukitoa sadaka kwa mkono wa kulia basi akikisha mkono wa kushoto hauoni. Walio nje wanasaidia sana lakini mkono wa kushoto hautakiwi kujua.SIJAONA WATANZANIA WALIOPO NJE WAKAFANYA YA MAANA kwa WABONGO wenzao(wakiwepo basi tujulisheni)....watu wataishia ktk matumbo yao, Familia zao na wale mmhh....
UBINAFSI, UKABILA, MAJUNGU, FITNA, UZEMBE, BAADHI HAWATAKI KUSOMA, WAMETOSHEKA AU KURIDHIKA KUBEBA MABOX, NA KULETA MAFRIJI NA MAGARI MABOVU...NA MAFISADI WA WABONGO kwakuwa WANAONA MNAPATA WANAWAWEKEENI MOT...ETI INSPECTION...MWAMVULI wa INSPECTION....
Labda Mwanakijiji anakusimulia vizuri. Uhuru wa Tanzania ulianzia uswahilini, lakini Nyerere na usomi wake alikubali kwenda uswahilini na kuchangia mawazo yake hukihuko uswahilini.halafu msisahau kuwa London ni kama USWAHILINI vile sasa muungwana naye kwa kuwa ni mswahili he feels more at home na waswahili wenzie London kuliko huko USA watu kutwa nzima mnaongea kidhungu tuuuu
boriiiiing
hata ningekuwa mimi ningewaavoid sana nyie watu wa USA
SIJAONA WATANZANIA WALIOPO NJE WAKAFANYA YA MAANA kwa WABONGO wenzao(wakiwepo basi tujulisheni)....watu wataishia ktk matumbo yao, Familia zao na wale mmhh....
UBINAFSI, UKABILA, MAJUNGU, FITNA, UZEMBE, BAADHI HAWATAKI KUSOMA, WAMETOSHEKA AU KURIDHIKA KUBEBA MABOX, NA KULETA MAFRIJI NA MAGARI MABOVU...NA MAFISADI WA WABONGO kwakuwa WANAONA MNAPATA WANAWAWEKEENI MOT...ETI INSPECTION...MWAMVULI wa INSPECTION....
Nzokankulu,
Mkuu maelezo yako ndio vichwa vinavyotakiwa Tz leo, kesho na kesho kutwa. Ni mawazo endelevu na yanayotafuta solution lakini kwa bahati mbaya ni kwamba utaonekana mchawi. Ethics za NDIVYO TULIVYO zinapingana na mawazo kama haya, mawazo yanayojipanga kuanza kazi ngumu ya kutafuta tiba ya umaskini wetu hali tunaweza endelea kuwa ombaomba na vikopo vyetu mitaani huku hesabu ndogo ikijengwa mamillionea 100 kabla ya 2010.
Shukran mawazo yako bomba kishenzi na sina la kuongeza isipokuwa ni kumwomba Mungu atokee mwenye kuyaona haya ndani ya Utawala wa Julius Caesar kisha kuyapatia majibu kulingana na mapendekezo yako!..sii rahisi.
Pili, kumbuka kwamba mtu yeyote anayekataa CCM na hasa wakimbizi toka Zanzibar huko UK wamepoteza na Uraia wao. Hivyo basi huwezi kusema unaipenda Tanzania bila kuwa mwanachama wa CCM... Ndivyo tulivyo na muhimu kufahamu hilo ikiwa unataka kuleta changes zozote ktk society inayokutambua wewe kwa rangi hizi mbili - Kijani na njano.
Mkuu mnaweza fikiria ni fanya joke lakini ndivyo ilivyo in reality.. Kama hamtakubali CCM basi serikali haiwezi kuwatambua iwe US ama Australia. Kwa hiyo ni muhimu kwenu ku give up something ili mpate something for you country. Kifupi, moja ya ilani za Ndivyo tulivyo ni kwamba - Wewe ndiye mwenye shida sio Tanzania. Tafsiri fupi inasema hivi:- Kama ni umasikini basi wewe ndiye maskini sio watu wote - watu (CCM) wanatesa.
SIJAONA WATANZANIA WALIOPO NJE WAKAFANYA YA MAANA kwa WABONGO wenzao(wakiwepo basi tujulisheni)....watu wataishia ktk matumbo yao, Familia zao na wale mmhh....