Ntaramuka
Senior Member
- May 2, 2008
- 169
- 27
Ukiongelea mpasuko uliopo hapa Zanzibar, waliowengi hasa walioko Tanzania bara huzaidi kuhusu CCM na CUF au UNGUJA na PEMBA. Ni kweli kuna mpasuko mkubwa sana na tofauti za waziwazi zinazoonekana kati ya wapemba na waunguja kiasi kwamba wapemba hukosa hata kuajiriwa kwa sababu tu ya upemba, hali ambayo hupelekea kwa waombaji wa ajira ambazoziko chini ya muungano kulazimika kuandika maombi maalum bara ili waweze kuajoriwa.
Sio siri hili la CCM VS CUF na UNGUJA VS PEMBA lipo, lakini katika hali ya kushangaza kuna ubaguzi mwingine mkali sana na mbaya zaidi unaoendelea hapa unguja, huu ni ubaguzi wa KUSINI na KASKAZINI.
Kama kiongozi mwenya mamlaka fulani akitoka mkoa wa KASKAZINI NGUJA, basi wale wa upande mwingine wa KUSINI UNGUJA, yaani MAKUNDUCHI, MUYUNI nk. wanaumia vibaya mno.
Ubaguzi huu ni mbaya zaidi na ambao bila kuangaliwa vizuri zaidi unaweza kuliangamiza taifa la zanzibar.