Ubadhirifu mkubwa Benki ya Posta

YALIYOMO


1.0 UTANGULIZI
1.1 Kughushi barua ya bodi ya Benki ya posta ili kuongezewa mkataba

1.2 Kuandaa mtandao wa kufanikisha UFISADI
1.3 Kutumia kampuni ya rafiki/familia kuiibia Benki
1.4 Kuiingiza BENKI katika mikataba mibovu kwa maslahi yake




2.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

2.1 HITIMISHO................................................................
2.2 MAPENDEKEZO.................................................











TAARIFA YA UFISADI UNAOFANYIKA NDANI YA BENKI YA POSTA UKIMHUSISHA MTENDAJI MKUU WA BENKI YA POSTA NDUGU ALPHONCE KIHWELE.


1.0 UTANGULIZI
Benki ya posta (TPB) ni Benki inayomilikiwa na serikali ya muungano na ilianzishwa kwa sheria ya Bunge ya namba 11 ya mwaka 1991 kama ilivyorekebishwa kwa sheria namba 12 ya mwaka 1992.

1.1 Kughushi barua ya bodi ya Benki ya posta ili kuongezewa mkataba
Kunako tarehe 20 November, 2006 kilifanyika kikao cha bodi ya wakurugenzi wa benki ya posta. Pamoja na mambo mengine kikao kilitaarifiwa juu ya mtendaji mkuu wa benki ya posta ndugu Alphonce Kihwele kuongezewa mkataba mwingine wa kuiongoza Benki ya posta kwa kipindi cha miaka mitatu. Hii ilitokana na kwamba kipindi chake cha tatu cha mkataba (miaka mitatu mitatu) kilikuwa kinaishia tarehe 25 November, 2006. Bodi ilisomewa barua kutoka hazina (Permanent secretary Treasury iliyosomeka kama ifuatavyo :

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA HAINA PINGAMIZI LOLOTE DHIDI YA PENDEKEZO LA KUONGEZEWA MKATABA WA MTENDAJI MKUU WA BENKI YA POSTA NDUGU ALPHONSE KIHWELE NA KWAMBA BILA PINGAMIZI LOLOTE IMEMWONGEZA MKATABA WA MIAKA MITATU KWA MASHARTI ATAKAYOKUBALIANA NA BODI YA WAKURUGENZI WA BENKI YA POSTA.

BODI YA WAKURUGENZI PAMOJA NA MAMBO MENGINE ILIREJEA MKATABA WA AJIRA WA TAREHE 10 DESEMBA 2003 NA KUUFANYIA MAREKEBISHO IKIWA NI PAMOJA NA KUBADILI CHEO CHAKE KUTOKA MKURUGENZI MTENDAJI NA KUWA MTENDAJI MKUU.

Barua ya hazina ilizua maswali mengi kwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho kwani wengi wao hawakumbuki ni lini Bodi ya Benki ya posta ilikutana na kumpendekeza ndugu Kihwele aongezewe kipindi cha nne kuihujumu BENKI.

Shaka ilitokana na ukweli kwamba nyongeza ya mkataba wa mtendaji mkuu wa Benki kwenda serikalini ilitakiwa itokanae na Bodi ya Benki lakini hakuna kikao cha bodi kilichokutana kumpendekeza. Maneno yaliyotumika kwenye barua kutoka hazina (Permanent Secretary Treasury) kama ilivyosomwa na makamu mwenyekiti wa BODI inaonesha kwamba kuna mapendekezo yalipelekwa ambapo Jamhuri ya Muungano haina pingamizi nayo.

Uchunguzi uliofanyika umeonyesha kuwa waliohusika na uhalifu huo ni ndugu Alphonse Kihwele, Casmir Nkuba (Kaimu katibu wa bodi), Makamu mwenyekiti wa bodi Ndugu Benedict Kapelega na mmoja wa manaibu mawaziri wa wakati huo na baadhi ya maafisa wa Benki kuu.

Uhalifu huo ulianza kuandaliwa mapema kwani tangu Kumalizika kwa mhula wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Posta Ndugu Paul Mkanga kwa makusudi hadi leo hakuna aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa BODI kwani kuwepo kwa mwenyekiti kungeharibu mpango mzima wa kufanikisha uhalifu huo.

Kuna taarifa kuwa hakuna uteuzi wa mwenyekiti wa bodi utakaofanyika hivi sasa kwani nafasi hiyo inamsubiri makamu mwenyekiti wa sasa ambaye ni mtumishi wa shirika la POSTA ambaye anatarajiwa kustaafu posta mwezi Agosti/Septemba 2008. Mikakati inaandaliwa ili mara amalizapo ajira yake ya shirika la posta ateuliwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Posta.

Ameweza kubanwa na BoT kuhusu hesabu za Benki kwani awali ili aongezewe muda kuliongoza Benki alikuwa anawalazimisha watengeneza mahesabu idara ya fedha kuhakikisha wanatoa hesabu zinazoonesha faida anayotaka kinyume na ukweli ili awaite waandishi wa habari kuitangaza ikiwa ni mbinu ya kudanganya umma ikiwemo na bodi ya wakurugenzi ili aongezewe muda kulihujumu shirika. BoT wameagiza kuondoa katika mahesabu mambo yote yaliyoharibu ulali wa hesabu za benki ili yajulikane kama hasara….ni yale yaliyotokana na kuharibu mahesabu ili alipoti faida anayotaka kwa kuwa hayakuwa ya kweli yanachafua hesabu za benki. Benki imeagiza yote yalipotiwe kuwa ni hasara ndiyo sababu amebadili mbinu ya namna ya kuongezewa muda wa kuharibu shirika.

1.2 Kuandaa mtandao wa kufanikisha UFISADI
Mtendaji mkuu ameanda timu ya vijana wake ambao ndiyo anashirikia nao kufanikisha UFISADI wake.Timu hiyo inaundwa na wafuatao.Mkuu wa kitengo cha sheria ndugu Casmir Nkuba ambaye alikuwa mwanasheria mwandamizi wa shirika akiwa ni kitengo ndani ya ofisi ya Katibu wa Shirika (corporation Secretary) baada ya utendaji wake mzuri uliofanikisha kuongezewa kipindi cha nne cha mtendaji mkuu kama ahsante kwake mtendaji mkuu aliamua kuivunja ofisi ya corporation secretary na kuunda idara mbili,moja ikiwa ni ya sheria na nyingine ikiwa ni mambo ya bodi na kupendekeza uteuzi wa ndugu Nkuba kuwa mkuu wa Idara mpya ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango wa kuweka nafasi ya makamu mtendaji mkuu wa shirika ili Casmir Nkuba apewe ikiwa ni maandalizi ya kuweka mtu wa kusimamia UFISADI.
Mwingine ni mkuu wa kitengo cha Masoko pamoja na Mkuu wa kitengo cha Fedha.

1.3 Kutumia kampuni ya rafiki/familia kuiibia Benki
Kumekuwepo na utaratibu wa kulipa watu binafsi au makampuni ya marafiki zake pasipo kufuata taratibu zozote za fedha. Mara nyingi hati za madai zinapitia ofisini kwake na kupelekwa idara fedha kwa ajiri ya malipo bila kuanisha kazi iliyofanywa na zinalipwa kwa kutoa huduma za ushauri (Consultancy) bila maelezo yoyote.

Ni kwa kutumia kampuni ya rafiki/familia yake alifanikisha kutumia kiasi kikubwa cha fedha kupitia utengenezaji wa kaunta za BENKI pale Ubungo Plaza ambapo jumla ya shilingii MILIONII MIA SABA ZIMETUMIKA. Ni huu mradi wa Ubungo Plaza ulioleta mtafaruki kati ya mtendaji mkuu (Alphonse Kihwele) na aliyekuwa mkuu wa huduma za Benki wakati huo (George Nyatega) ambaye kwa sasa ni Mtendaji mkuu wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU. Ambapo Nyatega alipinga uteuzi wa kampuni usiofuata taratibu ambao ulikuwa ni wa bei kubwa sana ilikadiliwa kutumika shilingii milioni Mia Nne (Nyatega hajui kwamba alikataa hujuma ya milionii mia Nne ukweli hadi sasa wametumia karibu shilingii milionii mia saba na mtafaruki mwingine umeibuka kati ya mtendaji mkuu (Alphonse Kihwele) na Mkuu huduma za Benki Ndugu Mwakyandile dhidi ya malipo mengine ya karibu milioni mia moja. Kampuni inayohusika imegundulika kuwa ni ya mtoto wa rafiki ya aliyejulikana kwa jina la MBEDULE inaitwa PATTY PLAN. Ubungo plaza ni mmoja kati ya miradi mingi ya KIFISADI inayofanikishwa na Ndugu Kihwele bila kufuata sheria ya PPRA huku akisisitiza kufuata sheria hiyo kwenye ununuzi wa vitu kama bahasha.

Akishirikiana na mwanasheria wa shirika wamefanikiwa kuiibia Benki kiasi cha Shilingi milioni tisa kwa kesi ya kupanga kati ya mtendaji mkuu wa Benki akishirikiana na mwanasheria wa Shirika kwa kumtumia Maj.Gen.Mstaafu Ligate Sande na ambapo Ligate Sande aliishitaki Benki ya Posta. Ili kufanikisha wizi huo waliamua kutumia mawakili wa nje ya Benki kama kiini macho huku Ligate Sande akiwakilishwa na Kampuni ya sheria inayomilikiwa na mwanasheria wa Benki ndg Casmir Nkuba! UHUJUMU WA WAZI kabisa.

Makampuni mengine yaliyotumiwa na mtendaji mkuu kufanikisha ufisadi ni CEK Company na Vaginga ambazo kwa pamoja zilikopeshwa kiasi cha sh.1.6 Billion; wakurugenzi wazalendo walikataa pendekezo la kutaka wakopaji hao waongezewe 2 billion ili waweze kufufua biashara zao ili walipe mikopo yote. Ilishindikana baada ya kamati ya Mikopo na mkurugenzi wa Fedha wa wakati Huo James Mpayo kuhoji na kukataa pendekezo hilo. Kama wameshindwa kulipa 1.6 Billion watawezaje kulipa 3.6 billion? Mpaka leo hii hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kurejesha fedha hizo ingawa kuna mali ya dhamana iliyowekwa wakati wa ukopaji. Mtendaji mkuu na timu yake ya mafisadi wanasaidiana na wahusika kuhakikisha benki hairudishiwi fedha hizo.


1.4 Kuiingiza BENKI katika mikataba mibovu kwa maslahi yake
Mkataba kati ya BENKI ya Posta na Federal Bank of Middle East ni kielelezo tosha cha Mikataba ya kifisadi yenye nia ya kuliangamiza shirika.

Benki ya posta imeingia mkataba wa uwekaji na uendeshaji wa machine za kutolea fedha ATMs na FBME ikiwa ni pamoja na utoaji wa Card za kutolea fedha kwenye mashine za ATM (Uhuru Card) moja kati ya makubaliano ya kifisadi katika mkataba huo ambao ulikuwa siri mpaka pale baadhi ya wafanyakazi wenye uchungu na shirika walipokataa kuwalipa FBME/TANPAY mamilioni ya fedha kwa mujibu wa mkataba ambapo FBME/TANPAY walilazimika kuonyeha kipengere kinachohusika na malipo yaliyokuwa yanakataliwa.

Kipengere cha mkataba kinatafsiriwa hivi:
FBME/TANPAY itatengeneza uhuru cards kwa ajili ya wateja wa TPB ambapo TPB itawalipa FBME shilingi elfu kumi na mbili (12,000) kwa kadi inayotolewa kwa mwaka wa kwanza.mwaka wa pili kadi ile ile FBME/TANPAY watalipwa shilingi elfu nane na mia nane (8800) na mwaka wa tatu FBME watalipa shilingi elfu nane mia sita (8600) uhai wa kadi ni miaka mitatu hivyo basi kadi ya mteja itakuwa imekwisha muda wake atatakiwa kupewa kadi nyingine ambapo TPB itatakiwa kulipia 12,000, 8,800 na 8,600 kwa miaka mitatu tena.

Kwa hiyo Uhuru card inauzwa kwa jumla ya shilingi 29,400. TPB huwatoza shilingi kumi na tano elfu wateja wake wanapojiunga na Uhuru Card ambapo 12,000 zinapelekwa FBME/TANPAY. Kwahiyo Uhuru card inatakiwa iuzwe kwa karibu shilingi elfu thelathini na tatu.12,000 + 8,800+8,600 pamoja na 3,000 ya TPB pamoja na malipo ya shilingii 15,000 kwa card mteja wa uhuru card anatozwa shilingii mia tatu na hamsini kwa kila atumiapo uhuru card kuchukua fedha, ambapo shilingi mia tatu (300) zinapelekwa FBME/TANPAY na shilingi hamsini (50). Hizo shilingi 8,800 na shilingi 8,600 walipwe FBME/TANPAY kutoka kwenye mapato gani? JUHUDI za kutaka FBME walipwe hizo Fedha zikifanywa na mtendaji mkuu zimekuwa ngumu kutoka na msimamo mkali wa baadhi ya wakuu wa idara ambapo alifanikiwa kuchota karibu milioni 200 na kuwalipa FBME /TANPAY kwa mtindo tajwa hapo juu ikiwa ni Nje ya 12,000 wanayolipwa kila mwezi kwa kadi zilizotolewa kwa wateja. Wakuu wa idara walishauri kuvunjwa kwa mkataba huo kwani gharama za kuvunja mkataba zilikuwa chini kuliko gharama za kuubeba mkataba hu. Amekataa katakata kufanya hivyo. Juhudi za wafanyakazi kuieleza bodi ya wakurugenzi na wizara zimekuwa zikikwamishwa na watendaji wa wizara na baadhi ya wajumbe wa bodi ambao wanatumiana kimaslahi binafsi. Kwa ujumla mtendaji mkuu wa Benki ya posta ni kikwazo kwa maendeleo na ufanisi wa benki ya posta katika zama hizi za utandawazi. SHIRIKA LIMEMZIDI HANA UWEZO WA KULIONGOZA KATIKA ZAMA HIZI ZA UTANDAWAZI.

2.0 HITIMISHO
Haya yaliyoandikwa hapo juu ni kiasi kidogo mno cha maovu yatendekayo ndani ya benki yanayoshusha molali kwa wafanyakazi, sisi wafanyakazi tumefanya juhudi kubwa sana kujaribu kudhibiti uhalifu huu ikiwa ni pamoja na kuusema waziwazi kwenye vikao vya wafanyakazi wote pamoja na baraza kinyume na kuwa tukitegemea yapunguwe san asana huwa ni buguza na usumbufu mkubwa wanofanyiwa wote wanaothubutu kuhoji dhidi ya hujuma hizo. Barua zimeandikwa kupelekwa wizarani mara nyingi lakini hakuna kinachofanyika zaidi ya kumrudia mwenyewe akisisitiza kuwa hakuna anayemuweza. Iligundulika kuwa barua zilizokuwa zinapelekwa wizarani hazikuwa zinamfikia waziri wa fedha bali zilikuwa zinaangukia mikononi mwa wanamtandao wake na kumrudia ambapo alikuwa anaanzisha msako wa kutafuta waandishi wakati mwingine akipigisha kura wakurugenzi kama zile za kutambua majambazi ili tu amjue mwandishi. Barua nyingine zilipelekwa ofisi ya waziri mkuu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
2.1 MAPENDEKEZO
Tunaomba OFISI YA WAZIRI MKUU iunde tume kuchunguza ukweli wa haya tunayoyasema ili ukweli ujulikane hatimaye shirika tulinusuru. Tunaomba asihusishe wizara ya fedha kwani yenyewe kupitia baadhi ya maafisa wake ikiwa ni pamoja na waziri wa fedha Ndg Mustafa Mkullo ni watuhumiwa. kwa upande wa waziri wa fedha utata unatokana na ombi lake la mkopo wa shilingi milioni mia mbili likipigiwa chapuo na Makamu mwenyekiti wa Bodi, kutokana na uzalendo wa baadhi ya wakuu wa idara walikataa kupitisha milioni mia mbili, lakini kutokana na shinikizo la makamu mwenyekiti wa bodi akapewa mkopo wa milioni hamsini. Kama Waziri mkuu au yeyote anayehusika ataanzisha uchunguzi tunaomba achunguze mwenendo wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Posta kwani kwa sasa bodi ni kama waigizaji tu ‘Ze COMEDY’ bila kujijua wamenunuliwa kwa malipo ya vikao vya bodi kwani bodi huweza kutana mara tatu au nne kwa mwezi (kila kikao ni TZS 300,000.) kwa kila mjumbe wa bodi kwa kikao kimoja. Mara nyingi akitaka kuwaroga huweka vikao viwili kwa siku; kimoja hukiita special (bila special agenda) na kingine huita cha kawaida hakuna mjumbe wa bodi anayehoji ubadhirfu huu.
 
hapa mimi husema tuifananishe serikali ya kikwete na wananchi kama ze komedi group na watazamaji, hata ze komedi wafanye upuuzi wa kiwango gani kwenye TV kazi kubwa ya wanaotazama ni kukenua na wengine kuanguka kwa kucheka. Haya yetu si ya kucheka maana tunanyongwa tukiwa macho na tukielewa, umma mkubwa wa watanzania hawana taarifa juu ya haya na hao ndio wengi. Akili yangu inauma sana kwamba utawaelezaje wale wasio na taarifa kuhusu haya wakuelewe na wapate uchungu halisi kuhusu kinachoendelea nchi hii? tunaoona uchungu na kupiga ukunga kwa kujifungua shida mpya kila siku ni wachache tunaojua kuna uwezekano wa kutozaa shida hizi ama basi kuwa na uzazi salama. Jamii kubwa ya watanzania wameridhika na maisha ya kuzaa shida mingi iwezekanavyo, leo azalie stendi, kesho kwenye toroli akipelekwa hospitali 14Kms kutoka home kwao, siku ingine azalie nyumbani, wengine waishie kupata (sikumbuki wanaitaje) lakini akina mama wanakaa muda mrefu na uchungu matokeo sehemu ya haja kubwa na ya mkojo vinaingiliana kwa mbano. Baada ya kuzaa anakojoa bila breki... kwetu kawaida. Tunahitaji mikakati ya kisomi kwenda mbele kwa haraka, vinginevyo watu weupe wanaozuia maendeleo ya watu weusi hawako ulaya, ni mijitu myeusi iliyoko hapa hapa Afrika na Tanzania hii. JF tujikaze zaidi akili zetu tufikirie mbali kwa haraka zaidi, tunashukuru sana kwa nondo zinazoletwa hapa kwenye floor, tunaomba tuzitumie kufikiria mustakabali wetu, wanaoleta hizo nondo wanaweza kuwa na mipango mizuri pia ya kusonga mbele maana wanajua ni sumu gani zinapikwa kwa ajili ya wasiojua sumu zikoje. Samahanini, nina maneno mengi mno wana-JF...
 
Looh!! kabenki kenyewe kanaongozwa kimtulinga na huyo kiwele wao maana kawafukuza kazi wale aliowatuumu kuwa wametoa siri za ufisadi wake. wizi mtupu. mzee mweneyewe kustaafu hataki wakati umri wake sasa miaka 68 bado yupo tu kwa mkataba. alistahafu mwaka 1997 baada ya kutimiza miaka 60 na anaendelea kuwepo kwa mikataba tu. Hivi nchi hii hakuna wengine wakuweza kuongoza hata hivi vibenki vidogo vya kimachinga kama hako ka posta ?? hebu wanabaraza mnijuvye. SIasa za kiwele na Mugabe hazina tofauti, ataki mtu wa kupinga kile anachosema hatakama ni utumbo wewe kubaliana naye tu. menejiment yake waoga kama nini kwa kuhofu yale yaliyowatokea wale wenzao waliofukuzwa kazi.
Bodi nayo zekomedi kweli, lkihoji kitu anawapeleka ulaya kula nchi. Majuzi wametoka Indonesia kujifunza utendaji kazi, hivi nani anapaswa kujifunza utendaji kati ya bodi na watendaji ambao ni wafanyakazi. Jamani ufisadi hata bodi nayo inahusika. hao wajumbe wenyewe wanakesi za jinai huko kwao posta. yupo mama Malogo na Kapelega wana kesi za wizi wa magari ya shirika na bado wamo kazini na wanaongoza Benki ya posta ah jamani WIZI MTUPU

bORA Mzee kibiongo nijikalie na kibiongo changu nisione mambo haya ya mchwa kutafuna nchi namna hii.
 
Back
Top Bottom