Ndivyo ilivyo kwa mashirika ya Umma kutumiwa kwa masilahi ya wanasiasa na marafiki zao. Mfano mwingine ni TANESCO.
Ili Watanzania waweze kupona kuna umuhimu mkubwa sana kwa haya mashirika ya umma yawe na uwazi mkubwa sana. Nadhani usiri mkubwa sana katika shughuli za haya mashirika ya Umma ndio tatizo kubwa sana, ambapo wanasiasa na mafisadi wenzao wanatumia kwa manufaa yao.
Hatuna haja ya kuuza mashirika yetu eti tumeshindwa kuyaongoza. Mazingira ya mashirika ya umma ndo yanatakiwa kubadilishwa, hasa hasa kwenye kuripoti shughuli zake kwa jamii ikiwa ni pamoja na mahesabu yake.
Tunaweza kuiga uwazi uliopo kwenye mashirika yaliyokuwa listed kwenye masoko ya hisa, kwamba pamoja na wale viongozi wa mashirika kuongoza mali zisizo zao, zinazomilikiwa na umma (general public), lakini sheria zimewekwa kusaidia kuyaongoza mashirika hayo kwa ufanisi na pia kuepusha wizi na ubadhirifu unaoweza kufanywa na viongozi.
Mimi nadhani hilo ndo litakuwa moja ya suluhisho kubwa la matatizo ya mashirika yetu ya umma.
Wenye ufumbuzi mwingine tafadhali tuchangie.....