Ubabaishaji wa makampuni ya uwakala

KasomaJr

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
367
139
Ni aibu na ni hali ya kusikitisha pale makampuni ya uwakala wa ajira wanapotoa taarifa za upotoshaji zisizo thibitishwa. Ninayo Mifano kadhaa lakini kwa uthibitisho juu ya post yangu ya leo ni juu ya hawa Zoom Tanzania ambao wametangaza kazi ambazo kimsingi hazipo katika orodha ya kazi zinazotangazwa na taasisi au kampuni husika. Hili nimelithibitisha toka kwa vyanzo vya ndani kabisa toka taasisi husika.

Kwa mfano:

1. Taasisi ya international youth foundation (IYF) walitangaza kazi ya administrative assistant tangu miezi ya sept 2014, na kwa taarifa nilizonazo (pamoja na kwamba website yao inaonyesha mwisho wa maombi ulipaswa kuwa november 1, 2014, ila ukweli kazi ili ilishajazwa na mtu karibu mwezi mmoja sasa uliopita. Hili Nalo ni tatizo lingine la taasisi kutangaza nafasi ya ajira wakati muda wa mwisho wa kutuma maombi haujafika, tayari wameajiri mtu)

Hebu fuatilia hizi link mbili uone uzushi huu:

IYF wao wanasema deadline ni November 1, 2014 administrative assistant | iyf

Zoom Tanzania wao wanasema deadline ni November 14,2014 administrative assistant job in other, tanzania

2. Taasisi ya JHPIEGO wao hawajatangaza kazi ya Senior Finance and administration officer lakini hawa jamaa wa Zoom Tanzania wao wanasema kuna hiyo nafasi, na nimecheck na jamaa zangu wanaofanya kazi hapo wananiambia hakuna position kama hiyo.

Ushahidi huu hapa:
https://jobs-jhpiego.icims.com/jobs/...cation=13533--
senior finance & administration officer job in other, tanzania

Sasa waungwana haya mambo ya kupoteza muda wa wa watu, vijana wanaohangaika kutafuta kazi na vi rasilimali kidogo ya fedha, huu ni uhuni na upuuzi unaopaswa kulaaniwa kwa nguvu zote. Kuna hata sasa ya hii career agencies kufanyiwa utaratibu namna gani wanavyoendesha shughuri zao, huenda wanayafanya haya kwa kutambua ukweli ama kwa makosa.

Hii Ni cyber crime kuna haja ya ku report hizi habari katika taasisi za kisheria ili hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe ili kukomesha haya.


 
erxana kaka kwani utapeli umekuwa mwingi hadi inakera kwani wakikosa cha kutangaza wanaamua kuunda nafasi za kazi ili tu waonekane wanatangaza sana nafac za kazi loooooh! zoom tz nadhani manajisoma hapa upuuzi muufanyao tumeugundua na oneni aibu basi
 
kumbe bado kuna watu mnaApplay kupitia zoom, hao ni makanjanja na wamejawa na utapeli humo.
 
Zoom wanatumia mtandao wao kutangaza kazi hizo ambazo hazipo,ili wapate viewers wengi,kitu ambacho ndiyo faida kubwa kwao.
 
Back
Top Bottom