Mamkala ya Mapato Tanzania (TRA) inabagua baadhi ya shahada wakati wa kuajiri

emmyfrancie

New Member
Mar 20, 2024
2
0
Mimi ni mmoja wa wahitimu wa elimu ya juu. Bachelor of commerce in banking and finance.

Swali langu kwa TRA ni kwamba kwanini watu waliosoma finance wanaruhusiwa kuomba kazi TRA na watu waliosoma Banking and finance wanakataliwa?

Watambue kwamba watu wa banking and finance ni lazima wasome masomo yote ya finance halafu wanaongeza na masomo ya banking.

Naamaanisha kwamba watu wa banking and finance masomo ya finance ni core subjects not option subjects.

Watu waliosoma banking and finance wanauwezo wakufanya kazi TRA kama walivyo watu wa finance, hapo limeongezeka neno banking tu.

Ndio maana kuna baadhi ya kampuni wakihitaji muhasibu, finance management officer n.k huwa hawasasahau watu wa account, finance, banking na watu business administration kwasababu hizi kozi zinashabihiana.

Ombi langu ni kwamba katika maombi ya kazi yajao ya TRA watu banking pia wasinyanyashe kabisa, endapo hawatawachukua watu wa banking basi na watu wa finance pia wasiwachukue.

Wenu katika ujenzi wa Taifa.
 
Back
Top Bottom