Uamuzi wa kufuta kikosi kazi cha kukagua leseni una mengi ya kujadiliwa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,889
Ni uamuzi uliokuja kwa kuchelewa kidogo maana madhara na hasara nyingi vimekwisha tokea... Huu uamuzi hata hivyo pamoja na mengine yote unahitaji pongezi za dhati kwa IGP.. Lakini sasa asiishie hapo tuu bali aungane na mamlaka nyingine kufanya na kurekebisha haya yafuatayo .. Nizitaje kwanza mamlaka husika

Polisi kikosi cha usalama barabarani
Polisi kikosi cha ukaguzi wa leseni
Polisi kikosi cha kuidhinisha leseni
Mamlaka ya mapato
Tan roads/ Tarura
Vyuo vya udereva na washika dau wengine!

Polisi kikosi cha usalama barabarani.. Hiki kinanuka rushwa na hili liko wazi.. Kwa asilimia zaidi ya 60 ya ajali zinatokana na rusha
. Rushwa inafanya gari mbovu iachwe iendelee na safari
. Rush inafanya dereva mwenye makosa asizuiwe kuendelea na safari
. Rush inamfanya dereva mwenye historia ya ajali za mara kwa mara asifungiwe leseni yake
. Rush inamfanya dereva asiyekidhi viwango kuruhusiwa kuendesha gari hasa za mizigo na abiria
Umbumbumbu wa sheria ama kutojali
Traffic wengi wana hii shida, tafsiri yao ya baadhi ya sheria za barabarani ni majanga! Na anaweza kusimamisha gari na bila kuielekeza mahali salama pa kupaki ili aikague

Kikosi cha polisi cha ukaguzi na kuidhinisha leseni..
Hapa hakuna weledi, hakuna taaluma na taratibu hazizingatiwi kabisa! Kinachozingatiwa ni rushwa.. Ujuzi pia sio muhimu, pesa!
Laki na nusu mpaka laki 2 kulingana na dalali na uharaka ama kaliba ya mtu inampatia mtu leseni ndani ya masaa 72!

Huangaliwi umesomea wapi udereva
Hufanyiwi majaribio kuthibitisha udereva wako
Huhakikiwi umri wako
Huhakikiwi afya yako hasa ya akili, macho, masikio na magonjwa mengine
Kinachiangaliwa ni cash yako

Tuna maelfu ya madereva wasiojua chochote kuhusu sheria za usalama barabarani lakini wana leseni halali.. Mfano wa wazi ni hawa bodaboda

Tuna maelfu ya madereva wasio na ujuzi na uzoefu kwenye vyombo wanavyoendeshab lakini wana leseni zenye madaraja ya vyombo husika

Tuna raia wa kigeni kwa mamia mengi tu wana leseni za udereva Tanzania lakini ukiwauliza wamesomea chuo gani ama wamehakikiwa na mamlaka gani wanabaki kukutolea macho na kujichanganya kwa maelezo ya aibu.. Wote hawa wamenunua nyaraka hii muhimu sana

Mamlaka ya mapato nao hawajishughulishi kufanya uhakiki wa nyaraka za malipo, it is always short.. Akishakabidhiwa na polisi ama dalali yeye ni chap kwa haraka anaidhinisha na serikali inaingiza mapato.. Mengine hayamhusu

Tanroads/Tarura
Hawafuatilii ubovu na uharibifu wa barabara kwa haraka ni wazito na sometimes wanafanya kazi chini ya kiwango
Kukosewa kwa alama za barabarani
Kuweka Alana zisizostahili sehemu husika
Vyuo vya mafunzo ya udereva
Hivi navyo vina lawana zake maana
Baadhi hutoa elimu duni juu ya udereva na matumizi ya barabara
Elimu juu ya vyombo vya moto
Uchumi
Kuuza vyeti

Washika dau wengine ni
Wakandarasi wasiozingatia usalama kazini
Waenda kwa miguu waliojawa na dharau na kiburi wanaodhani gari linaweza kumpisha yeye

Kuna hili la mwisho ambalo linarudi kwenye kikosi cha ukaguzi kipengele cha magari mabovu ( vehicle inspectors) kuna sticker zinatolewa kila mwaka, wiki ya nenda kwa usalama
Aisee hapa ndio kama sio kuchosha basi ni maajabu tupu na pengine ni Tanzania pekee
Wiki ya nenda usalama ilipaswa kuwa wiki ya ukaguzi wa ubora wa gari, uchakavu, ubovu nk nk! Kisha gari ikishathibitishwa kukaguliwa ndio hupewa sticker ya ukaguzi.. Huku kwetu ni wiki ya kuuziwa sticker zenye nembo na majina ya wafanyabiashara walioshinda tenda ya kutoa sticker kwa mwaka husika.. Hakuna ukaguzi

Kama IGP anedhamiria kutokomeza/kupunguza ajali, madhara ya mwili na uharibifu wa miundombinu kukifuta kikosi kazi cha leseni hakutoshi kuna haya mengi ya kufanyiwa kazi na yanahitaji maandalizi makubwa na kujitoa hasa..

Kinyume chake itakuwa business as usual.. Na excuse ya kusema ajali ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu!
 
Wakati wa kuapishwa
VIPAUMBELE 3 VYA MKUU WA MKUU MPYA WA POLISI TANZANIA

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura ameahidi kuzingatia:

Sheria na utaratibu

Maadili, nidhamu ya jeshi la polisi

Haki kwa raia katika vituo vya polisi na katika mwingiliano wa polisi na raia katika jamii

Kwahiyo tunaamini katika hayo ya leseni tutaona mabadiliko makubwa.

20230222_124026.jpg
 
Dereva kama huyu wa gari dogo ambaye hakuzingatia sheria za usalama barabarani na kukatisha bila tahadari amesababisha ajali mbaya, uharibifu, majeruhi na kifo leo asubuhi
 
Haikuwa juhudi, huyo dereva wa mwendokasi ni muuwaji.

Amesababisha kifo cha mwenda kwa miguu.
Alikuwa main road kuna Rav 4 ikakatiza barabara kuu bila tahadhari, katika kuepa asiigonge ndio yakatokea hayo
 
Kwamba leseni zainatolewa kihuni.

Ok,wacha tuone matokeo ya hatua hii.
 
Back
Top Bottom