UAMSHO wasalimu amri kwa Polisi!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wananchi wa Zanzibar wakiwemo wafuasi wa Kikundi cha Uamsho kilichotangaza kufanyika kwa mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba mjini hapa, kimetii amri ya Jeshi la Polisi kwa kutoonekana kwa muumini ama viongozi wa kikundi hicho katika viwanja hivyo.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema leo kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kudhibiti maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar na hivyo kutojitokeza tena kwa wafuasi wa kikundi hicho kama ilivyotangazwa awali.
Inspekta Mhina amesema Kikundi hicho cha Uamsho kupitia kwa Kiongozi wake Sheikhe Farid Hadi, juzi kilijigamba kufanya Mhadhara mkubwa leo arasili katika viwanja vya Lumumba mjini hapa hata baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyiko, kimeshindwa kufanya hivyo kufuatia agizo la Jeshi la Polisi lakuwataka wasitishe vinginevyo wangekabiliana na mkono wa dola.
Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Mussa Ali Mussa, alitangaza kuupiga marufuko mhadhara huo na kuwataka wananchi na waumini kutohudhuria na kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo angechukuliwa hatua kali.
Kufuatia agizo hilo, Polisi wa Operesheni maalum leo, walimwagwa katika viwanja vya Lumumba huku magari yenye askari wa kutuliza ghasia yakiranda kwa kila eneo kumkabili yeyote atakayekaidi na kufika kwenye viwanja hivyo kwa madhumuni ya kuhudhuria mhadhara huo.
Hatua hiyo ya Polisi imeweza kudhoofisha kabisa hali ya majigambo ya viongozi na wafuasi wa Kikundi hicho cha Uamsho waliotangaza kufanya mhadhara huo hata baada ya serikali kupiga marufuku.
Viongozi wa kikundi hicho ambao walionekana kugawanyika waliwajulisha baadhi ya wafuasi wao kuwa hali isingekuwa swari kwa upande wao kutokana na Jeshi la Polisi kusambaza makachero na askari wa kawaida katika maeneo mbalimbali ikiwemo Viwanja vya Lumumba palipopangwa kufanyika kwa mhadhara huo.
Ni wafuasi wachache tu walionekana kufika katika msikiti wa Mbuyuni kwa sala ya kawaida na pengine kupata taarifa za hatima ya mhadhara huo uliopigwa stop na Jeshi la Polisi.
 
Nikiona hiyo style ya Midevu ya kikundi Cha UAMSHO nashindwa kutofautisha na vile vikundi hatari vya Boko Haramu na Alishabab
 
muandishi pole sana mkutano ulifanyika na watu walihudhuria wengi sana viwanja vya malindi. UAMSHO hawana lengo la kuiingiza nchi yao kwenye mitego ya kijinga lengo kufikisha ujumbe kwa jamii na kutumia haki yao ya kimsingi

angalia hizi picha

uamsho1.jpg
Muhadhara wa UAMSHO wafanyika kwa amani

Salma Said,
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) jana imefanikiwa kufanya mhadhara wake katika viwanja vya Malindi kwa hai ya amani. Mhadhara huo awali ulipangwa kufanyika katika viwanja vya shule ya Lumumba lakini jeshi la polisi lilipiga marufuku na kutaka wananchi kutoshiriki katika mhadhara huo kutokana na hali ya kiuslama.
Viwanja vyote vya Lumumba jana vilionekana vimezingizwa na ulinzi mkali tokea majira ya saa sita mchana huku magari ya polisi wa kutuliza ghasya FFU wakizunguka zunguka katika maeneo yote ya mji wa Zanzibar.
Mwananchi ilishuhudia vijana mbali mbali wakiwa kando ya uwanja wa Lumumba na wengine kujibanza vipembeni wakisubiri kuingia uwanjani lakini kutokana na hali ya ulinzi kuimarishwa wananchi hao walishindwa kusogea na walikaa umbali mkubwa wa uwanja huo.
“Ulinzi naona sio wa kawaida na inaonesha hawataki watu hata kusogea umbali wa mita mia mbili, si mnaona mabunduki yake yalivyosimamishwa? Kila mmoja amebeba bunduki yake wamefunga kabisa uwanja” alisema kijana mmoja ambaye alikuwa amekaa kusubiri kuingia uwanjani.
Maelefu ya waumini walihudhuria katika viwanja vya Malindi katika manispaa ya mji wa Zanzibar ambapo viongozi wa jumuiya hiyo walikutana na kukaa msikitini na kuanza kwa sala ya alaasiri na baadae kuanza mhadhara ambapo awali baadhi ya watu walikuwa wakiogopa kusogea katika ameneo ya msikiti huo kutokana na ulinzi mkali kuka kando ya barabara zote za darajani, malindi na barabara ya kuendea Bwawani.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamishana wa polisi Mussa Ali Musa alisema mhadhara wa Lumumba haukuweza kufanyika kwa kuwa jeshi la polisi lilitekeleza amri ya serikali ya kutoruhusu mihadhara na mikusanyiko katika kipindi hiki.
Lakini alisema kufanyika kwa mhadhara huo katika viwanja vya Malindi wanahesabu kwamba bado hapo ni maeneo ya msikiti na hivyo hawajakataza watu kuendelea na shughuli zao za kidini iwapo watadumisha amani na usalama wa nchi.
Akizungumza katika mhadhara huo Sheikh Farid Hadi Ahmed amesema jumuiya na taasisi za kidini zitaendelea kufanya mihadhara yake na wataendelea kudumisha amani kwa kuwa lengo lao ni kutoa sauti yao ambao wanadai Zanzibar huru yenye mamlaka kamili.
Sheikh Farid alitoa pongezi wa jeshi la polisi na kamishna Mussa kwa kufahamu lengo la jumuiya hizo na kueleweshana namna ya kudumisha amani na utulivu hasa katika kipindi hiki ambacho wananchi wa Zanzibar wamegawanyika kutokana na misingi yao ya kivyama.
“Sisi bado tunahitaji kupata utulivu, amani na umoja na hivyo tunapaswa kuwa makini na watu ambao wamekusudia kutugawa lakini tuwe macho na watu kama hao” alitahadharisha Sheikh Farid.
Kwa upande wake Kiongozi wa Uamsho Sheikh Mselem Ally alisema wazanzibari wanadai Zanzibar yao na hivyo hakuna kitu ambacho kitawarejesha nyuma katika madai hayo hadi hapo watakapopata haki yao lakini wataendelea kudai mpaka mwisho wa nguvu zao.
“Sisi madai yetu ni kutaka Zanzibar yetu yenye hadhi na mamlaka kamili kwa hivyo haya yanayotokea ni lazima tuwe na busara na tuwe na subira katika kudai haki yetu lakini tutaendelea kudai mpaka mwisho” alisisitiza Sheikh Msellem.
Sheikh Msellem alisema wazanzibari baada ya kutenganishwa kwa miaka kadhaa sasa wanatakiwa kujua wanachodai ndnai ya muungano na wasikubali kabisa kugaiwa kwa misingi ya kivyama kwani kumekuwepo na kitendo cha makusudi cha kuwagawa waumini wa kiislamu.
Azzan Khalid Hamad ambaye alikuwa nje ya nchi kwa matibabu alisema wazanzibari wamegawanywa kiwa muda mrefu na katika hili ilitokea khitilafu na baadhi na watu kuchukua nafasi ya kutaka kuwagawa tena jambo ambalo alisema wameweza kulirekebisha.
“Wakati wenzetu watanganyika wanaendeleza nchi yao sisi tunagombanishwa lakini tunasema kwa sasa hamtugawi tena na tumeshawafahamu “ alisema na kusisitiza suala la umoja na mshikamano kati ya serikali na taasisi hizo za kidini.
Alisema taasisi hizo zina imani kubwa sana na Rais wao Dk Shein na Rais Kikwete lakini wanaamini kwamba kauli walizotoa wamezitoa kutokana na kupotoshwa na watendaji wao lakini wakaahidi kuwa na mashirikiano mema na viongozi wao kwani nia ni kuweka amani na utulivu katika nchi.
Jeshi la polisi lilionekana likiranda randa katika eneo la darajani, michenzani, na barabara za viwanja vya Malindi ili kudhibiti iwapo kutatokea vurugu lolote, lakini hata hivyo mhadhara umemalizika kwa salama bila ya kutokea fujo na wananchi wameondoka katika viwanja hivyo kwa usalama wakati jeshi hilo likiwa kando mno na wananchi waliokusanyika.

source: Muhadhara wa UAMSHO wafanyika kwa amani | Mzalendo.net
 
ahahahahaa! kweli haja kubwa unayo faridi na kushusha hilo gogo ni haki yako! Lakini choo ulicho ingia balahau, ni choo cha kike!
 
Kwahiyo mkutano uliendelea hata baada ya kupigwa marufuku? Wanzanzibar kweli ngangari!
 
ndugu mwandishi naona umeandika kuwa muhadhara haukufanyika ,lakini hapa naona picha umefanyika sasa na yupi mkweli au ndio nyinyi mlowekwa kupotosha uma wa watanzania kama huna uhakika na mambo bora unyamaze wangu
 
muandishi pole sana mkutano ulifanyika na watu walihudhuria wengi sana viwanja vya malindi. UAMSHO hawana lengo la kuiingiza nchi yao kwenye mitego ya kijinga lengo kufikisha ujumbe kwa jamii na kutumia haki yao ya kimsingi

angalia hizi picha

View attachment 55415

Lengo ulikuwa ufanyikie wapi ? Hivyo viwanja malindi si maeneo ya msikiti? UAMSHO WAMENYWEA...chezea dola weye...!
 
ndugu mwandishi naona umeandika kuwa muhadhara haukufanyika ,lakini hapa naona picha umefanyika sasa na yupi mkweli au ndio nyinyi mlowekwa kupotosha uma wa watanzania kama huna uhakika na mambo bora unyamaze wangu

Muandishi yupo sahihi ...mhadhara ulitakiwe kufanyika Lumumba lakini baada ya kukutana na mitutu ikiwa tayari wana uamsho waliufya wakaenda kufanyia mhadhara wao msikitini/maeneo ya msikiti... nilikuwepo
 
Tatizo ni kuwa media zimetangaza zaidi propaganda ya kitu kisichokuwepo kule zenj na hasa kwa wazenj. media zimekomaa kupandikiza chuki kubwa na mbaya sana miongoni mwa wabara na wazenj. Ndio maana mkutano ulifanyika na siyo kwamba polis hawakuona waliona sana lakini kwa umati huo there was no way out ya kuanza kuwapiga na wakati wao wamekaa zao kwa utulivu bila kumbughudhi mtu, sasa ni aibu kwao kwani kisingizio chao ilikuwa ni kutokuwepo usalama, mbona mhadhara umefanyika na hakuna aliyeguswa? Mbinu chafu huwa haziwezi kushinda nguvu ya umma.
 
Muandishi yupo sahihi ...mhadhara ulitakiwe kufanyika Lumumba lakini baada ya kukutana na mitutu ikiwa tayari wana uamsho waliufya wakaenda kufanyia mhadhara wao msikitini/maeneo ya msikiti... nilikuwepo

kama ulikuwepo kisingizio cha polis ni hali ya kiusalama sasa je kwa ulivyoona vipi hali ya kiusalama ikoje? kaka tatizo ni propaganda nyingi kuliko uhalisia na hicho ndicho kina ikost sana ccm sasahivi, kwani kila propaganda wanayoitengeneza inagonga ukuta. watu walio na akili salama huwa wanawashitukia fasta
 
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wananchi wa Zanzibar wakiwemo wafuasi wa Kikundi cha Uamsho kilichotangaza kufanyika kwa mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba mjini hapa, kimetii amri ya Jeshi la Polisi kwa kutoonekana kwa muumini ama viongozi wa kikundi hicho katika viwanja hivyo.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema leo kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kudhibiti maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar na hivyo kutojitokeza tena kwa wafuasi wa kikundi hicho kama ilivyotangazwa awali.
Inspekta Mhina amesema Kikundi hicho cha Uamsho kupitia kwa Kiongozi wake Sheikhe Farid Hadi, juzi kilijigamba kufanya Mhadhara mkubwa leo arasili katika viwanja vya Lumumba mjini hapa hata baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyiko, kimeshindwa kufanya hivyo kufuatia agizo la Jeshi la Polisi lakuwataka wasitishe vinginevyo wangekabiliana na mkono wa dola.
Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Mussa Ali Mussa, alitangaza kuupiga marufuko mhadhara huo na kuwataka wananchi na waumini kutohudhuria na kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo angechukuliwa hatua kali.

Kufuatia agizo hilo, Polisi wa Operesheni maalum leo, walimwagwa katika viwanja vya Lumumba huku magari yenye askari wa kutuliza ghasia yakiranda kwa kila eneo kumkabili yeyote atakayekaidi na kufika kwenye viwanja hivyo kwa madhumuni ya kuhudhuria mhadhara huo.
Hatua hiyo ya Polisi imeweza kudhoofisha kabisa hali ya majigambo ya viongozi na wafuasi wa Kikundi hicho cha Uamsho waliotangaza kufanya mhadhara huo hata baada ya serikali kupiga marufuku.
Viongozi wa kikundi hicho ambao walionekana kugawanyika waliwajulisha baadhi ya wafuasi wao kuwa hali isingekuwa swari kwa upande wao kutokana na Jeshi la Polisi kusambaza makachero na askari wa kawaida katika maeneo mbalimbali ikiwemo Viwanja vya Lumumba palipopangwa kufanyika kwa mhadhara huo.
Ni wafuasi wachache tu walionekana kufika katika msikiti wa Mbuyuni kwa sala ya kawaida na pengine kupata taarifa za hatima ya mhadhara huo uliopigwa stop na Jeshi la Polisi.
huna nia ya kuuleta ukweli hapa jamvini. ni unafiki ndio ulokusukuma, jf ni ya wasomi sio washabiki mnaoichafua watu kama nyinyi, mara hawajafanya, mara watu kidogo ulipooneshwa picha mara.... alimradi hueleweki
 
Nikiona hiyo style ya Midevu ya kikundi Cha UAMSHO nashindwa kutofautisha na vile vikundi hatari vya Boko Haramu na Alishabab

Najaribu kutafakari na kujiuliza Hivi amani ya Dunia ingekuwa vipi kama kusingekuwa na Uislam duniani????:ranger:
 
Polisi wa Zanzibar na Uamsho hawatofautiani, wanakula njama pamoja, we nenda huko mi niende huku...
 
Sasa ndo naamini kuna magazeti uchwara huu uliofanyika sio mkutano pambaf kadanganyeni mabwana zenu.Nyie jeshi la polisi mnatuchanganya tuu hoo mkutano haujafanyika shenzi kabisa wanatakiwa wajiuzulu wote hawa viongozi wa Polisi
 
Kwahiyo mkutano uliendelea hata baada ya kupigwa marufuku? Wanzanzibar kweli ngangari!

Siku zote Haki haiombwi BALI INADAIWA.

WaZnz wanataka Haki zao kimsingi na wameshazibainisha wazi. Wanataka Uhuru wao kama nchi na si vinginevyo.

Hongereni waZnz kuziona dhulma na kudai haki zenu.
 
Kwahiyo mkutano uliendelea hata baada ya kupigwa marufuku? Wanzanzibar kweli ngangari!

Siku zote Haki haiombwi BALI INADAIWA.

WaZnz wanataka Haki zao kimsingi na wameshazibainisha wazi. Wanataka Uhuru wao kama nchi na si vinginevyo.

Hongereni waZnz kuziona dhulma na kudai haki zenu kikatiba.
 
Back
Top Bottom