Uamsho wakana kuhusika na vurugu za Zanzibar

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
jisomee mwenyewe hapo chini
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU (JUMIKI) للجنة الدعوة الإسلامية

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR

Tarehe 27 MAY 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu. Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012.

Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.

Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu.

Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu. Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine. Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.

WABILLLAH TAWFIQ
 
Jackbauer:

Unajua tatizo kuu la Waislam? sio hapo Zanzibar tu, Dunia nzima Waislam hatuko Organized!

Haya yanayotokea unaweza kusema yalikuwa Instigated (yamechochewa na maneno yaliyomo katika hutuba za Maamiri husika wa UAMSHO shk Azan na Farid hususan) sikiliza hutuba zao za jana viwanja vya Pwani Vitisho na kuwahamasisha Wafuasi wao kuwa tayari Kufa. Hivyo Ukanusho huu ni wa kinafik.

Tuna Mashekh wanakariri sana Aya na Hadith Kwa Maslahi yao.

Kwa kusikiliza mihadha yao utaona wanawaburuza Wafuasi wao kusikoeleweka na hii inanirudisha nilipoanzia kutokuwa na mipango.

Mwanzo unakuwapo lakini uratibu wa mwendeleo na mwishilio inakua hakuna.
 
389183_10150807454736176_721596175_9892161_1192091760_n.jpg
 
SIKU MOJA NILIKUWA NAPITA KARIBU NA MSIKITI WA BONDENIHAPO ARUSHA KULIKUWA NA MKUTANO MKUBWA WA WANAOJIITA WAISLAMU SHEHE MMOJA AKWAANADAI ETI WIMBO WA TAIFA NA DUA (SALA) YA KUFUNGUA BUNGE NI LAZIMA IBADILISHWEKWANI NI ZA KIKRISTO....AKASEMA WATAPELEKA MAPENDEKEZO SERIKALINIVIBADILISHWE....MIMI KTK KUTAFAKARI KWANGU...NIKAJIULIZA SASA VIBADILISHWEVIWEJE BADALA YA ILIVO SASA HIVI........HAPO NDIPO NIKAGUNDUA JAMANIKUWA......FIKRA ZA ALIYENDANI MYA BOKSI HUTEGEMEANA SANA NA UKUBWA WA BOKSIALILOMO.
itafika mahala tafsiri ya uislam tanzania itakuwa ni ignorancy
 
Jackbauer:
Unajua tatizo kuu la Waislam? sio hapo Zanzibar tu, Dunia nzima Waislam hatuko Organized!
Haya yanayotokea unaweza kusema yalikuwa Instigated (yamechochewa na maneno yaliyomo katika hutuba za Maamiri husika wa UAMSHO shk Azan na Farid hususan) sikiliza hutuba zao za jana viwanja vya Pwani Vitisho na kuwahamasisha Wafuasi wao kuwa tayari Kufa. Hivyo Ukanusho huu ni wa kinafik.
Tuna Mashekh wanakariri sana Aya na Hadith Kwa Maslahi yao.
Kwa kusikiliza mihadha yao utaona wanawaburuza Wafuasi wao kusikoeleweka na hii inanirudisha nilipoanzia kutokuwa na mipango.
Mwanzo unakuwapo lakini uratibu wa mwendeleo na mwishilio inakua hakuna.

nakubaliana nawe kwa 100% kwamba hata kama hawahusiki,ila kauli zao zimewaingiza matatani,maana raia wameamua kufanya kwli baada ya kugundua kuwa wanachoambiwa na viongoz wao wa kiiman ni sahihi,pia si kila muumin wa kiislam ana elim ya hadith na aya za qu'an
 
so what?tamko halinihusu mimi mtanganyika,.zanzibar kumejaa vijana mateja kila mtaa sababu ya muungano,so pathetic
 
Hao viongozi wa uamsho wangekuwa na hata chembe ya uangwana/busara wangewaomba msahamha kwa (a) waislam wote na (b) wanzinzibari wote kwa haya yaliyotokea.

Build up ya machafuko ya jana imefanyika kwa muda mrefu. Mihadhara yenye kujaza watu hamasa chafu imekuwa mingi. Na kwa bahati mbaya video za mahubiri zipo. Sasa wanajitoaje? Huu ni unafiki wa hali ya juu.
 
......

Unategemea busara kutoka wapi wewe?

Huwajui hao!....

....
 
nakubaliana nawe kwa 100% kwamba hata kama hawahusiki,ila kauli zao zimewaingiza matatani,maana raia wameamua kufanya kwli baada ya kugundua kuwa wanachoambiwa na viongoz wao wa kiiman ni sahihi,pia si kila muumin wa kiislam ana elim ya hadith na aya za qu'an

Hawahusiki kivipi wakati ndio walionda polisi kutaka kuwaondoa wenzao selo?
 
Kimenuka wameanza kukataana !

Sasa hao waliotangaza ni wanauamsho wameyatoa wapi?
 
I'll never take shit from anyone! to me, fist meets fist, fire will be fought with fire, cha kutambua tu watz ni kuwa hatuna serikali,na kama ipo basi ina ajenda ya siri na mustakabali wa taifa hili, haiwezekani eti serikali ipo,dola wanayo,usalama wa taifa wapo,afu uvunjifu wa amani kama huu unatokea na tunaishia kupata blah blah kama hzi and the government is there, wa TZ the cost of maintaining peace sometimes involves shattering peace itself,tuache ujinga tuliozoea wa kuongelea taratibu na watu ambao wao wanajiona wako juu ya utaratibu husika na hakuna wa kuwawajibisha na serikali pumbavu imekaa kimya.TUTANYOOSHANA WENYEWE, THOUGH UNHEALTHY BUT WE HAVE NO OPTION.
 
Serikali ianzishe kampeni maalumu ya kuwapa elimu ya upendeleo waisilamu ili waelimike waache kufanya fujo.
 
Hao viongozi wa uamsho wangekuwa na hata chembe ya uangwana/busara wangewaomba msahamha kwa (a) waislam wote na (b) wanzinzibari wote kwa haya yaliyotokea...
Dini yao inawakataza kuomba msamaha
 
Tusiukashfu uislamu na waislamu kwa sababu tu ya hao wanaojiita "JUMIKI".....Waislamu wa zanzibar mara nyingi hubeza bara hakuna waislam wa kweli......hivyo kuna waislamu wanaoifahamu dini na umuhimu wa dini na kuenenda kama quran tukfu inavyosema.....hao wachache utakuta hata misikitini hawaendi,wamesikia uamsho wakanunua kanzu na baraghashia.
 
Back
Top Bottom