uaminifu...........

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,274
20,673
Asalam aleykum........wadau na wapenzi wa MMU.
Leo ikiwa ni siku nzuri tumeanza mfungo wa mwez ramadhani basi tumwombe Mungu atufanyie wepesi na atusamehe dhambi zetu zote ndogo kwa kubwa. atujalie tuisimamie nia zetu kwa uaminifu..

ninapenda weekend tujifunze na kujadilian juu ya hili jambo uaminifu hasa katika mahusiano yetu. Jamani kila mtu anapenda mwenzie awe mwaminifu kwake lakin je tunajua hasa roles za uaminifu katika mahusiano? labda nitaje roles chache tu hapa:-
- uaminifu huongeza kujiamini katika mahusiano hasa kwa yule umpendaye.
- uaminifu huthaminisha penzi kati ya wawili wapendanao na
-Uaminifu hukuza penzi kati ya wawili wapendanao

sasa je tujiulize kwa ukweli kabisa je tu waaminifu kweli katika mahusiano yetu? na je si kwasababu ya sisi kutokuwa waaminifu ndio maana thamani, kujiamini na kukua kwa penzi kumeondoka katika mahusiano yetu. Siri kubwa ya uaminifu ni chumbani (moyoni mwako) so jiasess kisha chukua hatua.

karibuni tujadili. Na inshalla Mwenyezi Mungu ataumba upya moyo wa uaminifu nafsini mwetu. kumbuka waweza kuurudisha uaminifu ulioupoteza katika maisha yako kwa yule umpendaye.
 
Kwangu mimi uaminifu katika mapenzi ni mirage. A hope or wish that you cannot make happen because it is not realistic.

but nisemapo uaminifu namaanisha upo moyoni mwa mtu you can't talk on somebody's position so to you lazima uwe unajua is it realistic or not? naamin huwez kumsemea mtu kamwe daima. hapa tuongelee nafsi zetu.
 
Hata kwenye nafsi zetu watu huwa ni wagumu sana kujitazama, kujikosoa, na kukiri utovu wao wa uaminifu. Kama hawatatafuta justification ya huo utovu basi watakuwa kwenye denial tu.
 
yani Nyani Ngabu umenikosha kweli mkuu, lakini nafikir kwakua hapa jamvini ndipo tunapojifunza and we dare talk openly, lets talk and make up ourselves for the betterment. hivi twawezaje kuimprove uaminifu wetu?
 
Last edited by a moderator:
Haya maisha kwa kweli hayako fair.. Unakuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na unapokuwa nae unakuwa huwazi wala huna mpango na wale wengine wanaokufungia break.. Sasa tatizo linakuja kumbe mpenzi uliyenaye kwanza sio mwaminifu pili hana hata mpango na wewe! Mpaka uje ushtuke muda umeshaenda na wale waliokuwa wanakupigia honi huwaoni tena maana ngozi teyari imesha sinyaa huna mvuto teeeeena! Lol.. UMEPOTEZA MUDA WAKO BUREEEE!!!
 
Hata kwenye nafsi zetu watu huwa ni wagumu sana kujitazama, kujikosoa, na kukiri utovu wao wa uaminifu. Kama hawatatafuta justification ya huo utovu basi watakuwa kwenye denial tu.

Sijui kwa nini umeleta somo gumu usiku huu tena Ijumaa mwanzo wa wikend............Hivi kuwa mwaminifu ni

1. kutokuwa na "mtu wa pembeni" au

2. moyo ulio ulio msafi usio na rekodi ya kuvunja uaminifu ama

3. Moyo mweupe kama theluji usioweza hata kufikiria kuvunja uaminifu
 
Haya maisha kwa kweli hayako fair.. Unakuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na unapokuwa nae unakuwa huwazi wala huna mpango na wale wengine wanaokufungia break.. Sasa tatizo linakuja kumbe mpenzi uliyenaye kwanza sio mwaminifu pili hana hata mpango na wewe! Mpaka uje ushtuke muda umeshaenda na wale waliokuwa wanakupigia honi huwaoni tena maana ngozi teyari imesha sinyaa huna mvuto teeeeena! Lol.. UMEPOTEZA MUDA WAKO BUREEEE!!!

neylu nilichogundua mimi kwa ishu ya uaminifu ipo moyoni mwa mtu na ndio characher pekee ya mapenzi ambayo iko possessed ndani ya nafsi ya mtu ambayo pia yaweza kutokujulikana pale inapokosekana.mara nyingi sana uaminifu huu uwe upo ama haupo ni mpaka upate uthibitisho mbali na hapo bali unabaki kuwepo kama ulivyo. ila ngoja tuwasubiri wadau watusaidie manake naona nachanganyikiwa tu.
 
Last edited by a moderator:
Kabla sijachangia naomba kujua mtu anaposema yeye muaminifu huwa anamaanisha nini?

dada cathe kwanza waitwa chit chat. haya ngoja ni define uamnifu ni ile hali ya kuwa mkweli kimatendo katika nyanja yeyote ile. inapokuja kwenye mahusiano basi neno hili huweza kujumuishwa si tu kwa kutokuwa mzizi la hasha bali hata kuwa mkweli unapokosea jambo.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kwa nini umeleta somo gumu usiku huu tena Ijumaa mwanzo wa wikend............Hivi kuwa mwaminifu ni

1. kutokuwa na "mtu wa pembeni" au

2. moyo ulio ulio msafi usio na rekodi ya kuvunja uaminifu ama

3. Moyo mweupe kama theluji usioweza hata kufikiria kuvunja uaminifu

ma brother hujakua usiseme kabisa platozoom. haya uaminifu hauko established kweye kutokucheat la hasha hata kwenye kusema ukweli unapomkosea mpenzi wako. usemapo moyo mweupe hapo sikuelewi so sijaweza kujibu
 
Last edited by a moderator:
ma brother hujakua usiseme kabisa platozoom. haya uaminifu hauko established kweye kutokucheat la hasha hata kwenye kusema ukweli unapomkosea mpenzi wako. usemapo moyo mweupe hapo sikuelewi so sijaweza kujibu

Kwanza futa kauli yako (red) usinifukuzie ndege bure............Hata mimi sikatai uaminifu unatakiwa kwenye angle zote, na hapo unaweza kurudi kwenye orodha yangu....ili uwe mwaminifu ni criteria gani zinatazmwa (au za kujitizamia) kwa mtazamo wako........kwamba hapa kwenye hivi vigezo hivi mimi kweli ni mwaminifu
 
haya nafuta kaulai yangu jamani platozoom amekuwa.. hapo sijui nisemeje manake iyo ya 3 ina mushkheri kidogo nikimquote Eiyer ambaye huwa anasemaga sijiapize maneno magumu.
 
Last edited by a moderator:
dada cathe kwanza waitwa chit chat. haya ngoja ni define uamnifu ni ile hali ya kuwa mkweli kimatendo katika nyanja yeyote ile. inapokuja kwenye mahusiano basi neno hili huweza kujumuishwa si tu kwa kutokuwa mzizi la hasha bali hata kuwa mkweli unapokosea jambo.

orait, vipi kama nakuwa mkweli, sio mzinzi na bado mwenzangu haniamini? Mi naona huo uaminifu ukamilike lazima uhusishe pande mbili. Na upande wa pili yaani mwenzi wako ndio atakuperceive kama wewe ni mwaminifu au lah. Kuna watu wazinzi na wanasema uongo lakini bado wanaonekana ni waaminifu mbele ya wapenzi wao. Huoni kama uaminifu ni vile wanavyokuperceive wengine na si wewe unavyojiona?
Halafu chit chat nimepita dada ila nimeshindwa cha kujibu. Heading yao imenistua sana. Nimetoka kimya kimya.
 
mpendwa sidhani kama uaminifu unongelewa kwa mtu yaani siku zote uamnifu wa mtu uko moyoni mwake iwapo nitasema ni msafi ili hali siko inamaana si mwaminifu na ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. so inapendeza ujiweke mwaminifu kweli hata kama machoni huonekani lakini your heart can witness that.

huko chi chat ni stori tu wewe watakiwa uende ukachangamshe lol
 
Back
Top Bottom