Maje Omary
New Member
- Jun 20, 2012
- 4
- 0
Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa tz. Ajira mpya ngazi ya cheti: mwl 244,400/= afya 472,000/= kilimo/mifugo 959,400/= sheria 630,000/=. Ngazi ya Diploma: mwl 325,700/=, afya 682,000/=, kilimo/mifugo 1,133,600/=, sheria 871,500/=. Ngazi ya Degree. Mwl 469,200/=, afya 802,200/=, kilimo/mifugo 1,354,000/=, sheria 1,166,000/=. Kwanini walimu mnanyanyaswa hivi katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Kisa cha kuwadharau na kuwapa hela kidogo ni nini? Eti sababu tupo wengi...hiyo siyo sababu. Walimu nawaombeni tuungane msimame imara kudai ongezeko la mshahara kwa 100%. Nawasilisha kwa uchungu mkubwa...maana tumekuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Tena sisi ndo tunatumika na wanasiasa..kwenye uchaguzi, sensa etc. Inatosha kupuuzwa kwa vihela hivyo, mnakosa gani ktk nchi hii?
Nchi hii imekosa dhamira ya dhati ya kisiasa ya kuboresha elimu yetu. Wanafalsafa wa Elimu wanaamini kwamba kila mtu anafundishika. Tatizo liko katika kudharau, kuonea, kunyanyasa na kuwapuuza walimu wetu huku bado tunawataka watufundishie watoto wetu kwa bidii na uzalendo wa hali ya juu. Wenyewe wanasiasa wetu wanatuaminisha kwamba ndivyo walimu wanapaswa wawe hivyo na Mungu aliwaumba hivyo. Uliona wapi nchi inawapuuza walimu wake kiasi kwamba wazazi wanadiriki kuwachapa viboko walimu mbele ya wanafunzi wao? Halafu mwalimu afanye nini? Baada ya kufanyiwa vitendo hivyo, mwalimu aende tu kuwafundishia watoto wa hao wazazi waliowapiga viboko hadi wafaulu? Ungekuwa wewe uzalendo wa namna hii ungeupata wapi? Nadhani atakayefanya hivyo lazima awe na moyo kama wanabiifulani.
Uvumilivu unakikomo chake katika jamii, na sasa tumefikia kikomo cha uvumilivu tunatakiwa kwa umoja watu, kwa maumivu na kupuuzwa kwetu tuungane kutafuta hakiyetu. Sekta zote ni bora hakuna sekta iliyobora zaidi ya nyingine. Tena ualimu ni sekta iliyobora zaidi kwani Bila mwalimu utampata wapi huyo mwanasheria, Daktari, Injinia, Mhandisi n.k. Serikali inapswa kuwa na dhamira ya kweli katika kuiboresha sekta ya Elimu kuanzia Elimu ya Msingi hadi vyuo vikuu. Nchi nyingi duniani ambazo leo zinasifika kwa maendelea, zilianza kwa kuwekeza katika elimu.