Tz bado sana

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
841
175
Unaweza kufikiria ni sehemu fulani ndani ya nchi ya Marekani(USA)vile ilivyo!Kumbe wala,ni Kenya tu hapo.Ama kweli Tanzania bado tuko nyuma sanaaaaaa.
 

Attachments

  • NB.jpg
    NB.jpg
    42.6 KB · Views: 98
Mimi ningeshangaa TZ kuwa na flyover ingali maji na umeme ni ya mgao
 
Unajua kenya wamewekeza sana kwenye jiji la Nairobi wakasahau miji mingine..
Huwezi ukafananisha Nyeri, Kisumu nk..na mji kama Arusha ni far behind.
 
Unaweza kufikiria ni sehemu fulani ndani ya nchi ya Marekani(USA)vile ilivyo!Kumbe wala,ni Kenya tu hapo.Ama kweli Tanzania bado tuko nyuma sanaaaaaa.
je, unajua kuwa wazo la 'barabara za juu' lilianzia hapa kabla ya Kenya!? na ukiunganisha dots inaonyesha budget iliyopita 2011/2012 waliahidi kuwa ujenzi ungeanza na hiyo ahadi sasa imesogezwa kwenye budget ya 2012/13 ambapo sasa wanagaongelea makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, ya Ubungo na zinginezo haziongelewi tena! Lakini hata hiyo ya TAZARA bado kuna utata maana AZAM anaendelea kupanua kiwanda!
Tuacheni tu Watanzania tubakie na ubingwa wetu wa kuongeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeea mpaka mwisho wa dunia.

 
Mkuu lukindo,ni kweli,sisi ni mabingwa wa kuongea sana.Ila njoo kwenye utekelezaji,kila mtu anajificha.Ukiohoji kulikoni,vinaanza visingizio mpaka inakuwa kero.Lakini pia,tunaingiza siasa katika mambo nyeti kwa jamii hili ndiyo tatizo kubwa kwa viongozi wa TZ.Na siasa yenyewe haina tija kwa watu;na ndiyo maana Rostam Aziz wakati anajiuzuru nafasi ya ubunge alisema,"...nimeamua kuachana na siasa ya majitaka."Kwa maana hiyo aliona kuna ubabaishaji/kubahatisha zaidi.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha! labda tusubiri viongozi wapya, serikali mpya, na watanzania wapya..maana waliopo sasa ni madomo-kaya wakutupwa ambao ni wachumia tumbo zaidi kuliko wapigania maslahi ya umma, hata km wengine waliopo kando wanajitanabahisha kuwa ni tofauti- ni 'vifaurongo' hao!
 
Back
Top Bottom