Leslie Mbena
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 207
- 677
TWAHA KIDUKU: MPIGANAJI BORA WA NDONDI KWA SASA TANZANIA.
Leo 21:30 hrs 29/08/2020
Twaha Kiduku mpiganaji mtulivu,mchokozi wa ngumi zitakazo kuweka kwenye kumi na nane yake ambayo itakukutanisha na jebu moja matata ya mkono wa kulia toka kwenye mwili uliojaa kwa mazoezi ya tofali na kusukuma tairi ya treka kupandisha Mlima Uluguru kupitia barabara ya Mji Mkuu,rock garden,Bahati Camp na kuteremka hadi Masuka Village kuelekea Masika kati kati ya Mji wa Morogoro.
Katika pambano lake na Dulla Mbabe, nyota nyingine katika ndondi za Tanzania, Twaha Kiduku alionyesha utulivu na kurusha makonde yake ya kulia na kushoto yaliyokuwa yakitua kwenye kichwa cha Dulla Mbabe, yakimsukuma Dulla Mbabe hadi kwenye kamba za ulingo katika sekunde za mwanzo hata dakika za mwisho za pambano,
Twaha Kiduku aliweza kuendeleza machachari yake ya awali hadi raundi ya 12 baina yake na Dulla Mbabe ambaye ni mrefu kiumbo na kuweza kupenyeza masumbwi ya kujibu mapigo pale shambulizi lilipoelekea kuvuruga utulivu wake,Ustadi wa Twaha Kiduku ulionekana pale alipovurumisha makonde 435 kulinganisha na 429 ya Dulla Mbabe na asilimia 35 ya makonde yake yalifika mahala pake kulinganisha na asilimia 19 ya mpinzani wake.
- Twaha Kiduku na staili ya Upiganaji wa Mjerumani.
Wajerumani ni watu wenye kutumia nguvu, kama umewahi kumuona mpiganaji "Brock lesnar" akiwaangamiza wapinzani wake kwenye wwe na ufc, Twaha Kiduku ndiye mwenye kutumia mfumo uleule wa Wajerumani katika kumchakaza mpinzani wake yeyote anayetokea mbele yake,
Kwa Tanzania, Twaha Kiduku ni mfano wa Rashid "Snake boy" Matumla ni muhimu kumtaja Rashid Matumla kama kipimo, standard au "measuring stick" katika ngumi za Tanzania,kwa mchambuzi wa ngumi,Yassin Ustadh atakubaliana nami kuwa rekodi ya Twaha Kiduku ya Ushindi wa mechi 13,kupoteza mechi 6 na draw 1 hii ni rekodi nzuri ya Ushindi na kupigwa ni sehemu ya changamoto ya mchezo.
Mada Maugo amewahi kupigwa na Francis Cheka,Francis Cheka amewahi kupigwa na Thomas Mashali,lakini bado Twaha Kiduku mwenye uwezo wa kutupa ngumi 221 akiwa ulingoni kunamfanya kuwa mpiganaji bora kabisa wa ngumi kwa sasa,
Katika ndondi ukipigwa idadi ya ngumi 221 zikatua bala bala katika paji lako la uso,hiyo ni idadi kubwa katika historia ya masumbwi, hali inayoweza kukufanya kujiuliza kila mara ni vipi Twaha Kiduku anaweza kupata nafasi ya kupiga idadi hiyo kubwa ya makonde katika paji lako la uso!?
Kwa takwimu ya jumla ya makonde 858 yanayoweza kutupwa ulingoni baina ya watu wawili,makonde 450 yakimkosa kila mtu na makonde 221 yakifika katika mwili wako,hiki ndicho kinachoweza kushangaza mpiganaji yeyote na kumpa salute yule aliyeweza kupenyeza makonde 221 katika paji lake la uso,
Nimalizie kwa kusema Twaha Kiduku si bondia tena wa kuachia kidevu chake kichakazwe na bondia yeyote na kwa sasa ni wakati sahihi wa kupambana na Bondia bora Hassan Mwakinyo,Twaha Kiduku anatisha, Moja ya sababu ya kwa nini Twaha Kiduku anatisha sana ni kwa sababu hadharau mpinzani na siku zote anataka kukabiliana na mabondia bora mfano wa Dulla Mbabe ambaye amepambana nae na baada ya pambano amekuwa bora na ndiyo maana Twaha Kiduku ni mahiri sana.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.
-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.